Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MKE ALIYECHUMA NAYE MALI | EP 13

27th Jul, 2025 Views 4



Majira ya saa 12 jioni, Garma alikuwa anaingia nyumbani kwake ๐Ÿš—. Baada ya kufunguliwa mlango na mama yake, aliingia ndani na kusimamisha gari katika eneo lake la kila siku. Alishuka huku akionekana kama mtu aliyechoka sana ๐Ÿ˜ฉ.

Alimtazama mama yake na kujiandaa kumpa salamu, lakini hata hakufanikiwa kufanya hivyo kwani mama yake alikuwa wa kwanza kuzungumza.

โ€œNilikuambia kunguru hafugiki, lakini hukutaka kunisikia ๐Ÿฆ,โ€ alisema mama yake kwa ukali.

โ€œKwanini?โ€ Garma aliuliza kwa mshangao.

โ€œSi huyu kiumbe wako unayemfuga kila siku kwa kumuona mwema ameondoka hapa ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ.โ€

โ€œKha! Ametoka? Ameenda wapi?โ€ ๐Ÿ˜ณ

โ€œKwani nawe siku hizi kichwa chako hakina akili au? Jana nilikuambia anataka kwenda wapi?โ€ Mama Garma alimzodoa mwanae bila haya.

Garma alivuta kumbukumbu na kukumbuka. Ghalfa, ndita zilitengenezwa kwenye paji la uso wake ๐Ÿ˜ .

โ€œKaondoka hapa na nani?โ€

โ€œNaelewa basi. Nimeona tu ametoka hapa, tena kanichimbia mkwara wa kufa mtu, akasema โ€˜Wewe mama lazima nikuueโ€™ ๐Ÿ˜ค. Kama unavyojua lile lisauti lake baya kama Burna Boy,โ€ mama yake alisema huku akiigiza sauti ya Mayner kama ya msanii kutoka Nigeria ajulikanaye kama Burna Boy ๐ŸŽค.

โ€œAise! ๐Ÿ˜ก Nitakuja nipige, niue halafu nifungwe. Yaani anakwenda kwa mganga? Uchawi! Uchawi tena? Huu uganga utamfikisha wapi? Dadeki zake! Ngoja kwanza!โ€ alisema Garma kwa jazba huku akitoa simu yake ๐Ÿ“ฑ.

Alicheza nayo na kumpigia Mayner, lakini simu haikupokelewa โ˜Ž๏ธ. Alipopiga kwa mara ya pili, bado simu haikupokelewa.

โ€œHawezi kupokea. Anajua ulimkataza na huko aliko anahisi tayari umeshajua,โ€ mama alisema kwa kejeli.

โ€œMama, hakuna shida. Unajua kila siku nakuona wewe ndiye mkosefu, kumbe huyu mbwa ndiyo mshenzi. Sasa kwa waganga kaenda kufanya nini jamani? Duh!โ€ ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ

โ€œUtajua mwenyewe. Ngoja nikale zangu. Basi hapo aje halafu umchekee. Wallah nitakubutua wewe pamoja na yeye!โ€ ๐Ÿ˜ค

โ€œMama, hata usinifundishe namna ya kupiga. Hii kazi niachie. Najua namna ya kumfanya. Nitamโ€™bumunda, hatokaa aamini maisha yake yote!โ€ alisema Garma huku akiingia ndani kwa hasira ๐Ÿ’ฅ.

---

Wakati huohuo...

Rasma na Mayner walikuwa njiani. Rasma aliendelea kuzungumza na Mayner lakini kimya kilitawala. Alionekana kama mtu aliyepoteza mwelekeo kabisa, akili yake ikiwa mbali ๐Ÿ˜”.

โ€œKama hutaki kusema au kuzungumza lolote, basi tulikuja huku kufanya nini?โ€ aliuliza Rasma kwa wasiwasi.

โ€œKujua kwamba naumwa, ila sio kuhama pale nyumbani. Natoka naenda wapi, Rasma?โ€ Mayner alijibu kwa jazba huku machozi yakimdondoka ๐Ÿ˜ข.

Kila kitu alichokuwa akikipitia kilizidi kumuumiza moyo. Hakuwa tayari kumuacha mwanaume aliyemchagua kwa moyo, kisha aanze maisha mapya kama vile hakuna kilichowahi kutokea. Badala yake, kama kifo kingekuwa mbele yake, basi alikuwa tayari kukikumbatia โšฐ๏ธ.

โ€œSijui ni wapi unashindwa kuchukua maamuzi. Unadhani mama atashindwa kukuua endapo ukiendelea kukaa pale nyumbani?โ€ Rasma alihoji kwa sauti ya uchungu.

โ€œUnajua nawaza mengi... hasa nikikumbuka kwamba sina pa kwenda. Unakumbuka nilivyouza nyumba ili kuongeza mtaji wa kampuni? Sasa naenda wapi mimi? Muda mwingine si mapenzi tu yanayonifanya nikakae pale, bali ni kukosa sehemu ya kwenda ๐Ÿ˜”,โ€ alisema huku machozi yakiendelea kumwagika ๐Ÿ˜ญ.

Rasma alitulia kwa dakika chache, kisha akaangaza macho huku na kule kana kwamba anatafuta majibu ndani ya nafsi yake. Kisha akasema:

โ€œTutaanza maisha mapya kwangu. Utaishi kwangu, na kama utapata mtu sahihi wa maisha yako, basi utaondoka tu ๐Ÿ .โ€

โ€œKukaa kwako? Si bora niende kukaa kwa Garma?โ€ ๐Ÿ˜’

โ€œKwanini?โ€

โ€œBado mama yako atazidi kunisakama.โ€

โ€œSidhani. Mama anaweza kufanya ujinga wote, lakini si kwangu. Mimi namweza mama. Huoni hata navyojibu ni vile ambavyo najisikia?โ€ alisema Rasma kisha akafikiria kidogo ๐Ÿค”. โ€œAu tukaongee na Laila? Unasemaje?โ€

โ€œLaila naye maisha yake ni hovyo. Pale kwake yupo na mama yake, kila siku wanajibizana. Sitaenda. Bora kidogo kwako,โ€ alisema Mayner kwa sauti ya huzuni.

โ€œKama ni hivyo, sawa. Hakuna shida kabisa,โ€ alijibu Rasma kwa utulivu.

Walifikia makubaliano ya kuishi nyumbani kwa Rasma. Walipanga kwenda nyumbani kwa Garma kuchukua baadhi ya vitu, kisha waondoke kuanza maisha mapya ๐Ÿงณ. Ingawa uamuzi huo ulikuwa mgumu kwa Mayner, hakuwa na jinsi zaidi ya kuukubali.

Alijiona anaenda kuanza maisha ya mbali na aliyempenda. Alijiona anakwenda kuvuna aibu ya kushindwa kuolewa ilhali ndoa ilikuwa karibu sana โ€” zimebakia kama siku 10 tu ๐Ÿ’”. Kadri alivyofikiria, ndivyo machozi yalivyozidi kumtoka.

Moyo wake ulimuumiza sana ๐Ÿ˜ญ. Macho yalikuwa mekundu, misuli ya kichwa ilijitokeza kwa hasira. Kamasi nalo halikubaki nyuma โ€” lilimwagika kwa wingi kuonesha dhahiri kuwa alikuwa katika hali ya kuvunjika moyo sana ๐Ÿ˜ž.

Walifika nyumbani kwa Garma na kusimamisha gari nje. Wakapiga honi ๐Ÿš˜. Dakika mbili baadaye, mlango ulifunguliwa na mama Garma ambaye alikuwa amefura kwa hasira ๐Ÿ˜ .

Mayner na Rasma walishuka bila hata kuingiza gari ndani. Mama Garma aliona ana kila sababu ya kuuliza:

โ€œMbona gari ipo nje? Mganga amewaambia hivyo au?โ€ ๐Ÿคจ

Swali hilo lilijibiwa na Rasma kwa dharau:

โ€œKaa hapo ulinde, wewe si mchawi?โ€ ๐Ÿ˜’

โ€œUnasemaje?โ€ Mama alifoka kwa hasira.

โ€œUmesikia,โ€ alijibu Rasma kwa jeuri, kisha akaingia ndani, lakini mama alimziba Mayner geti ๐Ÿšช.

Bahati nzuri, Rasma alikuwa ameingia. Mayner alibaki nje. Walitazamana na mama Garma kwa sekunde kadhaa, kisha mama Garma akasema:

โ€œInamaana wewe ndio unamchukua mwanangu na kumpeleka kwa mganga?โ€

โ€œNiache bwana, wewe vipi?โ€ ๐Ÿ˜ค alijibu Mayner huku akitaka kuingia ndani, lakini mama Garma alimshika mkono kwa nguvu.

Kitendo hicho kilisababisha kama shoti fulani โ€” mama Garma akalalamika, โ€œMamama!โ€ ๐Ÿ˜ตโ€๐Ÿ’ซ kisha akamuachia haraka.

โ€œEndelea kunishika. Si unapenda kushika shika watu?โ€ Mayner alisema kwa kejeli, kisha akaingia ndani kwa hasira.

Kulitoka msonyo mmoja mtakatifu uliojaa dharau ๐Ÿคฏ. Rasma aliyekuwa ndani aligeuka na kumuona Mayner akiingia, lakini kabla hajamaliza kushangaa, alikutana na kaka yake โ€” Garma โ€” aliyekuwa amefura kwa hasira, akiwa ameshika mkanda mkononi ๐Ÿชข.

โ€œMlienda wapi?โ€ aliuliza Garma kwa ukali.

โ€œWapi kufanyaje? Yaani mbona sielewi?โ€ Mayner alijibu huku akitaka kupita aingie ndani.

โ€œNani unamjibu hivyo?โ€ Garma aliuliza kwa jazba, kijasho kikiwa kinamtoka ๐Ÿ˜ค.

โ€œBwana, nenda kachukue vitu vyako tuondoke,โ€ alisema Rasma kwa sauti ya amri.

โ€œNawe dada unaungana naye huyu?โ€ Garma aliuliza kwa mshangao.

โ€œMuache aondoke tu. Hatuwezi kukaa na mtoto mchawi,โ€ mama Garma alisema akiwa mlangoni.

Kauli hiyo ilimchoma Mayner sana ๐Ÿ˜ก. Alirudisha tusi kama lilivyo:

โ€œNani mchawi? Mchawi ni wewe uliyemla mwanangu!โ€

Kutamka kauli hii ilikuwa ni kosa kubwa... kosa ambalo kama angejua, asingelifanya kwa siku ile ๐Ÿ˜ถโ€๐ŸŒซ๏ธ.

ITAENDELEA...

Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MKE ALIYECHUMA NAYE MALI | EP 13  >>> https://gonga94.com/semajambo/alifirisika-baada-ya-kumuacha-mke-aliyechuma-naye-mali-ep-13
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest