Nilipogundua mtu ninaye muelezea matatizo yangu ndiyo mtu ambaye yupo mstari wa kwanza katika kuharibu mambo yangu, Nilisimama na kuondoka,
Rafiki ambaye nilimpenda kwa dhati na kuamini atabaki na mimi wakati wa shida, Nayeye aliungana na maadui zangu kutaka kuniangamiza, Niliondoka mapema kabla mipango yao haijatimia,
Wakati nafika nyumbani kabla sijaingia ndani, Nilisikia familia wakinisema kwa maneno ambacho yalinifanya nikose furaha, Nilitikisa kichwa na kuonndoka,
Hata wakati sina kazi familia iliniona kama mtu asiyekuwa na mchango wowote katika familia, Sikusubiri hadi wanifukuze, Niliamua kuondoka,
Nimejifunza mengi wakati nipo peke yangu, Nimejifunza namna ya kuishi na maadui na marafiki, Nimejifunza kupambana na changamoto za kila aina, Nimejifunza kutokuogopa chochote katika maisha yangu, Lakini pia nimejifunza namna ya kutafuta pesa kujali muda na matumizi,
Siwezi kukata tamaa, Siwezi kutamani cha mtu, Siwezi kurudia yale yaliyoniumiza, Hata nikitizama nyuma yangu huwa natabasamu na kusonga mbele, Sababu bado naamini kile ninachokitafuta kipo kule ninapoelekea, Siwezi nikawa muoga wa majukumu yangu mwenyewe, Sababu najua majukumu yangu ni mimi mwenyewe,
Nitapambana na kila kilichopo mbele yangu, Sababu maisha ni mkusanyiko wa matukio,
Natumaini na wewe unayesoma hapa utakuwa na nguvu ya kupambana, Usichoke wala usikate tamaa jitahidi uwe mbele ya kile unachokipambania.
~Daudi~.