Giza lilikuwa nene sana, hata asiweze kuona mbele. Sauti za ndege aina ya Bundi zilisikika na kufanya msitu huo unaotenganisha vijiji viwili mahasimu kuzidi kumtisha kijana George ambaye kwa wakati huo alikuwa akikimbia kukatiza msituni hapo.
Mwili wake ulitapakaa damu, hakuwa na nguo yeyote yenye kufunika angalau sehemu yake ya mwili. Alikuwa uchi kabisa. Alionekana kuchoka lakini hakuhitaji kusimama kusubiri mahasimu wake wanaomkimbiza kwa mapanga, rungu, mishale na mawe. Siraha hizo za jadi zilitumiwa vyema kuujeruhi mwili wa kijana George.
Kwa mwendo wa saa mbili hivi, Akiwa bado akijitahidi kuyanusuru maisha yake ndani ya ule msitu, George hakuwa na uwezo tena wa kukimbia. Miguu yake ikawa mizito sana. Damu zikiendelea kumtoka. George alianguka chini, pembezoni kidogo mwa kinjia alichokua anakimbia nacho.
Akiwa chini akigarauka, George alisikia kelele za wanaomkimbiza zikizidi kumsogelea. Hakuwa na namna tena. Alianza kuona miti ikizunguka. Bila shaka ni kwasababu ya damu nyingi iliyommwagika. Mara akazima pale chini. George amezirahi.
Wale wanaomkimbiza walizidi kumsogelea. Ni wenye jazba sana na wenye nia ya kuua kwa dhana tu walizozibeba. Hawakuhitaji kumkosa wanaye mkimbiza.
"Angalia, tunakaribia Kijiji Cha pili. Simameni." Alizungumza Bwana Kim, kiongozi wa msafara unaomkimbiza George.
"Turudini, maana pia kunakucha" Aliongeza
************************
Usikose sehemu ya 2 🙏
Mimi ni Lipeta S Shaaban.