𝑺𝒆𝒂𝒔𝒐𝒏 𝒇𝒐𝒖𝒓
Huyu dada alitutazama, alishindwa kuvumilia. Taratibu aliondoka huku anaumia sana. Nilimuonea huruma, ila siwezi kumuachia baby wangu ambaye tunapendana sana. Sisi tulibaki tunapeana busu. Kisha nami nikashuka chini kwaajili ya kwenda kuanza maandalizi yangu ya kwenda mtoko na baby wangu.
Ile nimetoka tu, nakutakana koridoni na meneja anaenda kwa Boss. Aliponiona alianza kucheka akisema “wewe ni mbayaaa, nilijua tu kuna kitu na Boss. Kidogo nijichanganye, ningekosa kazi mimi. Ungeniambia mwenzio.”
Nikajikuta nacheka na kisha alisema “Anakupenda sana, naona na najua hili. Hakika, penzi ni ajabu. Boss wangu na ujeuri wake wote kapenda sasa. Sema nini Ndeana, una faida kubwa sana kwa Hotel yetu. Unatumia vizuri mtandao kuelezea hii Hotel, umeitangaza sana huko mtandaoni.
Hata kuna wateja wakija hapa wanajua ile page yako ndiyo ha Hotel. Hatusemi tu kwakuwa tunakulinda ila mshahara wako utaongezeka. Siri hiyo nakuibia. Endelea kupenda kazi yako. Na kwa taarifa yako kuna kazi zingine zinakuja wale watu wanaleta faida sana kwani Hajakuambia?”
Nikatikisa tu kichwa. Kisha aliniambia “Hongera, mimi nakutakia kila zuri. Ukifanikiwa utukumbuke maskini wenzako.”
Nikacheka tu, kisha nikaendelea kutembea. Meneja anabaki anasema “Ndeana huyo, Mrs Boss, mamaa Stewart. Wewe ni mzuri hata hivyo.”
Mimi nacheka tu.
Nilipofika tu chini marafiki wa kazini walinipa hongera huku wakitaka niwape mbinu na wao wanaume wao wawapende kama mimi.
Nakumbuka nilitabasamu tu huku nikisema “kila mwanaume anazo njia zake za kupenda. Sio wote watapenda au kukupenda kama anavyopendwa mtu mwingine. Muhimu ni wewe kupokea tu namna yoyote ya upendo.
Wapo wanaume wakimya na wapole sana hawaongei, wapo wanaume watakupa tu zawadi, wapo wanaume hata ujumbe hawezi kuandika na akiongea ni dakika moja nyingi. Kazi yako nikufurahia huo upendo jinsi ulivyo. Usije ukamuacha ukasema huyu hanipendi, kwasababu hafanyi moja mbili tatu.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 134
Hata wengine akiongea sana utasikia mimi nakupenda, kamaliza. Elewa hivyohivyo na inabidi kuelewa ufurahie. Furaha ya kwanza inaanzia kwako wewe mwenyewe. Anza kujipenda, vitu unatamani kufanyiwa anza kujifanyia.
Dada yangu aliwahi niambia kuwa huna mtu anakuambia anakupenda. Jiambie wewe mwenyewe Nakupenda sana Ndeana. Unaweza kuonekana kama kichaa ila huu ni upendo wa wewe na wewe. Jiambie maneno mazuri, jiumbie maneno mazuri.
Ndeana wewe ni mzuri sana, imara sana, utafanikiwa sana kwenye maisha yako. Nakupenda sana Ndeana. Jinunulie zawadi baada ya kazi zako tena ikiwezekana funga vizuri sana na wakutumie upokee, jitoe out, kama unapesa kalale sehemu nzuri.
Yote yanawezekana na hii inasaidia kupunguza lawama kwa mapenzi. Kosa kubwa sana kwenye mahusiano ni kulinganisha mapenzi ya mtu mwingine na ya kwako.
Au kutamani mpenzi wa mwenzako kwa kuhisi hata kwako atakuwa kama alivyo kwa mpenzi wake wa sasa. Ni kosa kubwa, kubwa sana. Ni hivyo tu rafiki zangu.Mengine ni mambo ya Mungu wala hakuna kingine.”
Basi walitabasamu wakisema “umesema vyema. Walinisifu na kunipongeza na walisema wananiombea heri nifike mbali na boss wao. Nami nilikubali ingawa sijui haswa nini nafsi zao zinaongea juu yangu.
Niliagana nao na kuingia kwa kile chumba chetu cha kubadili nguo. Joan alikuja na kusema “rafiki yangu wewe kiboko, kwanza video yenu imesambaa status za watu, huko instagram usiseme. Ninafuraha sana.”
Nilitabasamu tu nikisema “hata sina neno.”
Aliniambia Joan “katika watu wana bahati na wewe umo Ndeana. Huyu boss watu kibao walitamani kumpata ila wewe tena bila nguvu na wala huringi boss mpaka anakupigia goti. Kweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana.
Unajua Ndeana yale maneno ya kujipenda pengine labda ndiyo tiba yangu ya kwanza. Ila mimi nimejiweka kutegemewa furaha za watu na mimi kujiona sina bahati. Ila sasa nitabadilika, nitakuwa mpya kabisa kwasababu nampenda sana Joan. Asante kipenzi.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 135
Nilimkumbatia na kusema “safi sana, bila shaka unaendelea vizuri na maisha ya ibada.”
Aliniambia kwa furaha “vizuri sana huwezi kuamini hata baba mtoto alinitafuta baada ya muda wote kupita. Anataka sana kukutana na mtoto wake.”
Nikamwambia “kutaneni. Usiache kusali Joan.”
Alitabasamu na kusema “halafu shoga yako uvumilivu umemshinda leo kaacha kazi .”
Nikashangaa nikisema “wewe unasema kweli?”
Akaniambia “ndiyo hivyo rafiki yangu.”
Nikasema “na haya ndiyo madhara ya mahusiano kazini. Ni vile tu hatuwezi kuzuia. Mungu atusaidie kwakweli. Ila hakupaswa kuacha kazi bali kukubali tu.”
Joan alicheka akisema “utadhani Boss ndiyo mwanaume wake wa kwanza.” Kisha alitoka. Nami nikavuta pumzi na kuendelea na mambo yangu.”
Wakati ndiyo namalizia dada alinipigia simu akiwa na furaha sana aliniambia “wewe mtoto nini kinatokea. Umemfanya nini shemeji yangu hata apige magoti?”
Nikaanza kucheka nikisema “umeona wapi ndugu yangu umeona wapi?”
Alicheka akisema “Mr Fabian, kanitumia akisema mdogo wangu kampigisha goti ndugu yangu ndiyo tunacheka hapa.”
Nikasema “haifai hata kukusimulia kwa simu ndugu yangu. Nakuja nyumbani.”
Alicheka akisema “ndiyo uwahi sasa maana nina hamu ya kujua mimi.”
Nikacheka nikisema “naja leo nawahi kutoka wala usijali.”
Nilikata simu huku nikicheka.
Nilitoka mdogo mdogo mpaka nikafika getini. Wakati natoka tu. Alinitumia ujumbe wa Shukrani kwa zawadi yangu. Vitu vyenyewe vilikuwa hata sio vya kushukuru vile ila
alinishukuru kwa upendo na furaha sana. Nilisoma nikitabasamu, alisema kwa ujumbe “I find myself the luckiest man on earth because you make me feel so.You make me feel so safe and loved and I can’t really help myself from falling in love with you every second of my life..
I love you so so much *Heartbeat*, I love you so much my *Life precious gift*.. Thank you for coming into my life and bringing so much love, smile and brightness..
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 136
You have my heart Ndeana wangu, I love you my amazing Blessing(najiona ni mwanaume mwenye bahati duniani kwasababu unanifanya nijihisi hivyo. Unanifanya nijisikie salama na napendwa na siwezi kujizuia kukupenda kwa kila sekunde ya maisha yangu. Nakupenda sana mapigo ya moyo wangu, nakupenda sana zawadi ya thamani katika maisha yangu. Asante kwa kuja kwenye maisha yangu na kuleta mapenzi, tabasamu na nuru. Una moyo wangu Ndeana, nakupenda sana baraka yangu ya ajabu).
Unatembea na Roho yangu mama, Asante kwa zawadi. Nimezifurahia sana. Unajua sana kwanza umejuaje hata boksa zangu zilikuwa zimepungua.”
Mimi nilikuwa nimenunua boksa za kutosha, nilikuwa nimenunua vest, nilinunua mkanda mzuri, nikanunua wallet yenye maandishi “may this wallet never dry in Jesus name, nikanunua key holder yenye maandishi “Drive safe my sweet person. Nikanunua vikorokoro vingi na picha yetu pale tunakunywa juisi ya miwa picha nzuri sana, tena nilitengeneza kubwa sana.
Nilimjibu kwa uchache “sijafanya kitu kikubwa sana. Maana najua una pesa ya kutosha kununua kila kitu ila nilitaka nikupe zawadi. Nakupenda sana Stewart. Nakupenda.”
Alinijibu akisema “hii picha, ina hadithi ya penzi letu, hii picha inaseka kila kitu. Nashindwa kuacha kutabasamu kila nikiwaza. Sijui uliwaza nini kutengeneza hii kitu. Ila tambua umenipa kitu kikubwa sana. Ndeana unaweza tengeneza nyingine nyingi sana. Nimeipenda sana.”
Nikacheka, kisha alinitumia ujumbe “kama vipi leo tubebee na miguu ya kuku nimeikumbuka sana kwani wanatengenezaje hawa.”
Nikacheka na kusema “naenda kutengeneza nywele. Sitaki kucheka mimi.”
Akatabasamu na kusema “Nakupenda sana, nakupenda wewe mwanamke, nakupenda mno.”
Nami nikamjibu “nakupenda wewe mpuuzi.”
Akacheka tu.
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments