Nilimfuata na kuingia darasani na kumwambia "bi dada kubali kuwa hupendwi shoga yangu "
"Norah naomba uniache maana naona unanitibua "
"Aaaa sasa nakutibua kiaje wakati mimi mwenzako nakupa ukweli"
"Kwamba mi sijui ?"
"Kumbe unajua alafu unajitoa ufahamu ,haya hongera ila kwa maono yangu naona Me"
"We koma Meshaaa kama unaona anafaa mpe dada yako Nah si yuko single yule"
"Jamani sasa mbona unanuwahi kwani ni nimesema kuwa Mesha anakufaa akuuu "
"Kwenda huko najua ndo ulitaka kuongea hivyo "
"Haya dada " tuliendelea naratiba zingine kisha mchana tukaenda kupata chakula kwa mara nyingine tena bwana kachumbali akaja kukaa ,safari hiiAlimchamba mpaka nikamuonea huruma kaka wawatu na hakuwa akijibu chochote zaidi ya kuinama tu , basi Amaira alipomaliza kuongea akainuka na kuondoka kwa hasira.
Mesha akabaki akiniomba nikamuombee msamaha kwani hakuwa na lengo la kutukwaza ,nilimshika began na kusema "sikia Mesha haujakosea chochote najua ndio unampenda Amaira ila tambua yakuwa hakupendi sawa "
Alitabasamu na kujibu "Norah najua kuwa hanipendi ila nitapambana mpka nitakapo mkapa na ninakuhakikishia atakuwa wangu"
"Mmh na hizo rangi zako za viungo? Ila sawa kila lakheri kijana" niliinuka na kumfuata Amaira nakuongea nae kumwambia alichofanya sio kizuri maana hata kama hampendi sio sawa kumtolea maneno machafu namna ile .
Hakutaka kuongea nikaamua kumuacha jioni ilipofika tukaagana kila mtu akaenda kwake , nilifika nyumbani nikakuta mama mkwe akiwa nyumbani bila shida nikamsalimia na kuongea na watoto kidogo kisha nikaingia chumbani na kubadilisha nguo alafu nikatoka .
Nilivyofika tu akaanza kuongea " mtoto wa kike saizi ndio Unarudi nyumbani mumeo ndio anafanya kazi yakuwaogesha watoto na kuwapatia chakul"
"Imekuja kutafuta ugomvi tena ee?"
"Kutafuta ugomvi ? Mimi nakwambia ukweli unaniambia natafuta ugomvi ,hivi ndio ulivyofunzwa kuishi kwenye ndoa? "
Nilichukua maji na kumuuliza Selim maana wote waliuwepo wote pamoja na Jabir ila hakuna aliekuwa akiongea ,"Selim tunapika nini na wageni wako wameenda wapi ? Maana naona mko wenyewe"Kabla Selim hajajibu mama mkwe akaongea .
" Mimi nataka biliani "Selim akamuangalia na kujibu "Nimeshaagiza vyakula vya usiku hivyo mke wangu kaa upumzike " nisivyopenda kupika nilishukuru na kukaa pembeni mama mkwe kama kawaida yake akaendelea kuongea .
"Huyu mwanamke atakufilisi unapata wapi nguvu za kuagiza chakula wakati umeoa ina maana kazi yake ni nini kama sio kufanya majukumu yote ikiwemo kupika"
"Akinifilis kama ulivyomfilisi baba itakuwa vizuri zaid"Selim wewe ni wakunijibu hivyo mimi ? Haya unafuraha sasa ushaniharibia mtoto wangu sasaivi haniheshimu tena "
Selim hakumjibu Jabir akainuka na kufungua mlango uliokuwa ukigongwa ,akapokea vyakula na kuingiza ndani kila mtu akachukua chake na kuanza kula .
Mama mkwe akagoma kula eti anataka biliani Selim akaona isiwe shida akamuagizia yake ilivyoletwa hakula akadai imepikwa vibaya , acha Selim achukie na kuanzak kumgombeza "Hivi mama unamatatizo gani mbona unataka kusumbua watu saizi "
"Leo huyo nakusumbua ulivyokuaa unanikojolea usiku hukuona kama unanisumbua ila mimi kutaka chakula ninachokipenda ni usumbufu"
"Chakula si umeletewa au unachotaka nini tena '"
"Norah anipikie kingine maana hiki siwezi kula mimi"
Nilimuangalia bila kusema kitu nikasogeza kile chakula chake huku wao wanaendelea kubishana .
"We Norah kaniandalie chakula nataka kama hiki hiki ila usijaze mafuta" nitaka kutoa hilo neno Selim akanishika mkono na kusema .
"Mama mikono unayo ingia jiko pika mwenyewe"
"Nikapike hapa nikwangu kwanza nawezaje kuingia jikoni wakati kuna mkwe wangu "
"Kumbe unajua ni mkweo sio mjakazi wako ,alafu huu ni usiku kwann usirudi kwako maana umemtelekea mumeo na kuja kwenye nyumba za watu kuleta sheria zako"
Oooh nafukuzwa kama mbwa tena na mtoto wangu wa kumzaa haya Mungu yupo atajibu tu"
Jabir aliacha kuchat na kusema " aunt huu ni usiku kuna vibaka huko nje ingekuwa vyema kama utawahi kuondoka au kama huondoki toa taarifa kwa mumeo tusije pata kesi ya kuharibu ndoa yako."
"Na wewe kaa kimya naongea na mwanangu" Selim alinishtua na kusema kwa sauti ya chini "oya anzisha fujo basi mama aondoke maana mzee atapiga sm mda simrefu"
"Nikome unataka nipate kesi ya mauaji "
"Anzisha bwana uliona wapi mtu anakufa kwa kuambiwa maneno kidogo tu kwanza hakuna kesi ya mauaji kwa kuongea ukipiga ndio kesi ila kuongea hamna kesi"
"Mmmh haya ongea wewe aondoke mimi Sina mood ya ugomvi "
"Kwa hiyo hauongei?"
"Ndio hivyo "
"Fresh ila ninaumbea kama hutaanzisha fujo sikwambii" kusikia umbea nilichukua sm na kupiga kisha nikasema "Hello baba mkwe shikamoo" mama aliinuka haraka na kuondoka bila hata kuaga 😂
KWETU morogoro.