______________________________________
Aliongea ivyo akaondoka , Amina alienda kuleta dawa za kumeza nikameza, kidogo mzee akafika, nikamsalimia Kwa uoga kweli, tulikula, nikatoka kuongea na mzee pamoja na Mudy, mzee aliuliza kama tumemaliza tofauti zetu ndoa lini tusizini hovyo, " baba Mimi binafsi Niko tayali hata Sasa hivi ila mwenzangu akaomba iwe wiki ijayo, tutafunga kwanza ndoa Sherehe ndio tutapanga, nilishangaa Mimi ndoa, nikajifanya kukubali tu ila kichwani napiga hesabu ivi, Nina akili kweli Mimi niolewe na huyu shetani, mbwa ibilisi mkubwa huyu hapana��...
Tulimaliza kuongea siku hio tulilala hapo na mimi nililala na binti yangu Kwa amani kabisa, asubuhi kulivyokucha, nilikuwa wa kwanza kuamka, nikafanya usafi mikonono ilikuwa sawa, nikapika nilisaidiana na dada wa kazi na Amina wangu....
Anapenda kupika ilibidi nianze kumfundisha saivi chai binti yangu ni fundi hachemshi anakupikia chai chai kweli...
Mimi nilipika vitafunwa, Amina wangu Kwa mara ya kwanza kapika chai ya familia, siku zote alikuwa anapika kwangu tu, Leo kapika kwao tena ya watu wengi, wote hawakuamini wakadai nampa kichwa tu, hii chai ata dada wao haijafika kiwango hiki...
Tulibishana mpaka wakafungua CCTV ya jikoni, wajashuhudia Mimi wakati Amina anapika chai Mimi nilikuwa na deki hivyo hakuwa na mtu hata wakumwelekeza ni yeye mwenyewe...
Familia nzima ilifurahi, babu akatoa zawadi kwangu na Kwa mjukuu, baba mtu akatoa zawadi Kwa mwanae afu Mimi akasema tutamalizana ��, mnaielewa kweli hii jamani...
Tulikula tukasambaa Mimi niliaga kabisa make Leo ilikuwa siku ya kurudi kwangu, Amina alitaka kuondoka na Mimi nikamzuia kuwa Leo akae na familia afu kesho aje, Mudy alinitizama akakausha...
Nilipelekwa na Mudy mpaka kwangu, Kisha akaondoka, alivyoondoka tu, nikabeba vitu vya muhimu, nikawapigia nyumbani nikamueleza mama Kila kitu...
Mama akasema nipande gari sasa hivi, japo muda ulikuwa bado nikaona bora niunge unge nipande za Arusha afu huko ndo nitapata zile gari za jioni kuliko nisubili huku...
Nikaweka vitu sawa funguo za dukani na kila kitu Ili Sophia akija anisaidie kuuza vitu baadhi siwezi kubeba vitu nitashtukiwa, hata begi niliacha nikabeba kimkoba tu Cha nguo baadhi...
Nikatoka mpaka stend, nikakata ticket yakwenda Arusha, nikiwa nimekaa zangu natamani gari iondoke haraka, Mungu akawa upande wangu gari ikasema, imekimbia kama dk 20, ikapigwa mkono, mambo ya matrafic...
Gari ilisimamishwa akaingia trafk, alikagua gari Zima, akataka kutoka ghafra akaja kunisimamisha nikasimama akaomba nishuke mara moja nyie sijui nini kinaendelea mwenzenu...
Itaendelea...��
Full sh 1000
Njoo WhatsApp katika namba 0683944333.