Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 129

21st Aug, 2025 Views 61

๐‘บ๐’†๐’‚๐’”๐’๐’ ๐’‡๐’๐’–๐’“


โ€œTotoo, tunaweza kuondoka sasa?โ€
Nikawatazama wale wafanyakazi wengine namna wanatutazama na nilimtazama My boss na kusema kwa kichwa tu maana aibu zimenijaa nashindwa hata kuinua miguu yangu.

Alinishika mikono yangu na taratibu tulianza kutembea kuelea juu. Ofisini kwake yaani. Nilifika pale na yeye alinikalisha kwa kiti chake, nilikaa kwa kiti cha boss wangu. Mimi mtu wa maisha ya kawaida tu ambaye sio kukaa tu hata kuwa na ukaribu wa huyu mwanaume wa aina hii haikuwa ni kitu cha kawaida ila ndiyo amekua mpenzi wangu. Mbali zaidi kwangu huyu mwanaume hajivuni, linapokuja suala langu haofii kufanya lolote lile.

Alizungusha kiti upande mwingine, kisha neno la kwanza alisema โ€œSijakusaliti Ndeana. Tangu nimekutana na wewe, tangu nitamke neno Nakupenda kwako sijawahi kukusaliti.

Achana na kutamani tu nje, sijawahi hata kuwaza wala kufikiria kwamba mbali yako wewe ninatakiwa kuwa na mwanamke mwingine.

Ndeana, pumzi yangu inayoingia na kutoka, usingizi wangu ninao lala na kuamka, kazi zangu ninazofanya na kila ninapotembea au ninapokuwa ni wewe.

Nakuwaza wewe peke yako, nawaza mwanamke wangu nikupende vipi ili na wewe unipende, penzi letu liwe na furaha. Nawaza nikufanyie nini ili usihangaike nje na maisha haya.

Tafadhali Ndeana, najua usaliti ni nini, najua maana ya kupenda na kupendwa na wewe ndiyo umenifundisha. Nimekukosea kwasababu sikukuambia kuhusu Martha. Ni msunbufu tu ila siwezi kuwa naye.

Sitaki kukiri kila kitu kwako kwa maana unajua tayari nilikuwa mbaya sana. Ila yeye yupo kwaajili ya pesa bila pesa huwezi kuwa naye. Na sijui hata kwanini tangu nimekuwa na wewe kawa msumbufu sana.

Amekuwa akiniambia vitu vingi kuhusu familia yenu na kusema yeye ni bora kuliko wewe. Ila namjua sana, ndiyo maana nikakuchagua wewe. Totoo, dady loves you. Upendo wangu kwako ni upendo wa kweli kabisa.

๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 130

Sikutanii na namaanisha kila kitu. I love you kama namna neno lilivyo. Nakupenda sana, Nakupenda kuliko kitu chochote. Naomba usikasirike katika siku yetu nzuri namna hii. Naomba usikasirike ili tukafurahie hizo siku nilizokuambia vizuri. Ndena Please ongea kitu.โ€

Nilimtazama, mimi tena kutaka kudeka eti nami nimenuna nikaitikia tu โ€œsawa, hakuna shida!!โ€

Akanitazama na kusema โ€œhapa serikali iingilie kati. Ndeana hivi kweli unanijibu hivyo na unataka niendelee kupumua vizuri kabisa. Unakuaje hivi mtoto mzuri, nisamehe mzee wa watu mimi nitajifia bure unajua.โ€

Nikamtazama nikitamani kucheka ila hasira sasa, nilianza kuongea kwa upole maana nilitaka nianze kufoka. Nilikumbuka maneno ya dada yangu kuwa hawa viumbe hawataki kelele na wanawake wengi tuna kelele nijitofautishe nao nisifoke hawapendi kabisa kufokewa anaweza kuondoka na asirudi tena.

Nilivuta pumzi kwa kudeka nikasema โ€œulipaswa kuniambia nikae naye mbali, maana alikuwa anaingilia mpaka maisha yangu binafsi. Na alikuwa akijifanya kuniita wizo na vitu vingine kama hivyo akinichimba. Sasa ndiyo nini hivi.โ€

Akanitazama akisema โ€œnisamehe baby wangu, nimekosa mwenzio. Umenipigisha goti mbele za watu, unafikiri mchezo, niliona wazi nakupoteza. Na sipo tayari kuyabeba hayo maumivu ya kukupoteza kwasababu ninakupenda sana Ndeana.

Huyo sio wifi yako, wala sio rafiki mzuri kwenu. Naomba achana naye, mimi nimezaliwa peke yangu. Ukitaka kuitwa wifi basi niite mimi mwenyewe.โ€
Nikacheka nikisema โ€œsio mzima wewe.โ€
Akasema โ€œwaooo!!, hilo tabasamu, futa basi machozi.โ€

Nikafuta kisha aliniambia โ€œbaby asante kwa zawadi. Mungu akubariki sana. Ingawa unajua kuwa wewe ndiyo zawadi yangu kubwa sana kwenye maisha yangu.โ€
Nilitabasamu na akaniuliza โ€œeenh, umeniletea nini?โ€
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 131

Nikacheka na kusema โ€œhakuna kufungua mpaka mimi niondoke.โ€
Akacheka. Na kisha alikuja pale kwenye kiti, aliniinua mimi, akakaa yeye na kisha alinipakata. Mimi nikawa nafurahi tu maana kupakatwa nako ni raha haswa akupakate mtu anayekupenda sana na wewe unampenda sana.Ingawa huku moyoni ninajisikia vibaya sana. Maana wivu uliwaka baada ya kuona wizo wa mchongo akipambana kuvua nguo na kulazimisha busu ninalopewa mimi na yeye apewe.

Alinifungua droo na kusema โ€œnimekununulia zawadi. Ila Sharti lake kwa mwanzo tunatumia wote.โ€
Nikasema โ€œsasa zawadi ni yangu tunatumiaje wote.โ€
Akanitazama akisema โ€œuchoyo si ni haramu baby!!โ€
Nikacheka tu. Alitoa kitu cha kuchekesha kwa sisi watu wazima. Alitoa pipi, tena pipi kijiti . Kuna hizi pipi zilikuwepo kipindi fulani hivi zina umbo la love halafu zina radha tofauti tofauti. Na hizi pipi hata ile siku alinipeleka kununua vitu na hii alininunulia. Ni tamu sana. Nilimtazama na kucheka nikusema โ€œkwahiyo umenunua moja tu na unajua ni tamu.โ€
Akasema โ€œndiyo ujue kuwa sio malaki, mamilioni na pesa nyingi zitafanya ufurahie penzi lako. Haya sasa fungua tule.โ€
Nikacheka tu, nikafungua basi nikawa nakula na kisha namlisha. Ananitazama anasema โ€œafu wewe unanyonya sana kuliko mimi.โ€
Nami namwambia โ€œaku wewe hapo ndiyo mlafi.โ€
Akaniambia โ€œbasi nipe pipi yangu!โ€
Nakatalia, si akaanza kunitekenya. Basi nikaanza kucheka, yaani huko ofisini sijui kwasababu muda mwingi yupo peke yake tu sio ofisi za kuingia sana watu. Nilicheka mpaka nakaa chini. Nacheka mpaka machozi. Aliniinua na kusema โ€œbasi basi totoo, usije ukapaliwa.โ€
Nikamtazama na kusema โ€œnalipa, nitalipa tu.โ€
Alijipa ushindi akisema โ€œAnd the winner is Mr Stewart.โ€
Nikamtazama kwa kudeka tu.

Basi akacheka na kisha aliniambia โ€œsikia, nataka uende pale kwa aunt. Katengeneze nywele vizuri. Kisha mimi nitakufuata nyumbani. Nataka upendeze sana. Nataka utokelezee. Nitakufuata nyumbani, au nitakupeleka. Sijui nina kazi hapa ila unaweza kwenda tu hakuna shida.โ€
๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 132

Nilitabasamu, mara akashika simu yake. Baada ya muda akaniambia โ€œNjoo uone, unajua pale nalia nilikuwa nachukuliwa video. Basi Kaka Fabian kanitafuta hapa mpaka page za umbea wameshare.โ€
Nikasema โ€œwewe usiniambie!!โ€

Akatabasamu akisoma comment anasema โ€œwasichana wengi wanateseka sana na mapenzi. Ukiona Comment zao utajua. Mpenzi tuwaombee na wao wayapate mapenzi kama sisi.โ€
Nikacheka nikisema โ€œhakika, tuwaombee na wao wafurahie.โ€

Tukacheka na alisema โ€œeenh Mungu hawa watu wameshare sana itakuwa simu zao zimejaa lile tukio. Sasa hata najali, nasijali wala nini. Najali nini na nilikuwa natetea utamu wangu wa maisha. Wewe ni tamu yangu Ndeana, nitakutetea kivyovyote hata kama itagharimu maisha yangu ila nataka wajue kuwa wewe ni wangu. Na nakupenda sana.โ€

Kabla sijajibu, mlango uligongwa. Aliruhusiwa wakati huo mimi nimesimama na Boss wangu amekaa. Akaingia yule dada ambaye ananichukia. Boss alipomuona alinitazama na kuuliza โ€œwewe tena?โ€

Sasa nikaona ni bora niwaache niondoke zangu. Nikafika mlangoni na pipi kijiti yangu. Boss akaita โ€œtotoo, njoo mara moja.โ€

Nikarudi na kisha alimtazama yule dada alisema โ€œhuyu ni Ndeana, na ndiye mke wangu mtarajiwa. Unataka kufanya kazi kwa amanj basi sitaki kelele zote huko kazini kwenu. Unavyoniheshimu ndiyo umuheshimu. Sitaki kusikia lolote. Na kwasasa huruhusiwi kuja kwangu bila kupita kwa meneja.

Nitamwambia awatangazie maana naona mmenizoea sana. Mipaka, mimi ni Boss wenu, mbali na hilo nina familia yangu naheshimu. Kwahiyo kama ni kazi ongea, kama ni ujinga wako wa kila siku naomba uondoke eneo hili sasa hivu.โ€

Huyu dada aliinamisha kichwa chake chini kwa aibu. Na alinitazama kisha akamtazama Boss akisema โ€œlakini hata mimi Nakupenda.โ€

Eenh Mungu nipe uvumilivu ndiyo nilikuwa nasema moyoni huku natazama pembeni kama nicheke vile. Kumbe hata Stewart alikuwa anajisikia kama mimi. Tulipotazama tukajikuta tunacheka halafu Stewart alisema โ€œtoto, sasa unaondokaje, majaribu ni mengi. Nipe busu nishibe nipate nguvu ya kupambana.โ€

Malizia season four kwa sh 1000
No 0743433005 iko WhatsApp

๐‘ต๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ ๐’š๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’๐’Š๐’‘๐’ ๐‘ฝ๐’๐’…๐’‚๐’„๐’๐’Ž ๐‘ด ๐’‘๐’†๐’”๐’‚ 0743433005 ๐’‹๐’Š๐’๐’‚ ๐‘จ๐‘ฎ๐‘ถ๐‘บ๐‘ป๐‘ฐ๐‘ต๐‘ถ
๐‘ผ๐’Œ๐’Š๐’๐’Š๐’‘๐’‚ ๐’๐’Š๐’„๐’‰๐’†๐’Œ๐’Š ๐‘พ๐’‰๐’‚๐’•๐’”๐‘จ๐’‘๐’‘ ๐’Œ๐’–๐’‘๐’Š๐’•๐’Š๐’‚ ๐’๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ +255743433005 ๐’๐’Š๐’Œ๐’–๐’‰๐’–๐’…๐’–๐’Ž๐’Š๐’†.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

๐‰๐€๐Œ๐€๐๐ˆ ๐๐Ž๐’๐’ ๐Œ๐ˆ ๐๐€๐Ž๐๐€ ๐€๐ˆ๐๐” ๐Ÿ’๐Ÿ™ˆ๐Ÿ’ž: 129  >>> https://gonga94.com/semajambo/jamani-boss-mi-naona-aibu-129

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest