Simu ilipokatika nilibaki nimeganda na tabasamu la ajabu usoni. Nilihisi kama mshindi wa bahati nasibu, ingawa kile nilichoshinda hakikuwa pesa ilikuwa nafasi ya ndoto yangu.
Nilishika simu kwa nguvu, nikaiweka kwenye meza, kisha nikapiga magoti sakafuni. Machozi yalinitoka.
Sio ya huzuni, bali ya faraja. Nilijua hiki ndicho kipande cha mwanzo wa safari ndefu ya moyo wangu.
Niliinuka ghafla, nikaanza kupack nguo zangu chache shati mbili, suruali moja nzuri, kandambili, na sabuni ya kipande. Nikakumbuka hata kuweka
Nakumbuka mama yangu aliwahi niambia, “Maiko, hata maskini anaweza kuishi maisha ya heshima.”
Na sasa, nilikuwa nikiingia nyumba ya watu wa heshima sio kama mgeni, bali kama mfanyakazi mwenye ndoto ya kimya kimya.
Mungu ailaze roho ya mama yangu mahali pema peponi . Alikufa kifo ambacho sitakuja kukisahau . Kwa kukosa tu hela ya matibabu ndo kimenifanya leo niwe yatima . Baba naye aliaga dunia mapema sana kwa ajali mbaya ya pikipiki ikitokana na tabia yake ya kulewa ....
Ndugu nao walinikataa na kusema hawanitambuwi kwa kuwa hakuna cha kurithi zaidi ya jina la ukooo ambalo ndo ninalo mpaka sasa nimekuja mjini kupambana . Nilijikuta nikitokwa na machozi kila nikiwakumbuka wazazi wazi .
Saa tatu kamili asubuhi nilikuwa tayari nimeshaoga, nimevaa safi, na nimepakia kila kitu kwenye begi langu dogo la mgongoni. Nilitazama chumba changu cha kupanga kwa mara ya mwisho kuta zake zenye mipasuko, dari lililovuja, godoro bovu lakini ndani yake ndiko ndoto yangu ilianzia.
“Asante kwa kunilea hadi hapa,” nilisema nikifunga mlango.
Safari haikuwa ndefu, lakini kila hatua nilihisi kama hatua kuelekea kwenye hatima mpya. Nilipofika mbele ya lile geti jeupe la kifahari, nilivuta pumzi ndefu… na kabla sijagonga, geti likafunguka polepole kamera zilikuwa tayari zimeniangalia.
Mwanamke mmoja ambaye nilipomtazama moja kwa moja nilijuwa ni mama yake Loveness
“We ndo Maiko?”
“Ndiyo.”
“Ingia. Ulikuwa unasubiliwa ”
Niliingia ndani, moyo ukidunda.
Laikini nilipomtzama yule mama kama hajapenda mimi kuwa pale .Nilianza kupata wasiwasi sasa kama mama mwenye nyumba hanitaki nitaishije sasa....
Nilipiga hatua mpaka mbels nikamkuta Loveness anachezea laptop yake . Nilimsalimia lakini alinijibu tu juu juu nikaelewa sasa hapa kuwa haqa wawili hawajakubali niishi pale. Mzee Makani alitokea na kunikaribisha huku akizuga ili nisijifikie vibaya .....
Nilingia ndani lakini wao nyuma walibaki wakinisengenya. Na kuahidi kuwa maji nitayaita mmmha .Niliingia ndani nikaonyeshwa na mzee makani sebuleni,jiko chumba cha kulala ,choo na bafu . Na akaniahidi mazingira mengine nitayaona na kuyazoea kila siku.....
Akaniambia kuhusu mkewe na mwanaye kutopenda mimi kuwepo pale ,lakini aliniambia nivumilie wataelewa . Chanzo cha kuwa hivo akanisimulia kile kisa cha huyo mfanyakazi aliyewaibia vitu vyote .Niielewa na niligundua kuwa mzee makani ni mtu mwenye busara sana ....
Akikuwa haamini kama najua kuendeaha gari alinibeba na kwenda mpaka parking akakaa siti ya nyuma na kuniambia nimuendeshe kuna sehemu tunatakiwa kwenda ...
Basi nilingia na kuwasha gari yeye kakaa nyuma nilishangaa tunakoenda ni njia ya vijiwe nilivyokuwa ninaishi jamaa zangu kuniona nikiwa naiendesha ile gari kwa kuwa wanaijua walianza kushangilia ...
Mzee makani " hao wanashangilia nini?
" kwa kuwa rafiki yao nimepata kazi"
" hahah! Ila vijana bhana "
" ndiyo bosi "
" haya twende kwenye duka la nguo"
" sawa bosi"
Tulienda akanambia nichague nguo kadhaa nami nilifanya hivyo na tukarudi nyumbani . Ile kupaki gari na kushuka nilishtuka nilichokiona hata mzee Makani naye alishtuka!
Mama loveness anachome begi langu pamoja na ndala zangu .... Aiseee roho iliniuma sana
FULL 1500
0699286085
.