ENDELEA..........
Akiwa ndani ya gari aliwaza mambo mengi kuhusu maisha yake.
Alijitahidi sana kubana matumizi, hakuwa tayari kununua vitu hovyo japo nja ilikuwa inamkandamiza lakini alijikaza.
Baada ya masaa nane kupita alifika Jijini Mwanza.
Hakujua anaanzia wapi, stendi ya nyegezi ilikuwa imechangamka kuliko hata ya Jijini Dodoma.
Anakuja kushtuka akiwa hana begi, aliangua kilio cha uchungu kwa sababu hakuwa na akiba yoyote ya pesa.
Zaidi ya kupewa pole hakukuwa na msaada mwingine kwa ajili yake.
"Siku hizi binadamu ni mafundi wazuri wa kuigiza, juzi kati tumetoka kumchangia binti Mmoja akijitia katelekezwa kumbe alikuwa ni bonge la tapeli tu, hata huyu na mashaka naye" Mama Mmoja alizungumza akionekana kukwazika na namna Anjeli anavyopiga kelele za kuibiwa.
Upande wa Osman moyo wake ulizidi kufurukuta kila akimkumbuka Anjeli mfano wa mtu aliyekolezwa na madawa.... alishindwa kuvumilia alimshirikisha Asha Mlinzi wake wa karibu.
"Una mkumbuka yule binti aliniibia nguo zangu kisha akaziuza tulivyo kuwa Dodoma"
"Nakumbuka...." Asha aliongea huku akimtengenezea koti lake.
"Naomba umtafute kwa ajili yangu..."
"Kuna nini?...."
"Kuna jambo hatukumalizana ukimpata nitafurahi sana.... naomba ufanye kwa siri" Osman aliongea kisha akaondoka.
Asha hakuelewa kwanini Boss wake anataka kuonana na Anjeli,,,
Osman aliingia kwenye kikao, kulikuwa na haja ya kufanya mabadiliko katika magodoro yanayozalishwa na kuuzwa na Kampuni lake. Kwa wakati huu walihitaji kuwafikia hata watu wenye kipato cha chini kabisa.
Upande mwingine japo Victor ni Mlinzi wa Osman mara nyingi anatumika na Sabrina.
"Nipeleke Supermarket kuna vitu naenda kununua"
"Sawa...."
"J
Kabla hujaenda kujiandaa naomba nisikie kutoka kwako.. "
"Kitu gani mkubwa?"
"Ni kitu gani kilitokea mlipokuwa Dodoma?"
"Tofauti na kuhakikisha Boss anapata amani ya moyo hakuna kitu kilitokea"
"Akili yake ni kama haijatulia hivi...tuachane na hilo huenda nimekuuliza swali gumu" Sabrina aliongea kisha akaenda nje kumsubiria Victor.
Wakati anataka kuingia ndani ya gari Hilda alijitokeza
"Naomba tuambatane wote...." Aliongea.
"Usiwe na shaka ingia kwenye gari" Sabrina aliongea.
Safari ya kwenda Supermarket ilianza, hadithi za hapa na pale ziliendelea.
Upande wa Anjeli hakujua anaanzia wapi hivyo alikaa kwenye bench kubwa lililokuwa mbele ya duka la Mangi.
Asha alipita sehemu hii akielekea airport, laiti kama angegeuza shingo yake mkono wa kulia basi angemuona Anjeli hivyo zoezi la kwenda Dodoma lingeishia hapa.
Anjeli alijikuta akikumbuka kuhusu kitambulisho cha Taifa cha Mtu anyemtafuta.
"Haya maeneo kuna mtu anafahamika kwa jina la Osman!" Anjeli alijikuta akimuuliza Mangi.
"Unaongelea Osman CEO wa Kampuni la DreamCloud au Osman yupi" Mangi aliuliza.
Anjeli alijaribu kutoa sifa za Osman anaye zungumzia yeye.
"Bila shaka una muongelea Osman niliyekuelekeza Mimi..."
Wakati Asha anapanda ndege kuelekea Jijini Dodoma, Anjeli alipanda bajaji kuelekea ofisini kwa Osman.
Kampuni la DreamCloud lilikuwa limechukua eneo kubwa sana, hii haimkutisha Anjeli alipiga moyo konde. Kuonana na Osman haikuwa rahisi kama anavyo fikiria, hakuna aliyemsikiliza kwa sababu hakukuwa na makubaliano ya kuonana kati yake na Osman.
"Cha kukusaidia sana nenda kakae hapo getini, kama atapita hapo atakutambua. Ndio kwanza nimeajiriwa jana siwezi kufanya makosa," Dada wa mapokezi aliongea.
Anjel hakukata tamaa alikaa getini kwa Mlinzi akaendelea kumsubiria Osman.
"Angalia usije kukata gogo hapo kwa namna ulivyokaa na hofia usije leta ajali ya kinyesi hapo" Mlinzi aliongea.
Akili ya Anjeli ilikuwa mbali sana hakuwa akimsikiliza Mlinzi.
Osman akiwa anatoka ofisini kwake aingie kwenye gari alisikia sauti ya Mwanamke ikimuita.
Japo kulikuwa na umbali kidogo lakini alifanikiwa kuiona sura ya Anjeli.
Mapigo ya moyo yalienda mbio sana kana kwamba ameona joka mkubwa...........ITAENDELEA........
SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA
MTUNZI: NURU HALISI
SEHEMU 05
ENDELEA............
Osman alitaka kushoboka lakini anaamua kulinda heshima yake.
"Mlete huyo binti ofisini kwangu" Osman alimuagiza Mchoma taka kisha akarudi ofisini
Wafanyakazi wake walishangaa kwanini Boss wao karudi tena ofisini.
Baada ya kumuona Anjeli walipata majibu, waliamini binti huyu yupo hapa kuomba kazi.
Anjeli alikuwa na njaa sana, hakutaka kuzungumza chochote na Osman bila kupatiwa chakula.
Chakula kililetwa mezani,, muda wote macho ya Osman yalikuwa yakimtazama Anjeli.
Hakuelewa kwanini kaja Mwanza, alitamani ampige stop kula ili tu amjibu wasiwasi wake. Lakini kwa namna alivyokuwa ana kula kama ana fukuzwa aliazima uvumilivu kusiko julikana, hivyo alivuta subira.
Anjeli baada ya kushiba alipata jeuri ya kuzungumza.
"Nimekuletea boksa yako kwa sababu iligeuka kuwa mikosi kwangu.....yaani baada ya kusex na wewe tu maisha yangu yakawa magumu!... biashara zangu zote ziligeuka kuwa kilio si mchana wala usiku! mji...nga wewe ulichafua nyota yangu" Anjeli alizungumza huku akiivua boksa, kama angeiweka kwenye begi basi ingepotea pia.
"Kitu gani kimekuleta Mwanza, usiniambie Dodoma hakuna watu wanaonunua Madada poa tena" Osman alizungumza huku akikuna pua yake,
"Sikiliza Osman sina tamaa na chochote kutoka kwako.... boksa yako hii hapa, naomba unitolee mikosi yako yote ulioniwekea, nahitaji kujipambania mwenyewe kama zamani, tafadhali sana" Anjeli aliongea.
Sauti yake ilikuwa kelele kwa Osman
"Ahsante kwa kuniletea boksa yangu, kuanzia sasa huna mikosi aina yoyote" Osman aliamua kufunga mjadala.
"Ahsante naamini mikosi yote iliyokuwa inaniandama itabakia kwenye hii boksa" Anjel aliongea kisha akasimama tayari kwa kuondoka.
"Ni kweli umefunga safari kutoka Dodoma kisa hii boksa tu au ulinikumbuka" Osman aliuliza.
Anjeli alimtazama Osman kwa macho ya makadirio...alimpima kwenye mizani yake ya viwango aliambulia sifuri
"Huna maajabu yoyote kwangu...na wala siko hapa kuomba msaada wako,, boksa yako ilikuwa kikwazo kwangu nimeweza kuirejesha" Anjeli alizungumza kisha akaondoka.
Osman alibakia kuduwaa, akili yake ilikataa kuamini kama Anjeli kasafiri Dodoma to Mwanza ili akabidhi boksa.
"Mbwa huyu bila shaka yupo hapa kujiuza.. Dodoma kuna ukame sana ni lazima hata soko lake liwe gumu" Osman aliongea pekee yake.
Baada ya Anjeli kutoka nje ya geti alijilaumu kwanini kaondoka bila hata kuomba pesa ya nauli. Ujeuri wake ulimponza. Lakini pamoja na yote alijipiga kifua......
"Nimezoea kujipambania nitahakikisha napata mlango wa kutokea" Anjeli alijisemea kisha akaongeza mwendo.
Alianza kupita kila nyumba akiomba kazi za ndani.
Mwisho kabisa alifika kwenye nyumba namba 490.
Alianza kugonga geti..... Mlinzi anafungua akiwa kakunja uso wake.
"Natafuta kazi za ndani...." Anjeli alijieleza
Kabla Mlinzi hajajibu chochote, gari la Sabrina lilifika.
Mlinzi aliachana na Anjeli akashughulika kufungua geti.
"Huyo binti ana shida gani...." Sabrina aliuliza
"Anatafuta kazi za ndani...." Mlinzi aliongea.
Sabrina alimuangalia Anjeli kwa umakini mkubwa.
"Umepata kazi...." Aliongea kisha akaelekea ndani.
Hilda alimuonesha tabasamu Anjeli kisha akaelekea ndani pia.
"Nifuate...." Victor aliongea.
Anjeli hakuamini kama amepata kazi kirahisi namna hii. Hakujua kama sehemu hii ndio makazi ya Osman.
Wakati Anjeli anaingia jikoni kupika, Asha alishika simu yake akampigia Osman.
Alihitaji kumpa majibu kuhusu kazi aliyompatia
"Kwa taarifa nilizopokea huyo binti atakuwa Mwanza" Asha aliongea.
"Nisamehe kwa kuchelewa kukupa taarifa, nimefanikiwa kumuona na tumeweza kumaliza utata uliokuwa unatukabili, hivyo rudi nyumbani" Osman aliongea kisha akakata simu.
Aliingia kwenye gari kisha safari ya kwenda nyumbani ilianza.
Alikuwa amechoka sana, alimruhusu mkewe amvue koti. Bahati mbaya boksa aliyoletewa na Anjeli ilidondoka chini.
"Nimepita mtumbani nikajikuta nimevutiwa nayo..."Osman aliongea uongo ulionekana wa kitoto kabisa machoni kwa mkewe.
"Rangi yake ni nzuri...." Hilda anaamua kurahisisha mambo hakuwa tayari kusikia kweli....japo uongo uliozungumzwa ulikuwa unauma lakini ulifaa kuliko kusikia ukweli mchungu.
Kwa pamoja waliingia bafuni kuoga.
Kwa mara ya kwanza Anjeli aliandaa chakula cha familia ya Sabrina.
Osman na mkewe wanakaribia mezani kula.
"Nilifikiria Asha yupo, hii sahani inatakiwa kutolewa hapa" Sabrina aliongea kisha akamuita Anjeli.
Osman alijikuta akitetemeka ndani ya moyo wake baada ya kumuona Anjeli.
Anjeli hakuamini pia baada ya kumuona Osman..............FULL STORY 1000 WAPEMDWA. STORY TAMU SANA HII NA BADO NDEFU SANA.
KARIBU KULIPIA KWA NAMBA 0743770612 JINA JOFREY.
UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP KWA NAMBA 0683009150..