Akacheka akisema โkwa ulivyonichosha sitaki hata ufanye nini.โ Nikasema โya kweli hayo?โ Akacheka akisema โkwanza haramu. โ Tukacheka nikisema โunajua nasubiriwa na leo nawahi kutoka kwaajili ya maandalizi ya kesho.โ Akanitazama akasema โhata mimi nawahi kutoka naenda msaidia totoo kujiandaa. Sasa sikia ukitoka fanya unaloweza kanisubiri pale kona ya kanisani. Mimi nakufuata hapo chapu nakupeleka saluni nzuri mama yangu nilikuwa nampeleka hapo. Ukapendeze.โ Nikamuuliza โtunaenda wote saluni?โ Akaniambia akicheka โhaya nenda ubishi ni haramu.โ Nikacheka na kuanza kutoka. Wakati natoka tu, nikakutana na mfanyakazi mwingine mlangoni na yeye ndiyo alikuwa anaingia. Natamani ungemuona alivyokuwa ananitazama. Nikasema wewe usinitanie, mimi nikarudi tena ndani kwa Boss. Nilipofika tu. Boss alimuuliza yule dada โUnahitahi nini?โ Yule dada alinitazama jicho kali, kisha alisema โsamahani naomba kuzungumza na wewe.โ Boss alinitazama na kisha alimwambia โmara ngapi nikuambie hii sio sehemu ya kuja ovyo kila unapojisikia. Shida na malalamiko yenu nayapata kwa meneja. Haya nenda kamwambie matatizo yako ndiyo kisha utajibiwa na meneja.โ Huyu dada alijisikia aibu sana. Alinitazama kwa hasira akatoka. Alipotoka nikauliza โkwani huyu kafuata nini?โ Akaniambia akitabasamu โusijali baby, najua namna ya kumalizana mambo madogo madogo.โ Nikamtazama kwa jicho, akatabasamu akasema โbaby kununa ni haramu wallahi nakuambia, dini zote haikubaliki.โ Nikatabasamu tu na kutoka. Nilipotoka nilikwenda moja kwa moja kwa Joan. Joan aliponiona aliniambia โndugu yangu muda wote huo?โ Moyoni nasema angejua huyu mwenzake nimetoka kuchangamsha damu asingeniuliza maswali. Basi nikamwambia โnisamehe kipenzi, kuna maagizo ya Boss nikatoka kabisa hapa ndiyo narudi na nina njaa hatari, si unajua hata simu hatuna nikashindwa kukuambia rafiki yangu.โ Joan akasema โmimi nishakula, nimekubakishia. Kula basi haraka haraka tuondoke.โ Basi wakati nataka kula yule dada nimekutana naye kwa Boss akapita na kusonya. Joan akashangaa na kusema โkachanganyikiwa nini?โ
...
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 77 Nikamuuliza โkwani ni vipi huyu dada, nimekutana naye muda ule natoka kwa Boss. Basi alinitazama kwa jicho hilo nikaogopa.โ Joan alianza kucheka alicheka akisema โhao ndiyo wanaohangaika waolewe na Boss. Boss mwenyewe hacheki na kima, yeye akikupitia tu tayari si bora watulie kama mimi hapa?โ Nikashtuka na kuuliza โhata wewe pia?โ Akasema โndugu yangu kupata kazi sio rahisi hivyo, mtu mwenyewe ana dharau kama nini unaweza nenda naye room akaishia kukutazama tu. Ya nini mimi.โ Nikacheka tu, nikisema โtuondoke, nitakula tu nyumbani.โ Joan alisema โyamekuwa hayo, au unampenda Boss ndugu yangu. Kama unampenda bora usahau tu. Yile sijui hana Moyo.โ Nikacheka tu nikisema โnitamuanzia wapi mimi, na usikute anaye mke nyie mnahangaika tu.โ Naongea hapo moyoni kuna waka moto. Nachukia kusikia hayo maneno sana, ila nitafanyaje sasa na mtu kakiri. Nilichukia ila moyoni nasema โMungu anajua.โ Basi tulienda kuchukua simu, na kubadili nguo. Nilipowasha tu simu nilikuta na semeji zake zimejipanga. Honey babe Hunny bunny Honey pot My sweet person Totooo Kipenzi Ndeana wangu, na maneno matamu matamu mengi. Nikacheka tu. Na kisha ujumbe mwingine aliandika โ Nisubiri nilipokuambia, tunaenda saluni pamoja leo.โ Kiukweli siku hii sikuwa na story nyingi na Joan. Basi tulipotoka tu tuliagana vizuri tu. Nilitembea mpaka hiyo sehemu aliyoniambia. Nilimtumia ujumbe kuwa nipo hapo. Hakuchelewa ndani ya muda mfupi tu alifika. Niliingia ndani ya gari na alinitazama na kuniambia โUnaonekana umenuna kuna nini totoo!!!โ Nikamtazama na kumuuliza โKwani kazini umetembea na wanawake wangapi?โ Akasimamisha gari na kusema โNdeana nilijua umenielewa na yameisha. Ina maana unataka nilie tena. Mumy mimi mtu mzima ujue, please nipe muda. Ningekuwa sikupendi nisingekuwa nahangaika hivi. Please jiweke mbali na hayo mambo kama ni hivyo basi uache kazi.โ
...
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 78 Nikamtazama na kusema โNiache kazi kivipi sasa?โ Akavuta pumzi na kuniuliza โunanipenda mimi?โ Nikamtazama tu, akaniambia โnisikilize mimi, mimi nakupenda peke yako wewe tu.โ Nikaitikia kwa kichwa. Akaniita โNdeana!!!โ Nikaitikia โabee!!โ Akaniuliza โunajua kwanini napenda kukubusu?โ Nikamtazama kwa aibu na kusema โHapana, sijui?โ Akniambia โkwasababu kila busu lako linaanzisha maisha mapya ndani ya moyo wangu. Mwili wote unasisimuka na kuwa na furaha. Nakupenda Ndeana.โ Nikasema kwa upole โTuachane na hayo sasa tuendelee na safari.โ Akatabasamu. Basi akaweka nyimbo zake kama kawaida, kwa mara ya kwanza, tangu nitoke kwenye tumbo la mama yangu. Ninaonaga kwa tv tu, ila sasa hivi yananitokea mimi mwenyewe katika maisha yangu. Nilishuka kwa gari, na Boss akashuka. Kapendeza mwenyewe, anavutia yaani hata ukisimama ukisema huyu ni mpenzi wangu, lazima upewe maua yako. Alinishika mkono, alinibebea pochi yangu. Nilikuwa najisikia aibu sana. Tulitembea mpaka saluni. Ile tunaingia tu, wadada wote wa saluni wakaacha walichokuwa wanafanya wakatutazama. Kisha Boss wangu, aliita kwa sauti ya wote kusikia โAunt, nimekuletea mkweo leo, maana kila siku unanipigia kelele haya huyu hapa, anaitwa Ndeana, ni mke wangu mtarajiwa.โ Aunt sasa akashangaa akisema โStewart, usinambie unanitania, mbona mrembo hivi, nitambulishe vizuri.โ Mwanaume wangu sasa, alivyo anajiachia kwa raha, si mwenzenu nilianza kutambulishwa alianza kwakusema โAunt, she is my sweet person.โ Aunt sasa โumh!!, uhm!!โ Aliendelea akisema โMimi namuitaga totoo, Aunt huyu sasa ndiyo roho yangu, nampenda sana huyu mrembo anaitwa Ndeana. Ni mwanamke wa pekee sana kwangu. Ndeana huyu ni aunt yangu. Rafiki kipenzi wa mama yangu. โ Mimi sasa mpaka aibu wadada wengine wanavyoshangaa yaani huku moyoni nasema โNdeana mimi, sijawahi kupendwa hivi, zamani nilikuwa kama hawa wanaoshangaa.โ Basi nikasalimiana na Aunt kwa furaha na kisha Boss wangu alisema โNakaaa hapa nataka nione anavyopendeza. Naomba mtengeneze vizuri sana. Vyovyote ili mradi apendeze. Totoo enjoy kipenzi.โ ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐๐na leo mkikoment kama jana kesho mpaka mia๐๐ป
...
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 79 Nikacheka. Akasema โBaby kwani kukusubiri hapa ni haramu.โ Nikamjibu nikicheka โni haramu baby dini zote zinakataza.โ Akacheka akisema โumoja wa mataifa uingilie kati nakusubiri kipenzi.โ Watu wakajikuta wanacheka na kuanza kunongโonezana. Mimi na yeye tunatazamana na kukonyezana huku akiwa na pochi pembeni. Nyie mapenzi matamu mjue, mimi ndeana nawaambia. Basi tena, Aunt mkwe tena kajua mimi ni mkwe wake. Basi ananifurahia mwenyewe, ananitengeneza nywele akiwa na furaha sana.Boss wangu amekaa tu anachezea simu yake hana habari, wadada mule ndani wanapiga story wanamuangalia Boss wangu napata wivu maana wasije niibia njiwa wangu akapeperukia mbali sana. Nilipendeza sana, unajua kuna kule kupendeza mpaka wewe mwenyewe unajua wazi ya kuwa umependeza. Basi nilipomaliza Aunt mkwe alisema โmkwe wangu umependeza mno, yaani hapa sasa kila mawimbi yakivurugika njoo tunatengeneza mtindo mwingine. Hili wiki ni kama lilitengenezwa maalumu kwaajili yako. Stewart unasemaje, umemuona mwenzio.โ Boss alitabasamu na kusema โnimemuona aunt, ni mzuri sana. Amependeza sana.โ Akanisogelea na kisha akanishika mkono tulienda kukaa kwenye sofa pamoja. Akawa ananishika nywele zangu huku ananiambia โbaby hawa wadada wanaona wivu, itakuwa hawapendwi hawa.โ Nikajikuta nacheka na akaniziba mdomo watu wanatutazama. Mimi nikamwambia โhuna akili kabisa.โ Akatabasamu na kusena โNdeana wewe ni mzuri sana. Umependeza sana. Umependeza vibaya mno.โ Nikamwambia โNashukuru sana. Haya uliza basi gharama nilipie.โ Boss wangu alitabasamu na kusema โuna matatizo wewe. Nikusifie na Bill ulipe wewe. Hii ni juu yangu. Mwanaume akikusifia ahakikishe yeye ndiyo ana gharamia. Yaani akikusifia umevaa nguo mpya umependeza, viatu vipya ama chochote na yeye hana tatizo lolote lile, yupo tu kukuonea, anakufanyia makusudi mbinafsi.โ Nikamtazama na kusema โbaby lakini mwingine kipato kidogo?โ Akatabasamu akisema โkipato kidogo pia kuna vitu vidogo vya kunogesha penzi lao. Sasa baby niwe sina hela hata kijola ukose, hata kukupeleka kula mihogo nishindwe, masihara sasa.โ Nikacheka na kusema โuna maneno kama nini?โ
...
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 80 Aliinuka na kisha alienda kwa Aunt yake. Walizungumza kidogo kisha Aunt alinifuata na kusema โKipenzi, sasa usiwaze kuhusu nywele. Wewe njoo hapa kila ukiona nywele haifai. Njoo hapa na utengeneze. Ushalipiwa kabisa, na bill ikiisha mpenzi wako analipa hana shida.โ Nikamtazama Boss na kutabaasamu kwa kushangaa yaani, kisha akaniuliza โUtanishangaa tu totoo, hutonikumbatia?โ Nikacheka na kwa aibu nilikumbatia nikisema โAsante sana, Mungu akubariki.โ Basi alinishika mkono mpaka kwenye kioo eti akaniambia โhaya baby jishaue kidogo nakuchukua video hapa.โ Huyu mwanaume ana vituko yaani nikajikuta ninacheka. Basi tukapigana picha na tukiwa timekumbatiana huku tunaonesha picha na video za hapa na pale. Tukamaliza basi nakuambia nikabebewa pochi tena tukamuaga Aunt huku msalimie mama zikiwa nyingi, nitakuja na vitu kama hivyo. Nikafunguliwa mlango totoo mie tukaingia ndani ya gari. Mimi mwenzenu nimepata dereva binafsi, napelekwa nyumbani na nimepata furaha ndani ya muda mchache. Huyu mwanaume amenifanya nifurahie mapenzi ndani ya muda mfupi sana. Hata wiki hatujamaliza ila ananidekeza ananijali na kunitunza ni kama yaani tumejuana kwa muda mrefu sana. Ni kama vile tunajua miaka na miaka. Amenifanya nimzoee na amenifanya nijihisi huru kwake. Ninampenda, ila naona aibu nami kufunguka nahisi bado ni mapema sana. Basi mwenyewe kwa gari humo nilikuwa na furaha sana. Maana nasifiwa na kutaniwa tu huku na yeye akijisifia kuwa katika wanaume wamepata wanawake wazuri basi na yeye ni mmoja kati ya hao wanaume. Tulifika mpaka mitaa karibu na nyumbani. Alisimamisha gari na baada ya hapo alinitazama na kusema โTotoo, nimesimamisha kukuambia kuwa jambo ambalo linaenda kutokea kesho ni jambo kubwa sana. Ni jambo ambalo sikumbuki kama katika hotel yetu limewahi kutokea. Kwanza hotel itakuwa busy, kuanzia vyumba, na hata upande wa chakula. Pesa zitaingia za kutosha. Pia itatangazwa sana Hotel hii na tutapata watu wapya wengi sana. Yote haya ni kwasababu yako. Natamani nikufanyie kila kitu kizuri ndiyo uwezo sina.
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.