Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Mwanamama Sakina alisogea na kumshika Tina kisha akamwambia usijali hata hiyo harusi sisi ndio tutakao amua ifanyike au isifanyike... Inaendelea... Sehemu Ya 21 Mwisho.

31st Jul, 2025 Views 32



Lakini Mimi sikusema chochote, Nilirudi nyumbani na kwenda moja kwa moja hadi kwao na Edina sababu edina alikuwa tayari anaelewa kwamba kuna watu wanatakata kuharibu ndoa yetu hivyo haikuwa vigumu kumuelewesha nilifika na kuwaambia kutokana na mambo kuwa magumu mimi na mwenzangu tumeona ni bora hii ndoa tukafungie kijijini kwetu, Familia ya Edina walishtuka kidogo, Maana imekuwa ni ghafla sana harafu zimebaki siku chache ndoa kufungwa, Kwakuwa nyumbani kwao na Edina wanaelewa mimi sina tatizo na sijawahi kugombana na Edina harafu ukizingatia na mahari nimeshatoa ikabidi wanikubalie kuondoka na Edina ili ndoa ikafanyike kule kijijini, Lakini ilibidi Edina aondoke na mtu mmoja wa pale nyumbani kwao ili hata ikitokea changamoto tushirikiane.

Nilimpigia simu baba na kumwambia kwamba ndoa itafungwa hukohuko kijijini kwahiyo anza maandalizi ya kualika watu wachache wa karibu, Lakini sisi kesho tunaanza safari ya kuja huko.

Siku inayofuata zikiwa zimebaki siku tatu ndoa ifungwe, Niliondoka na Edina pamoja na ndugu yake mmoja tayari safari ya kuelekea kijijini kwetu ikaanza, Niliamua kufanya hivyo sababu niliona kama nitaendelea kubaki pale kwangu Sakina na Tina wanaweza wakaja kuvuruga ndoa isifanyike, Hivyo nilibana kufuri nyuma yangu na kuelekea kijijini.

Lakini wakati huo mwanamama sakina mambo ni magumu kule anadaiwa huku Sadiki anataka kumjua baba yake, Tina yeye alikuwa anaugulia maumivu ya kunikosa.

Tulifika kijijini tukakuta baba tayari ameshafanya baadhi ya maandalizi, Baada ya sisi kufika ikabidi nisaidiane na baba kuandaa mazingira, Lakini wakati huo Tina hana furaha na mpenzi wake Sadiki, Sadiki alianza kumsumbua mama yake ili amuelekeze alipo baba yake.

Sakina alikaa na mwanae na kuanza kumpatia story ilivyokuwa hadi yeye kupatikana... Baba yako alikuwa ni mwanaume ambaye nilimpenda sana na mahusiano ya mimi na yeye yalikuwa hayana tatizo, wakati huo mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye mgahawa, lakini yeye alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni moja ya ujenzi, nimeendelea kuwa nae kwenye mahusiano hadi nikapata mimba, lakini nilipomwambia kwamba nina mimba akawa amekataa na kusema mimba sio yake, nilijaribu kila njia kumuelewesha lakini akakataa, wakati tunaendelea na kuzozana kuhusu mimba, akawa amefukuzwa kazi, lakini wakati anafukuzwa kazi huyu mzee niliyeachana nae juzi wakati huo alikuwa ananifuatilia na kuniambia atanioa,

Baba yako baada ya kufukuzwa kazi akaamua kurudi nyumbani kwao, wakati huo mimi mimba ina mwezi mmoja, niliamua kwenda hadi kwao nikiwa na mimba yangu lakini baba yako alikataa mbele ya wazazi wake na kusema mimba sio yake, lakini pia alikuwa tayari ameshatafutiwa mke wa kuoa na huyo mwanamke atakayemuoa alikuwa ni rafiki yangu,

Baada ya kuwa amenikataa ikabidi nirudi na kumkubalia yule mzee anioe, na kweli akawa amenioa huku nina mimba, lakini yeye alikuwa hajui kama nina mimba ya mtu mwingine, kwakuwa ilikuwa bado ni ndogo hivyo nikaamua kumpatia yeye na kumwambia nina mimba yake na alikubali na ndipo maisha yalipoanza mimi na yule mzee ambaye wewe ulikuwa unaamini ni baba yako.

Sadiki aliuliza kwa sasa baba yangu yupo wapi na nikienda kumtafuta niseme mimi ni mtoto wa nani na baba yangu anaitwa nani,

Sakina akamwambia ukienda kumtafuta baba yako kamtafute kwa jina la Jua sababu ndio jina alilokuwa anatumia wakati huo, na ukimpata mwambie wewe ni mtoto wa Veronica.

Sadiki alishangaa na kusema mbona mama hilo jina sijawahi kusikia ukiitwa,

Sakina akamjibu hilo ni jina ambalo nilikuwa nikilitumia wakati huo bado sijakutana na huyu mzee. (Sakina akampatia maelezo ni wapi Sadiki aende akamtafute baba yake)

Wakati huo mimi na baba tumeshamaliza maandalizi na tumepumzika tukisubiri siku inayofuata ndio itakuwa siku ya harusi yangu ya kufunga ndoa mimi na Edina, Lakini wakati tumekaa tunaendelea na maongezi nikamuuliza baba, Baba sikueile nilipokuuliza kwamba wakati unafukuzwa kazi ulikuwa umemuoa marehemu mama au bado,mbona uliishia njiani!?

Baba alitabasamu na kusema wewe nae hiyo tabia yako ya kudadisi mambo bado unayo tu! Nikamwambia naomba unisimulie maana kuna kitu nataka nijifunze sababu tayari na mimi naelekea kwenye ndoa,

Baba akaendelea kunisimulia... Baada ya kuwa nimefunzwa kazi nilikuwa na mahusiano na mwanamke mmoja ambaye alikwa anaitwa Veronica, nimekuwa na mahusiano na Veronica zaidi ya mwaka mmoja na tulipanga kuoana, lakini nikaja nikagundua kumbe Veronica ana mahusiano na yule msimamizi wa pale kwenye ujenzi na yule msimamizi alipogundua kwamba mimi nina mahusiano na Veronica alinifuata na kuniambia niachane na Veronica. lakini wakati huo Veronica akawa amepata mimba na kuniambia ile mimba ni yangu, kwakuwa mimi tayari nilikuwa najua Veronica ana mahusiano na yule msimamizi wetu hivyo niliikataa ile mimba na kumwambia sio yangu,

Badae nilipoona Veronica anazidi kunisumbua kuhusu mimba, mimi nikaona bora niondoke yale maeneo nikawa nimerudi nyumbani, lakini niliporudi nyumbani nilikuta wazazi wangu tayari wameshanitafutia mke wa kuoa, na huyo mwanamke alikuwa ni rafiki yake na Veronica sababu Veronica tulikuwa tukiishi kijijini kimoja na kule kazini tulikutana tu, lakini kila mtu alikuwa akifanya kazi sehemu yake, Veronica alinifuata mpaka nyumbani na kuniambia mimba ni yangu lakini mimi nilikataa na mbaya zaidi Veronica alikuta tayari mimi nipo kwenye maandalizi ya kutaka kumuoa rafiki yake, Veronica aliamua kuondoka na kurudi kule alipokuwa akifanyia kazi na mpaka leo sijawahi kuonana nae wala sijui alipo, lakini nilipata habari kwamba Veronica aliolewa na yule msimamizi wetu.

Baba alipomaliza kunisimulia nilianza kutafakari mbona maneno ya baba na maneno ya yule mzee yanaenda lakini tofauti yake ni jina la mwanamke anayetajwa,! Nikaona labda story zinafanana ila sikumuuliza baba kama atakuwa anafahamu Sakina kwa sura, sababu wakati mimi nipo kwa Sakina baba alikuwa anamfahamu Sakina kwa jina tu,lakini hawakuwahi kuonana, ila hata hivyo mimi nikawa najiuliza Sakina aliwahi kuniambia kwamba anamfahamu mama yangu, Hii ikawa inanichanganya!?

Nikamwambia baba kumbe nawewe ulipitia changamoto nyingi, Baba akasema ndio maisha yalivyo, ikabidi kila mtu aingie kulala kusubiri siku inayofuata ambayo ndio itakuwa siku ya harusi.

Siku ambayo ilisubiliwa kwa hamu ikawa imefika asubuh na mapema Edina aliamka na kwenda kuoga sababu yeye alikuwa analala chumba kimoja na yule ndugu yake lakini pia dada yangu hakuwa mbali na yeye siku hiyo ya harusi alikuwepo lakini bwana shemeji ambaye ni mume wa dada, yeye alisema mambo ni mengi muda ni mchache hivyo alimpatia zawadi dada akaja nazo,

Shamlashamla za harusi zikaanza kama kawaida kinamama neno moja vigeregere elfu moja, Mambo yakawa mazuri hadi mida ya mchana wakati huo mimi nimesha jiandaa nimeoga safi marashi ya kunukia kila anayekuja ndani ananisifia nimependeza, Upande wa Edina ilikuwa ni nouma maana Edina alitupia nguo kali hadi wambea wakawa wananichombezaπŸ₯° eti (ukimuona utamjua) sasa jamani nisimjue kipenzi changu,

Hatimaye muda wa kufunga ndoa ukawa umefika, Viongozi wa dini tayari wamekaa mkao kwa ajili ya kutufungisha ndoa mimi na Edina, Nilimfuata Edina ndani na kumshika mkono kwa ajili ya kwenda kukamilisha swala la ndoa Edina alitoka akiwa amependeza hadi nikawa najiuliza kweli Edina kuanzia leo unaenda kuwa mke wangu,

Viongozi wa dini wakatufungisha ndoa na tayari Edina akawa mke wangu, Baada ya kuwa tumekamilisha swala la ndoa ikabidi tukae sehemu ambayo imeandaliwa kwa ajili ya bwana harusi na b-harusi ili kupewa zawadi,

Lakini wakati watu wanaendelea kutupatia zawadi, Nilimuona Sadiki akiwa anakuja pale harusini, Mh nilibaki na mshangao maana nilihisi katumwa na Mama yake aje kuharibu ndoa isifanyike lakini kwakuwa ndoa tayari nimeshafunga nikaona lolote nitapambana nalo,

Nikatulia na kusubiri nisikie kilichomleta, Sadiki alipofika alimsemesha yule aliyekuwa Mc wetu pale harusini, Kisha yule Mc wa harusi akasema jamani samahani kuna mgeni anamtafuta mtu anayeitwa Mzee Jua; Mh wote tulishangaa Jua ndio nani!? Baada ya kuwa hakuna mtu anayemfahamu huyo Jua, Mc akamwambia Sadiki hapa hakuna mtu anayeitwa Jua labda uendelee kumtafuta na sehemu zingine,

Wakati huo baba alikuwa amekaa karibu yangu lakini mimi sikumsemesha Sadiki hata yeye alinitazama lakini hakusema chochote, ikabidi ageuke kuondoka, Lakini wakati anataka kuondoka baba alisimama na kusema ni nani huyo aliyekuagiza uje kumtafuta Jua,

Sadiki akasema mimi ni mtoto wa Veronica na nimekuja kumtafuta baba yangu,

(Mh hadi hapo mimi nikawa sielewi yaani Sadiki ni mtoto wa Veronica yupi wakati mimi najua Sadiki ni mtoto wa Sakina)

Baba akamuuliza ulikuwa unamtafuta mzee Jua kama nani yako? Sadiki akajibu namtafuta Mzee Jua sababu ni baba yangu mzazi,

Baba akasema mzee Jua ni mimi hapa. Mh mimi pamoja na dada tukashangaa kwamba baba ana mtoto mwingine ambaye ni mkubwa kuliko sisi kingine baba anaitwa Jua jina ambalo sisi watoto hata hatulifahamu.!!

Nikamuuliza baba inakuwa vipi uwe mzee Jua. Baba akaniambia wakati nafanya kazi kwenye ile kampuni ya ujenzi nilikuwa nikiitwa Jua kutokana na ufanyaji kazi wangu sababu nilikuwa nafanya kazi hata wakati wa jua kali wengine wamepumzika lakini mimi nilikuwa nafanya kazi, Ndio maana hadi nikapewa jina la utani la Jua.

Baba akamwambia Sadiki kama kweli umeelekezwa na Veronica tambua kwamba mimi ndio baba yako unayemtafuta na wewe ni mwanangu. (Mh sikuwa na lakusema sababu ningesema huyu ni mtoto wa aliyekuwa boss wangu huwenda ingeanza kesi nyingine)

Sadiki alikuja pale aliposimama baba na kukumbatiana, Sadiki alimkumbatia baba huku machozi yanatiririka usoni mwake. Lakini wakati baba na Sadiki wamekumbatia kwa upendo ambao kila mmoja hajawahi kuwa karibu na mwenzie.

(Nilitazama kwa pembeni na kumuona Tina akiwa kwa mbali amesimama na begi mkononi huku analia, Niliongea kimoyomoyo... Tina nilikutaka lakini hukunitaka na sasa umenipoteza na unatamani kunipata Tina umejitahidi lakini umechelewa sana na kwaheri)

Sikumuuliza Sadiki kama alikuwa safari moja na Tina, Tukawa tumepata kaka ambaye ni Sadiki, Mtu ambaye tulikuwa na uadui mpaka wa kushikiana bunduki kumbe ni kaka yangu, Ikabidi tuanze kufahamiana na kusameheana yote ambayo yamepita, Ilibidi tumpokee na kuwa sehemu ya watu wa karibu zaidi. Sadiki akaniambia sasa ni ndugu hatuna tena sababu ya kugombana na kuchukiana, Tukapeana mkono wa kusameheana mbele ya baba,

Harusi ikamalizika vizuri kwa kupata ndugu, Wale waliokuja kwa ajili ya harusi muda ukawa umeisha kila mmoja akasambaa tukabaki wanafamilia na hapo tayari familia ikawa na watu wa nne.

Hiyo jioni wakati tunapiga story nikamwambia Sadiki baba jina lake ni Ntai Dah! Sadiki akasema na wewe jina lako litabaki kuwa David ila hili la Sadiki niachie mwenyewe, Bas ikawa ni furaha, Lakini Sadiki akasema mama yake Sakina aliuza ile nyumba na kulipa madeni hivyo Sakina kwa sasa anaishi kwa ndugu yake mmoja hukohuko mjini.

Tulipata muda wa mimi na Sadiki kuongea, Mimi nikamuuliza Sadiki wewe si mtoto wa Sakina? Sadiki akasema ndio lakini zamani mama yangu Sakina alikuwa anaitwa Veronica. Hadi hapo mimi na Sadiki tulikuwa na siri Sadiki yeye alikuwa anaamini mimi nilitembea na mama yake, Lakini aliamua kutokusema chochote na kuniambia hiyo itabaki kuwa ni siri ya hadi kufa. Na mimi nilimkubalia kwamba hiyo itabaki kuwa siri milele na milele hakuna kumwambia baba wala nani kila kilichotokea na kila tulichofanya tulikizika na kuanza upya.

Asubuh na mapema alipita jirani yetu wa pale kijijini na kutuambia kuna mtu inasemekana kanywa sumu akiwa ndani ya nyumba na amefariki, Tukaanza kushangaa Mh kujinyonga tena!!!

Ikabidi tutoke mimi na kaka na kuongozana na yule jirani kwenda kuangalia ni nani anayesemekana kapoteza maisha kwa kunywa sumu, Lakini kadri tunavyozidi kwenda nikaona tunaelekea nyumbani kwao na Tina, Tulipofika tulikuta watu wamejaa nyumbani kwao na Tina,
Tulifika hadi hapo kwao na Tina, Mama yake na Tina alikuwa analia huku akisema mwanangu nini kimekukuta umekuja jana na kuondoka leo,😭😭

Watu walikuwa wanaingia hadi ndani kuangalia Lakini mimi baada ya kuyasikia maneno ya mama yake na Tina nilikosa nguvu ya kuingia mpaka ndani, Sababu hata hivyo mara ya mwisho nilimuona Tina kwa mbali wakati nipo kwenye harusi yangu,

Kwakuwa watu walikuwa wanaingia ndani kuangalia, Kaka yangu Sadiki aliingia mpaka ndani ili kumuangalia huyo anayesemekana amefariki kwa kunywa sumu, Sadiki aliingia ndani na alitoka huku analia, Nilipoona Sadiki anatoka huku analia niligeuza mpaka nyumbani kwetu na kumwambia Edina jiandae tunarudi mjini kwenye nyumba yetu tukaanze maisha mapya,

Baba alishangaa mbona imekuwa ghafla nikamwambia baba naomba baraka zako nikaanze maisha nikiwa na mke wangu Edina, Tulipanda gari na kuondoka huku nyuma tukiacha msiba mzito kwa Sadiki kumkosa Tina..

Lakini ukweli ni kwamba Sakina alikuwa anajuwa kila kitu ndio maana hakuwahi hata siku moja kuniruhusu kushiriki nae tendo, Na hii siri ya kutokushiriki chochote mimi na Sakina, Tulikuwa tunajuwa wawili tu Mimi na Sakina, Na kuanzia hapo Sakina akawa ni mama yangu wa kambo,

Hivi ndivyo mapenzi na pesa yalivyobadirisha maisha yangu.

MWISHO WA SIMULIZI NDIO MWANZO WA SIMULIZI...

Mtunzi Daudi Songela
Mwandishi Daudi Songela
Whatsapp Namba 0629100976

~Daudi~

ukiondoka bila ku like wala ku comment...itakuwa sio poa ahsante wote....
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Mwanamama Sakina alisogea na kumshika Tina kisha akamwambia usijali hata hiyo harusi sisi ndio tutakao amua ifanyike au isifanyike... Inaendelea... Sehemu Ya 21 Mwisho.  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-mwanamama-sakina-alisogea-na-kumshika-tina-kisha-akamwambia-usijali-h
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest