Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Sakina akawa ameniambia inabidi nifanye mpango wa kuhamia mjini... Inaendelea... Sehemu Ya 9

31st Jul, 2025 Views 4



Kuhamia mjini ili niwe karibu yake. Siku inayofuata mwanamama sakina akanitumia pesa kiasi cha laki tatu akaniambia nifanye maandalizi ya kwenda mjini, Sehemu ya kwenda kukaa ipo na tayari ameshaniandalia. Lakini wakati huo mimi na tina mapenzi yamenoga mpaka tukapanga tina akimaliza masomo tutafunga ndoa, Lakini muda wa kurudi chuo ulikuwa umekaribia,

Niliona nisije nikaondoka nyumbani ghafla ilibidi nikae na wazazi wangu na kuwaambia nataka kwenda mjini nimepata kazi ya kuosha magari, Baba alionekana kama kutokupendezwa na mpango wangu wa kutaka kuondoka pale nyumbani maana aliona kazi zitakuwa haziendi, Lakini akanikubalia. Nilimtafuta tina na kuongea nae nikamwambia na yeye kwamba nimepata kazi ya kuosha magari, Hivyo muda wowote na mimi naenda mjini,

Kwakuwa tina nayeye muda wa likizo ulikuwa unakaribia kuisha tukapanga safari tuondoke kwa pamoja, Ilipokaribia siku ya kwenda mjini nilimpigia mwanamama sakina na kumwambia aniongeze pesa maana ile laki tatu niliigawa nyingine niliwaachia pale nyumbani,harafu nikanunua na mavazi ili niende mjini nikiwa safi, Lakini tina na yeye nilimnunulia nguo pamoja na kumpatia pesa kwa ajili ya kufanya maandalizi ya safari kuelekea chuo, lakini pia safari tutakuwa wote.

Wakati huo nilikuwa napata pesa kutoka kwa sakina kwahiyo nilikuwa namhudumia tina kwa kupata pesa kutoka kwa mwanamama sakina, Lakini tina alikuwa hajui kama nina mahusiano ya siri na mwanamama sakina,na sakina alikuwa hajui kama nina mahusiano ya siri na tina, Wakati mwingine tina alikuwa anashangaa kuniona nina pesa lakini sina kazi ya maana pale kijijini,

Siku moja kabla ya safari sakina akawa amenitumia pesa nyingine kiasi cha laki mbili, Sakina akaniambia amuagize mtu aje anichukuwe na gari, lakini nikamwambia nitapanda basi. Sababu tayari nilikuwa nimepanga kusafiri na tina. Maandalizi yakawa yamekamilika ilipofika asubuh na mapema nikabeba kila ninachoona kinanifaa na begi langu mgongoni nikampigia tina na kumwambia tukutane pale senta kwa ajili ya kusubiri basi, Basi haikuchelewa tukapanda na kuanza safari kuelekea mjini. Wakati tupo njiani sakina alinipatia namba ya mtu ambaye atanipokea nikifika,

Tulipofika mjini kabla sijampigia yule mtu ambaye anakuja kunipokea, Nikafanya kwanza mpango wa kuagana na tina ikabidi nimpatie tina kiasi cha laki moja kwa ajili ya matumizi ya pale chuoni, Tina akachukuwa usafiri wa kumpeleka chuo. Mimi nikampigia yule anayekuja kunipokea nikamwambia tayari nimeshafika, Akaniambia tulia hapohapo nakuja kukuchukuwa.

Baada ya muda yule mtu alifika pale stendi na kunichuwa nikaingia kwenye gari akanipeleka kwenye hoteli moja kubwa sana. Nilikuwa nashangaa sababu pia ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika mjini. Lakini pia wakati huo nilikuwa na namba ya dada yangu ila sikumtafuta. Tuliingia kwenye ile hoteli na ilikuwa ya ghorofa tukaingia kwenye lifti tukapanda hadi juu, Yule niliyekuwa nae alikuwa tayari ameshanichukulia na chumba, Alinipeleka hadi kwenye kile chumba harafu yeye akaondoka.

Nilimpigia sakina lakini hakupatikana, Nikaanza kujiuliza isije ikawa kanitelekeza. Usiku ule nililala peke yangu. Kesho yake asubuh na mapema niliamka na kuanza kuangalia mazingira ya pale maana nilikuwa juu ya ghorofa, Lakini hadi muda huo simu ya sakina haipatikani,

Nilikaa pale hotelini hadi mida ya saa nne ndio sakina akafika, Alifika na kunikumbatia huku akinipa pole kwa kulala peke yangu, Nilitamani sakina anipoze kwa kunipatia penzi, Nilimbeba mwanamama sakina hadi kitandani nilitupa tauro langu na kubaki na bukta, Nilikuwa tayari nimeshakamia kuburudika na mwanamama sakina, Lakini akaniambia nisiwe na haraka tuongee kwanza kuhusu biashara. Dah aliniboa kwakweli,

Ikabidi nimsikilize akaniambia nichague kazi ambayo itanifaa pale mjini hata kama itakuwa na mtaji wa mamilioni. Mimi kichwa changu kilikuwa hakipo kibiashara kabisa ilibidi niunganishe ule mpango wangu wa kuosha magari, Nikamwambia naomba nipate sehemu ya kuosha magari hata kama nitakuwa na vijana wa kunisaidia sawa. Mwanamama sakina alishaanga sababu alitegemea pengine ningetaja hata kuwa na kampuni, Lakini akaniambia sawa kwakuwa ndio kazi unayoona ni nzuri na unaiweza. Sakina akaniambia atanitafutia eneo na atanipatia mtaji wa duka la spea za magari Inamaana kwamba kutakuwa na garage pia. Sakina akaondoka na kuniacha pale hotelini.

Nilikaa pale hotelini zaidi ya wiki lakini sakina alikuwa akiniletea zile bahasha zake nampangia mipangilio ya kugawa pesa,na anapeleka kwenye biashara zake. Lakini nilijaribu kumuulizia kama ameolewa au alishawahi kuolewa,ila alikuwa akinijibu kwa kunizuga na kunisahaulisha. Wakati mwingine nilikuwa nashindwa kabisa kuelewa malengo ya sakina maana nikitaka kulala nae yeye hakosi visingizio hadi nikawa nahisi labda ana magonjwa mwilini mwake, Lakini pia nilikuwa bado nawasiliana na tina,

Baada ya siku kadhaa za kukaa pale hotelini sakina akawa ameshapata sehemu ambayo mimi nitafanyia kazi,pamoja na nyumba nitakayokuwa naishi, Badae alikuja na kunichukuwa akanipeleka hadi hiyo sehemu ambayo mimi nitakuwa nafanyia kazi. Nilipapenda sababu mazingira yalikuwa ni mazuri harafu ilikuwa ni karibu na barabara kubwa, Alinikabizi funguo na kuniambia kuanzia sasa hapa patakuwa ni mali yako,

Tayari nikaanza kazi ya kuosha magari, Kadri siku zinavyozidi kwenda sakina ile biashara yake ya kuniletea bahasha ikawa ni mara kwa mara, Nikajikuta muda mwingi nafanya kazi yake kuliko kazi iliyonipeleka pale, Alipoona kazi zinanizidi aliniambia nitafute vijana wa kuwa wanaosha magari harafu mimi niwe napokea pesa tu, Nikatafuta vijana mimi nikawa napokea pesa kama boss.

Sakina alianza kuwa ananiletea pesa zaidi ya milioni sabini, Aliniletea hadi kifaa cha kuhesabia pesa, Zile pesa nikawa nazifanyia mahesabu kisha naziweka kwenye mzunguko wa kugawana harafu sakina anakuja kuchukuwa wakati ambao kila kitu kipo tayari. Ilibidi tuteue chumba kimoja cha siri kwa ajili ya kufanyia kazi,zile biashara za sakina. Lakini nikawa napokea pesa nyingi mpaka nikawa naogopa, Ilibidi nianze kufanya uchunguzi ili nielewe zile karatasi zina kazi gani na pesa zinatoka wapi na kupelekwa wapi.

Lakini wakati huo tina alikuwa anakaribia kupata likizo ya muda mfupi na alisema kabla hajaenda nyumbani kule kijijini,atakuja kwangu na kukaa siku kadhaa ndio aende nyumbani...

Itaendelea...✍🏻

Zinahitajika Like nyingi na comment za kutosha ili kuendelea...

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Sakina akawa ameniambia inabidi nifanye mpango wa kuhamia mjini... Inaendelea... Sehemu Ya 9  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-sakina-akawa-ameniambia-inabidi-nifanye-mpango-wa-kuhamia-mjini-inaen
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest