Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

NIPE YOTE DADY SEHEMU YA 43

27th Jul, 2025 Views 101



Niliendesha mpaka nyumbani nikakuta baba na mama wakiwa wamekaa huku wakiangalia tv , nilisalimia na kuuliza "Mama wanangu wako wapi?"

mama alikaa vizur na kusema "watoto ? kwani wako huku!?""

"Sijui nimeambiwa kuwa Nasra amekuja kuwachukua nikahisi watakuwa huku"

"Mh hapana hawapo huku na Nasra alitoka na mtoto toka asubuhi "nilivyosikia hivyo sikutaka mambo mengi nikageuka na kuondoka .

Nikiwa njiani nikampigia Selim hakupokea tena nikaona nipige ofisin kwake nikaambiwa hayupo ,aisee kichwa kilipata moto
Nikaona hapa nirudi nyumbani maana sijui wameenda wapi, basi nilirudi nyumbani nikaingia ndani na kupika chakula kisha nikaoga na kukaa kusubiri.

Saa tatu na nusu nikasikia geti likifungliwa nikakaa tayar kuwasubiri ,mara akaingia Nasra na watoto,aliingia moja kwa moja na kukaa akanisalimia kwa upole bila kuonesha hasira nikajibu,"Salama dada karibu sana "

"Asante nimewaleta mabinti wapumzike sasa maana wamecheza mpaka basi " nilitabasamu na kuwauliza watoto,"wanangu wazuri mme enjoy e!?" walijibu ndio na kuniadithia walikoenda kisha nikawaruhusu wakalale baada ya wao kwenda nikamgeukia Nasra na kusema.

"Mh bidada kulikoni ukaja kuchujua watoto bila ruhusa yangu.?"
Alitaka kujibu ila akasita baada ya kumuona Selim nilimuangalia tu, Selim alifika na kusalimia nikaona namna Nasra anavyomchangamkia nikawa kama vile simuoni akajimaliza mwenyewe pale mimi kimyaa.

Baada ya kusalimiana Selim alinisalimia kisha akaenda chumbani Nasra akabaki akimsindikiza na macho mpaka akapotea, nikamshtua kwa kukohoa kidogo na kusema.

"Unaonekana kuvutiwa sana na shemeji yako ni handsome ee!?" alicheka kwa aibu na kujibu "Hamna ila nilikuwa nafikilia kitu tu"

"Hata mimi naona kama unafikilia kitu mh hatujamaliza kesi yetu kulikon unakuja kuchukua watoto bila kunipa taarifa?"

Alikaa vizur na kujibu "samahani wakati niliokuja ulikuwa haupo nikawa nimempigia sm shem nikajua atakwambia"

"Ulikuja hukunikuta ila shemeji yako ulimkuta?, unajua Nasra nakufahamu vizuri kuliko unavyofikilia , huo upuuzi unaotaka kufanya uishie huko huko dada unaroho mbaya wewe hivi huoni aibu kumtaka shemeji yako?"

"Norah chunga mdomo wako mimi nimekuja kuwachukua watoto ili wakacheze na sio kumtaka mumeo na kingine hili swala lilishaisha toka miaka hiyo kwann unataka kunihukumu kwa mambo yaliyopita?"
kukuhukumu ? mimi nakuhukumu kwalipi haya unayoyafanya unafikilia siyaoni? hivi leo mimi nawezaje kuja kwako kumchukua mwanao bila kukupa taarifa ,kwa kigezo eti nimempigia mumeo mume wangu ndio ndugu yako au mimi? na kwann ulimpigia yeye na sio mimi kwamba mimi sina simu ?"

"Umenilewa vibaya Norah mdogo wangu ,mimi sikuona shida kuongea na Shem maana sio mzazi mwenzako tu bali ni mumeo wewe ni yeye ndio maana nikampigia hata hivyo ulikuwa chuo nikahofia huenda ukawa kwenye kipindi"

"Umejuaje kama sikuhizi nasoma ?" alijing'ta ng'ata maana hata nyumbani sikuwahi kuwaambia kwamba najiendeleza na masomo sio nyumbani tu hata ukweni hawajui sasa kajuaje kama ninasoma, nilivyoona yuko kimya nikamuuliza "vp umekosa chakuongea ?"

"Am hapana ila mama mkwe ndio ameniambia "
"Ooh sawa , haya umesharudisha watoto unaweza kwenda mda umeshaenda au nikupe hifadhi ?"

"Hapana nitaondoka "

'"Vizur alafu kabla hujaondoka naomba uweke distance na wanangu na usije kurudia kuja kuwachukua bila ruhusa yangu nadhani umenielewa"

aliinuka na kumuita mwanae akaondoka , nilitoka seblen na kwenda chumbani nikafika na kukuta Selim akiwa anaoga nikatoka na kwenda kuchukua chakula nikatenga chumbani na kukaa kumsubiri ,haikuchukua mda akatoka akaanza kujichekesha anajua alichofanya nikaona hapa leo tutaambia vizur nikainuka na kufunga mlango akasema .

"Vp mrembo wangu mbona unafunga mlango ?''

"Ulikuwa wapi mpaka ukashindwa kupokea sm zangu ?'"

"kumekucha ,sikia mke wangu nilikuwa kwenye chakula cha jioni na rafiki zangu "

"Kwa hiyo siku hizi ukiwa na marafiki zako hupokei sm zangu?"

"hamna mke wangu ila sikuisikia alafu niliisahau sm kwenye gari ndio maana haikupokelewa"

"Selim kuna kitu unanificha ?"

"Hapana mke wangu kwann nikufiche ni hivyo tu"

"Nauliza tena kuna kitu unanificha ?"" aliweka tawel kitandani na kunifuata akitaka kunishika nilikwepa na kuongea kwa hasira .

"Niambie ulikuwa wapi maana najua haukuwa na marafiki zako wala ofisin haukuwepo "

"mama yangu nakwambia ukweli nilitoka na rafiki zangu kama huamini muulize Jabir "

"Selim mwizi anamjua mwizi mwenzie nimbie ulikuwa wapi kabla sijaanzisha vurugu na inakuwaje unampa Nasra watoto akazunguke nao huko nikiwa sina taarifa yoyote ,umeanza lini kwenda nje ya utaratibu wetu?"

Alinywea kama paka alienyimwa maziwa nikajua huyu kuna mahari ametoka wala hakutoka kwa rafiki zake wala ofisin ,nilichokifanya nilichukua chakula na kutaka kukirudisha jikon nikasita kwanza na kumuuliza "Nasra kajuaje kama nasoma?"

Alijibu kwa upole "Nimemwambia mimi" nilitabasamu na kumwambia "Okay nimekusamehe " hakuamini akauliza mara mbili mbili nikamwambia ndio sio kwamba nimesamehe ila hilo bomu nitakalo mlipia leo dunia itashangaa
Full 1000
Whataapp 0657171961
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY SEHEMU YA 43  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-sehemu-ya-43
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest