.
ILIPOISHIA....
Wakiwa katikati ya mazungumzo yao mazito, mwanamke mmoja mwenye nywele ndefu aliyevaa miwani myeusi, aliketi meza ya jirani. Alikuwa akiwafuatilia kwa makini, huku akijifanya anasoma gazeti. Macho yake yalikuwa makali kama ya mpelelezi. Hakuwa mgeni katika sakata hili la Chacha. Ni yule mwanamke mvamizi. Yuko hapa tena kuendeleza misheni yake.
SASA ENDELEA....
Mwanamke huyu aliyekaa pembeni akifuatilia kwa kina maongezi kati Madam Sandra na Dkt Marry anaitwa Rahma. Hilo ndilo jina alilopewa na wazazi wake. Hayuko hapa kwa bahati mbaya bali anapambana kuufichua ukweli wa siri nzito iliyopo nyuma ya Madam sandra na Dkt Marry.
Rahma ni nani?
Iko hivi....
Miaka michache iliyopita, Rahma alikuwa msichana wa kawaida kutoka kijiji kidogo kilichozungukwa na vilima na mashamba ya mpunga huko kyela. Alilelewa na bibi yake baada ya wazazi wake kupoteza maisha katika ajali ya barabarani akiwa bado ni binti mdogo. Licha ya maisha yake kuwa ya shida lakini Rahma alikuwa ni mrembo kupita maelezo, achilia mbali uzuri wa sura yake, lakini hata mwili wake ulivutia mno. Ngozi yake ya kahawia laini, macho yake makubwa yenye mvuto, midomo midogo ya kupendeza, na umbo lililojipanga kama sanamu ya kuchonga. Alihitimu elimu ya sekondari kwa tabu, lakini matarajio yake yalikuwa makubwa. Alijua kijiji hakiwezi kumpa maisha aliyokuwa akiota kila siku.
Siku moja Rahma aliamua kuondoka kijijini na kuja mjini Mbeya kutafuta kazi. Hakuwa na mwenyeji yeyote mjini, lakini aliamini urembo na akili yake vitamtengenezea njia.
Alizunguka mjini kwa siku nyingi, akipiga hodi kwenye maduka, migahawa, hata vituo vya magari, akiomba kazi. Mara nyingi alijibiwa kwa tabasamu la huruma na maneno. Wengine wakatamani kumtumia kingono ili kumpa kazi lakini Rahma hakuwa mzuri wa sura pekee bali hata akili yake aliitumia vema. Alijua kama atakubali kuutumia mwili wake kama mtaji basi baadae anaweza kuutumia mtaji kutibu mwili wake.
"Mjini maisha yalikuwa magumu, alilala kwenye vibanda vya mitaani, mara nyingine kwa marafiki aliokutana nao barabarani.
Siku moja akiwa na njaa kali, alivutiwa na bango lililokuwa limebandikwa kwenye ukuta wa duka la vipodozi:
Kampuni ya Sandra Beauty โ Tunatafuta wafanyakazi wa urembo na fashion.
Alisita kwa sekunde, lakini njaa ikazungumza kwa niaba yake. Aliingia ndani ya duka lile, na hapo ndipo maisha yake yakaanza kubadilika. Akaunganishwa na bosi wa kampuni inayotafuta waafanyakazi. Bosi hawakuwa mwingine bali ni Madam Sandra.
Baada ya kumpokea mgeni wake Madam Sandra alimtazama Rahma kwa macho ya kitaalamu, kisha akatabasamu baada kurishishwa na muonekano wa Rahma.
"Wewe ndiyo bidhaa ninayotaka" alisema kwa sauti yenye furaha ndani yake.
Rahma alipata kazi papo hapo. Alianza kama msafishaji wa sehemu za masaji, lakini uzuri wake ulimpa cheo haraka mno.
Madam Sandra alianza kumpa nafasi ya kushiriki matangazo ya vipodozi. Rahma alipigwa picha akiwa amevalia mavazi ya nusu uch, akiwa anapaka mafuta ya ngozi au akifanya mionekano ya kupendeza kwa lengo la kuvutia wateja. Ingawa Rahma alihisi aibu, njaa ilimfanya anyamaze. Kulikuwa na sheria moja madhubuti โ sura zao hazipaswi kuonekana kwenye picha hizo za kibiashara. Hii ndio ikamlindia heshima na kumfanya ajihisi huru kufanya kazi hiyo.
Lakini baada ya muda, Madam Sandra alipendezwa zaidi na mwili wa Rahma, akamtumia mara kwa mara. Kila tangazo lililomtumia Rahma lilikamata wateja wengi, hasa wanaume. Hii ilimfanya Madam Sandra amtumie kwa kila kampeni kubwa. Akaanza kuingiza pesa ndefu kupitia Rahma.
Siku moja alimwita tena kufanya tangazo la masaji, Madam Sandra alimweleza kuwa atafanya kazi na mwanaume mmoja aliyepangwa kama "mteja wa mfano." Rahma aliambiwa avae mavazi ya ndani tu, na kuonesha namna huduma ya masaji inavyofanyika. Rahma hakuwa na shaka, akafanya kwa weledi akiamini mambo si mabaya kwani sura zao huwa hazionekani katika matangazo ya kibiashara wanayofanya. Ingawa ndani yake kulikuwa na aibu na maumivu. Hata hivyo, pesa ilimfunga mdomo.
Matangazo yale yalichapishwa na kusambazwa mtandaoni. Lakini safari hii mambo yalienda tofauti na alivyozoea. Picha moja ya video ya masaji ilionesha wazi sura ya Rahma. Madam Sandra akajitetea kuwa ni bahati mbaya lakini kumbe alifanya kusudi. Sura ya mrembo Rahma ilikuwa ni kivutio kingine kwenye biashara yake.
Video ile ilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii. Marafiki zake, ndugu na hata mchumba wa Rahma aliitwa Chacha aliiona video ile isiyo na maadili.
Chacha alipigwa na butwaa. Alikasirika mno. Alimtaka Rahma amweleze kwa undani kazi hiyo ni ya aina gani. Walikwaruzana, wakagombana na Chacha. Mwisho Rahma akaeleza ukweli wote mbele ya mpenzi wake. Chacha akaapa kwamba kama Madam Sandra anaendesha biashara haramu ya kuwadhalilisha wanawake, basi angemfikisha kwenye vyombo vya sheria.
Rahma alijaribu kumnyamazisha Chacha, lakini hasira ya mpenzi wake ilikua kubwa. Alikuwa tayari kuufichua ukweli wote kwenye dawati la maadili na ukatili wa kijinsia.
Akiwa katika harakati za mwanzo,habari hizo zilimfikia Madam Sandra. Mwanamke huyo hakusita. Alijua hatari ilikuwa mbele yake. Muda wowote anaweza kupoteza chanzo chake kikubwa cha mapato. Hakutaka kukubali kirahisi. Akatuma kundi la majambazi kumshikisha adabu Chacha.
Usiku mmoja, majambazi walimvamia Chacha na Rahma. Walimpiga chacha wakamjeruhi vibaya kisha wakamchukua mbele ya macho ya Rahma.
Rahma alijaribu kupiga kelele, lakini kufanya hivyo ikawa ni kola lingine, alipigwa hadi kupoteza fahamu. Kisha wakamalizia kwa kumchoma visu mara tatu tumboni. Wakaamini kuwa amekufa, wakamtupa njiani katika mtalo wa maji machafu.
Walimchukua Chacha na kuondoka naye. Wakamtesa sana huku wakimlazimisha atoe nyaraka za ushahidi alizozikusanya katika upelelezi wake wakati anaandaa shitaka la biashara ya Madam sandra. Chacha aliwapa kila kitu akiamini watamuacha hai la hasha. Madam Sandra alitoa agizo Chacha naye auwawe.
Baada ya siku mbili, mwili wa Chacha akiwa ni marehemu ulifikishwa kwa Dkt Marry rafiki mkubwa wa Madam Sandra. Bila kusita, Dkt Marry alitumia kemikali ya acid kuteketeza mwili wa Chacha na kufuta ushahidi wote.
Lakini Rahma hakuwa amekufa. Aliokolewa na mzee mmoja mtaani ambaye alimkuta kwenye mtalo wa maji machafu akiwa na majeraha mabaya. Alitibiwa kwa siri kisha Rahma akarudi kijiji kwao. Baada ya kupona majeraha yake alirejea mjini akiwa na chuki ndani yake. Alijua ni nani waliomtendea ubaya huu yeye na mchumba wake Chacha. Na sasa alikuwa na lengo moja tu, KISASI.
Ndiyo maana alianza kumfuatilia Madam Sandra kwa siri. Akaingia nyumbani kwake usiku ule. Akamtuma mtoto mdogo kumpelekea Sandra bahasha yenye picha ya Chacha. Kila hatua aliyopiga ilikuwa na maana. Alitaka kumfanya Madam Sandra aogope, aishi kwa wasiwasi, na mwisho abomoe kila kilicho chake kabla ya kuuchukua uhai wake. Hakujua kuwa Madam Sandra naye si mwanamke wa kawaida. Nyuma yake anazo siri kubwa zinazomlinda. Siri zinazomfanya kuwa hapa alipo leo.
Je, Rahma ataweza kuucheza mziki huu wa kisasi sawasawa?
0788 967 317
FUATILIA SEHEMU INAYOFUATA...
Mtunzi: Saul David bril
WhatsApp: 0756862047
Kwa WhatsApp channel ๐๐ฝ https://whatsapp.com/channel/0029VaylcIKAInPiI2v4Cc0R
Tafadhali...
#LikeFollowShare #comentshare #CommentLikeShareFollow.