Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

*.A STRANGER WHO STOLE HIS HEART* _____________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*

1st Aug, 2025 Views 22



"Hiki ndo chumba changu ?"
Aliuliza Winnie akiwa haamini kama anaweza kutumia chumba kikubwa na kizuri kama kile

" Ndiyo miss Winnie hiki ndo chumba chako kwanzia leo nilitaka kufanya maandalizi mazuri zaidi sikutegemea kama utakuja mapema kama hukupenda kitu chochote au Kuna kitu unataka tuongeze niambie tu mimi " aliongea Mr Charles kwa heshima ingawa alikuwa na umri sawa na baba yake na Winnie Mr Patrick

" Hata usijali Mr Charles Yani kila kitu kipo vizuri sana na nimependa " aliongea Winnie huku anatembea kila Kona kuangalia mpangilio wa chumba

" Asante sana miss Winnie kwa kupenda huduma zetu ukihitaji chochote Kuna simu pale unaweza kutujulisha "
Mr Charles alitaka kuondoka Winnie alimzuia

" Subiri kwanza Mr Charles,Elian Yuko wapi ?"
Aliuliza Winnie

" Aaah boss Elian amepumzika hataki usumbufu "
alijibu Mr Charles kama alivyouluzwa

" Mmmmh okay na chumba chake Kiko wapi ?"
Aliuliza Winnie Mr Charles alitoka nje ya mlango wa chunba Cha Winnie akamuonyesha

" Chumba anachotumia boss Elian nikile pale mlango wa tatu kutoka hapa upande wa pili wa kordo "

" Kumbe chumba chake kipo karibu tu ,asante Mr Charles "
Winnie alirudi chumbani akajilaza kitandani alikumbuka kumpigia Tracy

" Yamepita masaa mawili unajua nilikuwa na wasiwasi sana " alilalamika Tracy baada tu ya kupokea simu ya Winnie

" Usiwe na wasiwasi bhna nilikuwa anaangalia mazingira ya chumba Yani ni bonge la chumba na kina mpangilio mzuri hatari Hilo li kitanda Sasa nitakuwa nachelewa kila siku kuamaka madam Nora ataongea kila siku mpaka mdomo upinde " alisema Winnie wote wakaanza kucheka

" Nionyeshe basi shonga mana unavyonitambishia "

" Subiri kidogo "

Winnie alimpigia Tracy vedio call

" Wow jamani chumba kizuri hatari Yani chumba changu kikifananishwa na hicho chumba chumba changu ni choo wallah"
Tracy alikisifia sana chumba alichokabidhiwa Winnie

" Umeona ee , basi shoga angu baadae ngoja nipange pange nguo zangu kabatini " Winnie alimuaga Tracy na kama alivyosema alienda kupanga nguo zake kabatini Winnie alipanganguo sio muda mrefu alikuja kuitwa na Mr Charles

" Miss Winnie chakula Cha mchana kipo tayari "

" Oh kumbe muda umeenda hivyo na tayari ni mchana , asante sana Mr Charles nakuja Sasa ivi "
Winnie alitoka chumbani kwake akaelekea dinning room Alikuta meza kubwa imejaa vyakula vya kila aina mate yalianza kumjaa mdomoni alivyta kiti akaka

" Mbona nyie mmesimama tu pembeni na hamji kuungana na mimi ?" Winnie aliwauliza wafanyakazi wa tatu waliosimama pembeni ya meza kwa msatari mmoja na kwa heshima

" Hapana miss Winnie sisi hatuwezi kula pamoja na wewe sisi kazi yetu ni kuhakikisha unakula vizuri na kama hukukipenda chakula tupo hapa unaweza kutuambia"
alisema mfanyakazi moja

" Oh basi sawa mimi nitaanza kula "
chakula kilikuwa kitamu sana Winnie alijitahidi kula lakini alishindwa hakuzoea kula peke yake mara zote nyumbani kwao hua wanakula familia nzima kwa pamoja na kingine hakupenda kula ikiwa watu wengine wamesimama tu pembeni yake kama maroboti

" Asanteni chakula ni kitamu sana sijapata kuonga "
Winnie aliongea huku anatabasamu

" Tunashkuru kusikia hivyo miss Winnie ukitaka kitu chochote unaweza kutuambia " wale wafanyakazi walianza kusafisha meza

" Mr Charles kwani Elian Yuko wapi na mbona wanasafisha meza yeye hatokuja kula chakula Cha mchana?"
Winnie alimuuliza Mr Charles

" Boss Elian bado amepumzika na kama alivyosema hataki usumbufu tunasubiri akiamka ataandakiwa chakula kingine "
alijibur Charles

" Anha sawa ,ninaweza kutembea tembea kwenye nyumba kuangalia mazingira ?"

" Ndiyo miss Winnie unaweza kufanya hivyo bila shaka "
Winnie alitabasamu alianza kutembea kwenye Lile jumba kubwa alimkagua mazingira alitembea sana mwisho alijikuta anafika floo za juu alikuta chumba kimoja kipo wazi akaingia ilikuwa ni maktaba

" Wow kumbe Elian ni mpenzi wa kusoma vitabu pia kama mimi " Winnie alisogea kwenye makabati ya vitabu alianza kukagua vitabu vilivyokiwepo

" Nitasoma hiki hapa " Winnie alichukua kitabu Cha Hadith alienda kukaa kwenye kiti na kuanza kusoma Alisikia hatua za mtu zikimsogelea aligeuka haraka sana na kwa wasiwasi

" Aaah kumbe ni wewe Elian "
Winnie alishika kifua chake upande wa moyo na alikuwa anahema mfululizo

" Mbona umeshtuka sana Kama umeona mzimu ?"
Aliuliza Elian

" Nilikuwa nasoma hiki kitabu kina mambo mengi sana ya kutisha"

Winnie alimuonyesha Elian kitabu alichokuwa anasoma Elian alitabasamu akaenda kukaa pembeni ya Winnie

" Kitabu kama hiki sio Cha kuogopesha hata kidogo kwanini uogope"

" Weee huenda hukuwahi kukisoma kinatisha sana "
Winnie na Elian walijikuta wanabishana Elian alisema kitabu hakitishi na Winnie aling'ang'ania kuwa kinatisha

" Tuache kubisha nataka kukwambia huu mwezi mmoja utakao kuwa hapa hakitatokea kitu chochote kati yetu nataka ufikile vizuri kama ni kweli umekubali kuwa mwanamke wangu na baada ya hapo patakuwa na mkataba " alisema Elian

" Mmh sawa na Nina uhakika haitakuwa mwezi mmoja tu kwasababu siwezi kukimbia kirahisi hivyo " alijibu Winnie kwa kujiamini

" Okay it's a deal " alisema Elian

" Nataka kukuomba kitu pia "

" Sema nakusikiliza " Elian alimuangalia Winnie

" Kuna orodha ya vitu ambavyo ningependa kufanya nikiwa na mpenzi wangu unatakiwa kunisaidia kuvifanya kwasababu na mimi nakusaidia kuondoka na hiyo ndoa usiyoitaka "
aliema Winnie

" Hapana siwezi kufanya hivyo Sina muda wa kupoteza "
Elian alitaka kuondoka Winnie alimvuta Elian alirudi kukaa kwenye kiti

" Please usikatae " Winnie aliongea huku anamminya minya elian kwenda mabega yake Elian alikuwa kimya sana Winnie alimchungulia aliona Elian amefumba macho Winnie alitabasamu akaendelea kumfanyia massage

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*.A STRANGER WHO STOLE HIS HEART* _____________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/a-stranger-who-stole-his-heart-_____________________________________-sehemu-ya-kumi-na-moja
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest