Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHHπŸ₯΅πŸ’˜ SEHEMU YA (02--03)

27th Jul, 2025 Views 56



Maria alichanganyikiwa aliingia ndani na kutoka
" Huyu baba anatamani kuf ia kwenye mikono yangu Yani anauza nyumba nikiwa humu humu ndani .

Maria alienda kumgongea baba yake lakini hakujibiwa ikabidi asukume mlango kitandani hakukuwa na mtu ,

Maria alitoka bila kuvaa viatu na kuelekea kwa mzee Tesha rafiki wa baba yake alijua kwa ule muda lazima atakuwa huko.

" Wewe binti mbona upo mbio mbio hivyo hata viatu hujavaa?
" Nina Raha gani ya kuvaa viatu wakati baba kashafanya madudu yake.

Hivi unajua baba yangu kauza nyumba? Maria alimuuliza Mzee Tesha alitulia kidogo Kisha akesema
" Hakuwahi kuniambia Hilo swala Ila Jana ndio nilisikia watu wakiongeea kuwa baba yako aliuza nyumba miezi mitatu iliyopita na kupewa muda wa kuendelea kukaa wakati mnajipanga kuondoka .

" Sasa pesa alizouzia nyumba kapeleka wapi?
" Itakuwa kachezea kamari na kunywa pombe si unajua huo ugonjwa wa baba yako.

Maria alishindwa kujizuia machozi yakimtoka. Aliondoka nyumbani kwa mzee Tesha huku akilia Sana mpaka akaishiwa nguvu akaanguka na kupoteza fahamu.

Watu walikusanyika na kumpatia huduma ya kwanza lakini hakuamka ikabidi wambebe na kumkimbiza hospital. Walipofika hospital Maria hakupewa huduma yoyote kwasababu hawakuwa na pesa .

Wakati majirani wakijadili lakufanya alifika rafiki yake Maria anaitwa Liya.
" Vipi Maria ameshapata matibabu?
" Hapana hakuna pesa hapa ndio tunajadiliana chakufanya .

" Nahitaji kuonana na doctor.
" Yupo chumba kile pale. Liya alienda kuonana na doctor. Doctor alimuelekeza sehemu ya kwenda kulipia.
Liya alienda kulipa pesa ndipo Maria akachukuliwa na kukimbizwa wodini kwenda kupatiwa matibabu

Baada ya dakika tano daktari alitoka liya akamfuata
" Doctor rafiki yangu a aendeleaje?
" Maria anaonekana anamsongo wa mawazo ndio umemsababishia kuwa katika Hali Ile , Ila Hali yake sio mbaya amepumzika kwa Sasa unaweza kwenda kumuona lakini hutakiwi kuongea nae Sana .

Liya alimshukuru na kuelekea kwenye wodi aliyolazwa Maria
" Oooh jamani Maria wangu ona ulivyo uso wako umepauka Sana inaonekana Kama mtu ambae hajala kwa siku nzima . Aliongea Liya huku akimkumbatia
" Nitaondoka saa ngapi?
" Wewe Hilo sio swala la kuwaza utaondoka hapa mpaka utakapopata nafuu sawa?

" Lakini nipo sawa naomba ukaongee na doctor.
" Doctor kasema utaondoka kesho .
" Lakini haujapenda kuongea nae, natamani kurudi nyumbani.
" Achana na habari za nyumbani ngoja nikakuletee maziwa unywe kidogo
" Hapana siwezi kula mahali hapa . Liya alimuangalia nesi aliyekuwa anamchomoa drip lililoisha..

" Samahani nesi unaweza ukaongea na doctor amruhusu rafiki yangu.
" Sawa nitajaribu maana Hali yake unaendelea vizuri. Nesi aliondoka baada ya dakika chache akarudi
" Doctor amekubali mtaruhusiwa lakini Maria bado anahitaji kuangaliwa kwahiyo Hilo jukumu utalifanya wewe.
" Sawa nesi Hakuna shida nitamuhudumia .

Maria na Liya waliondoka hospital na kurudi nyumbani . Liya alimuandalia supu na kwenda kumsimamia anywe mpaka aimalize . Siku hiyo Liya alilala kwakina Maria akimuhudumia .

Bryan akiwa amelala chumbani kwake alikuwa anaweweseka akiwa usingizini Mara alikurupuka na kupiga kelele huku jasho likimtoka .

alikuwa anaota ndoto mbaya kuhusu kif Cha wazazi wake, tangu wazazi wake walipofariki kwenye ajali ya gari, alikuwa akiota ndoto hiyo kwa muda wa miaka 15 . Hawezi kusahau kabisa kifo Cha wazazi wake.

Bryan ananyanyuka kitandani na kunywa maji ya kunywa Kisha akarudi kukaa kitandani na kukumbuka kile kilichotokea miaka 20 iliyopita.

Kipindi hicho Bryan alikuwa na miaka 5 alikuwa ndani ya gari pamoja na wazazi wake walitoka kwenye mapumziko , bwana Theodore baba yake (Bryan) alikuwa anaeendesha gari Mara simu yake ikaita , alipokea na kuanza kuongea Mara alipata Kama mshituko

hakuangalia alipokuwa anaelekea Mara ghafla gari ilipoteza muelekea na kutokea ajali mbaya Sana iliyosababisha vifo wa wazazi wake na yeye pekee ndio alikuwa hai

Bryan alikosa usingizi alikaa kitandani mpaka kulipokucha alienda bafuni akaoga alipotoka akaenda kwenye chumba Cha kubadilisha nguo .

Chumba chake Cha nguo kinafanana na duka la boutique. Alikuwa na nguo nyingi Sana na za gharama , saa za mkononi za kila rangi , tai na viatu vya kutosha .

Siku hiyo alivaa suti ya dark blue na shati jeupe . Alipomaliza kuvaa alitoka na kwenda kupata kifungua kinywa wafanya kazi wake walipomuona walianza kutetemeka , nae aliona jinsi walivyo waoga alitabasamu bila wao kujua .

alikaa na na mfanya kazi wake vailet akaanza kumuhudumia kwa uwoga huku akitetemeka kumbe alikuwa kammwagia boss wake chakula bila kujua .

Bryan alisimama kwa hasira
" Hivi wewe Ni kipofu huoni Kama umenichafua? Unajua gharama ya hii suti? Vailet alijiinamia na kuomba msamaha lakini Bryan aliendelea kufoka

" Hii suti hata Babu yako hajawahi kuimiliki inakuwaje wewe ukaichezea hivi kijakazi maskini wa mwisho.

Kuanzia Sasa umefukuzwa kazi sitaki kukuona hapa. Nyie mliobaki fanyeni usafi hapa. Baada ya kutoa amri Bryan alienda chumbani kwake alibadili suti nyingine Kisha akaondoka kuelekea hotelini. Alipofika alimwambia secretary wake amtafutie wafanyakazi wawili.

Maria aliamka akawa amepata nafuu akaenda bafuni kuoga ,alipotoka alivaa top nyeupe na suruali ya jeans ya blue Kisha akatengeneza vizuri nywele zake Kisha akaenda sebleni akamkuta Liya kajilaza kwenye Kochi anakoroma .

Alimuacha alale akaenda jikoni na kuanza kupika . Harufu ya mayai ya kukaanga ilimfanya Liya aamke na kwenda jikoni , akimkumbatia Maria kwa nyuma na kumpiga busla shavuni

" Mgonjwa wangu umeamka na nguvu mpya
" Nenda kaoge upige na mswaki unanuka mdomo. Maria alimtania wakacheka
" Sawa rafiki yangu naenda , lakini usisahau kuwa nakupenda .

" Najua unanipenda mpaka unaumwa na ingekuwa mwanaume ungenitongoza na Mimi ningekukataa. Liya aliondoka huku anacheka . Baada ya kutoka kuoga liya alivaa nguo za Maria akatoka nje wakaungana pamoja na kuanza kula
" Mmh chakula kitamu Sana
" Acha kuongea wakati wa kula
" Yani nimekusifia huwezi hata kusema Asante.

Walipomaliza kula Liya alitaka kusimuliwa kilichotokea na Maria alimsimulia kila kitu
" Mungu wangu hivi huyu Ni baba yako mzazi kweli?

Kwasababu hakuna baba atakaeweza kuuza nyumba kwaajili ya kucheza kamari
" Hilo swali nimejiuliza Sana . Lakini Kama asingekuwa baba yangu mama angeniambia
" Na Sasa hivi Yuko wapi maana tangu Jana sijamuona

" Nitajuaje kuhusu Hilo.
Mara mzee Temba aliingia huku akitapatapa na mwiliwake wote ukinuka pombe
" Oooh na hasemwi kashafika . Maria alisimama na kuanza kumfokea
"Baba wewe Ni mtu mbaya Sana sijui hata kama wewe Ni baba yangu .

Kwanini umeuza nyumba na hela umechezea kamari, umejaribu kila kitu tutaishi wapi , au unataka tukatangetange mtaani?

Mzee Temba alimsukuma na kumwambia
" Ondoka hapa wewe na mama yako mlikuwa Kama mizigo kwangu yeye ameenda kakuacha wewe

Sasa na wewe utatafuta kwa kwenda ikiwezekana kakae nae kwenye kaburi lake . Maria alilia Sana Lia alimbembeleza na kumfariji .

Mzee Temba alienda chumbani kwa Maria akakuta 2000 aliichukua na kuondoka nayo. kabla hajafika mbali Maria alihisi baba yake atakuwa kachukua kitu alimfuata na kutaka kumsachi mzee Temba akamsukuma

" Maria achana na huyo mzee atakuja kukuumiza. Maria alilia kwa uchungu liya akamkumbatia na kumbembeleza mpaka Maria akanyamaza .

" Maria unaweza kuja kukaa nyumbani kwetu kwa muda mpaka utakapopata sehemu ya kuishi .
" Asante ,sijui ningefanya Nini bila msaada wako , wewe sio rafiki tu Bali Ni ndugu yangu.

Ninafurahia uwepo wako kwenye maisha yangu. Nakupenda Sana Liya.
" Basi bwana unajua unanisifia Sana mpaka Naina haya
" Mjinga wewe.

Bryan alikuwa anaelekea ofisini kwake kila alipopita wafanyakazi walimsalimia lakini hakujibu. Huko nyuma baadhi ya wafanyakazi walimteta

" Jamani huyu boss anajiskia Sana sijui anajiona Nani? Anahisi dunia yote kaibeba . Freya muhudumu wa mapokezi aliwaambia wenzake

" Nawaonea huruma Sana Yani mnamsema boss au mna hamu ya kuachishwa kazi.Bryan aliendekea kufanya kazi zake Mara aliingi zakia

" Boss nimepiga simu kila sehemu lakini nimekosa mtu wakufanya kazi .
" Una maanisha Nini unaposema hivyo?

Hivi upo serious kweli na kazi yako au ipo hapa kwaajili ya kunitania na kula pesa zangu za bure ? Sasa hakikisha unanitafutia kijakazi kabla ya kesho na ukiendelea kushindwa Ni Bora uache kazi maana huwa sipendi watu wanaoshindwa.

" Samahani boss nitahakikisha nampata lakini watu wengi hawataki kufanya kazi kwako kwasababu ndani ya huu mwezi umeshafukuza vijakazi 20.

" Aiseee kumbe wewe mjanja unajua mpaka idadi ya wafanyakazi niliowafukuza , alooo Mimi nilikuwa sijui idadi yao Ila nashukuru kwa kunijuza .

Alafu kumbuka wewe Ni secret wa kawaida tu ambae unafanya kazi kwangu hivyo ninapokuagiza Jambo lazima ulitimize.

Toka ofisini kwangu. Zakia alitoka haraka huku akiwa amenywea aliwapita Freya na Ave Kama hajawaona .

Freya na Ave wakaanza kumcheka
" Kayakanyaga huyo so nilikwambia kibao kitamgeukia huyu boss wetu ni kichefuchefu.

Maria na Liya walikuwa wanaangalia picha kwenye simu ya Liya
" Lia mpnzi wako mzuri Sana alafu mnapendezana Sana .

" Umeanza na usitake kuniambia umeaanza kumtamani mpnzi wangu.liya alimtania Maria .
" Sasa Liya twende tukaangalie movie nimechoka kumuangalia huyu boyfriend wako.

" Sawa twende kwanza hata Mimi sitaki umuangalie maana udenda unakutoka kwa kumtamani . Waliingia ndani na kuweka movie ya kikorea wakawa wanaangalia.

" Hebu kwanza nikuulize swali la maana kabla haujanogewa na movie. Liya alimwambia Maria . Maria Ali alisimamisha movie na kumsikiliza
" Hivi ulikumbuka kuomba ruhusa kazini kwako?

Maria aliweka mikono kichwani na kusema
" Mungu wangu nilisahau kabisa kuhusu Hilo sijaomba ruhusa hapa najua Sina kazi .

" Kwani unajuaje Kama huna kazi .
" Kwa ninavyomjua yule boss wetu hapa Sina kazi sijui nitaishije hapa mjini na haya majanga yaliyonikumba..

" Lakini huna uhakika Kama huna kazi .
" Kwahiyo unanishauri nifanye Nini?
" Kesho nenda kazini ukifukuzwa unarudi nyumbani.

" Siwezi kwenda kuaibika haya yaliyonikuta yananitosha nitatafuta kazi nyingine. Baada ya Maria kuchukua huo uamuzi walikatisha maongezi wakaendelea kuangalia movie .

Kesho yake Bryan wakati anaelekea ofisini kwake alikutana za zakia . Zakia alimsalimia lakini Bryan hakujibu Ile salamu .bali alimwambia
" Namuhitaji Maria ofisini kwangu.
" Maria hayupo .
" Hajafika kazini mpaka saizi?mtafute popote alipo aje ofisini kwangu haraka..

Itaendeleaaaaaa

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHHπŸ₯΅πŸ’˜ SEHEMU YA (02--03)  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-sehemu-ya-02-03
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest