Walikula hadi walipomaliza, kisha Rasma alienda kuoga. Alipomaliza, alijiweka sawa kisha akaondoka huku akimuacha Mayner nyumbani.
Upweke ulikuwa kwa Mayner. Aliendelea kuwaza kuhusu maisha yake mapya. Nyumba ya Rasma haikuwa kubwa, ilikuwa ndogo yenye vyumba viwili na sebule. Ingawa vyumba havikuwa vikubwa, lakini alikuwa na sehemu ya kujivunia na alikuwa analipa kodi kwa serikali.
Akiwa kitandani, aliendelea kuchezea simu yake huku akijaribu kufuta picha alizopiga na Garma. Ilikuwa ngumu kwake kufuta baadhi ya picha ๐ข lakini maneno ya mwanasaikolojia yalijirudia kichwani mwake. Alijikuta akifuta kila picha. Kuna muda chozi lilimdondokea kwenye kioo cha simu ๐ญ. Alilifuta, lakini bado haikupunguza maumivu ya aliyokuwa akipitia.
"Ya Allah! Kama hili ni jaribu kama yale mengine, basi naomba uniepushe nalo." ๐๐ฝ alisema huku akiendelea kufuta picha.
Wakati akiendelea kufuta, simu yake iliita. ๐ Jina la Laila lilitokea, naye alihisi huenda alitaka kuulizia kuhusu ndoa. Akawaza kwa sekunde kadhaa kama apokee au la, lakini mwishowe aliamua kupokea.
"Baby..." โค๏ธ aliongea kwa sauti ya upole, yenye kitetemeshi ndani yake.
"Mayner unafanya nini? Nitaweka wapi sura yangu? Kumbe ulienda kuroga? Ulienda kuroga khe! Hadi sasa nimeanza kukuogopa." ๐ค alisema Laila.
Mayner alijikuta akiingia katika dimbwi la mawazo ๐คฏ badala ya kujibu kile alichoulizwa.
"Nani amemuambia Laila hizi habari?" alijiuliza bila kupata jibu.
"Nani ambaye amekuambia?" alimuuliza.
"Khe! Kwani ni siri unadhani? Kila mtu anajua. Nipo hapa ofisini nimechambwa! Mashoga wamenichamba ๐ฉ, tena wanasema umeachika. Mbona unajidhalilisha hivi lakini?"
"Laila, kuna mengi ambayo huyajuiโฆ ni kama vile Mungu alivoficha historia ya shetani. Vyema ukatafuta ukweli." ๐
"Ukweli upi? Wa kwenda kwa mganga au kuna mwingine? Niambie, maana sijaona sababu ya wewe kwenda kwa mganga bwana!" Laila alifoka kwa hasira.
Mayner aliona bora akae kimya ๐ถ ili asikilize rafiki yake. Ingawa maneno yake yalikuwa yanamuumiza ๐ข, hakuwa na jinsi โ alijikaza.
"Kuhusu ndoa... ngoja tuongee ya msingi sasa." alisema Laila.
"Hakuna kinachoendelea kati yangu na Garma." ๐
"Mh! Kwanini? Umepetwa na chizi gani?"
"Hakuna, ni maamuzi tu. Unashangaa mimi kuchukua maamuzi ya ghafla?"
"Hapana, ila ndoa si kila kitu kilikuwa tayari?"
"Utayari wa ndoa hauzuii penzi kuvunjika. Mimi si aina ya wanawake wanaoweka ndoa mbele. Ingekuwa hivyo, ningeolewa na kila mwanaume aliyesema anataka kunioa. Nachoangalia ni mapenzi ya dhati โค๏ธ. Kama hayapo, unadhani hiyo ndoa nitaifurahia?"
"Mh!" ๐
"Guna, tena guna haswa ๐ ila fahamu kuwa hakuna kitu ambacho hakikuwa tayari ila nimeona sio ndoa wala Garma cha muhimu kwangu. Nadhani nataka kuanza maisha mapya, kila mmoja apambane na hali yake."
"Basi nimekoma, nimekomaa mimi ๐. Najuta kushadadia mambo ya watu. Ila ni sawa, huo ni uamuzi wako, hakuna wa kuingilia."
"Asante kwa kunielewa." ๐ Mayner alisema na kukata simu.
Baada ya kukata simu, alijitupa kitandani kwa hasira ๐ก. Ndita zilijitokeza kwenye paji la uso wake. Alitazama kidole chake kilichovishwa pete mwezi uliopita. Alijawa na hasira zaidi ๐ค. Akataka kuivua, lakini alisita kidogo.
"Labda huko mbeleni mambo yatakaa sawa..."
Alijikuta akiwaza juu ya pete ile. Moyo wake ulizidi kuumia ๐ alipokumbuka kwamba hata pete ile alivishwa siku aliyojifungua mtoto ambaye sasa hayupo ๐ญ. Sababu ya pili, aliyemvisha naye hayupo pia.
"Sina chaguo... nitatafuta sonara, hii pete nitauza." alijisemea kwa sauti ya chini.
---
Rasma alifika nyumbani na kugonga geti. ๐ช Dakika chache baadaye, Mama yake alitokea na kufungua.
"Umesahau nini?" ๐
"Acha maswali. Nipishe niingie ndani."
"Kufanya nini?"
"Dawa yangu. Jana ilipotea, ilikuwa kwenye chupa."
"Kwahiyo?"
"Khe! Sa kwahiyo nini wakati naitaka? Wewe vipi bwana?"
"Dawa ni yako au ya yule mchawi mwenzako?" ๐ง๐ฝโโ๏ธ Mama aliuliza kwa kejeli.
"Sijaja kishari. Naomba unipishe nikatafute dawa yangu." alisema Rasma, huku akijaribu kulazimisha kuingia. Lakini Mama yake alimzuia kabisa.
Hasira zilimshika ๐ค. Akamtazama Mama yake juu hadi chini, akimeza fundo la mate kwa hasira.
"Dawa humu ndani hamna! Nenda zako!" Mama Garma alitamka kwa msisitizo.
Wakati huo Garma alikuwa akitoka ndani.
"Mama kuna nini? Mbona umesimama muda wote?"
"Si huyu! Eti anakuja hapa anasema anataka dawa yake. Mara sijui nini!"
"Sikilizeni! Acheni hizo! Nataka dawa yangu. Niliiacha hapa jana usiku!"
"Bwana, ebu toka! Hakuna dawa hapa!" ๐ alisema Garma huku akifunga geti kwa nguvu.
"We mbwa! Nikikuona tena nitakuua au nakuitishia mwizi! Mnataka dawa ili mkaroge zaidi au?" ๐คฌ alifoka Garma.
Rasma aliendelea kugonga lakini hakufunguliwa. Baada ya muda, akaondoka huku akiwa na wasiwasi kuwa huenda dawa ipo kwake nyumbani.
---
Nyumbani kwao, mazungumzo yaliendelea:
"Nahisi walikuja kupandikiza kitu." ๐ alisema Mama.
"Nilihisi hivyo pia, ndiyo maana sikutaka aingie."
"Mtoto wangu amekuwa mchawi. Ila yule mbwa sijui nimfanyeje."
"Mama, niachie mimi. Nitamuonyesha kuwa hanijui!" ๐ก alisema Garma kisha akaenda chumbani.
Mama yake alibaki kwenye msongo wa mawazo ๐. Alipoingia chumbani, aliinama chini na kutoa ukaango aliyoweka nywele jana. Alipozitazama alishtuka:
"Mungu wangu ๐จ! Hii ni nywele ya Rasma... Mwanangu anakuwa chizi! Chizi mwananguuuuuu!" ๐ญ aliangua kilio.
Garma alisikia na kukimbilia chumbani.
"Mama kuna nini?"
"Namwazia marehemu baba yako... Sidhani kama angekuwepo haya yangetokea..." alijifanya.
Garma aliona ukaango:
"Mama, ni nini hicho?"
"Dawa... hizi, ni zile walizoacha kina Rasma."
"Tupeleke kuzitupa basi! Unakaa vipi na uchawi?"
"Acha tu zikae hapo. Siku nikiamua nitazitupa."
"Sawa Mama, nitakupa furaha. Uwe na amani." ๐ค
"Aya baba, hakuna shida." Mama alisema, akashusha pumzi nzito ๐ฎโ๐จ.
"Ahsante Mungu." ๐๐ฝ
.......
Rasma akiwa amelala usingizi mzito ๐ด, alianza kuota mtu alimshika mkono na kumpeleka eneo la giza lililozungukwa na mawe ๐ชจ.
"Tunaenda wapi?"
"Kwa mganga."
"Kufanyaje?"
"Kwani mwanzoni mlienda kufanyaje? Wewe ni chizi, unatakiwa urudishe akili zako!"
"Mimi si chizi! Nani amekuambia?"
"Huoni unavyochakaa? Ona nywele zako zinavyonyonyoka! Twende huko!"
Rasma alistuka kutoka usingizini ๐ฐ, akiwa anatokwa na kijasho kingi. Mbele yake alimuona Mama yake akimpa dawa.
"Kunywa dawa hii mwanangu."
"Ya nini Mama?"
"Ile uliyosahau nyumbani."
"Mbona mganga hakusema hivyo?"
"Alikuongopea tu. Hii nayo unatakiwa uinywe. Huoni mwenzako alinywa? Aya kunywa." ๐
Rasma aliipokea na kunywa hadi kumaliza. Alipotaka kumpa Mama yake ukaango, alishtuka kuona Mama hayupo! ๐ณ
Akapiga kelele โ kelele iliyokuwa mwanzo wa uchizi wake. ๐คฏ๐ข Alianza kupiga kelele usiku kucha, akitema mate hovyoโฆ
Hivi ulishawahi kununua kitu kutokana na hela uliyokuwa nayo..!? Vile mfuko wako upo muda huo, ndivyo unafanya manunuzi ya kitu unachokipenda.
Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..