ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 105
Nikatokwa machozi nikisema βbaba!!, baba yangu.β
Aliniambia kwa hofu βtangulia tunapokutanaga, nakuja sasa hivi. Relax baby. Relax mpenzi wangu.β
Sikuwa naweza hata kurelax, sikuweza hata kumjibu. Hata simu yangu niliacha palepale na kuanza kukimbia kuelekea mahali tunapobadili nguo.
Ilikuwa hivyo, nilipofika katika chumba hicho nilikuta Joan pia anabadilisha nguo. Namna muonekano wangu ulivyokuwa, aliponiona alipata hofu. Joan aliniuliza βKuna kini kwani Ndeana, mbona mara hivyo.β
Nilmtazama tu, nikawa nabadili nguo nikisema βdada amesema baba yangu anaumwa sana.β
Joan aliniambia βbasi kwakuwa na mimi ndiyo natoka basi naomba tuongozane nikusindikize huonekani kuwa sawa.β
Nilimtazama na kusema βAsante kipenzi ila wacha niende nikaone kwanza hali tutawasiliana.β
Nakumbuka Joan alivuta bahasha, kisha akanipatia na kusema βmeneja, ametupa kila mmoja bahasha yake kwa kazi ambayo tumefanya. Pia mapumziko siku tatu.β
Nikavuta pumzi na kusema βnashukuru sana, Asante sana Joan. Basi kwaheri tutawasiliana.β
Nilitoka mbio mbio mpaka sehemu ambayo Boss aliniambia tukutane. Nilipofika pale yeye pia hakuchelewa sana alifika. Haraka alinifungulia mlango wa gari. Nikaingia. Alinitazama kwa huruma na kunipatia simu yangu ambayo tayari ilikuwa imevunjika. Aliniambia βmpigie dada anakutafuta sana.β
Nilipokea simu ya dada tulikuwa tunaelekezena vitu kama mnavyojua familia tu. Basi alinielekeza hospitali aliyompeleka baba yetu na mimi nikamuelekeza Stewart na alikuwa ananitazama kwa huruma tu.
Nakumbuka tulifika mpaka hospitali, kwa nilivyokuwa nilikuwa nasahau hata kama nipo na Stewart maana nilikuwa natembea haraka kiasi yeye ndiyo ananikimbilia. Dada aliponiona tu tukakumbatiana kwa kulia. Dada alisema βmdogo wangu, baba anaumwa, madaktari wanamshughilikia. Tumuombee baba yetu.β
Nilimtazama dada yangu nikilia sana, huku nikimuuliza βdada, baba atapona kweli, atapona.β
Dada aliniambia βmdogo wangu jikaze sasa. Nafahamu unavyompenda baba. Ila kulia ni uchoro huo ilihali mtu anapambania maisha yake kwaajili yetu. Tunatakiwa kumtia moyo nasi kwa kuwa majasiri na kumuombea.β
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 106
Nikawa naitikia kwa kichwa nikisema βkweli dada, ni kweli lakini nashindwa mimi, nashindwa.β
Stewart aliingia, aliponiona nalia namna ile, alikuja kunikumbatia. Dada alibaki anatutazama tu hata alienda kukaa sehemu ambayo kulikuwa na benchi maalumu la kukalia watu wanaosubiri huduma.
Nakumbuka Stewart alivyosema βTotoo, nipo hapa pamoja na wewe. Huwezi kulia na kuumia peke yangu, mimi ni sehemu yako kipenzi. Tumekuwa familia, tumekuwa wamoja. Naomba jikaze, tulia na haya kwa pamoja tutashughulikia.β
Tukiwa katika hali hiyo ya kufarijiana, aliingia Martha. Alifika mpaka tulipokuwa tumekumbatiana, aliniita βwiii, wizou jamani, usilie hivyo. Unapokuwa unafanya hivyo unazidi kuharibu. Baba atakuwa sawa tu. β
Nilimtazama na kusema βAsante sana dada Martha.β
Kisha akasalimiana na Stewart, kama kawaida ya watu wanaofahamiana kisha alienda kumfariji rafiki yake ambaye ni dada yangu.
My boss, alinifuta machozi na akaniuliza kuhusu baba yangu utambulisho wake na vitu kama hivyo. Kisha akanishika kwa upendo na kwenda kunikalisha mahali akisema βnisubiri hapa, naenda kuzungumza na daktari.β
Nilitabasaku kiuchovu na unyonge nikimtaka asichelewe kurudi.
Nilibaki pale, huku Martha akiniuliza βbro ameenda wapi tena?β
Nikasema kwa upole βanarudi sasa hivi.β
Akasema βooh basi mtaniagia, kwa maana rafiki yangu ulivyopiga simu unalia ikabidi niache kila kitu. Tupo pamoja , Mungu ni mwema kila kitu kitakuwa sawa. Baba atapona na atarudi kwenye ubora wake.β
Dada akajibu βAmina kipenzi, Mungu atusimamie.β
Aliondoka, mimi na dada tulibaki pale tukiendelea kutiana moyo na kufarijiana. Tuliongea kuhusu matibabu ya baba na dada aliniambia kuwa kuna pesa ya mtu ameazima kwaajili ya kuwahi hospitali.
Pia dada yangu aliniambia βMdogo wangu, hatukupata muda wa kuzungumza kwasababu sikuwa nataka kukusumbua kazini. Baba hali yake sio nzuri kwa muda kidogo. Hivyo ile pesa nikawa natumia kumnunulia dawa. Ilibaki kidogo ndiyo nimeongezea na nyingine. Sasa itakuaje mdogo wangu.β
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 107
Nilimtazama dada na nikamwambia βdada huna haja ya kuelezea kuhusu pesa. Najua wewe ni dada yangu. Ni wajibu wetu kumlinda baba. Umefanya vizuri lakini sasa, vipi na wewe hilo tumbo lako?β
Dada alinitazama na kusema βmdogo wangu, tumbo langu nikisema nikuelezee huwezi kunielewa kwasababu mimi nina uwezo wa kuvumilia matatizo. Ila mdogo wangu hali sio nzuri. Tumalizane na baba hili tumbo pia inabidi tufanye vipimo kama ulivyo shauri.β
Nilimtazama na kusema βdada mimi naogopa, kukaa na tatizo kama hivu hila utatuzi ni hatari sana dada. Siku hizi magonjwa mengi sana. Unaweza kujua ni tumbo la kawaida kumbe hapana. Unaonaje na wewe ufanye tu vipimo ili wote wawili mpone kwa pamoja.β
Dada alinitazama na kutabasamu, kisha machozi yalimtoka akitazama mbele akisema βshemeji yangu ni bonge la bwana. β
Nami nikatazama na kutabasamu machozi yakitoka.
Alikuwa ni Stewart, My Boss, ndiye aliyekuwa anakuja kutoka kwa daktari. Alipofika alituambia βsasa tafadhali mnaweza kuacha kulia au na mimi nianze kulia?β
Mimi na dada tulitazama na kisha alitabasamu na dada alisema βtunanyamaza.β
Alitabasamu na kusema kwa upole βsasa, nimeongea na daktari. Sasa baba yupo kwenye chumba ambacho tutamuona muda wowote tutakavyo. Pia sasa atabadilishiwa dawa, wala msijali kuhusu chochote mimi nipo pamoja na mimi.
Mkumbuke magonjwa kama sukari, na shinikizo la damu yapo kwa wazee wengi ni umri tu. Hivyo sasa tutambadilishia mtindo wa maisha yake kuanzia kula na matibabu yake. Ila inabidi mnipe ruhusa mniachie mimi.β
Dada alinitazama na alijikuta anatokwa machozi akisema βMungu akubariki sana Shemeji, sina hata neno la kusema zaidi ubarikiwe. Mdogo wangu asante sana, tungefanya nini peke yetu.β
Nilimtazama nikitokwa na machozi nikiuliza βStewart kwahiyo baba yangu anapona si ndiyo, hakuna baya litatokea.β
Akanitazama na kunikumbatia akisema βtoto!!, ondoa hofu.Mungu atatusaidia. Na nakuahidi baba atapona. Hata hivyo hali ya afya yake sio mbaya sana. Akitumia dawa zake vizuri, akila vizuri na kuzingatia maagizo ya daktari anaweza kupona kabisa.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 108
Niamini mimi.β
Nikafurahi sana nikisema mbele ya dada yangu, tena nikiwa nimemkumbatia. Nakumbuka nilisema machozi yakitoka βNakupenda sana Stewart, nakupenda, wewe ni bora sana, Nakupenda.β
Stewart hakujibu alibaki kanikumbatia tu, hata dada aliona hilo. Alisema βShem, tunaweza kwenda kwa baba sasa.β
Alinitazama na kusema βbila shaka, twendeni.β
Tulianza kutembea kuelekea huko, tena mimi na yeye tukiwa tumeshikana mikono na dada akiwa nyuma yetu. Tulifika mpaka chumbani kwa Baba alikuwa ametundikiwa mipira mingi sana.
Mimi sio mtaalamu wa afya ila kumuona baba yangu kwenye hali ile yalikuwa ni zaidi ya maumivu. Nilijikuta natamani hata niseme mara mia namna nampenda baba yangu. Baba yangu ametulea kwa upendo tangu mama alipotuacha.
Ni baba mzuri kwetu, sikuwa tayari kumuona na yeye anapoteza maisha. Sijui labda kwasababu mama yetu hayupo ila sisi tunampenda sana baba yetu. Vile mimi na dada yangu tulisogelea kitanda, na kuanza kumuuliza baba kama yupo sawa tena tukilia.
Baba yetu alikuwa anatutazama tu kwani hakuwa katika hali hata ya kuongea. Alikuwa vibaya sana. Nilisema kwa upole βBaba Nakupenda sana, nakupenda mno baba. Unanipenda na kunilea katika njia sahihi.
Na sasa umelala hapa zile baraka zako nitazipata wapi sasa. Leo nilikuwa nirudi nyumbani nikusimulieni namna kazi ilivyokuwa nzuri na tumemaliza si ndiyo Stewart.β
Stewart kwa huruma alitutazama tu, dada yangu na yeye alikuwa akisema yake kwa upande wake. Hakika kumuona mtu anayeugua na ni kipenzi cha maisha yako inaumiza sana. Inauma sana. Ndivyo nilivyokuwa ninaumia kumuona baba yangu kitandani hawezi kufanya lolote lile.
Labda nikuulize wewe, mara yako ya mwisho kumwambia mama yako, baba yako, dada au kaka yako, mlezi wako yeyote ambaye anakulea kwa upendo hata ukawa wewe, mara yako ya mwishi kumwambia neno hili kutoka moyoni NAKUPENDA, asante unanilea na kunitunza vizuri ni lini?.
Au unafikiri neno hili ni kwaajili ya mapenzi tu. Hapana, siku hii nilitambua kuwa hata baba yangu anastahili kusikia maneno haya mazuri yenye nguvu ili ajue kuwa anatakiwa kuishi kwaajili yetu.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 109
Ninatamani kukuambia acha kila kitu unachofanya na umwambie mlezi wako neno NAKUPENDA uone namna atafurahi na kukupa baraka nyingi sana. Haijalishi magumu unapitia walau basi uwe na mtu anasema nakuombea.
Nakumbuka sana, My boss aliposema βkwasasa baba hawezi kufanya lolote. Daktari pia alishauri tumuache peke yake pengine labda turudi baadaye. Mnavyokaa hapa na kulia mnampa wakati mgumu baba. Mnanielewa?β
Tukawa tu tunatokwa machozi. Maskini Boss alinichukua mimi na dada yangu na tulitoka nje. Alisema βsasa niwapeleke nyumbani kisha tutajua nini kifanyike.β
Niliitikia kwa kichwa. Dada yangu alisema βShem, wewe mpeleke mwenzio, mimi ni baki hapa. Linaweza kutokea tatizo na asiwepo mtu wa karibu. Mdogo wangu, usiache na nguo za kubadilisha baba.β
Nikamtazama na kusema βdada, umetoka kuniambia unaumwa, na sasa hivi tena unataka ubaki. Twende wewe ukapumzike, mimi nitarudi kwa baba.β
My boss akauliza βShem, unaumwa nini tena?β
Akatabasamu na kusema βusijali Shem, kidogo tu tumbo linanisumbua.β
Mimi nilikazia, βsio leo ni ugonjwa wa muda mrefu, dada mbishi sana.β
Boss wangu akasema βsikieni, ugonjwa ni rahisi sana kuingia mwilini ila kutoka ni ngumu sana. Tumezoea kuumwa na kunywa dawa bila kupima. Ukiona umefanya hivyo na bado unaumwa tu ujue ni tatizo linahitaji matibabu. Shemeji yangu, na wewe sasa unatakiwa kupima ili wote tuwe wazima. Si kitu kizuri kuzoea ugonjwa unaweza kuta ni tatizo linatakiwa tibika haraka kabla halijaleta madhara.β
Nilimtazama dada nikisema βkweli dada. Pima na wewe. Walau kwanza tujue tatizo, matibabu tutajitibia taratibu.β
Boss wangu mwenyewe sasa na huu utambulisho wa lazima nakuambia alimshika mkono dada yangu akisema βusiogope, mimi nitakuwa hapa kumsaidia mdogo wako, sasa ondoa shaka. Naomba twende kwa daktari ukajielezee kisha ufanyiwe vipimo.β
Dada alitutazama na kutuuliza βmna hakika ni salama lakini.β
Stewart akamtazama na kusema βndiyo shemeji yangu. Ni salama.β
Basi tuliongozana mpaka kwa daktari. Dada alijielezea, akachukuliwa vipimo pale hospitali. Nasi tulikaa kusubiri majibu.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 110
Ni kweli dada yangu alikuwa anaishi na ugonjwa kwa muda wote huu. Alikuwa anafuga ugonjwa ambao ulimgharimu maisha yake. Dada yangu alikuwa na Kansa ya kizazi ambayo ilikuwa imemuharibu sana. Suluhisho la daktari ilikuwa ni kizazi kiondolewe kwa haraka sana yaani hakuna muda wa kupoteza zaidi ya kufanya hivyo tena huku daktari akisema dada yangu aliwezaje kuishi na hali hii muda wote huo.
Unataka kujua tulipokeaje hili, hatukupokea vizuri hata kidogo. Dada yangu alilia akisema βsitaki mimi, nitaishi vipi sasa bila kuwa na kizazi changu. Ina maana mimi sitakuja kuitwa mama maisha yangu yote. Ina maana mimi kuwa mama nisahau. Ndeana mdogo wangu, nataka kuwa na mwanangu, nataka kuja kuitwa mama. Ina maana ndoto zangu za kuja kuwa mama bora zimeisha kweli?, ina maana, Mungu wangu!!, Mungu wangu!!, nimekosa nini mimi!!β
Aisee!!, dada yangu alilia kwa uchungu sana, Stewart alimkumbatia kwa uchungu akimbembeleza kuwa βshemeji yangu tulia, huu sio mwisho wako. Ni vizuri tumewahi kidogo. Ingekuwa na madhara kwako. Sikia shemeji, wewe kuitwa mama sio mwisho. Kuwa mama sio lazima mtoto atoke tumboni kwako. Mtoto yeyote ukimpenda na kumjali unaweza kuwa mama yake. Nakuomba shemeji yangu, usikate tamaa. Muhimu sasa ni wewe upone ili ushirikiane na mdogo wako kumtunza baba. Nakuomba.β
Dada yangu alizidi kulia, na hata mimi pia roho iliniuma. Kama mnavyojua tunavyopendana na dada yangu. Ila bado nilimsihi akubali. Daktari pia aliongea lake na kisha dada yangu alikubali na aliomba apate muda na mimi. Na wote walitoka nikabaki na dada yangu.
Dasa yangu alishika mikono yangu na alisema βNdeana mdogo wangu nakupenda sana. Ninaumia sana kupokea haya majibu ila nataka kuishi. Mboni za macho yangu bado zinatamani kukuona wewe na baba yetu.Nataka bado kucheka na kupiga umbea na wewe. Ndeana lolote likitokea kwenye upasuaji wangu usiumie sana na badala yake umtunze baba vizuri sana. Uishi na baba vizuri na nilitaka nikuambie, mwanaume wako ni mzuri sana. Ana huruma na upendo sana. Ni ngumu sana dunia ya sasa kumpata kama yeye. Muheshimu mdogo wangu, mjali na umpende sana. Sitapenda kuona mkigombana
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005


Maoni