Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

*SEKRETARI NANAH* SEHEMU YA 0️⃣1️⃣

19th Jul, 2025 Views 23



Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani

Mawasiliano: 0763 595006

Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y

*ONYO*

Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.

KARIBU.

"Wewe umemuona shoga ako?"

"Nani?"

"Yule Bi Mkosi"

"Umemuonea wapi na wewe?"

"Anakuja kwenye kampuni yetu nama glass yake makubwa, nadhani amepata kazi kwasababu kaning'iniza kitambulisho kikubwa shingoni".

"Hauko seriously wewe, unamuongelea Nanah au?"

"Huyohuyo".

"Habari zenu" Maongezi yale ya watu wawili yalikatishwa na sauti nzito kutoka kwa mwanamke ambaye ni kiongozi wa pale.

"Salama" walijibu wafanyakazi wote na mbele yao alisimama binti mmoja aliye one kana kuvalia sketi ndefu na blausi ambayo kwao yalionekana kama ya kishamba tu.

"Huyu anaitwa Nanah ni mfanyakazi mpya katika kitengo chetu cha designer na atakava nafasi ya yule aliyeondoka. Nahitaji mumuonyeshe ushirikiano wa kutosha".

"Ndiyo Boss" walijibu wafanyakazi wakike wawili waliokuwa ndani ya ofisi ile ndogo na wote walijulikana kama ma designer.

"Karibu Nanah".

Nanah aliinua macho yake juu kutizama ni nani huyo anayefahamu jina lake.

Alikutana na tabasamu la kinafiq kutoka kwa mapacha hawa wawili Kurwa na Dotto.

Alishtuka kuwaona pale kwani anawafahamu na anajua timbwili lao.

"Ooohh mnafahamiana?"

"Yeah alikuwa maarufu sana huyu chuoni, alimtongoza mwanaume siku ya graduation yetu na akakataliwa". Alijibu Doy (DOtto) kama alivyopenda kujiita na Kurwa alicheka.

Alicheka na yeye Boss akimtizama akijua ni utani tu wa mabinti wa kike wa Rika hilo.

"Basi niwaache, Bob Risky hajafika hadi sasa hivi?"

"Bado" alijibiwa.

"Sawa akija mwambie aje ofisini kwangu nina kazi naye". Aliondoka na kumuacha Nanah akiwa bado amesimama huku Doy na Kurwa wakimfuata na kuanza kumkagua.

"Miwani ile ile, mi nguo mikubwa mikubwa kama unaenda msikitini bado huachi".

"Hahahaha mwangalie na hivi viatu vyake mithili ya wamama wa Huru" aligongelea msumari Kurwa na walicheka kwa nguvu huku wakipashana mikono yao.

"Haya karibu, meza yako hiyo hapo" alizungumza Doy na kumuonyeshea meza.

Nanah alisogelea meza aliyo ambiwa na kutoa pochi yake.

"Mungu wangu muone.... yani na mapochi ya kuning'iniza yenye mikamba mirefu kama mitoto ya msingi jamani?"

"Mi kwanza nashangaa ujasiri wa kumtongoza Brown aliutolea wapi?" Aliuliza na yeye Kurwa.

"Hivi we Bi. Mkosi hujui kwamba umepata ajira ndani ya kampuni namba 3 kwa ukubwa Afrika kwenye swala la designer? Yani hata wafanya usafi wanakuzidi kwanzia mavazi hadi muonekano".

"Na miwani yake kama Daktari wa macho"

Hahahaha walicheka kwa sauti na kupasha mikono.

"Hii mabintiiii" aliingia ndani Bob Risky akiwasalimia na vilisikika nkodonkodo za kike.

Nanah aligeuka kutizama na alishangaa kukutana na mwanaume ambaye amejiugeuza mwanamke kwa kujipaka ma shade hadi kuvalia viatu vya kike na kusuka nywele zake huku sura yake ya kiume ikimsaliti.

"Hi Bob" Kurwa na Doy waliitikia salamu na Bob alienda akaweka pochi yake pamoja na kahawa yake kwenye meza yake iliyokuwa karibu na Nanah.

Bob alipomtizama Nanah , kwa haraka sana Nanah alipeleka macho yake chini huku akitengenezea miwani yake vizuri.

"Huyu mshamba ni nani?" Aliuliza huku akienda kuinua kichwa cha Nanah kwa kidole chake kimoja.

Alimkagua sura yake na kutoa kidole chake.

"Una sura nzuri, sema unajizeesha" alizungumza hilo na alipewa taarifa ya kuwa anaitwa.

"Girls natumaini, ile kazi niliyowapa jana mmeimaliza"

"Ooohh Bob kazi ilikuwa ni nyingi sana jamani tungewezaje kumaliza jana jana?"

"Nyie ni wavivu sana , haswa Doy mdomo tu ndo mwepesi. Naenda kwa Head of designer (Boss) nikirudi nikute mmemaliza"

"Bob hapana japo tupe lisaa limoja"

"Ok lisaa limoja" alijibu Bob na kuondoka akiliza viatu vyake.

Doy alimpa ishara Kurwa ya wampe hiyo kazi Nanah.

Kurwa aliinuka akiwa na ma file 3 na kwenda kuyabwaga kwenye meza ya Nanah.

Aliyeshtuka na kutengenezea miwani yake kama kawaida kisha akainua macho kumtizama.

"Ufanye hiyo kazi hapo, mimi na Doy tutafanya ya lile file moja ni ngumu sana".

"Sawa" alijibu Nanah akikubali na bila hata kutizama kazi yenyewe ni kazi gani.

Kurwa alirudi kwenye kiti chake akiwa anacheka na alipasha mikono na mdogo wake Doy.

👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠

"Brown" aliita mwanamke mmoja jina hilo huku akionekana makamo kwenda na bila shaka huyo ndiye aliyekuwa mama yake Brown.

"Mdogo wako Bieber anakuja kutoka Marekani leo, uwende ukampoke".

"Mama anapajua nyumbani atakuja mwenyewe" alijibu Brown ambaye zilionekana kabisa yeye na mdogo wake hazivii hata kidogo.

"Mtamaliza lini tofauti zenu? Mkumbuke ninyi ni ndugu na mko wawili tu. Alafu wewe ni mkubwa na yeye ni mdogo".

"Sioni udogo wowote kwahuyo mwanao zaidi ya kiburi tu" alijibu Brown.

Brown alipanda gari lake akiwa amevalia suti safi na kuondoka.

"Kuna nini tena mama?" Aliuliza binti Shalha na huyo alikuwa mke mtarajiwa wa Brown.

"Nimemwambia Brown, mdogo wake Bieber anakuja lakini ndo kama unavyoona ameondoka bila kunipa jibu linalo eleweka".

"Anakuja saa ngapi naweza kwenda kumpokea Mama".

Mama Brown alimshika mkono Shalha.

"Una roho nzuri sana Shalha na najua Brown anakwenda kupata mke mzuri kabisa, nakuomba tu uzidi kum vumilia".

"Usijali mama" alijibu Shalha akitabasamu.

"Ngoja na mimi niende kazini".

"Sawa binti yangu Mungu akutangulie".

"Amina mama" alijibu Shalha na kulielekea moja kati ya magari 4 yalikuwa yamepaki eneo la parking.

Mama Brown alimtizama mkwe wake huyo mtarajiwa ambaye ndani ya miezi 2 anakwenda kuwa mkwe wake kamili akiondoka ndani ya jumba lake la kifahari.

👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠

Nanah akiwa anatembea na kahawa alizotumwa na Doy pamoja na Kurwa aliweza kupamiana na mtu na kudondosha kahawa zote mbili.

"Samahani" aliomba radhi bila kutizama anamuomba nani na kutengenezea miwani yake vizuri kisha akaikutanisha mikono yake.

"Nanaaah!!" Aliita Brown kwa sauti ya mshangao na Nanah alipandisha macho yake kutizama nani anamuongelesha.

"Hahahahahah" Brown aliangua kicheko kikubwa akimnyooshea mkono.

Na tukio hilo Nanah alilifananisha kabisa na tukio la siku ya mwisho alipomuomba Brown azungumze naye na Brown alimwambia aje kwenye ukumbi.

Taa zikiwa zimezimwa upande watu wanapokaa, na kuwamulika wao tu.

Nanah alitoa ua nyuma ya mgongo wake na kumnyoshea Brown

"Naomba uwe mpenzi wangu, nakupenda Brown".

Brown alitabasamu kwa mbali kisha akalipokea lile ua.

"Samahani Nanah ila nina date na Shalha" alijibu hivyo Brown na ukumbi mzima uliangua vicheko.

Na hapo ndipo Nanah alipofahamu ya kuwa hawakuwa wenyewe eneo lile bali wanachuo wote wa chuo kile.

Aliona aibu isiyo elezeka na hata siku hiyo hakuweza kubaki tena pale na kusherehekea kumaliza kwake elimu yake ya mwisho.

Alirudisha kumbukumbu zake na Brown alitaka kumshika lakini alirudi nyuma.

"Nanah ni mimi Brown" alijitambulisha Brown akitaka kumshika kwa mara nyingine tena na Nanah alirudi nyuma zaidi.

"Usitake kuniambia mbele yangu kasimama Bi Mkosi" alisema hilo Shalha akienda kusimama pembeni ya Brown na kumshika mkono.

"Anaitwa Nanah, siyo Bi Mkosi".

"Nitamuita Vyovyote ninavyotaka kuna shida kwani?' Aliuliza Shalha akimtizama Brown ambaye aliondoka na kumuacha pale.

Itaendelea In Shaa Allah

@highlight.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*SEKRETARI NANAH* SEHEMU YA 0️⃣1️⃣  >>> https://gonga94.com/semajambo/sekretari-nanah-sehemu-ya-0-1
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

TREVOR CHALOBAH 🫡

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 28💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

🌹I MISS YOU 🌹

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 22💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest