ENDELEA............
Mama alinisogelea karibu na kuniambia.
"Onesha tabasamu Olivia au kunatatizo!?"
"Ndio mama tena sio dogo"
"Tatizo gani!?"
"Twende tukaongelee pembeni!"
Mama alinishika mkono tukaelekea pembezoni kidogo tukiacha ndugu wakicheka na kufurahi pamoja huku wakicheza.
"Ayaa tumeshafika kuna tatizo gani!?"
"Mama huko kazini nimekutana na shida"
"Shida gani!?"
"Boss kaniambia kama nataka kazi sitakiwi kuolewa kwa sasa ivi"
"Nini wewe!?"
"Ndivyo alivyoniambia"
"Kwanini usiolewe? na tangu lini mtu akapangiwa maswala yake binafsi?"
"Hata mimi nashindwa kuelewa kwakweli, kaniambia kitengo alichonipa hakifai kwa sasa kufanya kazi nikiwa ndani ya ndoa na tena amenipa siku moja tu ya kufikiria na ikifika kesho anataka nirudishe jibu"
"Makubwa sijawahi kuona kazi ya hivyo mimi"
Mama alichoka kama nilivyokuwa mimi, aliegemea ukutani na kuniuliza.
"Kwahiyo wewe umeamua nini?"
"Sijui yaani sielewi chakufanya, nashindwa namna ya kumwambia Isaac mbaya zaidi kazi yangu inamshahara mkubwa kuliko hata yake"
"Hilo kweli ni tatizo"
"Yaani sielewi chakufanya sielewi kabisa mama"
Wote tulikaa kimya na mama aliniambia nimpe mda ili ajadiliane na baadhi ya ndugu zangu.
Baada ya mda walijadiliana na ushauri walionipatia ni mimi kuamua kusitisha ndoa yangu ili walau nianze kazi kwanza na baada ya hapo nitafunga ndoa kwa kipindi kingine na Isaac, nilikubaliana nao licha ya kwamba vyote vilikuwa mhimu kwangu.
Nakumbuka ilipofika mida ya saa 3 usiku Isaac alinitafta akitaka kuongea na mimi kwenye simu, moyo wangu ulikuwa mzito kumpa habari mpya ila sikuwa na namna zaidi ya kufungua mdomo wangu.
"Na jambo ninalotaka kukwambia Isaac"
"Jambo gani!?"
"Kuhusu ndoa yetu!"
"Yes! nilijua lazima ni mambo ya ndoa maana unatamani sana wiki ijayo ifike kwa hamu!"
"Hapana sio hivyo"
"Sio hivyo kivipi tena mbona unaniweka njia panda Olivia!?"
Nilikaa kimya kwa mda na baada ya hapo nikaongea.
"Kuna jambo zito limejitokeza huko kazini linahusu mpaka ndoa yetu Isaac"
"Jambo gani!?"
Baada ya kuniuliza nilimwambia kila kitu na maamuzi yaliyofanyika upande wa familia yangu yaliyomwacha mdomo wazi isaac, hakuwa tayari kukubali kuona ndoa yetu ikisogezwa mbele kwa sababu tu boss wangu kasema na alinipa nifanye machaguo mawili ya kuacha kazi ili ndoa ifungwe au niendelee na kazi na mambo ya kuoana yafe hapo hapo.
"Utanisamehe Isaac tayari familia yangu imeshafanya maamuzi na mimi pia nimekubaliana nayo"
"Kumbe ulikuwa hunipendi Olivia maana kama ungekuwa unanipenda usingekubali ndoa yetu isitishwe sababu ya kazi"
Kiukweli alikuwa na haki ya kulalamika na hata kama ingekuwa upande wangu ningelalamika kama ilivyokuwa kwake na huwenda mimi ningelalamika zaidi yake, nilichomjibu ni kuwa nimeamua kuchagua kazi na sio ndoa tena kitu kilichomuumiza na kukata simu kwa hasira.
Isaac alibaki kutuma jumbe za lawama kitu kilichonifanya niiweke simu pembeni na kulala na asubuhi ilipofika niliamkia kazini kwa ajili ya kwenda kumpatia jibu boss, nilikaa sehemu ya mapokezi kwa ajili ya kumsubiri na Eliza aliyekuwa sehemu ya mapokezi aliniongelesha.
"Ndio kazi za sasa ivi hizi Olivia kazi kwanza mambo ya ndoa baadaye!"
"Na wewe uliambiwa kama mimi nilivyoambiwa!?"
"Akhaaa mimi nilifika na kuanza kazi tu hakuna aliyeniuliza kama nimeolewa au la"
"Na...
"Habari zenu!"
Sauti ya boss ilinifanya nishindwe kumuuliza vizuri Eliza, wote tulisimama na kutoa heshima mbele ya boss aliyeniambia nimfate kwenye ofisi yake.
Tuliingia ndani ya ofisi na kabla hata sijakaa boss aliniuliza.
"Umeamua nini? ndoa au kazi?"
"Kazi boss!"
"Hahahahaha!"
Alicheka na kuniambia nikae kwenye kiti akiwa ni mtu mwenye furaha tele.
"Hayo ndiyo maamuzi sasa, tena usiwe unaniita Boss niite Chris"
Aliongea na kuanza kusogea upande wangu akitoka sehemu yake na aliponifika alisimama kwa nyuma na kuongea kwa sauti ya chini.
"Leo utaanza kazi lasimi ila mkataba utasaini baada ya kumaliza kazi!"
"Haina shida!"
Nilijibu nikisubiri kupewa maelekezo kwa ajili ya kuanza kazi yangu lakini nilichowaza kilikuwa sicho kwani nilishangaa kuona Boss akiushika mgongo wangu na kuanza kuupapasa na kunifanya niinuke haraka kwenye kiti nilichokuwa nimekaa na kumgeukia.
"Boss!"
"Tulia Olivia leo tunaanza na hii kazi ndogo tu na baada ya hapo utasign mkataba wako"
Sijui hata hali ya kujiamini niliitoa wapi, nilijikuta nikianza kumfokea Chris pasipo kuogopa kama ni boss wangu baada ya kuona kanivunjia heshima na kwa hasira nilitoka ofisini na kuubamiza mlango mpaka Eliza mwenyewe aliyekuwa kakaa mapokeza akabaki kushangaa na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wamekusanyika kwa nje baada ya kusikia kelele zetu.
"Olivia!"
Aliniita lakini sikutaka kumsikia zaidi ya kuondoka.
Nilijikuta nikijidharau mwenyewe kwa kukubali kusitisha ndoa yangu kisa kazi na ndipo niliposhika simu yangu na kumpigia Isaac na bahati kwangu alipokea simu.
"Isaac!"
"Nini!? unakipi cha kuniambia?"
"Naomba maandalizi ya ndoa yaendelee kama kawaida"
"Ndoa ipi!?"
"Ya mimi na wewe!?"
"Nimeshagahili sitaki tena kukuoa, uwe na maisha mema!"
Isaac aliongea na kukata simu pale pale.........ITAENDELEA.
Namba ya malipo 👇🏻👇🏻
LIPA NAMBA 67027625 - VODACOM JINA JOHN ELIAS..