"Machoni Mwangu Kuna Jibu"
π
Usiku huo haukuwa wa kawaida kwa Zainabu. Alikuwa amekaa juu ya dari ya ghorofa ya pili ya hosteli yao, akitazama anga lililojaa nyota. Kilio cha ndani kilikuwa kimya, lakini macho yake yaliwasema yote. Alikuwa amechoka na kubeba hisia ambazo hazina jibu, moyo wake ukimuita mtu mmoja tu β Ayoub.
Ayoub alikuwa kijana mnyenyekevu, mwenye akili, mwenye ndoto kubwa, lakini pia mwenye ukimya wa kuumiza. Aliongea kwa macho zaidi ya mdomo, na kila alipomtazama Zainabu, kulikuwa na kitu ambacho hakijawahi kusemwa.
Zainabu alijiuliza tena na tena, "Hivi ananipenda au ananionea huruma tu?" Kila mara Ayoub alipokuwa karibu naye, moyo wake ulipiga kwa kasi isiyo ya kawaida. Alimpa kila dalili, kila ishara, lakini Ayoub hakuwa amesema lolote. Si ndiyo wanaume wa sasa? Wanaacha moyo wa mwanamke ukitafakari hadi uchoke.
Siku moja, baada ya somo la jioni chuoni, walitembea wawili kando ya njia ya miembe. Ukimya ulikuwa mwingi, lakini ulionekana kuwa na maana.
βZaiβ¦β Ayoub aliiita kwa sauti ya taratibu, kana kwamba alikuwa anapima uzito wa moyo wake.
βNaam?β alijibu huku moyo wake ukicheza ngoma ya matarajio.
Ayoub alitazama mbele kisha chini, akatazama tena nyota, na mwishowe akasema, βKuna watu hujua wanachotaka, lakini hukosa ujasiri wa kusema.β
Zainabu alisimama. βNa wewe je? Uko katika kundi hilo?β aliuliza.
Ayoub alimwangalia kwa macho yenye huzuni, kisha akasema, βSema kama unanipendaβ¦β
Zainabu aliduwaa. Kwa mara ya kwanza, maneno yale yalikuja kama radi angani. Hakujua kama ajibu kwa moyo au kwa mdomo, kwa sababu tayari moyo wake ulikuwa umesema muda mrefu uliopita.
Usikose sehemu inayofuata......
https://chat.whatsapp.com/F6Rgb34kPMFFcunjm4sSxO?mode=ac_t.