Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Aliniuliza je kama pesa zimepotea ni nani wa kulaumiwa... Inaendelea... Sehemu Ya 11

31st Jul, 2025 Views 7



Mh nilianza kujiuliza hadithi yake ina maana gani Lakini wakati natafakari, Gari la yule mzee lilikuwa tayari limesha kamilika kufanyiwa usafi, Yule mzee alinyanyuka na kuniambia usifikirie sana kuhusu jibu la swali langu lakini siku gari yangu imechafuka nitaileta kuja kuosha hapa sababu naona vijana wako wapo haraka sana. Yule mzee akawa ameondoka, lakini nilikuwa najiuliza kwani huyu mzee ni nani au ndio mume wa sakina, Sababu hadi wakati huo nilikuwa bado sielewi kama sakina ameolewa au hajaolewa,

Badae nikapata muda wa kukutana na sakina, Nikamueleza kwamba kuna mzee alikuja kazini kwangu lakini sikumuelewa maana alianza kunisimulia hadithi za mafumbo, Sakina akaniambia inawezekana huyo mzee alikuja kwa ajili ya kuchunguza jambo au kufanya upelelezi maana haiwezekani mtu akusimulie hadithi za mafumbo harafu aishie kukusimulia,hapo kuna kitu hakipo sawa.

Mwanamama sakina akaniambia inabidi niache kuwa naenda kulala kwenye ile nyumba ya kifahari ambayo alininunulia yaani niache kila kitu nirudi kwenye maisha yangu ya kawaida, Ili yeye afanye uchunguzi sababu alianza kuhisi kuna watu wanatufuatilia, Nilimuuliza kwa nini na yule mzee ni nani, Akasema utaelewa wakati ukifika,lakini kwa sasa fanya kama nilivyokuagiza ila kazi ya kuendesha makampuni yangu itabaki palepale utakuwa unaniandikia latiba harafu mimi nitakuwa nasimamia kama msaidizi. Kwakuwa makampuni yake yote yanatumia jina langu nikaona hakuna shida, Lakini ukumbuke jina la Sadiki sio jina langu bali nilipewa na sakina, Na ndio jina ambalo linatumika kwenye kuendesha makampuni. Kiukweli nilikuwa sielewi kwa nini sakina alinipa jina la Sadiki.

Baada ya kutokuelewana kidogo na sakina ilibidi nikubali nikawa nimerudi kwenye ile nyumba ambayo nilikuwa naishi mwanzo, Nikaendelea kufanya kazi ya kuosha magari nikiwa na vijana wangu wa kazi lakini pia nilikuwa nikiandika mipangilio ya hisa kwenye biashara za sakina,

Nilipoona mwanamama sakina kama vile haeleweki ikabidi nifanye mpango wa kumuibia pesa, Nikafanikiwa kuchakachua pesa kutoka kwenye makampuni ya sakina, Kisha nikaenda kununua nyumba pembezoni mwa mji, Nikanunua nyumba yangu na nikaiandikisha kwa jina langu kamili David Ntai; ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu na niliinunua kwa siri wala sakina hakujuwa kama kuna nyumba nimenunua kwa siri, Ile nyumba nilipoinunua nikaiacha vilevile bila mtu. Maana niliona sakina kama ameanza kutokueleweka bas anaweza akanibadirikia hapo mbeleni,

Wakati huo mahusiano mimi na tina yalikuwa bado yanaendelea na tina alikuwa hataki kuniita jina la Sadiki wakati wote tina alikuwa akiniita David sababu alisema hilo ndio jina ambalo amezoea kuniita toka tukiwa kijijini, Lakini pia tina alianza kuniuliza kuhusu kazi ninayofanya nje na kuosha magari sababu kwa pesa nilizokuwa nazo kwa mtu anayeosha magari pekee hawezi kuwa nazo, Tina alikuwa anahisi labda nauza madawa ya kulevya, Ilibidi nimwambie ukweli ili kumtoa wasiwasi nilimwambia ukweli kwamba tofauti na kuosha magari huwa natengeneza program za biashara kwenye makampuni na wananilipa pesa, Nilimueleza namna ninavyofanya hadi kupata pesa nyingi kiasi kile, Kiufupi ndani ya muda mfupi pale mjini nilikuwa kijana mwenye pesa nyingi sana ingawa nipo nyuma ya mtu,

Lakini hadi wakati huo tina nilikuwa sijawahi kumpeleka ninapoishi. Baada ya siku chache toka nihamie kwenye ile nyumba ya zamani, Tina akawa amenipigia simu na kuniambia muda wowote anaweza akaja kwangu na hataki kufikia guest,

Lakini toka nimerudi kwenye maisha yangu ya kawaida tukawa hatuonani kabisa na sakina, Mwanamama sakina akawa anatuma mtu kuijia zile documents za biashara, Nikaanza kuhisi kama vile sakina anataka kunitenga.

Siku ya tina kuja kwangu kunitembelea ikawa imefika, Tina alinipigia simu na kuniambia nimeshatoka chuo niijie nipo huku mjini, Akawa amenielekeza sehemu aliyopo ikabidi nitoke kwenda kumfuata, Kwakuwa wakati huo sakina alikuwa hafiki pale nilipopanga nikaona nimfuate tina nimlete hadi pale kwangu angalau anifariji maana nilikuwa mpweke sana,

Nilitoka nyumbani na kuchukuwa usafiri hadi pale tina aliponielekeza,lakini nilimkuta tina akiwa anamalizia kuagana na mwanafunzi mwenzake wa kiume, (wivu ni sehemu ya mapenzi). Nilifika na kumuuliza yule ni nani? Lakini wakati naendelea kuongea na tina ilifika gari nyeusi aina ya Noah kabla haijasimama walishuka watu watatu na kunikamata,walinichomolea simu yangu mfukoni na kuitupa chini,wakati nauliza kwani kuna nini,tayari nimeshatupwa ndari ya gari na kufungwa kitambaa cheusi kichwani huku mikono yangu inafungwa na kamba, Niliisikia sauti ya tina kwa mara ya mwisho akiita... David,,,David

Wakati tunasumbuana ndani ya gari nilichomwa sindano na kupoteza fahamu, Nilikuja kuzinduka nipo kwenye chumba ambacho kina giza mfano wa mtu aliyefumba macho, Nilikaa kwenye kile chumba siku mbili bila kula wala maji ya kunywa, Siku ya tatu nikiwa nimekata tamaa ya kuishi na kuamini nitafia kwenye kile chumba. Nilisikia sauti ya mtu kama namfahamu, Yule mtu alifika na kusema washeni taa (taa ikawashwa) lakini yeye alijificha kwenye giza, Baada ya taa kuwaka kwa mwanga wa kufifia, Yule mtu akasema mpatieni chakula ikabidi nipewe chai ya moto sababu nimelala siku mbili bila kula na nilikuwa naelekea kuimaliza siku ya tatu,

Nilipomaliza kula kidogo hali yangu ikawa sawa, Yule aliyekuwa anaongea akiwa gizani alijitokeza kwenye mwanga nilipomuangalia vizuri alikuwa ni...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Aliniuliza je kama pesa zimepotea ni nani wa kulaumiwa... Inaendelea... Sehemu Ya 11  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-aliniuliza-je-kama-pesa-zimepotea-ni-nani-wa-kulaumiwa-inaendelea-seh
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest