Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Ikabidi watoto wote wa mzee waende hospitali kwa ajili ya kwenda kupima kipimo cha DNA. Inaendelea... Sehemu Ya 19

31st Jul, 2025 Views 5



Kuna hospitali moja ambayo mzee huwa anaenda kutibiwa akiwa anaumwa, Mzee akapendekeza waende kwenye hiyo hospitali, Mwanamama sakina alipogundua hospitali ambayo itafanya vipimo vya DNA ilibidi aende kwenye ile hospitali kabla ya wengine hawajafika, Sakina alifika kwenye ile hospitali mapema na kuwapatia pesa madaktar watakaoshughulikia swala la vipimo,kisha akawaambia wafanye ujanja wowote ilimladi sadiki aonekane ni mtoto wa yule mzee, Sakina alipomaliza kuwapanga madaktar alirudi na kujifanya kama hakuna kinachoendelea...

Wakati huo mimi nahangaika kupata pesa ya mahari, Baada ya kuwa nimefikisha kiasi cha laki tano nikaona ni vyema nifanye mpango wa kupeleka posa kwao na Edina, Sababu pale ilikuwa kwa baba yake lakini mama yake anaishi sehemu nyingine, Nikatafuta mtu wa kupeleka posa,kweli posa ikapelekwa, Lakini pale kwao na Edina walishangaa kuona muuza mihogo wa nyumbani kwao ndio anataka kumuoa Edina, Walishangaa lakini walikubali,

Baada ya posa kukubaliwa nikaona ni vyema kuongea na baba yangu ili kukamilisha taratibu za kwenda kupanga mahari na kutoa mahari na mambo mengine yaendelee, Nikaongea na baba,kweli baba akawa amekuja pale kwangu lakini hakuja mikono mitupu bali alikuja na pesa ya kuniongezea kwenye mahari, Ikawa imefika kama laki nane hivi, Kwakuwa baba ni mgeni maeneo yale ilibidi nitafute mzee mwingine kwa ajili ya kusindikizana na baba kwenda kuelewana mahari, Walienda na kuelewana mahari ni laki saba, Ikabaki sisi kwenda kutoa,

...Hospitali mzee na watoto wake pamoja na mashahidi na wanafamilia wengine akiwemo na sakina walifika pale hospitali kwa ajili ya kupata vipimo, Wale madaktar waliopewa pesa na sakina ili wafanye udanganyifu wakaanza maandalizi ya kushughulikia maswala ya vipimo, Lakini wakati wanataka kuanza vipimo kamili alifika daktar mkuu wa ile hospitali na kuwaambia wote walikuwa wanashughulikia swala la vipimo wakae kando, Kisha yule daktar mkuu akawaita wasaidizi wake ambao ni tofauti na wale waliopewa pesa na sakina. Mwanamama sakina hanaga aibu alimuuliza Dokta kwa nini umefika na kuharibu utaratibu wa vipimo, Dokta akamwambia mimi ndio dokta mkuu wa hapa na ninapanga kila kitu harafu mimi ndio mtaalamu wa hivi vipimo vya DNA. Dokta alianza kuwachukua vipimo mzee pamoja na watoto wake.

Upande wangu huku mambo yakazidi kuwa mazuri baba na mzee mwenzie waliende nyumbani kwao na Edina kwa ajili ya kwenda kutoa mahari, Mahari ilipokelewa na vigeregere vikapigwa, Wakapanga hadi na tarehe ya harusi lakini pia dada yangu nilimwambia kuwa hivi karibuni kutakuwa na harusi sababu nimeshapata mchumba na kila kitu kimeshakamilika, Dada yangu alinipongeza kwa hilo,

...Baada ya vipimo kukamilika sadiki akaonekana sio mtoto wa yule mzee, Sakina alihisi kuchanganyikiwa aliondoka pale hospitali huku anasema (madaktar wametoa majibu ya uongo) Ikabaki sakina kwenda mahakamani kwa ajili ya kupewa talaka, Lakini kabla ya kupewa talaka uchunguzi ulifanyika na kugundulika kuwa sakina ana mali nyingi za siri pamoja na makampuni na ikaonekana sakina alikuwa akimuibia mume wake. Akaambiwa arudishe mali zote ambazo anazimiliki kwa siri,

Sakina akajidai mjanja akasema zile mali anazomiliki sio zake wala sio za mtoto wake, Mwanamama sakina akacheza mchezo ili asinyang'anywe zile mali, Akasema zile mali ni za kwangu sababu zile mali zake zote zilikuwa zimeandikwa kwa jina langu lile ambalo alinipatia la Sadiki, Baada ya kuonekana zile mali pamoja na biashara zake zote sio zake ikabidi mimi nifuatwe kwa ajili ya kwenda kutoa ushahidi kwamba ni kweli zile mali ni zangu.

Wakati huo baba yangu akasema wakati tunasubiri tarehe ya harusi yeye arudi kwanza nyumbani kule kijijini akaendelee na mambo mengine harafu ikikaribia siku ya harusi atakuja ili tuje tupange mambo ya harusi, Hata hivyo hatukupanga kuwa na sherehe kubwa bali tulipanga ifungwe ndoa ya watu wachache ili kuepusha gharama, Ilikuwa ni asubuh nilitoka pale nyumbani nikimsindikiza baba kwenda kupanda basi ili aende kijijini Lakini pia nilichukuwa na pesa kidogo ili nikamnunulie Edina zawadi,

Lakini wakati namsindikiza baba kuaelekea stendi tulipita sehemu watu walikuwa wapo kwenye ujenzi, Baba alianza kuniambia huwa nikiona watu wanajenga kama hivi huwa nakumbuka mbali sana,sababu huwa nakumbuka miaka ya nyuma niliwahi kufukuzwa kazi na msimamizi wa ujenzi bila hata mimi kuelekewa,nakumbuka nilisingiziwa nimeiba cement pale kwenye ujenzi na nilifukuzwa bila hata kupewa pesa ya malipo ambayo nilikuwa nadai,

Sasa mimi nikawa nawaza mbona story ya baba inaendana na maneno ya yule mzee alipokuwa akinisimulia kule kituo cha polisi!? Nikajaribu kumdadisi baba kwani baba ulikuwa tayari umeshamuoa marehemu mama, Baba akasema ebu kwanza tuachane na hayo,unajua sasa hivi unaelekea kufunga ndoa kwahiyo inabidi uandae mazingira ya kuwa kama mwanaume. Nilimsindikiza baba hadi stendi akapanda gari na kuanza safari ya kuelekea kijijini, Lakini mimi ikabidi nianze kuangalia sehemu ambayo naweza nikapata zawadi ya kumpeleka Edina, Nikawa nimeingia kwenye duka ambalo wanauza nguo pamoja na urembo, Nikachagua nguo nzuri na viatu pamoja na nguo za ndani,πŸ₯° Nilipomaliza nikalipia vitu nikatoka,

Lakini wakati natoka pale dukani nje nikakutana na mwanamama sakina akiwa na tina, Walionekana wakiwa kwenye sura za kuhuzunisha sana, Dah nilitamani kucheka maana walikuwa wanahuzunisha. Sakina aliomba kuongea na mimi lakini kwa kuninyenyekea sana, (nikamsikiliza) sakina akanieleza kila kitu hadi walipofikia na akaniambia kwamba anaelekea kupewa talaka lakini kabla ya kupewa talaka mali na biashara zake zote vinachukuliwa kwahiyo kwakuwa anatumia jina langu kwenye mali zake na biashara zake, Aliniomba mimi nikatoe ushahidi mahakamani kwamba zile mali ni zangu harafu nikizikomboa tutagawana...

Itaendelea...

Mtunzi Daudi Songela
Mwandishi Daudi Songela
Msomaji Ni Wewe...

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Ikabidi watoto wote wa mzee waende hospitali kwa ajili ya kwenda kupima kipimo cha DNA. Inaendelea... Sehemu Ya 19  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-ikabidi-watoto-wote-wa-mzee-waende-hospitali-kwa-ajili-ya-kwenda-kupi
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest