Nikaongoza mpaka kwenye gari akanifungulia mlango wa mbele baada ya mie kuingia nae akaingia akawa ananitazama juu mpaka chini hapo ndo nikashtuka baada ya kugundua mavazi yangu ,macho yake yalijaa tamaa tu
"Nambie!!" Ndo nikamshtua
"Unajua salma naomba usinielewe vibaya" akaniwekea mkoni wake kwenye paja langu, nikashtuka lakini nikavunga kama sijajali hivi ,nikabaki namtazama nisikie anataka kusema ninii??
"Tangu nimekuona ile siku gafla sana ,nimevutiwa sana nawe ,nimejikuta hata kulala nalala kwa tabu sanaaa kuna muda nikianza kula nawaza kama umekula na nashindwa kabisa , naomba unipe nafasi nikupe dunia ingine ambayo wewe unastahili kuishi"
Mh huyu kaka nilimtazamaaa jinsi anavyoongea macho yake yamejaa sana tamaa ya ngono alikuwa ananiangalia kwa tamaa na vile nilikuwa nimevaa , nilikuwa kimyaa tu
"Kwahiyo salma utanipa eeh???" Akaanza kunishika shika paja
"Kaka Samahani naona unaenda kuvuka mstari wako " niliutoa ule mkono wake juu ya mwili wangu
"Nitakupa chochote salma nitakupa maisha"
"Maisha teyar ninayo sijui utanipa yapi???" Sikusubiri anijibu nikaona tu ananichanganya nikafungua mlango wakati nataka kutoka alinivuta , alinivuta kijora nikajikuta kimefunguka, ilibidi niwahi kujifunika tena nguo
"Salma naomba nielewe tafadhali "
"We kaka vipi sitakiii ,nimesema sitakii ahhh" ilibidi niwe mkali sasa
"Unataka pesa??" Aliniuliza ,nilimtazamaaa sana nikamuona ni mpuuzi tu
"Sihitaji!! Naomba usije tena kwangu" nilitoka kwenye gari nikamuacha ananitazama kwanza nilimuona kama muhuni na amekaa kihuni huni tu .
Nilirudi mpaka ndani,nikafunga zangu mlango nijilalie tu , nilipo shika simu nikakuta msg nyingi nyingi na alex pia amenitumia sikuwa nimeisave namba ake nikampigia mdogo wangu huko nyumani nikamwambia anitumia jina la Alex linaandikwa vipi ili nisave .
Alipo nitumia tu nikaisave ndo nikampigia lakini hakupokea iliita ilipo kata alituma sms aah mi ananikera mara kibao nishamwambia sielewi mie lakini bado tu amekazana aaa ..
Siku inayofuata niliamua kwenda nyumbani kwa mama ,nililala huko siku mbili , ile siku ya pili ndo siku ambayo nilikua nimepanga kurudi kwangu nishapata na wazo la kufanya biashara gani ,sikutaka tena kushinda nyumbani bila issue yeyote ile , inno alinipigia simu akaniuliza nipo wapi amekwenda nyumbani sipo nikamwmbia nipo kwa mama akaomba nimuelekeze nikamwambia hata usijali huku ni mbali sana , akanibembeleza sana kuwa anataka kuja mana nilimwambia najiandaa kuondoka ,alinilazimisha kweli nikamwambia poa ilibidi nimuelekeze tu aje huko
Baada ya Inno kukata simu ,zilipita kama dakika mbili hivi alex akanipigia simu
"Jamani msg zangu ndo hujibuu" kabla hata ya salamu akaanza kunipa lawama
"Wewe ni wa ajabu sana, mara ngapi nimekewambia mi sijui kusoma???"
"Embu acha zako bwanaaaa , haya nambie upo wapiii nakuja mtaani kwako sasa hivi"
Sasa nikajiuliza kwani hajui kama inno kaja nyumbani ?? Au inno hajamwambia??
"Nipo kwa mama"
"Nielekeze nije kumuona mama" mungu wangu sasa hawa inakuwaje nilijikuta nashindwa kufanya maamuzi ,sikuwa najiamini ,inno kasema anakuja sasa hivi Alex hii imekaaje hawa watu si inabidi wawe wanapeana taarifa kuhusu mie na mara zote inno mi najua anaagizwa na alex sio yeye kuja kuja tu kwangu bila Alex kuwa na taarifa halafu mie sijamzoea huyu kaka ile kupiga story siwezi ila alex nakuwa huru kuongea chochote kile
Ilibidi tu nimuelekeze mana aliningangania sanaaa ,nikatamani kumwambia Inno pia anakuja ila nikakausha watajua wenyewe bwana ...
Wa kwanza kufika alikuwa ni Alex ,nikamkaribisha vizuri nikamtambulisha kwa mama na vile mama alikuwa teyar anastory za alex alimpokea vizuri sana ,alex nae hakuja kinyonge alikuja na mazaga zaga kama yote mama yangu ndo kucheka mpaka jino la mwisho si unajua wamama wetu wa kiswahili hawa ni kazi kweli ..
Nikashangaa huyu kapitia sa ngapi hivi vitu mana alimpa mama mpaka madera yale ya msomali matatu na vitenge jamani nikaona aibu hata ..
Inno alinipigia simu akasema ameenda nyumbani nikajua mpo wote!!" Nilimwambia alex ili kumpa taarifa mana inno alikuwa anapiga simu muda huo nikahisi tu anataka nimuelekeze labda amekaribia
"Mmh alikuwa kwako??" Akaniuliza huku anaonesha mshangao
"Ndio"
"Mi hakunambia hata nami sijamwambia sijamtafuta tangu nitoke kazini ,nimekuta moja kwa moja hapa "
"Ooh afu nae huyu anapiga mana nilimwambia sipo nipo huku akasema nimuelekeze " nikaendelea kujibalaguza
"Mpokee umuelekeze asije enda njia ingine buree" alex kama kawaida yake amechangamka mi nikapokea, kweli inno alikuwa mitaa ile ya nyumbani akaja , nilimuona kama amesita kidogo baada ya kumuona alex lakini wakachangamkiana kweliii
"We dogo mpuuzi sanaaa , unajua jana ile aah yaani we achaa hahaha" wakawa wanaongea hata sikuelewa mada zako ila walikuwa wanacheka kweli ..
Mi nikamraibisha inno nikamtambulisha pia kwa mama kama ndugu yake na alex na pia ni mapacha kabisa wa kuzalia yaan hawa sio marafiki ni pacha kabisa na wanafanana vizuri tu ,
Baada ya muda mi niliondoka na Alex ndie alinipeleka nyumbani inno akasema ye kuna sehemu anaenda hatokwenda kwangu mi nikasema sawa haina shida ..
Tulifika kwangu ilikuwa giza tayar limetanda .
Nikapika tukala na alex ananipigisha kila aina ya story baada ya kumaliza kula akaniambia anaondoka nikamtania mi najua unalala hapa alicheka akanambia kama unataka nitalala nikasema hapa leo nenda kwako bwana tukawa tunataniana ananiambia unanifukuza haya mi naenda, nikatoka kumsindikiza kwenda kwenye gari
"Afu nilitaka kusahau umeona!! kilichonileta ni kwamba kesho kuna sherehe ya mdogo wake felix anamaliza chuo naomha uwe kampani yangu please " nikacheka nikamuuliza kampani kiaje ?? Akasema twende wote ili nisiwe bored peke yangu tutaenda ,nikasema ndio hata usijali itakuwa sangp akasema wanaanza sa kumi mbili jioni ila nitakuijia mapema nikasema sawa
Wakati huo tumefika kwenye gari yaan tunaongea huku tumesimama pembeni , nilipata hisia kama vile kuna mtu anatuangalia nilipo geuka kwa mbele nilimuona Juddy amesimama kweli anaangalia upande wetu, sikutaka hata alex ajue naangalia nini nikarudisha macho chap .
Alex aliondoka mi nikarudi ndani hapo nawaza lazima shoga atanifata tu lakini wala hakunifata ,mama akanipigia simu anasema huyu rafiki yako mlipoondoka tu ye alirud hapa nikamuuliza Rafiki yangu yupi?? Akanambia sijui ndo i nani sijuiii ,nikasema innno??? Akasema enhee huyo huyo ,nikashangaa inno kaenda kufanya nini nyumbani ???
ITAENDELEA....
KWETU morogoro.