Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

JAMANI BOSS MI NAONA AIBU πŸ’πŸ™ˆπŸ’ž 1- 5 🚩🚩🚩🚩🚩

31st Jul, 2025 Views 82




Maisha muda mwingine ukisema uyaelezee kwa ukubwa unajikuta hata hujui wapi unaanzia na wapi unamalizia.

Kwasababu wengine maisha yametupitisha sehemu ambazo hata unajiuliza hapa nimepita vipi. Unajiuliza imekuaje nimevuka hapa. Na hivyo hivyo ndivyo mimi Ndeana ninashindwa kufunguka na kuelezea zaidi. Ila kwakuwa ninatamani wanawake wajifinze kutoka kwangu. Nitasema ingawa sijui nitasema mangapi maana ni Mengi sana, naahidi nitapita hatua kwa hatua. Kituo kwa kituo mpaka pale nitakapoona kuna watu wananielewa mimi kwa uzuri kabisa.

Ndotp ya kila mtu ina gharamiwa, unaweza kugharamia ndoto yako kwa muda, pesa na utu wako uamuzi ni wako. Kwa maana ndoto si ile unayoota ukilala, bali ni ile inayokunyima usingizi, ndoto ni ile inakufanya unyong’onyee na kukukosesha raha mpaka itimie. Hivyo ndiyo ilivyo kuwa. Mimi Ndeana nilikuwa ninayo ndoto katika maisha yangu. Ndoto yangu ilikuwa ni kufanikiwa sana katika kazi yangu ambayo nimesomea.

Mimi nimesomea mambo haya ya kuhudumu mahotelini. Nishafanya kazi sehemu nyingi nyingi sana. Matatizo ni mengi mno kama kuoneana wivu, mshahara mdogo, kunyanyasana na mambo mengine mengi mengineyo hali inayopelekea kufukuzana kazi au wewe mwenyewe kuacha kazi.

Jina langi mimi ninaitwa Ndeana. Jina sio rahisi kusikika mara nyingi. Najua, ila nalipenda sana jina langu. Ni jina pekee ambalo huwa nahisi linanifaa peke yangu dunia nzima. Ndiyo kwasababu huwa silisikii sana watu wakiitwa jina hili.

Ninaye dada yangu, pia ninaye baba yangu ambaye huyu ndiye baba na huyu ndiye mama kwetu kwa maana baba yetu alifariki mimi nikiwa bado mdogo. Hivyo kwa nguvu na upendo wa Mungu dada yangu na baba wamepambana kuhakikisha napata kilicho bora katika maisha yangu.

Siku moja, naikumbuka vizuri sana siku hii. Nilikuwa nimetoka kazini kwangu nikiwa na maumivu sana. Kwasababu mimi ni moja kati ya watu ambao corona ilituathiri. Nilisimamishwa kazi wakati huo kwa maana hotel haikuwa inajiweza sana hata kulipa wafanyakazi wote katika kipindi kigumu kama kile.

SEHEMU YA 02

Nilipofika nyumbani kwetu, nilipitiliza ndani. Na dada yangu naye alikuwa nyumbani siku hii ni wazi alitoka kwenye mahangaiko yake. Dada yangu ananijua, namna nilivyokuwa ni wazi kuna kitu hakikuwa sawa hivyo alinifuata chumbani kwangu.

Nilikuwa nimekaa chini nimejiegemeza ukutani nalia sana. Dada yangu aliniita kwa upole sana β€œNdeana mdogo wangu.”
Nilimtazama na machozi yakanitoka nami nikaita β€œdada!!”
Akaniuliza kwa upendo β€œmdogo wangu kuna nini tena unanitisha dada yako?”

Baada ya kuniuliza vile tu mimi nilianza kulia kwa uchungu nikisema β€œsijamaliza hata miezi 6, tayari nimesimamishwa kazi. Kwanini mimi na sio wengine. Ina maana mimi sikidhi mahitaji yao. Dada unajua nilivyohangaika kupata ile kazi. Unajua kabisa. Sasa nitafanyaje mimi.”

Dada alitazama na mimi akaniambia hivi β€œsikia mdogo wangu, hizo ni njia za Mungu. Kwenye maisha yako vitu vinapoondoka tena vingine kwa maumivu makali sana. Na vingine ni kama vile unapasuliwa chupa masikioni mwako ili mradi ukose utilivu.

Usijali kabisa. Unaweza poteza vitu, watu wa karibu na mambo muhimu sana. Unajua kwanini mdogo wangu, Mungu hawezi kushuka kutoka Mbinguni aje kuanza kuongea kama hivi tunavyoongea. Bali yeye humpa mtu kile anatakiwa kupata katika maisha yake.

Mdogo wangu, niamini pale hustahili kuwepo wewe, wewe ni wa majuu, wewe ni zile hotel kubwa kubwa nyota tano. Jitazame kwanza ulivyo kazuri, jitazame ulivyo, ninachokupenda mdogo wangu pamoja na mazingira ya kazi unajitunza sana. Sikia leo pumzika, mwambie Mungu asante, naomba kile ninachostahili kupata.”

Nilimsikiliza dada yangu kwa makini sana. Kisha nikamwambia dada yangu β€œdada wewe unasema tu. Sasa huu uzuri una kazi gani. Ndoto zangu nifanye kazi hotel kubwa hapa Dar. Ila naishia kufanya kazi hotel hazina hata maana na bado nateseka, sasa nitafanyaje mimi dada, ina maana Mungu haoni wengine wa kuwaondoa bali mimi tu.”

Dada akanitazama na kusema β€œsikia, pumzika sasa. Kisha tukiamka kesho anza tena kutuma Cv yako kwenye hayo mahotel unayotaka.”

SEHEMU YA 03
Nikajikuta nacheka nikisema β€œHotel gani jiji hili haina Cv zangu. Kila hotel hapa inanijua mimi japo sio kwa sura ila jina langu, Ndeana lipo. Hapa dada nawaza niende Zanzibar, niende labda Arusha hata sijui yaani.”
Dada akanitazama tu na kutabasamu halafu aliniacha pale chumbani.

Hatukuwa matajiri, hatukuwa maskini wale wa kushindwa kupata chakula ingawa hatukula tunachotaka kila siku ila tulikuwa na maisha yetu nashukuru Mungu. Basi niliinuka pale chini na kusimama dirishani nikajifuta machozi huku nikiwaza nini nifanye. Kiukweli sikuwa na la kufanya zaidi ya kujitupa kitandani.

Mimi sio mweusi sana wala sio mweupe. Nina rangi yangu tu nzuri ya kuwaka sana na kuvutia. Sio mnene sio mwembamba wala sio wale watu wa kati. Nina mwili wangu hivi, yaani ni kama nilikuwa niwe mwembamba ila nina nyamanyama. Ni mrefu, nina mguu mzuri sana wa kuvalia nguo fupi, yaani nina mguu mzuri.

Na ni wale watu wasio na mwili ila wana shepu fulani hivi nzuri sana mpaka huwezi kuelezea. Na kiuno changu chembamba. Yaani ni balaa balaa. Sifa hizi hata mimi mwenyewe nilichoka kuzisikia. Na vile nina macho makubwa malegevu acha tu. Mimi ninajijua kwakweli nina uzuri wangu. Na najipenda sana na najitunza sana.

Muda wa kupata chakula cha usiku dada yangu aliniita nami nilitoka nikiwa nimechoka sana. Nilikutana na baba yangu na aliponiona aliniambia kwa upole β€œNdeana mwanangu, nimesikia kilichotokea. Ila hupaswi kuwa na huzuni kabisa mwanangu. Unajua hili tatizo sio wewe tu limekupata, watu wengi wamesimamishwa kazi tena hata hivyo mimi nashukuru Mungu sasa utakaa nyumbani utulie maana huko Hotelini kila siku kukutana na watu mwisho mwanangu upate hivyo virusi. Tulia nyumbani unipikie maharage baba yako.”

Dada yangu alianza kucheka. Alicheka sana huku akisema β€œyaani baba una mchokoza mdogo wangu, muache ale.”
Nikamtazama dada yangu na kusema β€œdada unacheka, mwambie baba mimi sijasoma upishi, sitaki mimi baba.”
Basi familia yangu ilikuwa pale kunifariji na nikajikuta tu naanza kuzoea maumivu hata nikawa nacheka pamoja nao.

SEHEMU YA 04

Maisha ya kukaa nyumbani bila kazi ni magumu sana. Umeamka upo tu, unakula unachezea simu unalala. Ni magumu sana kwa mtu ambaye umezoea kwenda kazini kisha upate changamoto ukae tu nyumbani. Mateso yake hayaelezeki. Dada yangu yeye alikuwa akienda kwenye mambo yake. Yeye hufanya biashara ya kuuza vitu kama mapazia, mavazi, mashuka na vitu vingine vingi maofisini.

Mimi ndiyo dada wa nyumbani tena. Nilikaa huku nikihangaika kutuma cv yangu huku na kule mpaka mwezi ukatimia mimi nipo tu sina dili lolote. Nilianza kujiona namna nachakaa, nachoka, nabadilika. Kusema ule ukweli wa moyo, kuoga asubuhi kwenda kazini ni raha sana. Ndiyo ni raha mno mimi ni shahidi katika hilo.Nilikuwa nateseka sana kwa kuishi bila kazi na wakati mimi ninatamani sana kufika mbali zaidi kwenye hii kazi yangu kiasi huwa nawaza hata kuwa na mgahawa wa kishua pale nitakapofanikiwa. Ni ndoto bado hazijatimia.

Siku moja jioni, dada yangu alinikuta sebuleni nikihama kochi hili kwenda kochi lile na lile. Aliponiona tu alikuwa amacheka akisema β€œNdeana, Ndeana mdogo wangu niulize kuna nini?”

Nikamtazama na kusema β€œkwani dada huwa unaishiwa uongo haya kuna nini?”
Akaja kukaa karibu yangu na akaniambia β€œnilikuambia mimi, pale hustahili kukaa. Mungu atakupandisha juu juu sana.”

Nikasema kwa upole nikiwa na kimuhemuhe cha kujua β€œdada Vanessa, si uongee sasa kwani kuna nini?”

Akatabasamu na kusema β€œile hotel kubwa unaitamani, unaiwaza na kutamani ukafanye kazi pale ni hotel gani vile.”
Mimi haraka haraka nikataja.

Dada akaniambia β€œkama hujawahi kuomba Mungu mdogo wangu omba sana leo, utapata hiyo hotel, ila sharti ukipata usituache familia yako,”
Nikacheka na kusema β€œfamilia gani sasa na wewe dada. Mimi na nyie mpaka kifo. Na sitaki ngonjera mimi niache nipumzike. β€œ

Dada yangu nakumbuka aliniambia β€œsitanii. Ninaye mteja ambaye ni kama dada kwangu sasa. Anafanya kazi kwenye kampuni kubwa huko posta. Nikamuelezea kuhusu wewe na namna unapambana kupata kazi. Akaniambia anafahamiana na boss wa hiyo Hotel ni mtu wake wa karibu. Akimwambia kuwa ni mdogo wake anataka kazi basi hukawiii mdogo wangu.”

SEHEMU YA 05

Nikatoa macho na kuziba mdomo wangu nikiuliza β€œwewe dada Vanessa. Unasema kweli?”
Dada yangu Vanessa alicheka na kusema β€œsasa kumbe, kwanini nikutanie. Mdogo wangu, kaniambia kesho saa tano nimpigie yaani nimefurahi sana.”

Nilifurahi sana, nilimkumbatia dada yangu na kusema β€œdada asante kwa kunipambania. Mungu tusaidie tupate hiyo nafasi, Fanya jambo Mungu.”
Dada Vee aliniambia kwa upendo tukiwa tumekumbatiana β€œmpaka hapa tayari, tusibiri hiyo kesho saa tano mdogo wangu. Ila nimekusifia sana usiniangushe.”

Nikatabasamu tu na kusema β€œunavyoongea ni kama vile nimepata kazi tayari dada.”
Dada aliinuka akitaja jina la hiyo hotel huku anasema β€œkama nakuona vile mdogo wangu, kazi ushapata mimi ndiyo Vanessa dada yako. Ushapata mdogo wangu.”
Mimi nikawa nacheka kwa furaha mpaka nataka kulia. Kama kweli nikipata ndoto yangu itakuwa inafanikiwa. Ndoto inaenda kutimia.

Nikuambie tu hii siku ilienda vizuri sana kwangu. Nilikuwa naisubiri hiyo kesho saa tano kama vile sijui nasubiri nini. Hotel nimetajiwa ni ndoto yangu. Sijui niseme nini unielewe. Ni kama vile Agatha kesho usikie unaenda kukutana na Shigongo anaenda kutimiza ndoto zako.

Mpendwa wangu, kitanda nilikuwa naona kidogo maana ni nina biringika ni huku ni kule. Sina neno hapa zaidi, hamu ya kwenda kwenye hiyo hotel imenikaba. Yaani ni kama vile msanii wa mziki unaambiwa unaenda kukutana na msanii mkubwa na atakusaidia. Basi ndiyo kwangu ilikuwa hivyo.

Nashika simu, naanza kuitafuta ile hotel na kuangalia ilivyo natabasamu tu. Nawaza nivae nini hiyo siku nikiitwa ili niendane na hadhi ya ile hotel. Hotel kubwa sana hapo Dar maeneo ya Posta. Ninatamani kama niitaje na jina ila wacha tuseme tu Hotel kubwa sana maarufu yenye hadhi kubwa mno. Hawalali watu wa kawaida, watu wanalipa dollar tu. Moyoni nabaki kusema Mungu nionekanie na mimi na familia yangu. Mungu usinipite.

Dada yangu alikuja chumbani kwangu, alinikuta bado naitazama Hotel kwa simu. Alitabasamu na kusema β€œmdogo wangu, unaonekana huamini kabisa.”

Nikatabasamu na kusema β€œdada wewe unaamini kuhusu hili. Unajua mimi nahisi ni ndoto tu yaani.”

Muendelezo 1000
Njoo WhatsApp 0781858056.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

JAMANI BOSS MI NAONA AIBU πŸ’πŸ™ˆπŸ’ž 1- 5 🚩🚩🚩🚩🚩  >>> https://gonga94.com/semajambo/jamani-boss-mi-naona-aibu-1-5
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest