ENDELEA.......
"Ondoa hii sahani..." Sabrina aliongea.
Anjeli alinyoosha mikono yake akachukua sahanj, sijui ni nini kilimpata lakini mikono yake ilimsaliti sahani ikadondoka chini.
"Sa...sa... samahani!" Aliongea akiwa anatetemeka.
"Kama samahani yako inaweza kuirudishia uhai hiyo sahani umesamehewa, tofauti na hapo naomba uondoke" Sabrina aliongea akiwa kashikiria moyo wake.
Victor aliwahi kumnyanyua akampeleka chumbani kwake.
Mshtuko alioupata ulikuwa ni mkubwa sana kiasi kwamba alishindwa kula.
"Ondoka nitavitoa hivyo vipande vya sahani..." Hilda aliongea baada kuona Anjeli ana churuzika damu.
Anjeli alielekea chumbani kwake akiwa mwenye hofu kubwa.
Alishindwa kuelewa kwanini Osman yupo hapa.
Ila baada ya kuitafakari vizuri sura ya Sabrina, aligundua watu hawa wana uhusiano wa damu.
Usiku wake ulikuwa mgumu sana, alipoteza kujiamini hasa akifikiria ajali ya moyo aliyomsababishia Sabrina.
"Vipi kama atakufa!...." Anjeli aliwaza mbali.
Hakuwa tayari kupandishwa kizimbani kwa kosa la mauaji.
Akili ya kutoroka ilimuijia, baada ya kuhakikisha nyumba yote imepoa. Alifungua dirisha akaanza kupambana kujipenyeza mpaka akafanikiwa.
Alianza kutembea kwa kunyata, lakini ghafla alihisi kuna mtu nyuma yake.
"Unaenda wapi usiku huu..." Osman aliongea.
"Naomba unisaidie kuondoka hapa, nyota yangu na yako haziendani endapo tutakaa kwenye eneo moja hivi nahofia kusema nitakuwa ni mtu wa mikosi tu" Anjeli aliongea.
"Naelewa umezoea kutembea na Wanaume wa kila rangi, ni ngumu kwako kuishi kama Mfanyakazi mahali hapa....kuliko utoroke subiria kupambazuke uondoke kwa kuaga" Osman aliongea huku macho yake yakiwa kwenye lips za Anjeli.
Anjeli anashindwa kuelewa ni kitu gani huyu mtu anashangaa, aligeuka nyuma lakini hakukuwa na kitu
"Una lips nzuri sana, kwanini usizitumie kuonja sukari au chumvi huko jikoni na si kubadilishana mate na kila Mwanaume anayekuja kwako!" Osman alishauri.
"Una zungumza vitu gani wewe Mpuuzi! hivi hujui ile sahani imepasuka kwa sababu yako!...wewe ni mtu wa mikosi sana ni vile hujijui tu" Anjeli aliongea.
"Rudi ndani ukalale, huwezi kupita hapo getini pengine kama utampa Mlinzi Lushwa ya ngono lakini kwa jinsi navyomjua atakutumia kisha atakurudisha ndani..." Osman aliongea.
Anjeli alibakia kukodoa macho asijue ni kitu gani aseme, baada ya akili yake kufikiria vizuri alimshika mkono Osman akiwa katika sura ya kipole
"Naomba unisaidie kuniombea msamaha kwa Sabrina....tafadhali sana" Anjeli aliongea.
Mkono wake ulikuwa unampa raha fulani hivi Osman...mwili wake wote ulianza kusisimka.... maumbile yake yalianza kufurukuta kisa na maana kashikwa tu mkono.
Taratibu alianza kuusogeza mdomo wake ambusu Anjeli, ubongo wake haukuwa ukifanya kazi hata kidogo zaidi ya kufikiria ngono.
Hakuwaza kama yupo eneo la hatari, Anjeli aliachia sonyo baada ya kuyasoma mawazo ya Osman.
Alimuachia mkono kisha akarudi ndani.
Wakati yote haya yanaendelea Hilda alikuwa juu ya kibaraza akiwatazama.
Hakutarajia kama Mume wake ni mshenzi kiasi hiki.
Alirudi chumbani kwake akiwa mwenye hasira.
"Sahani haikuvunjika bahati mbaya, wawili hawa watakuwa wana fahamiana" Alijisemea kisha akakaa kwenye kiti akaanza kusoma kitabu.
Osman anashtuka baada ya kumkuta mkewe amekaa.
"Nilitoka nje kuzungumza na Victor, siku ya kesho nitakuwa na ratiba ngumu sana" Osman aliongea huku akijitahidi kuficha umbile lake lililosimama sababu ya kushikwa tu mkono na Anjeli.
Hilda aliachia tabasamu kisha akaendelea kusoma kitabu.
Asubuhi na mapema sana Asha anafika nyumbani kwa Sabrina Kutoka Dodoma.
Alitembea kwa haraka sababu alikuwa na shauku ya kumuona Osman.
"Sitaki kuamini mpaka sasa hivi kalala!...kuna muda sielewi kazi ya Victor ni nini" Asha alijisemea huku akiangalia saa yake.
Alipitiliza ndani bila kuvua viatu vyake, Anjeli anasikia hasira baada ya kuona tope na wakati amemaliza kudeki.
Kwa hasira alianza kudeki huku akimtukana mtu aliyemrudisha nyuma.
Wakati anamalizia kudeki alishtukia akigeuzwa kwa nguvu.
Macho yake na ya Asha yalikutana,
Anjeli hakuwa akimfahamu Asha hivyo alijikuta akimkodolea tu macho.
"Zimesalia dakika 20 kikao kianze, nenda kawashe gari..." Sauti ya Osman ilisikika akiwa na Victor.
Asha aliondoka, kwa mara nyingine aliacha tope tena
"Ondokeni nirudie kudekiiiii!" Alijikuta akizungumza kwa jazba, sauti yake ilitapakaa nyumba yote kiasi cha Sabrina kushtuka usingizini.......ITAENDELEA.........
SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA
*__________________________________*
SEHEMU 07
ENDELEA.......
"Una mpazia sauti CEO wa Kampuni ya DreamCloud au unanipazia Mimi!" Victor aliuliza.
"CEO ndio ana kibali cha kuchafua mazingira kwenye hii dunia!.... fanyeni kunipisha tu" Anjeli aliongea.
"Tuondoke!" Osman aliondoka, si mtu wa kupenda kelele.
Victor alianza kulalamika lakini jicho moja la Osman lilimtuliza.
Asha aliondoa gari, ndipo anashtuka kama viatu vyake vinatope.
Aliamua kukausha, kwa sababu kama angekiri kuwa yeye ndio kachafua nyumba basi Victor angezungumza mpaka kesho asubuhi.
Siku zote huwa wanashindana kuonekana bora kwa Osman.
Upande wa Sabrina anatoka chumbani kwake akiwa na nguvu mpya, hakuwa akikumbuka kuhusu tukio la jana.
"Nitafurahi kama Wageni wa hii nyumba watashindwa kutofautisha kati ya Mfanyakazi na Boss, naomba baada ya kumaliza kazi zako uende saluni....kadiri utakavyo onekana kuwa na muonekano mbaya kwangu ndivyo nitazidi kupunguza mshahara wako" Sabrina aliongea.
"Sawa... nitajitahidi kupendeza" Anjeli aliongea kisha akatoka nje kumwagilia maua.
"Baada ya kumaliza kumwagilia maua naomba unisaidie kufua hizi nguo, tafadhali sana naomba nguo zangu zisifuliwe na mashine" Hilda aliongea kisha akaweka kapu la nguo chini.
Anjeli alimwagilia maua chapu chapu, baada ya kumaliza alichukua nguo afue.
"Nguo zote za hii nyumba hufuliwa kwenye mashine, ni marufuku Mfanyakazi wa ndani kutumia mikono yake kufua pengine kama ni adhabu, peleka hizo nguo kwenye mashine" Sabrina aliongea baada ya kumfuma Anjeli akifua.
"Lakini Hilda kasema nguo zake huwa hazifuliwi kwenye mashine...." Anjeli aliongea.
"Ziache hapo atafua mwenyewe....jiandae tunaenda saluni" Sabrina aliongea kisha akarudi ndani.
Baada ya Anjeli kumaliza kazi yake aliondoka na Sabrina.
Hilda anashangaa kuona nguo zake zipo chini.
Aliachia tabasamu baada ya kuelewa kwanini ziko hapa. Aliziweka kwenye mashine akaanza kufua.
Upande wa Anjeli akiwa saluni alipendeza sana, Sabrina aliachia tabasamu baada ya kuona Mfanyakazi wake kawa katika muonekano mzuri.
"Twende ofisini kwa Osman nahitaji upafahamu, kuna muda huwa napenda Kijana wangu ale chakula changu ni jukumu la Mfanyakazi kumpelekea chakula" Sabrina aliongea.
Anjeli alitaka kusema analifahamu Kampuni la Osman lilipo lakini alijizuia.
Wafanyakazi wote walikuwa wanamtazama Anjeli kwa namna alivyopendeza, Sabrina alizidi kutabasamu.
Osman akiwa ofisini na Asha alishangazwa na ujio wa Mama yake, hakuwa akimtambua Anjeli kutokana na alivyopendeza.
"Nimemleta Anjeli hapa alifahamu eneo lako la kazi....Asha naomba umtembeze kila sehemu" Sabrina aliongea.
Asha aliongoza njia akiwa haelewi maana ya yote haya.
Machoni kwa watu Anjeli alionekana kama boss na Asha kama Kijakazi.
Alimpeleka mputa mputa kiasi kwamba Anjeli alitoka jasho.
"Hili ndio eneo lote la Kampuni ya DreamCloud....naikumbuka vizuri sana sura yako, naomba kujua kwanini ile siku ulikuwa unapiga mnada nguo za Osman" Asha aliuliza.
"Ni vyema kama utamuuliza Boss wako kwanini nguo zake zilikuwa zinauzwa..." Anjeli aliongea.
Asha aliachia tabasamu kimtindo baada ya kugundua binti huyu ni jeuri.
Alimtazama vizuri macho yake aliweza kuziona chembe chembe za udada poa, alivuka mpaka kwa kumvutia tisheti yako.
Tattoo ya nyota ndogo ilionekana kifuani kwake.
"Bila shaka ulikuwa ni Dada poa wa usiku mmoja kwa Osman.." Asha aliongea kisha akamtengenezea tisheti yake.
Anjeli si mtu wa kupenda vurugu, mara nyingi hujitahidi kuwa mlokole hasa majira ya mchana.
Alimshukuru Asha kwa kumuonesha mazingira kisha akaondoka.
"Kwanini Sabrina karuhusu msichana mzuri kama huyu kuwa Mfanyakazi katika nyumba yake!" Asha alijiuliza asipate majibu.
Anjeli anaingia ofisini kwa Osman kwa mara nyingine tena.
"Nadhani umeoneshwa kila mahali tunaweza kuondoka sasa...." Sabrina aliongea.
Anjeli alitikisa kichwa kuashiria ndiyo, macho yake na ya Osman yaligongana kuna namna walikosa hewa.
Sabrina hakuelewa kwanini wawili hawa wana babaika.....alimtaka Anjeli waondoke.
"Muache kuna mzigo upo supermarket nitaenda kuuchukua kisha atakuletea" Osman alijikuta akiongea.
"Sure!.." Sabrina aliongea kisha akaondoka.
Osman alijikuta akisimama baada ya kuhakiki mlango umefungwa, tamaa ya kumbusu Anjeli hata kidogo tu ilikuwa juu sana.......ITAENDELEA........
Kwa sh 1000 unamaliza mpaka mwisho wa simulizi hii
Njoo WhatsApp 0781858056.