Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MTEULE WA KUZIMU SEHEMU YA 8

31st Jul, 2025 Views 2


msaidizi wake alimuuliza 'dokta vipi mbona kama umezubaa??,. Kuna dawa tumeisahau, hebu nenda famacy uilete haraka, sasa alibaki peke yake akaona ni muda pekee wa kuikata kiu yake, lakini kabla hajaanza kutimiza azma yake, mlango wa theatre ulifunguliwa. Mery alisonya kwa ghadhabu "aaaa shiit ".mery nini tena 'mganga mkuu aliuliza,, ' hapana bosi, kuna mtu nimemwagiza dawa sasa naona anachelewa ukizingatia mgonjwa tumeshampasua, hiyo dawa umemwagiza wapi?, chumba cha dawa mkuu. Kwa nini uanze upasuaji kabla hujakamilisha vifaa vyote, yule kijana aliingia akishika dawa mkononi, Mery alichukia kweli kwa mpango wake kutibuliwa. Mganga mkuu akamwambia " nilikua na shida ya kuongea na wewe, nikaambiwa upo huku, nimekusubiri nami nataka nitoke nimeamua nikufate tu, hebu malizia kumshona tuongee kidogo. Mchungaji aliekua akimuombea yule mgonjwa hakupendezwa kwa tukio alilofanyiwa na dokta Merry aliona kama amedhalilishwa, ikizingatia ndio kwanza kanisa lake jipya hivyo alikua katika harakati za kutafuta waumini, aliamini kabisa kupona kwa yule mgonjwa ingemjengea sifa kubwa, akasema huyu dada hanijui ngoja nikamtafute huko huko, hapa kila mtu ana njia yake ya kutafuta maisha .Dokta Merry alipokamilisha alimuamuru mgonjwa arudishwe wodini, walipotoka walikutana na ndugu wa mgonjwa, akawauliza mgonjwa wangu anaendeleaje dokta??, yuko vizuri usihofu, sasa hivi watamtoa kumpeleka wodini,, " asante sana dokta sijui nikupe nini,, "ni uwajibu wangu au wetu kuokoa maisha ya watu. Mganga mkuu alimgeukia mery ' katika hospitali yangu ningekua na madokta kumi Kama wewe ningefurahi sana. Hahaaa kwa nini bosi??. Unajitaidi sana kuokoa maisha ya watu hii itapelekea hospitali yetu ipate sifa nyingi siku za usoni ,.unajua bosi mtu lazima uipende kazi yako. Hata mi naona ivi kuna mgonjwa alikua mahtuti kiasi kwamba nikampa rufaa, nasikia ukazuia asihamishwe " ndio mkuu ",na ukamtibia kwa sasa anaendelea vizuri " mery alitingisha kichwa ",hongera sana inaonesha ulikua makini sana darasani. Hapana mkuu basi tu. Walifika eneo ambalo dokta Pita aliegesha gari yake alipanda na kuondoka pale hospitali, Mery alirudi wodini kumuangalia mgonjwa wake kama ameshazinduka, alimkuta kweli amezinduka ameshaekewa dripu mkononi, akaona ni muda muafaka sasa wa kurudi nyumbani kupumzika, alitoka nje kuifata gari yake, kabla hajafungua mlango ,alishikwa bega ,kugeuka alimuona mtu ambae hakua na kumbukumbu nae, nikusaidie nini??, akaambiwa naona umenisahau, kweli nimeamini mla ndizi husahau bali mtupiwa maganda ndie hukumbuka. We kaka vip?.siyo vipi naomba unisikilize tena kwa umakini ,mambo ya kuharibiana mi siyapendi, dokta Merry alikunja mikono kifuani akaegemea gari yake alimtazama juu hadi chini akawa ameshamkumbuka alitulia kimya kumsikiliza. We unaringia utaalamu wako hata mimi ni mtaalamu tena kukuzidi, sasa naomba tusiingiliane,siku nyingine usirudie we mwanamke, unatibu kwa sindano mi ninatibu kwa jina la yesu, acha kupambana na mwanaume. Dokta Mery alimtazama kisha akafungua mlango wa gari lake akaingia ndani akimshuhudia akiishia zake .Mchungaji alipofika kwake uku akisema nimemkomesha, siku nyingine hatorudia tena, wagonjwa awasubiri hospitali, alipofungua mlango alishikwa na butwaa kumuona Mery akiwa ametulia kwenye kochi, akiwa kwenye hali ya mshangao 'akaambiwa kalibu,.akauliza we umeingiaje??, akajibiwa kwa swali kwani na wewe umeingiaje ,.mlango ukajifunga pasi na kufungwa, mchungaji alipogeuka kutazama nani ameufunga mlango na kumkosa ikabidi amtazame tena Mery 'ajabu hakumuona ' ,haa huyu ni jini au mchawi, sauti ikajirudia tena ",huyu ni jini au mchawi ",kijasho kikaanza kumtoka pale pale akaanza kukemea, shindwa kwa jina la yesu. Mery akajitokeza tena mbele yake, mchungaji alishtuka hadi kuanguka chini. Unaogopa nini?, we si mwanaume, uliejipanga kuja kunikabili,. Hhapana we dada utakua mchawi nasema shindwa kwa jina la yesu.Mery alicheka akatoa muungurumo Kama radi, palepale alianza kubadilika kua wa blue pamoja na macho yake kuwa Kama ya paka ,mchungaji akajihisi kujikojolea, alishindwa kufanya chochote mwili wake haukua na nguvu hata ya kusukuma karatasi,Mery alipanua mdomo ,meno yake marefu kama simba yaliyonekana vyema machoni pa mchungaji. Akamwambia unafikiri Yesu wako atakuokoa wewe unaezulumu sadaka za watu, umefanya kosa sana kuja kunitukana, nasikita hutaliona jua tena, alimkamata shingo na kuipeleka mdomoni mwake, meno makali yalipenya kwenye shingo ya mchungaji, alifyonza damu mpaka ikaisha, ndipo alimwachia, alianguka Kama jiwe chini, bado Dokta Mery hasira zimempanda, alianza kuurarua ule mwili, kisha akatoweka nao pale hadi kwake, akamkata uume wake akauweka pembeni. Baada ya hapo alirudi kwenye umbo lake la kawaida,.kesho asubuhi watu walikua wakishangaa mwili uliokua umetupwa pembezoni mwa barabara, kila mtu alisema lake wengi wakiamini alikua mlevi alitafunwa na mbwa kutokana na mashimo ya meno yaliyoonekana shingoni. Dokta mery alimwambia Tina Leo usiku nitakupigia simu kuna sehemu nataka unipeleke,. Wapi tena??, utajua tu muda ukifika. Kwa nini tusiende mchana Mery?. aaa, usiku huwa ni mtulivu na ni mzuri kwa safari, tukafanikiwa kwenda na tukarudi utakua Tina mwingine kabisa, mwenye jina kubwa na uwezo wa hali ya juu katika mambo mbalimbali, Tina aliguna mhhhh

SEHEM YA TISA
nesi Tina aliguna mmhh""akajiuliza hiyo safari ya usiku wanakwenda wapi, Tina toka yuko shule ya msingi alipenda sana mambo ya uongozi,kusikilizwa,kuheshimiwa,ni vitu alivyokuwa anavipenda, hakupenda kupangiwa bali alipenda apange. Hivyo pale hospitali mambo ya kuamrishwa, kupangiwa alivichukia sana ila kutokana na elimu yake ndogo na maisha ya kwao yalivyo ilibidi awe mtiifu tu. Sasa alivyoambiwa na Merry kwamba wakirudi kwenye hiyo Safari atakua mtu tofauti ,ilimgusa Kwan siku zote alitamani awe hivyo. Usiku ulipofika aliisubiria simu ya Mery mpaka akachoka mwishoe usingizi ukampitia, alikuja kushtuka usiku sana baada ya mkojo kumbana lakini kabla hajatoka kitandani aliona mwanga mkali chumbani kwake, woga ukamshika mala Mery akatokea, hapo alizidi kuogopa, Mery alicheka ',bado unaniogopa?, hujanizoea tu Tina, usiniogope bwana we ushakua rafiki yangu, haya jiandae tuondoke.Mbona usiku sana Mery tusubiri basi hata kupambazuke kidogo,. Mery akamwambia hebu nipe mkono wako kwanza, alipompa tu Tina alishtukia wapo pembezoni mwa bahari, macho yalimtoka kwa muujiza ule. Usihofu Tina, hapa ndio tunapoianza safari yetu, akianza kukanyaga maji akimwashiria Tina amfate ambae muda huo bado alikua amesimama pembezoni mwa maji. Twende we mbona bado umesimama tu,, "hapana Mery mi siwezi kuogelea nitazama na kufa. Kwa hiyo nisikuue siku zote nikuue Leo, kuwa na amani Tina yakanyage hayo maji tunachelewa. Alipoyagusa tu maji akajiona yuko barabarani wakiwa na dokta Merry,. Ulikua unaogopa nini? huna haja ya kushangaa tena, unatakiwa kuzoea mazingira tulipo si duniani. Tuko wapi kwani?. Huku kunaitwa kuzimu. Kuzimuuuu!!!!!!!!,. Ndio Tina hujawahi kusikia Kama kuna kuzimu??,. Nishasikia lakini huku wanakuja watu waliokufa. Hahaaa si kweli Tina mbona wewe uko huku na wala hujafa??, wakiwa bado wanajibizana gari ikawa inakuja, gari lile lilimshangaza kidogo Tina, kwani lilikua linarudi kinyume nyume lilipofika kwao likasimama, akafikiri labda limewarudia wao ,Mery akamwambia naomba uniangalie mimi nitakavyopanda nawe upande hivyo hivyo, baada ya gari kusimama ,Mery aligeuka akapanda kinyume nyume, Tina hakuwa na jinsi nae aligeuka akaingia kinyume ,alipokaa kwenye siti alishangaa kumuona dereva ni yule mzee aliefariki kule hospitali baada ya yeye kusalimiana nae mzee Sixbert. Si alikufa huyu mbona yuko hai na anaendesha gari .akaambiwa Tina huku huruhusiwi kuwaza ya duniani, utawaona wengi ambao kule duniani mnaamini wamekufa, ila hawajafa kikweli huwa wanachukuliwa kuja kufanya kazi mbalimbali. Huwa wanaletwa na nani??. Wanaletwa na watumishi wa kuzimu. Ndio akina nani hao watumishi wa kuzimu. Hahaaa utawajua tu Tina. Gari ilisimama wakashuka kwa mtindo ule wa kinyume nyume na kuanza kutembea hivyo hivyo, Tina alishuhudia miti iliyoota kuanzia juu kuja chini, mizizi ya miti ikielea tu angani hata nyumba zao zilijengwa kuanzia juu kuja chini, msingi ulikua hewani paa inaangalia chini, ina maana zilielea angani. Tina aliguna mhhh kumbe kuna vitu vya ajabu hivi makubwa haya. Waliikuta ngazi wakapanda kuingia ndani wakakuta kuna bonge la disco watu wako bize kucheza "ajabu hata mziki ulianzia mwisho kurudi mwanzo ",ni miziki ile ile ya duniani. Tina twende tukacheze basi. Miziki haieleweki siwezi kuicheza .Mery akamwambia utaizoea tu ngoja mi niende nikacheze maana nimelimisi sana disco la huku ,mery akaingia kucheza aliselebuka haswaa, Tina aliwashangaa kuwaona wakifurahia mziki usioeleweka, unaoanzia mwisho kwenda mwanzo, baada ya kucheza kidogo alitoka akamfata Tina. Nifate huku roho yangu sasa imesuuzika nililimis kweli disco letu, alimpitisha sehemu mbalimbali lengo lake ni kumpunguzia presha ya kuzimu, waliwakuta watu wakicheza karata mpira na baadhi yao Tina aliwafahamu kabisa wengine mazishi yao alihudhuria ila kule bado wako hai, alimpeleka sehemu ambako alikuta vyakula vingi kama kuku chipsi mayai, pilau, nyama ya mbuzi. Tina alikua mloo kweli wa nyama za kuku na chips alizifakamia kweli, mery alibaki kumtazama akatabasamu " ngoja nimweke sawa akili zake zitulie. Mery njoo tule mbona unashangaa. We kula Tina vyakula vya duniani. Kuzimu kuna vyakula vingine tofauti na vya duniani,. Vipi hivyo??. tulia utavifahamu si ndo umefika, huku kila kitu ni tofauti na duniani, nafikiri umeona tunavyotembea,lile gari, mziki .baada ya kutoka pale waliingia kwenye ukumbi mkubwa uliokua na vitambaa vyekunde, viungo vya binadamu ndio mapambo ya ukumbini. Tina akaanza kutetemeka
ITAENDELEA
FULL 1000
0699286085.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MTEULE WA KUZIMU SEHEMU YA 8  >>> https://gonga94.com/semajambo/mteule-wa-kuzimu-sehemu-ya-8
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest