Nikafika sitting room na kuanza kulia😭😭😭halafu sijui nalia nini😁kwamba nimeitwa housegirl au mke mwenzie😒Hakim akaja pale sitting room na kuanza kuniomba msamaha sijui nisiumie nafsi yule mwanamke washaachana muda tu,ni anaforce mambo tu na anafanya hivyo ili kuniumiza nisimjali🥺🥺🥺lakini wewe kuweza mimi roho ilizidi tu kumuuma halafu sasa ndio nishampenda Hakim naona wivu balaa😔😔😭Hakim alijaribu kunielewesha ila juhudi zake aligonga mwamba,
"Ndio maana mimi nilijua tu utakuja niumiza😭😭😭kwahiyo mimi siendani na wewe? Naonekana kama housegirl wako?"
"Kulthum mama nimekwambia yule ni mtu wa zamani,hivyo lazima aongee shit ili kukuumiza wewe moyo wako,wewe ni mke wangu thamani yako ni kubwa sana kwangu😘😘😘you are such a beautiful girl, nakupenda mpaka basi,hawezi kukufikia yule wewe cha kwanza ni mke na yeye atabaki kuwa zilipendwa"
"Achana na mimi,unaniona mtoto sana wa kudanganyika eeeeh...??"
"Nielewe,tusikosane kwa masuala madogo kama haya,bado tuna safari ndefu sana ya kuyafikia malengo ya ndoa yetu"🙏🏻🙏🏻
"Naomba uniache,sijisikii kuongea chochote na wewe"
"Mara tukasikia honi ya gari ,mimi sikutaka hata kwenda kufungua geti😔🥺nilihisi kama yule Agness karudi 😁😁😁🙆🏻♀️Hakim alienda na akarudi akiwa na rafiki ake Adam,ndie alikuwa amekuja nilifuta machozi Fasta🥺🥺🥺kabla shem Adam hajaona🤸🏻♀️🤸🏻♀️🤸🏻♀️tulisalimia na nilimchangamkia sana huwezi jua kama siko sawa🤔 ila aliniuliza mbona kama macho yangu yamekuwa mekundu😒nilimjibu kuwa macho yananiuma😩😩akasema hakai sana amepita tusalimia tu na anatukumbusha kuwa jioni ndio birthday party ya mtoto wake hivyo tusisahau kwenda,kisha akaaga na kuondoka
Nilirudia kununa upya😂😂😂ila Hakim akasema eti amependa nilivyoficha madhaifu yetu kwa mgeni😂🤭😔sikumjibu kitu mimi, nishamnunia😭😭😭😭😭😭baadae nikapika chakula cha mchana tukala😋😋😋tukajiandaa na kwenda tulipoalikwa,huko nako nilimchangamka sana tu,mnuno utaendelea tukiwa nyumbani 😁😁😁🤸🏻♀️kule tulilishana tulicheza wote huwezi jua nina vihasira vyangu
Kwakuwa ilikuwa party ya mtoto tu haikuchelewa kuisha, tukarudi nyumbani mapema sana,nilisusa kulala na Hakim nikaenda kulala chumba kile kingine(nilipokuwa nalala) asubuhi niliamka na kuandaa chai na kuendelea kufanya shughuli zingine,Hakim alivyoamka wala sikumsalimia😒😒😒mimi nimenuna bhana🥺🥺🥺
"Kulthum mke wangu,hivi mbona unataka tuishi kama wanyama tunaamka hata salamu hakuna,kama hatujuani"
"Wanyama kivipi? Na tusijuane kivipi? Wakati mimi nakujua wewe Hakim na wewe unanijua mimi Kulthum...!"
"Shut up....!" Alitaka kunipiga kibao akaghairi🙈yaani kingetua kwenye shavu langu sijui ingekuwaje 🥺🥺🥺
"Hivi kwanini unataka mimi nifikie hatua ya kukupiga? Mbona unanikosea adabu hivyo? usitake tuishi kibabe sana humu ndani...yaani unanikasirikia kwa mambo ya ajabu, kitu cha kuelekezwa hutaki, unapenda kushindana na mimi eeeeh....!?"nilinyamaza kimya ndugu zangu😂😂nijibu ili nipigwe...!?😂😂😂 zaidi tu machozi yalianza kunimwagika,ila machozi yangu sijui yana matatizo gani yaani yanawahi kumwagika hata kitu kiwe cha kawaida tu😂😂😂😂😂😂Hakim aliondoka bila kunywa chai sijui nae kasusa🤔🤔🤔
Nilishinda nyumbani nikiwa najisikia ovyo,uchovu kwa wingi...ukijumuisha na hasira na wivu basi nikashindwa kufanya kazi yoyote ile😂😂😂nililala tu nilipojaribu kunywa chai nikasikia kichefuchefu na kuitapika tu😩😩😩sijui nina nini....!? kimoyomoyo nishajua ushatabiri nilichonacho ndugu msomaji😂😂😂nilishinda kwa kutafuna tafuna vitu tu sikupika,njaa yenyewe sina😂😂😂Hakim alirudi na kunikuta nimelala kwenye sofa tu akanipa hi sikumjibu🤭🤭🤭yeye si alitaka kunipiga 😏😏asiniongeleshe😂😂😂😂😂
"Kulthum haujapika mke wangu?"
"Ndio sijapika"
"Why? unategemea nini? nile huko nilipo toka?"
"Kwani mimi ni mpishi? Kwani hotel zimewekwa kwa ajili ya nini..!?"🤔😩
"Unanijibuje?"
"Mimi naumwa,ndio maana nimeshindwa kupika"😩nilijiepusha na kipigo mapema 😂😂😂maana nilivyomjibu vile yasije nikuta ya asubuhi👐
"Unaumwa nini? Umeanza lini kuumwa?'' nikasema moyoni mbona kama haamini? kwamba namdanganya au?🤔🤔
"Tangu usiku"
"Okay pole" aliniacha na kwenda zake chumbani,mbona hata hajali pole kavu hivi😂😂😂👐👐👐nimeyatimba😩😩naye kanuna sijui 😔😔😔 jamani sa nitaishije mimi nilitamani anibembeleze🙆🏻♀️napenda akinibembeleza🥰🥰🥰
Nikawakumbuka wa kwetu kwanza nimtafute mama🤸🏻♀️nikampigia
"hello mwanangu"
"Shikamoo mama"
"Marahaba,vipi familia huko?"
"sisi wazima mama sijui nyiee huko"
"Nasi ni wazima kabisa"
"Nimewakumbuka sana 😔yaani acha tu"
"Jamani,hata sisi pia tumekukumbuka,ila inabidi uzoee maana ushakuwa na mji wako,ila unaweza omba ruhusa ukaja tuona mara moja sio mbaya"
"Sawa mama nitakuja tu usijali,ila najisikia ovyo sana leo"
"Pole,nini shida?"
"Mwili hata siuelewi kabisa, sijui maralia"
"Au mjamzito tayari mwanangu?"
"Mmmh....! sidhani.... kwanza hata najua dalili zenyewe"😔
"Unajisikiaje kwani?"
"Homa si homa,maralia si maralia mara kichefuchefu na uchovu"
"Oooh pole mama,labda ni maralia inaanza kesho uende kupima,na kama unahisi na mabadiliko mengine kwenye mwili wako basi pima tu na ujauzito"
"Sawa mama,kesho asubuhi nitaenda,halafu nitakupigia nikwambie"
"Sawa mwanangu,uwe na jioni njema....umsalimie mkwe wangu"
"Zimefika mama,msalimie baba na kaka Mustafa"
"kaka ako ameenda kwenye shughuli zake nitamsalimia akirudi" kakaangu wa mwisho bado alikuwa anakaa nyumbani wengine wawili wenyewe walishakuwa na miji yao
Nilipomaliza kuongea na mama,Hakim akawa ametoka sijui hata alipokuwa anaenda nami sikumuuliza niliendelea na yangu,ila nikasema itakuwa kanikasirikia vibaya mno na asiwe anaenda kwa yule Agnes🥺🥺🥺maana dada ametimia kila idara yule👐nilichomzidi sikuona,yaani Hakim ana akili kweli? amuache mwanamke mzuri vile anioe mimi....! nikakumbuka si tulifungishwa ndoa ya mkeka,pengine anaishi na mimi kunihurumia tu lazima aendelee kuwa na yule dada😭😭😭😭halafu mimi eti ndio namletea jeuri😁😁😁nilijikuta mnyonge sana🥺🥺nikajaribu kupiga simu yake akawa hapokei,nilivurugwa🙆🏻♀️🙆🏻♀️🙆🏻♀️
ITAENDELEA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.