81 Nakuomba sana uwe makini leo, ulale mapema na uamke mapema maana wewe ndiyo tunakutegemea. Najua utakuwa umetingwa sana mwezi huu wote. Nashindwa kusema nitakukumbuka sana, nitakumiss ila sitaacha kukuona hilo kaa ukijua na pia usiku najua utakuwa unapata muda kidogo kwaajili yangu si ndiyo totoo.โ Nukamshika mikono na kusema โusinishukuru zaidi inatosha sasa. Kikubwa ni kuwa Mungu ametusaidia na tutafanikiwa. Sijawahi kufanya kazi kubwa kama hii ila nakuahidi nitafanikiwa. Ila nina kitu nafikiriia..โ Haraka akaniuliza โni kitu gani hiko?โ Nikavuta pumzi na kusema โKuhusu wageni wetu na sehemu za kulala najua mnashughulikia sasa. Ila kumbuka mimi na wenzangu wawili tu ndiyo tunaotakiwa tuwahudumie hawa wageni. Sasa kama hivi tunaishi mbali nafikiria..โ Akasema โumewaza kama mimi totoo, kusema ukweli tumeandaa chumba kwaajili yenu mpaka kazi iishe.โ Nikatabasamu. Akatabasamu pia na kusema โSi unajua nimetoroka kazini, hapa natafutwa sana, ila nikaona mpaka nikulete kisha nirudi.โ Nikamwambia kwa upole โAsante sana, Haya rudi basi kazini.โ Akaniuliza akitabasamu โkivipi sasa bila busu, yaani wewe kunibusu ni mpaka kifo kinichukue.โ Nikacheka nikisema โmjinga kweli wewe.โ Nikambusu kama anavyopenda basi nikashuka ndani ya gari. Basi nikawa natembea mwenyewe najua nimependeza. Nywele yenyewe ya gharama. Sitaki kuongea sana maana walimwengu kupendwa hawajazoea na hata wakipendwa wanaogopa. Basi nikae kimya ila nywele ni nzuri sana, na pia ni nywele ya gharama. Saluni yenyewe sio saluni zetu hizi, nimepelekwa saluni yakishua. Basi natabasamu nikikumbuka wale wadada nimewaacha kule. Natabasamu vile wanahangaika kututazama mimi na Stewart. Nilifika nyumbani bahati mbaya palikuwa kimya sana. Hapakuwa na baba wala dada yangu. Hivyo niliamua kwenda tu chumbani kwangu. Nilipofika nikachukua kioo changu ambacho nacho nahitaji kununua kipya tu. Kioo ni cha elfu moja na bado kimevunjika ovyoovyo.
...
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 82 Baada ya hapo nilikuwa natabasamu tu ila nilikuwa nikikumbuka Joan na yeye amelala na mwanaume wangu nachoka yaani moyo wangu unaniuma sana. Natamani hata nisiwe rafiki wa Joan. Ila nakumbuka dada yangu, na hata mwanaume amesema ukweli isije ikanifanya nikaanza kuchukia Hotel nzima. Nikajikuta ninasema โHekima ni muhimu sana, Hekima. Nilikuwa nimechoka kusema ukweli, usingizi haukuniacha, nikasinzia pale kitandani. Nilikuja kushtushwa na dada yangu. Baada ya mimi kuamka tu dada alianza kusema โwacha weee!!, wacha weee!!.โ Sasa mimi nimesahau hata kama nimependeza kichwani nikawa nashangaa tu.Nikasema โdada kuna nini kwani?โ Dada alisema โHivi unqjua kuwa umependeza sana. Mdogo wangu nywele ya gharama umetoa wapi?, nywele imenyooka hii unajua.โ Nikamtazama na kujikuta nimeanza kucheka kwa sauti. Nilicheka nikisema โMambo ya shemeji yako hayo.โ Dada akasema โweee, boss wako huyo?โ Nami natamba nikisema โnani tena?โ Dada akaniambia โinuka twende sebuleni kwanza nimekuja na miguu ya kuku, utumbo na chips, najua unapenda huwezi kukataa.โ Nikasema โnakaaa vipi kwa mfano dada.โ Dada alicheka akisema โumbea wa leo hatari eenh.โ Basi tulifika wenyewe tukawa tunakula namwambia โbasi dada yangu, nikapelekwa saluni.โ Dada sasa anasema โwee!!!, ikawajeโ Namuambia namna alivyobeba pochi na kunitambulisha. Dada alicheka akisema โsasa huo ndiyo utambulisho, sio ile kutana na huyu ndiyo mwenzangu ninayekuambiaga, tunaimba wote kwaya, pale kazini tupo wote.โ Nilicheka nikisema โdada bora hiyo ina maneno mengi. Unakumbuka yule mjinga alivyokuwa ananifanyia yaani tukienda mahali linasema โHuyu mshikaji wangu, anaitwa Ndeana.โ Basi tukacheka mno. Nikamsimulia dada pia kuhusu yote yaliyotokea na alivyonielezea na kisha nilisema โkusema ukweli nashindwa kujizuia nampenda sana dada. Ila naogopa na mimi kuwa wazi kwake si ataniacha si eti?โ Dada alisema โhuo ni ubinafsi mdogo wangu. Mapenzi ya upande mmoja yanauma na yanachosha sana. Fikiria ungekuwa wewe, unafanya anavyokufanyia na huwezi hata kusema nakupenda.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 83
Si unaona unasababisha matatizo. Na umekaa hapa unazungumzia wanawake wanavyohangaika wapate mahusiano. Mdogo wangu kuna zaidi katika mapenzi. Mapenzi ni kujaliana, kupendana, kuelewana, kufurahiana, kuombana msamaha na mambo mengi kama hayo.
Katika mapenzi kila dakika ina maana, kila sekunde ina maana. Unavyofanya hivi mwenzako anaumia ni vile hawezi kusema na pengine kakupa muda kuwa zikifikika wiki mbili au wiki hasemi kama ananipenda basi nitamuacha.
Mdogo wangu. Unatakiwa kufurahia sasa kuachwa, au kuolewa ni mipango ya Mungu. Huwezi kusema sitamwambia mpenzi wangu namna nampenda kwanza sio mume wangu, wewe unajuaje?.
Wewe furahia sio kwaajili yake pekee. Hata wewe utakuwa na furaha hata ukiachwa utakuwa na kitu cha kusema, na ukiolewa pia utasimulia namna pendo lenu lilivyo.
Ndeana kama unampenda leo na wewe mwambie namna unampenda, mwambie namna alivyo wa muhimu kwako. Utaona namna anavyofurahia na hapo ndiyo utajua namna gani alivyokuwa anatamani kusikia maneno kama hayo.โ
Nilivuta pumzi na kusema โdada unajua una hekima sana kwenye suala la mapenzi. Mungu akujalie mwanaume mzuri.โ
Dada alitabasamu akisema โSina papara mdogo wangu ni suala la muda tu.โ
Nikatabasamu na kisha dada aliniambia tuendelee kula huku akikumbushia eti huyu mshikaji wangu anaitwa Ndeana basi tunacheka mpaka baba anaingia alitukuta na hali hiyo.
Alikuwa na mfuko akitushangaa kwa kusema โwanangu wanangu, nini kimetokea mbona furaha namna hiyo.โ
Tukacheka tu tukisema โkaribu baba. Karibu basi nikainuka na kumpokea mfuko. Baba alisema โKuna zawadi zenu humo, sasa sijui nimepatia.โ
Tukatazama na kusema kwa pamoja โZawadi, eenh baba zawadi gani tena.โ
Baba alisema tufungue ili tujionee. Waooo!!, waoo!!, baba alikuwa ametuletea viatu, sendozi za chini chini. Tulifurahia sana na kusema โbaba asante, baba asante sana tunakupenda.โ
Baba alitabasamu tu, tulimkumbatia baba yetu na yeye alikuwa amefurahia akisema โnimepita sehemu nikatamani. Sasa mmpendeza.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 84
Tukacheka. Kiuhalisi hivi viatu vilikuwa ni vya kawaida, bei yake ni ndogo sana, ila namna vimekuja kwetu, vimekuja na upendo pesa haiwezi kununua. Nikavipenda sana, nikavifurahia sana.
Kusema ukweli baba alitushangaza na kitu kama hiki boss alisema kuwa hata kama sio tajiri kuna vitu tu vya hadhi yenu vinaleta furaha ili mradi tu vimekuja na upendo kama ambavyo dada kaniletea miguu ya kuku.
Kumbe kila mmoja anaweza kufurahia kwa hadhi yake bila kuumia. Turidhike na hali zetu na kufurahia nini mazingira yanatupa.
Baba yangu pia hakupitwa na kupendeza kwangu. Alinisifia akisema โunaonekana kama bibi harusi leo.โ
Dada alicheka akisema โnimemwambia mimi.โ
Nyumba ikawa na vicheko juu ya vicheko na kisha nami nikawaelezea kuhusu kazi ambayo tunayo kuanzia kesho. Hakuna ambaye alipinga, wote walinipa baraka zao. Huku baba yangu akionekana mwenye furaha akisema โMungu ambaye tunamuomba amejibu maombi.
Nilitabasamu na kisha kama familia tuliongea hili na lile huku baba akimuuliza na dada biashara yake. Dada naye alisema yake basi familia ikafurahi.
Mimi niliwahi kuingia chumbani. Dada naye alinifuata na kusema โmdogo wangu nimesahau kitu ingawa nakujua mdogo wangu huna marafiki. Ila muweke mpenzi wako mbali na marafiki. Wasimzoee wewe ndiyo mlinzi weka mipaka. Usije ukathubutu kujinadi kwa unayofanyiwa naamiji kitu kizuri wao wenyewe wataona. Wewe kazi yako ni kupendwa na kupenda tu.โ
Nikatabasamu, nikamkalisha dada kitandani nikisema โasante sana dada.Nakupenda. Ila nina kitu. Nataka dada yangu uende hospitali ukaangalie hilo tumbo kwanza. Nilipewa pesa kidogo ya maandalizi. Nakupa laki mbili sawa dada. Nataka upone na usijitese kufanya kazi ngumu. Ukichoka acha. Pia pesa kidogo baba yetu apate dawa nami nikiwa kazini nikipata kidogo nakuwa natuma kwaajili ya familia yetu. Sawa dada.โ
Dada yangu alinishangaa na kunikumbatia akisema โuna roho nzuri sana mdogo wangu. Wewe sio mbinafsi. Na unaipenda familia yako. Mungu akubariki sana. Mungu azidi kukufungulia mdogo wangu. Sina neno nakupenda tu.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 85
Nilimwambia kwa upole โdada huna sababu ya kulia kwasababu jukumu la familia yetu ni letu pamoja. Wewe ndiyo rafiki yangu, ndugu yangu, ni kama mama. Dada nakupenda sana.โ
Tulikumbatiana na nilimpatia pesa. Dada alifurahi sana. Alifurahi mno. Niliona hilo.
Basi dada yangu alitoka chumbani na aliniacha nikiwa na amani sana moyoni. Nilishika simu yangu, sikuona ujumbe wowote. Nikakumbuka maneno ya dada yangu nikaona ni heri nami nimuoneshe upendo. Sijui ninafanya nini ila nitazoea. Ndipo na mimi kwa mara ya kwanza, nilichukua simu yangu na kuanza kuandika.
Nilikuwa na mengi moyoni ila siku hii nilisema โStewart, Asante kwa kila kitu. Wewe ni mwanaume mzuri sana. Kuelezea ninavyokupenda peke yake haitoshi. Ninatafuta kitu cha kuubebea upendo ambao ninao kwako nakosa kabisa.
Mapenzi yangu kwako ni makubwa. Asante unanipenda nw unanijali. Sina kitu cha kukupatia zaidi ya penzi langu la dhati na la kweli. Nakupenda sana Stewart wangu, natamani kungekuwa na neno kubwa zaidi ya neno nakupenda ila hakuna na sijui nifanye nini ujue namna nakupenda. NAKUPENDA.โ
Nikasoma huu ujumbe, nikasema โMungu wangu sijui nimeweza, sijui sasa nifanye nini. Nifute nianze upya au nifanye nini. Nikaituma ule ujumbe na kuweka simu yangu pembeni. Kwasababu nilikuwa naona aibu yaani. Nawaza sijui atapokeaje ule ujumbe.
Basi mimi nikaenda kuoga, na niliporudi simu yangu niliikuta ikiita. Niliitazama alikuwa ni Boss wangu. Nilitabasamu na kujisema โMy boss.โ
Basi Nikapokea, Boss aliniambia โNdeana ni wewe?โ
Nikamuuliza โvipi mbona sielewi, unauliza kuhusu nini tena.โ
Akaniuliza kwa kimuhemuhe โumesema unanipenda si ndiyo, unanipenda sana. Umesema unanipenda.โ
Nikatabasamu na kujibu kwa sauti ya chini โNakupenda sana.โ
Akacheka sana akisema โNdeana unanipenda kweli, kama ambavyo mimi Nakupenda.โ
Nikamwambia kwa masihara โumeniambia niwahi kulala leo ujue!!โ
Akasema โacha utani Ndeana hapa serikali iingilie kati. Nakuacha vipi ulale na ndiyo kwanza penzi limeanza upya.โ
Nikacheka sana.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 86
Ni kweli inaonekana alikuwa anasubiri kwa hamu sana siku hii itokee. Alifurahi sana na hata aliniruhusu nilale kwa maana kazi ya kesho ni muhimu kwa maslahi ya Hotel yetu tunayofanyia kazi. Nilikuwa natabasamu tu muda wote. Moyoni ni kama nimetua mzigo mzito sana baada ya hili kutokea. Ninafuraha sana.
Ninakumbuka sana asubuhi hii, niliamka nikajiandaa vizuri sana. Wakati natoka nilikutana na baba na dada pale nje. Baba yangu alinitania akisema โsasa ndiyo nakuona vizuri zaidi. Binti yangu umependeza sana.โ
Nilitabasamu na kisha baba alisema โDada yako amenielezea mwanangu. Mungu akubariki uwe na moyo huo huo. Asante sana. Nafurahi kuona mnapendana. Nafurahi sana.โ
Nilitabsamu na kusema โNashukuru baba, kila kitu kitakuwa sawa.โ
Baba alisema โNi furaha kuona mmoja kati ya familia hii anafanya kazi katika hotel ya ufahari. Nimekuombea usiku wote mwanangu ikawe heri kwako.โ
Nikatabasamu na kusema โKila siku unanibariki baba yangu. Ina maana leo hutoshika kichwa changu.โ
Baba akacheka na kusema โNjoo binti yangu.โ
Nilimsogelea, nikainama mbele yake akabibariki. Na dada yangu pia alinibariki. Nikafurahi sana na kuondoka zangu.
Nilifika katika geti la Hotel, wakati naingia simu yangu ikaita. Alikuwa ni Boss na yeye aliniambia โNdeana kabla hujaingia ndani naomba njoo parking, ninataka kukuona.โ
Nikashangaa nikisema โtunaweza kuonekana lakinu.โ
Aliniambia โsijali nani ataona kwa maana mwisho wa siku kila kitu kitakuwa wazi. Hata hivyo kwanini tunajificha?, please njoo.โ
Nikavuta pumzi yangu na kuelekea aliposema. Baada ya kufika tu alinionesha ishara nami nikamfuata. Alinifungulia mlango wa gari, nilipoingia tu alisalimia vizuri na kisha aliniambia โNakuomba geukia upande wangu, nataka nione sura yako nzuri.โ
Nikatabasamu tu, nakumbuka alichukua mkono wake akanishika uso wangu kwa upendo.
Huku ananitazama usoni, kwa utulivu na mahaba mazito aliniambia โNdeana unaweza?, unaweza kusema tena yale maneno ya jana nikiwa nakutazama, unaweza kusema unanipenda sana ukinitazama, unaweza kusema mimi ni mwanaume wa pekee kwako ukinitazama.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 87
Tafadhali totoo, niambie unanipenda. Nataka kuona midomo yako mizuri na laini yenye muonekano wa kupendeza ukiniambia namna unanipenda, Please niambie baby, nataka kukusikia, nataka kukuona, niangalie usoni na uniambie unanipenda, please baby.โ
Mimi sijawahi kuwa na mwanaume mtulivu namna hii. Anaongea maneno unasisimuka mpaka unahisi kujikojolea kwa furaha. Nilijikuta namtazama machozi kwa mbali na nikasema nikimtazama usoni tena kwa kumaanisa. Nilisema โYes, Nakupenda sana Stewart, Nashindwa kujizuia hisia zangu. Kila nikitaka nikae mbali na wewe upendo unazidi. Your so sweet, Romantic, lovely, wewe ni waajabu sana. Ni kama vile mapenzi yameumbwa kwaajili yako. Unanifundisha kupenda, Nakupenda.โ
Alinitazama kwa hisia, akisema โDont stop, usiache kuongea, usiache kunipenda. Endelea kuongea. Ndeana maneno yako yameumba kitu kipya moyoni. Maneno matamu yanayotoka kwenye kinywa na moyo wa mwanamke mwenye heshima, mtulivu, na mpole kama wewe ni sababu mpya ya mwanaume kuishi maisha marefu. Ndeana, usiache kuniambia namna unanipenda, ili niweze kuishi maisha marefu na kukupenda zaidi unatakiwa uumbe maisha mapya kwa kuniambia Nakupenda kila siku. Nakupenda Ndeana, nimefurahi sana na nakutakia kila jema katika kazi yako. Mungu akubariki.โ
Nikamtazama na kusema โAsante sana, basi naomba niende.โ
Akanishika mkono na kusema โtotoo si tukikubaliana uchoyo ni haramu.โ
Nikacheka na kusema โndiyo baby dini hairuhusu ni haramu.โ
Akasema โsasa mbona unaninyima busu langu.โ
Nikacheka lakini nilimbusu na kisha nilitoka huku akiniambia โNakupenda.โ
Tena wakati sijafika hata mbali alinitumia ujumbe akisema โNdeana wangu, umependeza sana. Umependeza.โ
Nikatazama nyuma na kucheka tu kisha nikaelekea sehemu nahitajika.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 88
Basi niliingia ndani nikasalimia baadhi ya wafanyakazi wenzangu wakawa wananitazama tu wananipandisha wananishusha. Moyoni nikawa najiuliza tatizo hata sielewi. Basi ilinibidi nitulie tu nimtafute Joan, aliniambia yupo chumba cha kubadilishia nguo na vitu kama hivyo. Nikapanda mpaka sehemu ya kubadili nguo. Nilipofika tu kitu cha kwanza nikauliza โKuna nini jamani, ninasalimia watu huko chini hawanijibu wananinyari tu.โ
Joan alimtazama yule dada mwingine na kusema โVumilia tu, na itafika muda utazoea. Watu wamechukia kwanini wewe ndiyo usimamie hili na wakati kuna wakongwe na hawajapata nafasi.โ
Nikavuta pumzi na kusema โMakubwa haya, sasa mimi hapa kosa langu nini?โ
Yule dada mwingine akasema โhata sisi tumewaambia badala yake wakaanza kutusema na sisi na vitu kama hivyo yaani maneno kibao.โ
Nikavuta pumzi na kusema โni sawa hata hivyo hapa ni kazini. Kazi yetu ni kufanya kazi na kurudi nyumbani. Mahusiano mazuri ya wafanyakazi ni muhimu ila hatuwezi lazimisha tusipotakiwa. Hatupaswi kukasirika ila kufanya kazi nzuri. Tuvae tukaanze kazi. Wanatakiwa kujifunza kutoka kwetu na sio kulalamika.โ
Joan alitabasamu na kusema โsahihi kabisa.โ
Basi tulivaa na baada ya muda ilikuja taarifa Boss anatuhitaji chumba cha dharula nasi tulitii. Baada ya kufika mule, ile naingia tu macho yetu yakagongana na kisha akatabasamu kiwizi.
Kisha akawa ananitazama na kunikonyeza. Wale wenye mahusiano ya hivi hapa wanaelewana, na mimi natabasamu ili mradi tu kumchanganya. Kisha nacheka kidogo unajua tena kunogesha penzi letu eenh.
Basi alitoa maelekezo yake kikubwa ilikuwa ni kuhusu wageni, hivyo usafi, utulivu na mambo kama hayo. Basi ndiyo hivyo alipomaliza macho yote kwangu, meneja naye alisema yake kisha walipomaliza wengine wote waliondoka, akabaki meneja, Boss na sisi watatu.
Mimi nilikuwa namsikiliza huku tunakonyezana na baada ya hapo sasa wakati anatoka si akajichanganya akasema โTotoo, Ooh sorry!!, sorry!!, Ndeana all the best na Team yako.โ
Nikashtuka na kisha kuzuga nikajibu โasante sana boss.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 89
Na wengine wakajibu hivyo, kisha Joan akanitazama na kusema โtotoo!!โ
Nikacheka nikisema โYes, dada yangu aliyeniunganisha hapa. Anapenda kuniita hivyo, anapenda sana sasa na Boss kazoea hivyo kutoka kwa dada.โ
Nikazuga zuga pale, meneja akatoa maelekezo na akatuacha. Basi tukabaki tunacheka tu huku nikisifiwa nimependeza nywele ya gharama na vitu kama hivyo huku wakifikiri nimetoka familia nzuri kumbe kumbe familia yangu inanitegemea nipambane mambo yaende sawa.
Chuki, wivu, majungu na vitu kama hivi havikosekani kazini. Kwasababu nimepitapita mahali basi hili halinipi shida kabisa. Halinisumbui mimi watajua wenyewe.
Wageni walianza kufika, nasi tuliwapokea. Wageni hawa walikuwa ni wengi sana. Yaani tofauti na ambavyo tulikuwa tunategemea. Kulikuwa na viongozi wa nchi, kulikuwa na watu wa mataifa mbali mbali. Tulifanya kazi sana siku hii, tulifanya sana kazi. Nakumbuka kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja ndiyo mkutano wao ulikuwa unaisha.
Basi wakati watu wanatawanyika, ninakumbuka niliitwa na huyu mtu mkubwa sana kwenye ule mkutano. Ni mmoja kati ya viongozi wakubwa sana.
Alinisimamisha na aliniambia โAsante sana kwa huduma nzuri, hakika sikuwaza kama Tanzania kuna huduma nzuri kama hizi.โ
Nikatabasamu na kusema โkaribu sana, na sisi pia tunayo furaha kufanya kazi nanyi.โ
Akatabasamu na kusema โhuu hautakuwa mwisho, tutafanya kazi pamoja na nitaleta na wengine. Mnastahili pongezi.โ
Nikatabasamu na kumjibu โtutafurahi sana.โ
Akacheka akisema โUnaitwa nani muhudumu mrembo kuliko wote.โ
Nikacheka na kumjibu โNdeana, naitwa Ndeana.โ
Akasema โwaoo!!, Waoo!!, jina zuri kama wewe ulivyo. Wewe ni mzuri sana. Natumai tutazunguka zaidi. Naitwa Mr Tarick. Here is my busness Card.โ
Nikapokea na kusema tu โNashukuru sana. Asante.โ
Akatabasamu na kuanza kuondoka. Ile mimi nageuka nyuma ili nibebe vitu vyangu nakutana na uso wa Boss, hakuwa na furaha. Niliita โBoss!!โ
Alinitazama na kusema bila hata tabasamu โNifuate Ndeana.โ
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃkivumbi leo๐๐mjue leo ilikuwa nisipost nimebanana hatari ila nilipokumbuka ni haramu weee nikakurupuka๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ป
MWISHO WA SEASON TWO
SEASON THREE IPO WHATSAPP KWA SH 1000 UNAISOMA
๐ต๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐ฝ๐๐
๐๐๐๐ ๐ด ๐๐๐๐ 0743433005 ๐๐๐๐ ๐จ๐ฎ๐ถ๐บ๐ป๐ฐ๐ต๐ถ
๐ผ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐พ๐๐๐๐๐จ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ +255743433005 ๐๐๐๐๐๐๐
๐๐๐๐.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.