Ilikuwa asubuhi muda wa saa mbili na nusu. Baridi kali ilikuwa imetanda katika mikoa mingi ya Tanzania na kanda ya Afrika Mashariki kwa ujumla.
Maeneo ya Mbauda Jijini Arusha ndipo kulikuwa na tatizo kubwa la baridi kali sana, mabinti zaidi ya 80 waliovaa kwa nidhamu walikuwa wamejikunyata katika viti vya mapokezi katika ofisi ndogo ya kampuni ya Terejo Co Ltd huku wakionekana kujawa na wasiwawasi kana kwamba kuna shughuli waliokuwa wakaifanye ndani ya ofisi hiyo.
Ghafla gari nyeusi kuanzia vioo, rangi hadi tairi iliingia katika ofisi ile alishushwa mtu mmoja aliyeonekana mwenye pesa nyingi sana, alikuwa mweupe mwenye miwani, umri wa makamo miaka kati ya 35 hadi 40.
Alitazama kushoto kulia akawaona mabinti wakiwa wamesimama wengi sana akatabasamu na kufunga mlango wa gari paah! Gari ikarudi nyuma maana dereva alikuwa sio yeye.
Alitembea kuwapita mabinti wale akawasalimia "MORNING" alisema kwa sauti nzito huku akitabasamu
"MORNING" mabinti walisalimia kwa nidhamu kisha akaingia ndani.
Waliendelea kusubiri kwani walikuja kwa ajili ya kufanya interview (mahojiano) kwa sababu kulikuwa na nafasi za kazi zimetangazwa siku sio nyingi.
Nusu saa tu baada ya Boss kuingia, alitoka mfanyakazi mmoja wa kike na kusimama mbele ya wale wasichana
"JAMANI NAOMBENI UTULIVU" alisema mwanamke huyo maana mabinti walikuwa wakiongea sana "NITAITA MMOJA MMOJA KISHA ATAINGIA NDANI KWA AJILI YA INTERVIEW KATIKA CHUMBA NAMBA 3"
Wasichana wale mioyo iliwadunda, uoga hawajui ni maswali gani ataenda kuulizwa. Jina likasikika la kwanza
"ADELINE WERAUFOO KITOMARI" aliita mwanamke yule, moyo wa msichana mmoja ukamdunda
"NIPO" alisema kwa sauti hafifu
"CHUMBA NAMBA 3" alisema yule mwanamke na kurudi ndani.
Adeline aliingia huku akitetemeka, alipofika ndani tu hivi, chumba namba tatu, alimkuta yule mwanaume aliyekuja na gari akiwa amekaa kwenye kiti kizuri halafu anatabasamu
"SHIKAMOO" alisema Ade kwa uoga
"wooow...marahaba karibu ukae mrembo" alisema boss huku akitabasamu na kuonyesha meno halafu akafinya jicho moja. "Keti mtoto mzuri" alisema
JE. ITAKUWAJE? USIKOSE SEHEMU YA PILI YA KIGONGO HIKI CHA NIKIKUPA UTAMU UTANIAJIRI? 🪭🪭😳
#MrAB
NIKIKUPA UTRAMU UTANIAJIRI? 🪭🪭😳 02 🔞
Hadithi fupi fupi
Na BURUDAN
Insta: @Burudan_Simulizi
Adeline alitazama kando kulikuwa na kiti cheupe, akatabasamu na kukisogelea akakaaa
"Mi naitwa Dk Jonas Vengu Unaweza kunikumbusha unaitwa nani?" aliuliza mhoji
"Naitwa Adeline Weraufoo Kitomari"
"Oh....nice, unajua kwanini uko hapa?"
"Nimekuja kwa ajili ya Interview"
"Sawa, sasa mimi ndo interviewer hapa na ndiyo mkurugenzi wa hii kampuni, naomba nikuhoji, je nitumie lugha ya Kiswahili au Kiingereza?"
Ade alitabasamu na kuangalia chini "Yoyote tu unaweza tumia"
"Sawa kwa sababu wewe ni mzuri basi natumia Kiswahili kwa ajili yako wewe pekee....hivi una elimu yoyote kuhusiana na Marketing?"
"Ndio, nina shahada niliipata katika chuo cha SAUT Mwanza"
"Wow, ulimaliza mwaka gani?"
"Nilimaliza 2017"
"Baada ya kumaliza ulishawahi kufanya kazi popote?"
"Ndio nilifanya katika kampuni ya Poasana Dar es Salaam"
"Sawa embu nieleze una uwezo gani katika kumshawishi mteja?"
"Oh ninatakiwa nitumie lugha rahisi na ya kumfanya ajione yeye ni mteja pekee, na kuisifia bidhaa pia, sitokubali kuiangusha kampuni"
"Woow" alisema Mhoji huku akimnyooshea mkono "Safi sana" alisema na kumpa mkono binti kama vile wanasalimiana.
"Asante"
"Haya unaweza kuinuka usimame pale niangalie mavazi" alisema muhoji
"Sawa"
Adeline aliinuka alikuwa binti mrefu mrefu mwembamba mwenye mwili kama ile ya Wasomali na Watusi wa Rwanda.
Binti alikuwa amevaa suti ya kike iliyomkaa vizuri, ya rangi ya blue nyeusi, akamtazama muuliza maswali anamkagua kwa macho kuanzia juu mpaka chini
"Unaweza kwenda tutakupigia simu" alisema Jonas Vengu "Uniitie Tumaini Malata"
"Asante" Ade alisema na kutoka nje
Wakati anatoka ndipo Interviewer alipata fursa ya kumuona upande wa nyumba binti alikuwa slay queen mtoto mkali sana.
"Wow, she's very cute" alisema na kutia nyota kwenye jina la Ade kwenye karatasi
Baada ya dakika moja aliingia binti mwingine ambaye alikuwa mweusi aliyesuka penseli kichwani halafu akamtazama
"Samahani boss Tumaini Malata bado hajafika" alisema
"wewe kwani ni nani?"
"Erica"
"Erica, uko kwenye interview pia?"
"Ndio"
"Karibu basi nikuhoji wewe kwanza"
"Asantee" alisema Erica na kuingia ndani, binti alitabasamu USIKOSE NO 3
NIKIKUPA UTRAMU UTANIAJIRI? 🪭🪭😳 03🔞
Na BURUDAN
TUNAENDELEA TULIPOISHIA
Erica alitabasamu kwa ukarimu ili kumridhisha bosi wake ambaye alitarajia amuajiri katika ofisi hizo za Terejo Co Ltd
"Karibu uketi" Alisema Dk. Jonas
"Thank youuu" binti alisema huku akizidi kucheka cheka. Aliketi na kumtazama mhoji.
Jonas alipotupa jicho kifuani mwa binti, aligundua binti hakufunga vishikizo vya juu, aliacha sehemu ya maziwa yake makubwa wazi halafu alichezea vidole vyake vyenyewe, alikuwa mrembo japo sio mzuri, naamini naeleweka.
"Mbona jina lako silioni" alisema Jonas
Erica alizidi kutabasamu, na kujipendekeza "Samahani mimi ni msichana ambaye nilishindwa kumaliza chuo kwa sababu ya kukosa ada, niliishia mwaka wa pili na vigezo vyenu ni mtu mwenye shahada, nimeomba ila sikuitwa kwa ajili ya interview, nimeamua kuja kuongea na wewe boss, na naona kwa sababu ni kijana mwenzangu utanifikiria maana unajua hali halisi ya maisha mtaani" alijieleza kwa kina halafu akajikuna kwenye nywele zake zilizosukwa siku moja kabla
"Sir" alimuita na Jonas aliinua macho akamtazama binti akasema "Niko tayari kwa chochote ili mradi tu nipate kazi" alisema binti
"Tayari kivipi? Hujakizi vigezo tazama hapo nje kuna watu zaidi ya 80 unanipotezea muda kumbuka wanahitajika watu 8 tu kwa ajili ya masoko"
"Boss please" alisema binti na kuinuka akamshika kidogo mkononi "Ntakupa chochote unachokitaka ili tu unipe kazi hapa kwako, nitafanya kwa utiifu na pia hicho utakachokitaka nitazidi kukupa hata baada ya kupata kazi hapa" alisema mtoto wa kike kisha akageuka na kumuonyesha sehemu za nyuma zilizojaziana mifuko miwili mikubwa yaani wowowo halafu akaanza kutembea kwa madaha
Jonas alikuwa mwenye tamaa nzito
"Usiondoke, acha namba hata kama sio hapa kwenye kazi nina uwezo mkubwa wa kukusaidia kimaisha...." alisema
"Woow asante" Erica aliongea na kurudi nyuma akamuambia "Andika"
Jonas alishika kalamu na karatasi akaanza kuchora namba ambayo mtoto huyo aliitaja, kisha Erica aliondoka
"Naaam.....nitaanza na huyu" alisema Jonas kwa tabasamu na kuiweka karatasi ile katika mfuko wa shati "NEXT" alisema....ITAENDELEA
Naaaam, simulizi hii muendelezo unapatikana kwa sh 1000 ya kitanzania
Namba ya malipo na WhatsApp ni Airtel Money 0781858056 jina la mpokeaji ni Anjela
Ukishalipa nipe taarifa WhatsApp.