Alimsogelea karibu Zaidi lakini kelvin hakuonekana kuwa na uoga wa aina yoyote ile Zaidi Zaidi anamtazama tu na kujisemea “ huyu kajuaje hili?
Lakini kabla hajazama kabisa kwenye mawazo mengi.rashidi alimwambia mtu aliyekuwa kasubiri mlangoni
“we dogo ingia fanya haraka “ Kelvi alishtuka baada ya kuona mtu anayeingia ni Bosco AKA kipikipiki posta tayari kadakwa na anavomjua Rashid ni mwalimu ambaye anapiga bakora kama kaajiliwa kwa kazi hiyo.
Akajua hapa tayari dogo kasema kila kitu kisha Rahidi kumrusha roho kelvin alimwambia dogo aende bila kumuuliza chochote hali iliyosababisha naswali mengi sana kichwani kwa kelvin .
Naye alimsogelea Zaidi na kumuuliza “nini sababu ya kumleta dogo na kumruhusu aondoke bila kujua nini dhamira ya kumuita ?
“hapana kelvin unajua kwa nini nimemuita ,unajua kwanini yupo hapa ,unajua kivipi ana husiana na wewe hivyo sikuwa na haja ya kumhoji chochote kile kwa sababu ameijibu vyote ndani ya ofisi ya nidhamu.
Aliendelea”na kawaida ya mimi huwa sipendi kuuliza kitu mata mbilli ni mara moja tu na wanafunzi wananielewa ndo maana wananiita WAKILI.
Kama aliyosema dogo ni ukweli hebu jaribu kukaa mbali na wanafunzi wangu utarudi kijijini kwenu ukalime .kisha Rashidi akaondoka akijuwa tayari kichwanu kwa kelvin kuna maswali mengi sana
Alikuwa akipiga hatua kelekea ofisini lakini moyoni mwa kelvin kutakuwa na vita kubwa yaani anajua kuwa kwa sasa in muda sahihi wa kupigania penzi la Nasra .
Kweli kama alivyohisi kelvin moyoni alikua na mawazo sana ukichukulia ndo kazi pekee anayodhani itasaidia kuboresha Maisha ya mama yake nay a kwake pia .Sasa ikija kesi kwamba ana mahusiano na mwanafunzi ana uhakika kazi atakuwa hana Tena.
Upande wa nasra anajua kabisa kwa majibu aliyonpa Rashid na anavyomjua Rashid hawezi kumuacha salama lazima ana mpango maalumu na alivyomuona kule jikoni nan je akamkuta yule dogo kipikipiki posta wa penzi lao .
Akajua tayari kumekucha dili limeshambumburuka yaani limeharibika .hajakaa sawa akaja yule yule yaani bosco
“nwalimu rashid anakuita ofisini”alisema bosco alionekana ni mtu aliyechoka hii ilitosha kudhihilisha kuwa huko ofisi ya nidham moto umewaka
“sawa naenda” aliinuka na kufunika daftari la biology alilokuwa anasoma kiguu na njia mpaka ofisini lakini mapigp ya moyo yanakimbia kijasho kwa mbali…
Aliingia ofisini kama kawaida na kukaa kwenye kiti .”nimeitikia wito wako mwalimu”
“anhaa vizuri sana Nasra mpenzi wangu”
“weeeh tena ukome mshenzi wa tabia “
“yaani unaiitaje we mtoto”
“nimesema mshenzi wa tabia “
“oooh hahah!! Kweli mtoto umeota mapembe”
“mi naondoka naona huna jipya”
“ amha sawa nenda lakini anayekupa jeuri nimempa” . nasra alisita maana alikuwa tayari ana piga hatua kutoka nje …….
“ah! Mbona umesita? Unaogopa kama mkuu wa shule akijua una mahusiano na kijana mpishi ,handsome boy Kelvin na hututaki watu wenye vitambi watu wenye hela sawa mi ndo nataka nikamwambie mkuu wa shule kila kitu.
“mwalimu yule mpishi sina mahusiano naye”
“utajua hujuwi mi ndo naipeleka kesi huko”
“mwalimu usifanye hivyo”
“nifanyaje sasa?”
“acha hilo lipite usije msababisha kijana wa watu kufukuzwa kazi kwa wivu na tamaa zako”
“tamaa sio haya toka ofisini mjinga wewe”
“mwalimu jamani”
“mwalimu ? kafanyaje”
Nasra alimvuta mwalimu Rashid na kumpiga dend.. huku machozi yakimtoka mwalimu Rashid alitulia……… lakini muda huo kelvin naye aliingia ofisini humo humo na kulishudia hilo jambo alishtuka ……….
FULL1500
0699286085.