Endelea ๐ป
"Una support Liam amuoe huyu mrembo au unapinga" Rayuna alimtupia swali Ali akiwa bado mlangoni
Watu wote walimgeukia Rayuna kwa kukosa uvumilivu
"Inaonekana kura yangu pekee ndio ilikuwa imesalia....anastahili" Ali (dreva wa Bi. Fatma) alipiga kura
"Familia yangu imevutiwa na wewe hivyo usije kufikiria kurudi Kijijini kwenu" Liam alimuambia Sultana
"Hauna haja ya kuonesha upendo wako kwake mbele yetu....unanifanya nisikie wivu kwa sababu nipo single" Rayuna alimchana Kaka
Watu wote walicheka, macho ya Ali yalimpa ishara Bi. Fatma kuwa kuna makubwa yamepatikana
"Ali rudisha hiyo mikate share yako haipo hapa mezani....nifuate jikoni nikuandalie chai" Bi. Fatma aliondoka na Ali kijanja
Rayuna aliachia tabasamu, hata bila kuambiwa lakini anaelewa kwanini Ali hakuepo kwa siku kadhaa ndani ya jumba la dhahabu
"Sultana sitaki kuamini kama utamaliza mikate yote hiyo pekee yako.....fanya haraka nakusubiria nje unisindikize Supermarket" Rayuna aliongea kisha akaondoka
Liam alijikuta akimuangalia Sultana kwa namna alivyokuwa ana kula bila kuremba. Kila macho yao yalipokutana mioyo yao ililipuka kama petroli kwenye moto.
Upande wa Sona, alifika Uwanja wa ndege... alihitaji kuchunguza kama kweli Rayuna alikuwa Japan.
"Ni ngumu kuomba rekodi ya watu waliokata tiketi Japan kuja Odes....lakini kwa kuwa jambo hili lina husiana na usalama wa Jiji letu nitakusaidia" Msajili wa ndege aliongea
Sona alikaa kusubiria, baada ya dakika 25 rekodi yote ilitumwa kutoka Japan
"Mbweha huyu.....hana bahati" Sona alijisemea kisha akaondoka baada ya kugundua Rayuna ni mshenzi mmoja hivi anayestahili kufa kabla ya jua kuzama.
Sultana na Rayuna waliingia katika Supermarket ya Rich Hill......
"Nasikia unapenda sana keki.....nitanunua kwa ajili yako" Rayuna aliongea
Sultana aliachia tabasamu
Wakiwa katika kuchagua, milio ya risasi ilisikika
"Bila shaka kuna mhalifu mahali hapa.....Polisi watafanya kazi yao wekeza akili yako kuchagua keki tamu" Rayuna aliongea
Lakini ghafla risasi ilipasua keki aliyotaka kuishika Sultana.
Mtu aliyevalia mask usoni mwake aliachia risasi mbili zikapenya kwenye kichwa cha Rayuna
Baada ya kutimiza lengo lake aliondoka kama upepo
"Su... Sultana, najua kila kitu kuhusu wewe na Sona, sikutaka ufe kwenye kina kirefu cha bahari hivyo nilikusaidia. Flash niliyokupatia kupitia keki hakikisha unaitunza.....Sona ni bonge la shetani ni lazima alipe makosa yake yote. Ili yote yawezekana hakikisha unaolewa kwanza na Liam..." Rayuna aliongea kwa kutitia
"Ra...yuna" Sultana alilia kwa mara ya kwanza alishuhudia namna binadamu anavyokata roho
๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป
Upande mwingine, Bi. Fatma alishikwa na mshtuko baada ya Ali kumueleza kila kitu kuhusu Sultana
"Ameishi kama Kahaba tangu akiwa na miaka 16..... sielewi kama atafaa kuwa mke wa Liam" Ali aliongea
"Sultana hana tofauti na malaika na ndio maana alitoka salama tunduni mwa Simba....kama dhambi yake ingekuwa ni kubwa asingetoka hai. Nina uhakika alikuja Jijini Odes kumtafuta Sona na si kingine....." Bi. Fatma aliongea
"Nakumbuka Sona alidai yeye ni yatima asiyekuwa na ndugu....hii inatosha kusema uhusiano wao si mzuri" Ali aliongea
"Kama wameamua kuishi kama watu wasiojuana Mimi na wewe hatupaswi kuingilia" Bi. Fatma aliongea
"Najiuliza tu Sona alipata wapi ujasiri wa kumsindikiza Dada yake kwenye tundu la Simba?....ni kama alikuwa ana furahia anguko lake" Ali alidokeza
"Ni mapema sana kutoa hukumu, kwa kuwa hatujui chanzo cha ugomvi wao Mimi na wewe hatupaswi kuhukumu" Bi. Fatma alishauri
Kabla Ali hajatia neno mlango uligongwa, wote kwa pamoja walikaa kimya kumsikilizia mtu anayeingia
Walijikuta wakisimama baada ya Sultana kuingia akiwa ametapakaa damu..... mgongoni kwake alionekana kambeba mtu
Bi. Fatma alipiga hatua taratibu ajionee mtu aliyebebwa mgongoni na Sultana
Itaendelea ๐ฅ.