Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Nilitaka kuondoka mzee akaniambia... Inaendelea... Sehemu Ya 15

31st Jul, 2025 Views 6



mzee akaniambia kabla hujaondoka achana na mke wangu,haya ondoka haraka na upesi. Niliondoka bila kuonana na tina lakini nilikuwa nawaza au mke wa yule mzee ni sakina maana nilikuwa sifahamu kama sakina ameolewa au hajaolewa. Wakati nipo barabarani narudi nyumbani na kichwani mawazo mengi, lilikuja gari na kusimama karibu yangu nilitaka kukimbia lakini dereva wa ile gari alishusha kioo na kuniambia vipi au umenisahau!? Nilipomuangalia vizuri alikuwa ni yule jamaa ambaye alikuwa ananiletea bahasha kipindi cha zamani wakati ule tunaanza mahusiano na sakina.

Yule jamaa akaniambia twende unaitwa na boss sakina, Dah nikaona labda ana kitu kingine cha muhimu, Ikabidi nikubali nikaingia kwenye gari yule jamaa akanipeleka hadi sehemu ambayo yupo sakina, Tulimkuta sakina yupo kwenye baa kubwa ambayo huwa inatumiwa na matajiri kwenye starehe, Nilimkuta sakina akiwa anakunywa soda kama kawaida yake,

Mwanamama sakina akaniambia kaa hapa tuburudike, Nilikataa, Sakina akaniambia kaa sababu najua hujaonana na tina na kama unataka kuonana na tina lazima kwanza uongee na mimi,

Nilikaa na kumsikiliza sakina, Kwanza alianza kwa kunipa pole, Akaniambia pole kwa msiba wa mama yako sababu najua ni maumivu kiasi gani mtu huyapitia pale anapofiwa na mzazi, lakini pia mama yako alikuwa ni mpole sana, ila niliumia baada ya kusikia kifo chake, sababu alifariki ghafla sana. Mwanamama sakina aliongea mengi hadi kuhusu mimi na tina, kumbe kipindi kile tina alikuwa anakuja nampeleka guest kumbe yote sakina anayajuwa, Hadi mimi kutekwa.

Alipomaliza kuongea nikamuuliza yule mzee aliyenikataza nisionane na tina ndio mume wako? sakina alicheka kwanza kisha akanijibu ndio,yule ni mume wangu.

Palepale nikagundua kumbe zile pesa ambazo ziliibiwa ndani hadi kupelekea mzee kuzimia, Kumbe sakina ndio alikuwa anachukuwa na kuleta kwenye biashara zake, harafu kingine nikawa najiuliza anasema mama yangu alikuwa mpole wakati sakina hajawahi hata kufika kwetu wala kuonana na wazazi wangu, hii nayo ilinipa mshangao kidogo!! Nilimuuliza sakina kwani ulikuwa unafahamiana na mama yangu, Sakina akanijibu niliwahi kufahamiana nae hapo kabla.

Nikamwambia sakina yote sawa lakini kama wewe ndiye ulikuwa unaiba pesa za yule mzee kuwa makini sana, sababu washindani wadogo wadogo wameshatoka nje ya mchezo, Sakina aliona ni maneno ya kawaida, akaniambia nisiwe na wasiwasi kwakuwa nilimfanyia kazi kubwa kuhusu biashara zake sakina akaniambia atanipatia mtaji ili nianze biashara yangu,

Tukaendelea na maongezi, Baada ya muda kidogo akafika rafiki yake na sakina, Yule rafiki wa sakina alifika na kuanza kuniita shemeji huku ananipa pole kwa kupotea siku nyingi, Kisha akatoa simu yake na kuomba apige picha na mimi, Kiukweli mimi nilikuwa sifahamiani na yule rafiki yake lakini ndio hivyo nilishangaa tu ananizoea na kuniita shemeji, Sakina akaniambia usiogope huyo ni rafiki yangu wa muda mrefu sana, Rafiki wa sakina alianza kupiga selfie/picha na mimi mara apige amenikumbatia, Lakini mimi nikachukulia ni mambo ya kawaida tu,

Tumekaa pale sakina akaniambia nije siku inayofuata yeye atanikutanisha na tina ili niongee nae, na sehemu ya kukutania ni kule kwenye hoteli yake ya kifahari, Nikamwambia sawa nitakuja,lakini nikaona muda unaenda na kule ninapoishi ni mbali, Ikabidi niwaage na kuwaacha pale lakini wakati nataka kutoka sakina alitoa kiasi cha laki mbili na kunipatia, Niliikataa pesa ya sakina na kumwambia baki nayo. Sababu na mwanzo alianza kwa kunipatia pesa mwisho nimejikuta nateseka,

Nilitoka kwenye ile baa na kuelekea sehemu ambayo naweza nikapata usafiri wa kunisogeza kule kwangu, Lakini wakati natembea nilianza kuhisi kama kuna mtu ananifuatilia ilibidi niongeze mwendo lakini nikaangalia pembeni yangu nikamuona mtu na yeye anazidi kuongeza mwendo ilibidi nianze kukimbia na yule mtu alianza kukimbia, Nikagundua kumbe ananikimbiza nilianza kukimbia huku napita kwenye vichochoro vya pale mjini, lakini wakati nazidi kukimbia niligundua kumbe wapo wengi wengine wakawa wamenizunguka kwa mbele, Nilikimbia hovyo nikajikuta nimetokezea sehemu wanayotupa takataka/majalalani Nilishtukia nimepigwa teke na kuanguka chini wakati nataka kusimama ili nijitetee mmoja wa wale walionipiga alitoa bastora na kuniambia (tulia)

Nilitulia na kuweka mikono yangu kichwani nikijua leo nakufa. Alifika kijana mmoja ambaye ni kiongozi wao lakini kwa mwonekano ni kama vile tunalingana umri, Alifika na kuniuliza kwa nini unatembea na mama yangu, harafu kingine umemrubuni mama yangu hadi anatumia jina lako kwenye makampuni yake kwahiyo unataka kuja kumfirisi, nyie ndio vijana ambao mnatembea na wamama waliowazidi umri ili mpate pesa, brother pesa haitafutwi kwa namna hiyo, harafu inaonekana hili jina la sadiki unalitumia lakini sio jina lako, yaani umeamua kutumia jina langu ili uwe mmiliki wa mali za mama yangu nakwambia hilo haliwezekani na halitatokea kamwe,

Aliichukuwa ile bastora na kuielekeza katika kichwa changu,lakini wakati anataka kufyatua risasi,,,simu iliita mfukoni mwake aliitoa na kupokea, Kisha aliongea machache na kunipatia niongee na yule aliyepiga, Kumbe alikuwa ni sakina, Sakina akaniambia usiogope huyo ni mtoto wangu lakini naona anafanya mambo ya kipuuzi,lakini hawezi akakufanya chochote sababu nimeshamwambia akuache...

(ukweli ni kwamba huyu ni mtoto wa sakina na yeye anaitwa sadiki lakini pia ameshagundua kwamba mimi nina mahusiano ya siri na mama yake na anahisi mimi nataka kumiliki mali za mama yake, lakini kwa nini sakina alinipa jina la sadiki ambalo ni jina la mtoto wake??)

...Nilipomaliza kuongea na sakina kupitia simu nikampatia mwenye simu, Kwakuwa mama yake amesema nisifanywe chochote, ilibidi waniache niondoke.

Nilifika nyumbani kwangu usiku, Asubuh palipokucha nilikiwa bado nimelala alikuja mtu na kunigogea mlango nilitoka na kufungua kumbe alikuwa ni Edina, Alinisalimia na kuniuliza mbona bado umelala au unaumwa, Nikamjibu hapana siumwi ila nimechoka tu, Akaniambia jana nilikuletea chakula lakini sikukukuta kingine pale nyumbani wanatafuta kijana wa kuwa anawauzia mihogo yaani anachimba na kupakia kwenye baiskeri na kuwa anatembeza mtaani,kwahiyo kama kuna kijana unamfahamu ni mwaminifu utanijulisha, Nikamwambia sawa nitaangalia, Lakini wakati huo mwanaume naelekea kuishiwa ile pesa niliyotokanayo kijijini, Edina akasema harafu usiondoke chakula chako cha jana bado kipo, Dah nikaona mambo ya kulishana vipolo asubuh,,,Mh sawa,

Edina akawa amenilete chakula kumbe alikuwa amepika asubuh ileile, Nilikula nikamwambia badae naenda mjini nadhani naweza nikapata na mtu wa kuuza mihogo yenu.

Ilipofika mida ya saa tisa ikabidi niende mjini kwa ajili ya kwenda kuonana na tina, Sababu sakina aliniahidi kunikutanisha na tina, Nilitoka nyumbani na kuelekea kule kwenye hoteli ya sakina, Nilifika na kumkuta tina akiwa peke yake amenisubiri, Nilipomuona tina nilimsogelea na kwenda kutaka kumkumbatia, Lakini tina alinisukuma na kunitupia ile simu yangu ambayo niliipoteza kipindi kile nimetekwa...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~

Like ziwe nyingi ili nipate nguvu ya kuendelea....
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Nilitaka kuondoka mzee akaniambia... Inaendelea... Sehemu Ya 15  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-nilitaka-kuondoka-mzee-akaniambia-inaendelea-sehemu-ya-15
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest