Elimu ni mkombozi siku zote.. Huyu ni George McLaurin ndiye mwanaume mweusi wa kwanza kukubaliwa Chuo Kikuu cha Oklahoma mnamo 1948, na alilazimishwa kukaa kona mbali na wazungu wenzake. Lakini jina lake limebaki kwenye orodha ya watu wenye heshima kama mmoja wa wanafunzi watatu bora chuoni. Haya ni maneno yake:
"Baadhi ya wenzangu walinitazama kama mnyama, hakuna aliyezungumza nami, kwa walimu sikuwa nikionekana hata kidogo, mara chache walijibu maswali yangu. Nilijitolea sana, mpaka baada ya wenzangu kuanza kunitafuta na walimu kuanza kunizingatia. Niliacha kuwa asiyeonekana kwao."
Elimu ina nguvu zaidi kuliko silaha..