Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

KATIKATI YA CHUMBA CHANGU KULIKUWA NA KABURI Sehemu ya nne.

27th Jul, 2025 Views 6



Siku ile sikuwa na namna ilibidi niwe mpole kwa Mama, nikajirudi kwake kwa kumuomba msamaha kuanzia yeye, mume wangu pamoja na wifi yangu. Ilinilazimu kufanya hivi maana sikuwa na jinsi ingawa nilikuwa naumia moyoni lakini ningefanyaje endapo kama nilitaka kumuaminisha Mama kwamba sikuwa na nia mbaya na wala sikutaka kusema lolote baya kuhusu Mume wangu na mpango wake wa kutaka kumuua.

Nakumbuka wiki moja ilipita tangu kutoka katika marumbano, Mama aliendelea kuishi pale nyumbani huku akiwa na furaha tu. Walikuwa wakiongea na Sofia, wakipiga story na kupanga mambo mbalimali. Nami nilianza kuona kwamba huenda kulikuwa na utofauti pale nyumbani, huenda hata wao wenyewe wameona umuhimu wa Mama.

Maisha yalirudi kama mwanzo, mume wangu alikuwa akimpenda Mama yangu. Alikuwa akimthamini na kumchukulia kama mwanamke ambaye amemletea mke mwema ambaye ni mimi. Sasa mambo yakabadilika, kubadilika kwake yalianzia kwa Mama mwenyewe ambapo siku moja tulikuwa tumekaa tunakula.

Nakumbuka ilikuwa tarehe 20-07-2019, tukiwa katika meza ya chakula kila mmoja akifurahia chakula kile. Mama aliuliza swali.
"Zamda, hivi hujachoka hili jina? “
“Unamaana gani Mama?”
“Mh! Nakushangaa unavyoitwa Zamda, Zamda halafu upo tu yaani unafurahi. Mie la kwangu nimeshalichoka sasa" sikumwelewa alikuwa amemaanisha nini lakini niliweka kijiko katika sahani kisha nikafunga swala na na kumtazama Mama, nikamuuliza
"Bado sijaelewa, una, unamaanisha nini Mama?"
"Umri wangu sasa hivi umekwenda, naumwa mara kwa mara. Kwanini usimlete mjukuu wangu" alisema Mama. Nikajua kwamba wimbo mpya wa kudai mtoto mle ndani lazima ungeanza, nilihisi hivyo kwa aslimia zote.

Nilishusha pumzi nzito kisha nikamtazama mume wangu ambaye alitingisha kichwa chake juu chini, chini juu kuhashiria kwamba alikuwa akiungana na Mama. Nilimtazama mara mbili mara tatu kisha nikasafarisha macho hadi kwa Wifi, naye pili nilimtazama. Niliona naye akiweka tabasamu kisha alisema.
"Bora mama umesema sasa"
"Enh! Acha niseme maana nimechoka, nimechoka haswa yaani Mie nimeshachoka. Nataka kuitwa Bibi fulani ila hadi leo naitwa Mama Zamda, Maam Zamda hadi nachoka sasa. Kwani unataka hili jina linifie enh?” Mama alikuja juu
“Mama kwanini unashindwa kunisiliza, nipe basi nafasi na mimi nizungumze”
“Ipi? Yakuniacha mimi nachekwa au kuna nyingine? Kuna nyingine nakuuliza maana wenzangu wote niliozaa nao pamoja, sasa hivi wana wajukuu kasoro wewe tu tena wengine ni wakubwa"
"Mama” Niliongea kwa hasira kidogo la
“Sio Mama, namtaka mjukuu wangu”
“Mtoto ni mpango wa Mungu"
"Acha kelele zako bwana, toa hicho kipandikizi mzalie Kazumari si ndio Baba?" Mama alimuuliza Mume wangu. Niliona Mume wangu akiitikia huku akiweka sura ya upole kabisa.

Kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana, uso wangu uliweka huzuni. Hamu ya kula chakula ikaniishia hapo, nilijua nini kinafuata maana ni mara nyingi sana nimesikia ndoa zikivunjika kuhusu kukosekana kwa mtoto. Moyoni nikajisemea "ni kipi haswa ambacho Mama anakitafuta? Kwanini asingeniambia wakati tupo wawili hadi tupo wote katika chakula, yaani mambo ya kuongea mimi na yeye anayaleta hadi kwa meza kweli jamani?"

Nilishindwa kuelewa lakini baadaye nilifunika kombe, nikasema acha maisha mengine yaendelee. Nikiwa kama mwanamke mnyenyekevu niliwaahidi kwamba Mwaka hauwezi kuisha kabla sijawapatia mtoto. Nilisema hivyo ingawa sikuwa na uhakika sana ila niliona ili ile mada isiwe kubwa sana basi natakiwa kuwaambia vile.

Hatimaye mwezi wa saba ukapita, ukaingia wa nane hadi wa tisa ukamalizika. Mtoto wa kike sikuwa na dalili ya mimba, sasa kelele ambazo zilikuwa zimepoa zikaanza tena. Safari hii alikuwa ni mume wangu ndio ananipigia kelele akisema.
"Namtaka mtoto, namtaka mtoto" nilikuwa njia panda, nikawa nimechanganikiwa mno. Zilikuwa hazipiti siku mbili kabla sijaubiriwa mahubiri haya ama wimbo wa nataka mtoto.

Moyoni nikawaza, nikasema natakiwa kumshirikisha rafiki yangu Debora kwakuwa huyu ndio alikuwa mtu ninayemuamini. Nilifunga safari na kwenda kwake kisha nikamwambia kila kitu kuhusiana na shida yangu, nilimwambia ukweli na maisha yalivyo tangu Mama kubakia pale nyumbani.

Debora aliniambia kwamba nimpe wiki moja baada ya hapo atanitafutia Daktari ambaye angeweza kuniambia mambo mbalimbali. Kwakuwa nilimwamini Debora, basi nilirudi zangu na kusubiri hadi hiyo wiki moja ilipofika. Tulienda kwa Daktari ambako tuliongea naye, vipimo vikafanyika huku akiniambia nirudi siku ya pili.

Siku ambayo nilipanga kurudi ilikuwa ndio siku niliyompoteza Mama yangu, Mama aligongwa na gari asubuhi wakiwa wanakwenda kwenye mazoezi yeye na Sofia. Sijui ilikuwaje lakini taarifa ya msiba ilinifikia nyumbani. Nilililia kama mwanamke, nililia kama mtoto. Unajua hata kama alikuwa amezeeka lakini bado nilihitaji kumuona lakini ndio hivyo, Mama akatangulia mbele za haki (nifupishe)

Baada ya mazishi ya Mama ambapo tulimzika kijijini, nilirudi zangu nyumbani lakini nakumbuka kule kijijini watu karibu wote niliokuwa nakutana nao ama tunakutana nao walikuwa na watoto wao. Wengi wao walikuwa ni rika kama langu, naweza sema nilicheza nao.

Hii ikafukua kaburi la kudiwa kwa mtoto, mtoto alianza kudaiwa sio usiku wala asubuhi wala mchana. Ilikuwa nikimpa salamu mume wangu, swali la kwanza lilikuwa 'unazaa lini?' tena ilifikia kipindi akawa ananitusi na kuniita majina ajabu kama Malaya na majina mengine ambayo yeye alikuwa akiyajua na kuona yangenifaa kwa wakati huo. Niliumia moyo, sikuelewa kwanini nimekuwa nikilazimishwa kusikiliza wimbo ambao naupenda lakini katika nyakati ambazo hazikustahiki.

Ikawa kama nikienda kazini na kurudi basi bado mume wangu alikuwa na maswali kwa kwenda mbele, wakati mgumu ukawa upande wangu. Wifi naye akaungana na mume wangu katika kunisomea risala. Asikwambie mtu kwa mwanamke kosa vyote katika ndoa lakini sio mtoto, sio mtoto kabisa maana waliniita mgumba na matusi ya nguoni tena muda mwingine walisema kwamba nimetoa mimba ndio maana sina uwezo wa kushika.

Kisanga na maswali ya nazaa lini yaliendelea hadi mwezi wa 10 ukaisha. Ulipoingia mwezi wa 11 nilirudi tena kwa Daktari ili kuchukua vipimo vyangu, nilipofika akaniuliza ilikuwaje hadi sikwenda siku iliyofuata na maswali kadha wa kadha nami nilimwelezea kila kitu. Uzuri ni kwamba alinielewa kisha akaniambia kwamba sina tatizo lolote, mwili wangu upo tayari kuzaa ni mimi tu ndio natakiwa kujipanga.

Basi Majibu yalipotoka ni kwamba yakanichanganya na kunilewesha kabisa kama mhitimu wa chuo aliyeahidiwa pindi akiwa chuo kwamba kazi ipo asome tu halafu baada ya kumaliza chuo, mtu aliyemuahidi kazi asionekane. Ndivyo ilivyokuwa kwangu. Siku hii nililewa haswa, tena nikanyong'onyea. Nilikumbuka matusi ambayo nilipewa na Mume wangu, niliishia kulia huku nikiwa katika gari.

Niliona sasa nina kila sababu ya kumshirikisha Debora juu ya mjibu yale. Nikafunga safari hadi nyumbani kwake, nilipofika nilimweleza kila kitu. Alinishauri kwamba huenda tatizo halipo kwangu bali yupo nalo Mume wangu kama inawezekana basi tukafanye vipimo wote kwa pamoja.

Niliona ni ushauri mzuri na napaswa kuufanyia kazi, nilipoondoka kwake. Nilirudi zangu nyumbani, nikapika na kuoga kisha muda wa chakula ulipofika tulikula vizuri na usiku tukiwa kitandani, nilimshirikisha mume wangu kwenda kupima huku nikimficha kwamba mimi nimeshapima tayari. Kazumar alinielewa vizuri tu, ila kunielewa kwake kulikuwa kwa mashaka.

Asubuhi ilipopambazuka tuliondoka na kwenda hospital tukapima na majibu tuliambiwa tufuate siku ijayo yaani kesho yake. Tuliporudi nyumbani, niliona mume wangu akiwa na mashaka hivi lakini muda mwingi alikuwa ni mtu wa kuchezea simu yake. Alikuwa akiwasiliana na ndugu yake ila kwa wakati huo sikujua.

Kumbe mambo yalikuwa hivi, miezi sita nyuma yaani mwezi wa tano. Mume wangu alikwenda kwa mganga ili kujiongezea umaarufu pamoja na mali. Alitaka kuzidisha nyota yake ya Ng'e ili ang'ae zaidi katika biashara. Mpango huu alimshirikisha ndugu yake ambaye ni Sofia. Mganga aliwaambia kwamba ili wafanikiwe wanahitaji kumtoa mtu mmoja kafara.

Nao katika kutazama nani ambaye anatakiwa kutolewa kafara hawakumuona mwingine bali ni Mama yangu lakini kwa bahati mbaya walichelewa kumuua kwa sababu ambazo nimekueleza hapo kabla. Kushindwa kumuua huku kuliwafanya miezi miwili kurudi tena kwa Mganga. Pindi waliporudi waliambiwa kwamba anahitajika mtoto lakini mtoto huyu anatakiwa kutoka katika damu zao. Damu hizi ni lazima Kazumar azae na Mama yake au Ndugu yake ambaye ni Sofia.

Haya ndio masharti waliyokapewa ambapo yalikuwa magumu kwa upande wao na waliambiwa kwamba wahakikishe kwamba wanazaa hata kabla mimba inapatikana hata kabla ya mwaka kupinduka. Vinginevyo mali zote pamoja na nyota ya Kazumar ingetoweka haraka mno.

Mpango wa kwanza wa kukamilisha hili ulikuwa unaratibiwa na Sofia ambaye alianza kumshawishi Mama ili akumbushie kuhusu mtoto ndio maana Mama alikumbusha hilo, na jambo la pili ni kunifunga kizazi ili nisizae kwani kutokuzaa kwangu kulikuwa ni miongoni mwa sehemu ya mashariti ambapo Kazumar hakutakiwa kuzaa na mwanamke aliyemuoa. Hivyo Mimi nilifungwa kizazi na maneno ya kejeli kutoka kwa Mume wangu alikuwa akifahamu ni nini ambacho anakifanya kwa wakati ule....

Hivi ulishawahi kununua kitu kutokana na hela uliyokuwa nayo..!? Vile mfuko wako upo muda huo, ndivyo unafanya manunuzi ya kitu unachokipenda.

Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KATIKATI YA CHUMBA CHANGU KULIKUWA NA KABURI Sehemu ya nne.  >>> https://gonga94.com/semajambo/katikati-ya-chumba-changu-kulikuwa-na-kaburi-sehemu-ya-nne
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest