Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Nilicheka na kumwambia nyoosha barabara wewe... Inaendelea... Sehemu Ya 7

31st Jul, 2025 Views 5



Tulifika hadi pale aliponielekeza mwanamama sakina, Nilimlipa wa boda akaondoka. Nikaingia kwenye baa ambayo amenielekeza nikamkuta mwanamama sakina akiwa anakunywa soda ya Pepsi, Nilimtania kuhusu utamu wa Pepsi, Lakini haikuwa shida nikaagiza na mimi Coca-cola bariidi,

Tulianza maongezi na mwanamama sakina, Yeye alikuwa na maswali mengi ya kuniuliza lakini mimi nilikuwa namuuliza mara moja moja sana, Tuliongea mambo mengi lakini mwanamama sakina yeye alionekana kuniuliza sana kuhusu mambo ya biashara, Aliniuliza kama kuna biashara nafanya au kama nilishawahi kufanya biashara, Lakini mimi nilimwambia biashara bado sijawahi kujaribu labda kama kufanya kazi ndogo ndogo. Mwisho wa maongezi mwanamama sakina akawa amenikubalia lile ombi langu la kutaka kuwanae kimapenzi, Lakini akaniambia, (nimekubali ombi lako la kuwa na mimi lakini naomba sana mapenzi yetu yawe ya siri kiasi kwamba mimi na wewe pekee ndio tuwe tunajuwa kinachoendelea) Nikamwambia usijali kuhusu hilo. Lakini niliwaza kwanini iwe siri.

Kuanzia hapo mimi na mwanamama sakina tayari tukawa wapenzi. Lakini kutokana na kwamba alikuwa na haraka akasema kwa leo tuishie hapa lakini nitaangalia muda mzuri wa kuja kuburudika na wewe,sababu hata mimi nilikupenda toka siku ya kwanza kukuona. Niliushika mkono wa mwanamama sakina na kumbusu, Hakika alifurahi na kuniambia raha kama hizi ninamuda sijazipata. Nilimwambia upo na mimi usijali utazipata.

Muda wa kuondoka ulifika nilimsindikiza mwanamama sakina hadi ndani ya gari lake, Kisha alitoa kiasi cha pesa na kunipatia kama matumizi, Sikutaka hata kuhesabu. Tuliagana yeye akaenda kwake na mimi nikarudi nyumbani. Lakini sikumuuliza kama ameolewa au anawatoto ila aliniambia anaishi mjini. Lakini kwa upande wangu huko mjini ndiko anakosomea tina, Na dada yangu pia ameolewa huko.

Mimi nilifika nyumbani mida ya usiku lakini nilikuwa na furaha sababu pia nimepewa pesa za kutosha, ilikuwa kiasi cha laki moja hivi, Nilijiuliza kama leo tu nimepewa laki moja je siku nimelala nae si atanipa hata milioni. Nilijaribu kumpigia simu ili nimuulize kama amefikia salama lakini simu ikawa haipatikani.

Nililala asubuh palikucha nikafanya kazi za nyumbani, Ilipofika mida ya jioni nilielekea mazoezini lakini pia siku hiyo tulikuwa na mechi ya ushindani, Diwani wa kijiji chetu aliandaa mbuzi ili atakayeshinda ataondoka na mbuzi, Tulicheza mpira kipindi cha kwanza kilimalizika bila kufungana, Tuliingia kipindi cha pili lakini hadi dakika ya 90 matokeo ni bilabila,

Refa akaongeza dakika tatu, Lakini ndani ya zile dakika tatu nilipewa pasi moja nzuri niliiunganisha hadi golini, Watu Gooool goool tulishangilia, Lakini wale wapinzani wetu wakakataa wakasema goli limefungwa kimakosa. Ikatokea kutokuelewana baina ya wachezaji hatimaye ikaanza vurugu, Ikawa ni kukimbizana ilibidi niwahi kwenda kuchukuwa simu yangu na vitu vyangu na kuanza kukimbia. Lakini wakati nakimbia kuondoka maeneo yale nilianza kucheka pale nilipomuona golikipa wetu anakimbia huku amebeba mbuzi begani, Kumbe golikipa wetu aliona hatuwezi kuondoka kizembe hivyo alipita na mbuzi wa mashindano.

Kesho yake asubuh ilibidi tualikane wote tuliokuwa uwanjani, Tulikusanyika sehemu moja na kushauriana tumchinje yule mbuzi tupate supu na kila mmoja aendelee na mambo yake, Lakini pia alikuja Diwani wa kijiji chetu akatusihi tusiwe tunafanya fujo kwenye sehemu za michezo.

Tulipomaliza kunywa supu wakati tunaondoka kuelekea nyumbani rafiki yangu mmoja akawa ameniambia kwamba tina amekuja likizo ya muda mfupi, Nikasema sawa maana niliona kama ananitania. Ilipofika mida ya jioni nikaona nitembelee mitaa ya kwao na tina, Ghafla nilikutana na tina uso kwa uso, Tina alikuwa amebadirika sana ule uzuri wake wa mwanzo ulikuwa umeongezeka mara mbili, Dah,,, nilishangaa sio kwa uzuri ule, Maana tina amezidi kuwa mrembo. Nikasalimiana nae nikamuuliza umekuja lini, Akasema nina siku tatu nipo nyumbani, Niliongea na tina lakini alikuwa anaonekana kama kunikataa kiaina, Ila sikujali hilo,

Lakini wakati naongea na tina simu yangu ilipigiwa, Niliitoa mfukoni kuangalia ni mwanamama sakina amepiga, Nilipokea na kumwambia nina kazi kidogo nitakupigia nikipunguza kazi, Sakina akaniambia pole na kazi lakini usisahau. Nilikata simu. Tina akasema kumbe siku hizi una simu,ni nani huyo unayemwambia utaongea nae badae, Nikamwambia ni baba kuna sehemu alinituma. Tukamalizia maongezi na tina tukaagana kwamba tutaonana kesho.

Nilipopata muda nilimpigia mwanamama sakina lakini simu iliita bila kupokelewa, Badae akanitumia ujumbe. Kesho Tukutane kwenye ile baa ambayo tulikutana mara ya kwanza. Nikamwambia sawa. Lakini wakati huo tayari moyo wangu umesharudi kwa tina, Ukizingatia tina amerudi amenona kweli shepu sio ya kutafuta mtoto ana kila kitu.

Kesho ilipofika kabla sijaenda kuonana na mwanamama sakina. Kwakuwa nilikuwa bado nina pesa ile ambayo alinipatia mwanamama sakina ikabidi ninunue simu na kumpeleka tina maana niliona nahangaika sana kumpata. Tina alifurahi kama kawaida yake maana nilimsajilia mpaka laini, Sasa maongezi mimi na tina yakawa ni muda wote.

Muda ulipofika wa kwenda kuonana na mwanamama sakina nilijiandaa kama kawaida yangu sababu niliamini mwanamama sakina atakwenda kunipatia kile ambacho amekuwa akiniahidi siku nyingi, Nilijipanga kwenda kufurahi nae kitandani. Nilifika hadi kwenye ile baa nikaiona gari ya mwanamama sakina, Lakini cha ajabu nilimkuta mtu mwingine kabisa ambaye simfahamu, Na alikuwa ni mwanaume.

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Nilicheka na kumwambia nyoosha barabara wewe... Inaendelea... Sehemu Ya 7  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-nilicheka-na-kumwambia-nyoosha-barabara-wewe-inaendelea-sehemu-ya-7
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest