Nilimpigia tena na tena 🥲🥲lakini akawa hapokei,sasa kwanini mwanaume nae ananuna jamani....!!!😢 machozi yakawa yananilenga lenga🥺 nikajiuliza hivi nalia nini...!? hivi ndo kupenda au maana nilihisi wivu unanikaba😂😂😂eeh...! Mungu wangu naelekea wapi mimi...!? najikaza siwezi🥲🥲si upokee simu mimi nitakufa na mawazo wewe kaka🥲🥲🥲nilikaa kama dakika 45,mawazo tele yaani😢😢😢nashindwa cha kufanya
Niliamua kwenda chumbani kwake,nilihisi kama nitamkuta huko😔😔😔sindo nikakuta simu yake kumbe kaiacha chaji🙄🙄🙄nikaichomoa kwenye chaji i wish niwe najua password niangalie yaliyomo yamo🤣🤣🤣amani kidogo ikarudi🙌hatakuwa hajaenda mbali🤗🤗🤗kama kaiacha simu basi atarudi soon,maana roho ilianza niuma au kaenda kwa yule demu😔😔😔hakiii roho inauma mdada nina uhakika kanizidi hadi dhambi 🥱🥱🥱mara paap akaingia chumbani na kunikuta,aibu zilinishika nikairudisha simu yake🙈
"Naomba unipatie hiyo simu" aliniambia,nilichomoa chaji na kwenda nayo hadi mlangoni alipokuwa amesimama nikampatia na mimi,akaiangalia na kuniuliza
"Ulikuwa unanipigia nini?"
"Simu...!"🥱
"Hayo ndo majibu ulofundishwa umjibu mume wako?"
"Kwani hapo nimekosea wapi...!? Umeniulizaje kwani?"
"Ulikuwa unanipigia kwanini?"
"Mara ya kwanza hata hujaniuliza hivyo"😔😔
"Tusilumbane,jibu sasa"
"Nilitaka tu nijue umeenda wapi,mimi tu nilipata wasiwasi"😔
"Wasiwasi wanini?"🤔
"Sijui ulipoenda....😔 Halafu umenikasirika mimi nashindwa nifanyeje"
"Mimi nimekukasirikia wewe...!? au naact vile ambavyo wewe umeamua...?"
"Kwani mimi nimekasirika makusudi au umenikasirisha"😔😔😔
"Tatizo kwani hapa ni nini...!? sijajali umeniambia unaumwa? kukuuliza habari za kupika au masuala ya jana,nambie nijue niombe msamaha right now"
"Hamna usijali, naomba nipite''
"Unajua kuwa unanikosea sana....!? why unafanya hvyo et..!?"
"Ni ngumu sana kuniambia nilichokukosea...!? bc whatever it's am sorry, yameisha sawa....!?"
"Sawa"
"Sawa nini...!?"🤔
"Si umesema yameisha jamani"
"Okay,unaumwa nini?"
"Siumwi sana ni homa tu"
"Tunaweza kwenda hospital sasa hivi?"
"Hapana nitaenda kesho"😔😔
"Sawa,nimenunua chakula huko twende tukale"
"Sawa"
Tukaenda kupiga msosi ila nilikula kidogo tu kikanichefua,nikaacha hivyo Hakim akasema nitakuwa kweli naumwa, kesho asubuhi niende hospital
Siku iliyofuata niliwahi kuamka nikafanya usafi na kazi zingine ila nahisi kama homa imezidi hivi🤔🤔🤔😩najikaza tu mama akanipigia nikamwambia nikimaliza kazi nitaenda hospitali kisha nitakuja mwambia nikishapima,akasisitiza nipime na mimba🤔😩Hakim aliamka na kuanza kujiandaa aende kazini akaniachia hela ya kwendea hospitali, nikamwambia
"naomba nikuulize"
"Sawa niulize"
"Kwanini hutaki niambia kuhusu yule Agnes?"🤔😩
"Nikwambie kipi tena kuhusu yule mwanamke...!? Jana si nilikwambia tumeachana..!? nikwambie kipi tena yaani story nzima tunaanza mahusiano mpaka yalipovunjika au?"
"Niambie tu nataka kujua,na kwanini aje mpaka hapa anaanza kuongea maneno mabaya 😭😭😭mimi naogopa siku atakuja nifanyia fujo"😩😩
"Niache kwanza niende kazini nachelewa kumjadili mtu asiye na faida yoyote kwetu,ni ex wangu basi hakuna kingine mimi naweza kukwambia....na hana uwezo wa kuja kukufanya chochote,labda tuweke mdada wa kukaa naye kitu ambacho hutaki au tumpe taarifa mlinzi abadili ratiba akae hapa hapa sio kuja jioni tu"
"Hamna bhana,mimi nasikia tu wivu kwani mmeachana lini??"
"Mwaka huu"
"Mmmh...!
" Sasa huamini kama nimeachana naye au?"
"Hapana,yaani kipindi kile unakuja kule Tanga kumbe una mtu wako??? Sasa mimi hapo nitakuaminije unanipenda zaidi yake......!!!! Na nina hakika upo na mimi kisa tu tuliozeshwa kilazima"😩😩😩
"Wala haipo hivyo, Nakupenda kutoka moyoni na hii ndoa ilipangwa,sijakuoa kwa bahati mbaya"
"Unataka kusemaje....!?"
"Acha niende kazini tutaongea baadae"🥰🥰akanikiss kiss😘😘😘nilibaki nimeganda nawaza hivi kaongeza kweli kwamba hivi ndoa yetu ilipangwa,kwahiyo wamenichezea picha na baba....!?🤔🤔🤔but hamna shida si nampenda siku hizi😂😂😂👐 nikawa nawaza yule mtoto niliyempiga ana undugu na huyo Agnes siendi tena ile saloon,pengine ndio wanaishi ule mtaa🥺🥺🥺
Nilijiandaa na kwenda hospitali,nikapima maralia na mimba🤭vyote vilikuwemo🤸🏻♀️🤸🏻♀️ nilifurahi sana kuambiwa nina mimba hatimaye ndoa imejibu,ila nikikumbuka suala la kuzaa kwa uchungu naishiwa nguvu🤭 nilirudi nyumbani nafika getini tu na Agnes naye huyo katika
"Wewe binti subiri kwanza.... mzima wewe...!?"🤔
"Ndio mi mzima" hapo majibu kiroho linadunda😅😅😅
"Vizuri,mimi sina ubaya na wewe kabisa...wala sina mpango wa kugombana,ila kama hutojali naomba urafiki na wewe kiroho safi.....ukiwa unahitaji kujua chochote kuhusu Hakim nitakusaidia maana namjua kuliko wewe.....nilikaa naye kwenye mahusiano miaka mitatu"
"Sawa dadangu,naomba usijali urafiki na wewe sio kitu kibaya"
'sawa, waweza nipatia namba yako tuwasiliane"
"Haya,lakini namba yangu sijaikariri nipatie yako nitakutafuta"
Agnes akanipatia namba yake nilipoingia tu ndani nikaifuta😅😅😅 nikampigia mama na kumwambia kilichotokea hospitali,akafurahi sana💋💋💋 akanambia niache ujinga sasa nakaribia kulea na mimi🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️ nikamwambia na suala la Agnes ni kama anataka nisumbua nafsi huyu dada🥺👐mama akaniambia nisithubutu kubwa na ukaribu naye tena nimtolee nje asinizoee👐👐👐 nilimkubali mama,nikamuaga.....sikutaka kumtafuta Hakim nilitaka nije nimwambie nyumbani na sio kwenye simu💋💋💋maana sikumwambia kuwa napima na mimba
Nikapika chakula cha mchana nikala,Hakim akanipigia na kuniuliza habari za hospitali nikamjibu tutakuja ongea😩 kisha nikalala😴🌚kupunguza uchovu.......nilishtuka saa kumi na mbili jioni,nilijimwagia maji nipate nguvu,Hakim akawa amekuja mwenyewe amebeba ua💐na chocolate 🍫🍫🍫 akanipatia sikulitaka hata,....
"Mke wangu una nini lakini...!? Nakupenda zawadi hutaki kweli?".
"Ndio sitaki mimi"😩
"Haupo sawa?"
"Ndio"
"Sawa,vitu vyako utavikuta chumbani naenda kukuwekea"akaniachia na kuondoka,huyu mwanaume mbona yuko hivi hata hanibembelezi kuniuliza tu nini shida mama na mimi nianze kujibebisha na kumwambia nina mimba yako baby🤭🤔😔 anashindwa....!? Namfuata🤸🏻♀️🤸🏻♀️
Nilinyanyuka na kwenda chumbani,nikakuta anabadili nguo aende kuoga
"Baby....!'' nilimuita
"Niambie"
"Nimekwambia siko sawa"
"Ndio nimesikia"
"Mbona huniulizi kwanini?"😔😔
"Gosh....! Napenda tu kuheshimu maamuzi yako mimi,sipendi nikukere zaidi"
"Dah....! Sawa"
"Yes,maana naona umenuna,umekasirika sijui huhitaji kero,ndio maana nakuletea zawadi pia hutaki niseme nini tena hapo?"🤔
"Kwahiyo sitakiwi kununa au?"😔
"Nuna mama,vimba kabisa.....wakukubembeleza niko hapa....haya niambie my wife nini shida mama,niambie mama"
"Nataka nikupe majibu ya hospitali"
"Ooh unaona sasa ukorofi wako unanichanganyia mambo mpaka nasahau kuwa unaumwa...!🤔niambie sasa umekutwa na nini?"
"Nina ujauzito mimi" machozi yakaanza kushuka😭😭😭
"Wow...! Hongera mke wangu,sasa na huu ukorofi wako ukijumuisha na mimba si nitanyooka mimi"👐👐😂😂
ITAENDELEA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.