Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

CHANZO NI BOSS 01

1st Aug, 2025 Views 23


WhatsApp 0748697173

Kwa jina naitwa Olivia ni mtoto wa pili kati ya watoto watano kwenye familia yetu, huu ni mkasa wa kweli kwa yaliyonikuta ulionifanya nikae mbele ya Zooper kuusimulia mkasa huu.

Mkasa wangu unaanzia hapa 👇🏻👇🏻👇🏻.

Ikiwa imebaki wiki moja ili niweze kufunga ndoa na mwanaume aliyekuwa akiitwa Isaac nilipigiwa simu na namba ngeni na nilipoipokea nilitaarifiwa tarifa njema za kupata kazi!, niliruka kwa furaha baada ya kupewa taarifa hizo mpaka dada yangu aliyekuwa akiitwa Norah akabaki kunishangaa.
"Kuna nini Olivia mbona makelele tena!?"
"Nimepata kazi dada!"
"Umepata kazi!?"
"Ndio"
"Wapi ulipopata!?"
Nilimfafanulia vizuri Norah sehemu niliyopata kazi na alinipongeza na kunikumbatia kwa furaha.

Kwangu ilikuwa ni wiki ya neema sana kwani ni wiki moja tu ilibaki niweze kufunga ndoa na mchumba wangu wa mda mrefu, nilijiona ni moja ya watu wenye bahati sana kwenye hii dunia na baada ya taarifa zile familia yangu ilinipongeza kwa kupata kazi hivyo niliamua kumshirikisha mchumba wangu na uzuri Isaac aliipokea taarifa ile kwa furaha huku akinisisitizia niendelee na maandalizi ya ndoa yetu kama kawaida.

Maelezo niliyopokea ni mimi kuwasili kazini siku inayofatia pasipo kuchelewa hata nusu dakika, nakumbuka siku iliyofatia ilikuwa ni siku ya jumanne, niliamka asubuhi sana mfano wa mtoto wa shule ya msingi aliyenunuliwa nguo mpya za shule na wazazi wake akiwa na hamu ya kwenda shule, mda ulifika nikafanya maandalizi kwa ajili ya kuondoka na kabla sijaondoka mama alinifata.
"Olivia mwanangu!"
"Abee mama!"
"Leo wageni wanaanza kuja hapa nyumbani kwa ajili ya harusi yako, najua leo ndiyo unaenda kuanza kazi kwa mara ya kwanza hivyo nakuomba sana uongee na boss wako ili akupe likizo kwa ajili ya maandalizi ya harusi yako"
"Sawa mama nimekuelewa!"
Nilimuaga mama na kuondoka na baada ya mda nilifika sehemu niliyoajiriwa na kupokelewa vizuri tu sehemu ya mapokezi.
"Msubiri boss mda sio mrefu atafika akupe mwogozo!"
"Haina shida dada!"
Nilikaa kwenye benchi lililokuwa pembeni nakumsubiri boss. Watu mbalimbali wake kwa waume walinipita nilipokuwa nimekaa huku baadhi yao wakinipa hi na wengine wakinipita pasipo kunisemesha.

Masaa matatu yalipita nikiwa nimekaa pale na ndipo baadaye alipowasili boss na kuniambia nimfate ofisini na kimakadilio umri wake haukuzidi miaka 38.

Nilifika na kukaa kwenye kiti huku nikiwa na hofu kiasi na boss alinitazama na kuongea.
"Karibu sana katika kampuni letu la....."
"Asante boss!"
"Kabla sijaendelea kukuuliza maswala ya kikazi nataka kujua kama tayari umeshaolewa?"
"Hapana boss bado sijaolewa ila nategemea kufunga ndoa wiki ijayo mimi na mchumba wangu"
"Unafunga ndoa!?"
"Ndio boss!"
Boss alionesha kushitushwa baada ya mimi kumpa taarifa na kuniacha njia panda, alinyamaza kwa sekunde kadhaa pasipo kuzungumza neno lolote lile na kuzidi kunitia hofu ila nilijikakamua na kumuuliza.
"Kwani kuna tatizo boss?"
"Tena kubwa sio dogo, tulijua bado hujaolewa ndiyo maana tukakuchagua wewe na hii ni kutokana na kitengo tunachokupa, ni ngumu tena sisi kukuajiri kama utakuwa mke wa mtu"
"Boss nitajitahidi na kupangilia mambo vizuri hata kama nitakuwa kwenye ndoa!"
"Hakuna cha kujitahidi hapa, chagua moja usitishe kuolewa kwa sasa ili upate kazi au uolewe ili ukatafte kazi sehemu nyingine"
Maneno ya boss yalinivuluga hasa nikikumbuka jinsi nilivyohangaika kutafta kazi kwa mda mrefu na ukizingatia kazi ilikuwa na mshahara mnono na malulupu ya kutosha, sikujua nimjibu nini Boss zaidi ya kubaki kimya tu.
"Nenda kesho njoo asubuhi ukiwa na jibu sahihi!"
"Sawa boss!"
Nilinyenyuka na kutoka nje huku mwili wote ukiwa umeloa kabisa na kilichonichosha ni maandalizi ya nguvu ya ndoa yangu yaliyokuwa yakiendelea nyumbani kwetu.

Taratibu nilisogea sehemu ya mapokezi kwa ajili ya kusign ili niweze kutoka nje na binti aliyenipokea kwa mara ya kwanza aliniongelesha.
"Vipi dada mambo yameenda vizuri humo ndani!?"
"Ndio ila tu kuna kitu boss kaniambia kimenichanganya"
"Kitu gani!?"
"Hapa nilipo wiki ijayo natakiwa kufunga ndoa lakini boss kaniambia kama nataka kazi basi sitakiwi kuolewa kwani kitengo nilichopangwa sitakiwi kufanya nikiwa mke wa mtu!?"
"Mmmmmh pole sana ila ndiyo utaratibu wa hapa ulivyo maana wafanyakazi wengi wa kike hatujaolewa"
"Kwanini!?"
"Sign hapa tu!"
Alilipotezea swali langu na kuelekeza macho yake kwenye daftari, nilitia sign na baada ya hapo nikaondoka huku kichwa kikizidi kugonga na nilipofika nje Isaac akanipigia simu na mimi nikaipokea.
"Hello mke wangu umeshalipoti kazini?"
"Ndio nimeshalipoti!"
"Umeyaonaje mazingira ya kazi lakini au tayari kuna watu wameshaanza choko choko kukutongoza?"
"Hapana Isaac hamna mtu aliyenitongoza!"
"Basi nakuomba kila atakayekuwa akikutongoza mwambie ivi (karibu kwenye harusi yangu nafunga ndoa na mwanaume wa ndoto zangu tu sawa Olivia!) "
Isaac aliongea huku akicheka na kuweka utani pasipo kujua mambo yaliyokuwa yakinisumbua kichwani.

Nilitamani kumwambia kile nilichoambiwa na boss ila nilihofia kuchafua hali ya hewa na nilichowaza ni kwenda kuongea kwanza na familia yangu kabla sijamshirikisha yeye.
Tuliongea mambo mengi huku nikijitahidi kuficha hali niliyokuwa nayo ili asiwe kugundua mpaka pale alipokata simu na mimi nikaendelea na safari ya kurudi nyumbani.

Baada ya mda nilifike na kumbe baadhi ya ndugu tayari walikuwa wameshafika kwa ajili ya maandalizi ya harusi yangu na waliponiona pale pale walinifata huku wakipiga vigelegele na kunikumbatia na kuanza kuimba nyimbo za kikabila kwa ajili ya tukio langu mhimu la ndoa yangu.

Haukupita mda mama naye alitoka nje pamoja na ndugu zangu wengine wakajumuika wote kwa kuanza kuimba pasipo kujua kama mwenzao na mazito ndani ya moyo wangu yanayohusu ndoa yangu ninayotamani kuwashirikisha...........ITAENDELEA.

Namba ya malipo 👇🏻👇🏻

LIPA NAMBA 67027625 - VODACOM JINA JOHN ELIAS..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CHANZO NI BOSS 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/chanzo-ni-boss-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest