Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SASHA (nauchukia mlango wa siri 01___02๐Ÿ˜ญ)

1st Aug, 2025 Views 41



Nash stories

Tsap 0773792227

Ep:1

Naitwa Sasha, asili yangu ni Muafrika...miaka yangu ni 49 ningependa unisome japo kidogo, kuna vitu natamani ujifunze kupitia Mimi... mwisho wa hadithi yangu nitafurahi kama utaniita Mwalimu kwa sababu haya mafundisho nayoenda kukupa ni maisha yangu halisi๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ.

Nilivyokuwa mdogo, Baba yangu alinisisitiza sana kuhusu elimu hivyo nilivyoingia darasani sikutaka mchezo nilisoma haswa.

Darasani nilikuwa kichwa kiasi kwamba Serikali ilinipeleka nje kujiendeleza na elimu ya chuo kikuu. Japo Mimi ni Muafrika lakini bado uzuri wangu ulikuwa tishio....

nilipata usumbufu sana kutoka kwa Wanaume lakini hawakunipata kwa sababu sikuwa nahitaji mahusiano kwa wakati huu, niliamini endapo nitajiingiza kwenye uhusiano basi nitapoteza muda mwingi kwenye starehe mwisho wa siku nitashuka kitaaluma, nauamini ule msemo usemao mshika mawili moja humponyoka, hivyo nilizingatia sana.

Nilinusurika kubakwa mara nne na Wanafunzi wenzangu, lakini hii haikunitisha kwa kuwa lengo langu lilikuwa ni kuiwakilisha vyema Nchi yangu nilizidi kupambana huku ni kiomba Malaika wangu Mlinzi anifiche dhidi ya watu wabaya.

Maombi yangu yalijibiwa sikupata usumbufu wala vitisho tena mpaka nilipomaliza masomo yangu Jijini Dar.

Nilirudi nyumbani kwetu nikiwa na ufahulu mzuri, familia yangu ilikuwa inajiweza...kwa kifupi Wazazi wangu wote walikuwa wanafanya kazi Serikalini, hivyo familia yetu haikuwa ikisumbuliwa na njaa ya pesa.

Baba na Mama walinifanyia sherehe kubwa kwa kurudi salama.... marafiki, ndugu na jamaa wote walialikwa. Ni kawaida yangu kupendeza, kwa kuwa sherehe ilikuwa inanihusu Mimi nilipendeza sana. Siyo kwamba najisifia lakini kioo huwa kinaniambia ukweli.

Zawadi nyingi zilitolewa na kila mtu alinipongeza kwa kurudi salama, sikuwa bubu nilishika kipaza sauti ni katoa neno la shukurani
"Nimefurahi kuwaona mahali hapa, nilihofia kuwa poteza kwa sababu hatukuwa na mawasiliano takribani miaka nane. Nashukuru kuona bado mnanikumbuka, kwa sasa nimerudi ikiwa kuna mtu atakuwa na jambo la siri la kuzungumza na Mimi au swali lolote mlango upo wazi karibuni sana....nawapenda na nina wathamini, ahsanteni" nilizungumza kwa sauti iliyotulia

Watu wote walipiga makofi....Baba alishika kipaza sauti kuwa shukuru watu wote waliofika, Mama alifanya hivyo pia. Sherehe ilimalizika kila mtu alishika njia kurudi nyumbani kwake.

Zawadi zote ziliingizwa chumbani kwangu, nilikuwa na shauku ya kuona nini vimefungwa kwenye maboksi... zawadi zilikuwa nzuri. Nilizipitia kisha nikapanda kitandani kulala uchovu ulitesa mwili wangu.
Kulivyo pambazuka asubuhi niliamka bado macho yangu yalikuwa mazito ....nilichukua simu yangu ya mkononi nikaangalia muda, ilikuwa ni saa tano asubuhi. Nilijisikia fedheha kulala muda mrefu namna hiyo, sijui nini kilinipata nilirudia kuyatazama yale maboksi tena... niligundua kuna boksi moja sikuwa nimeliangalia.

Nilishuka chapu kitandani nikalifungua.... nilishtuka ndani ya moyo wangu baada ya kuona pete pamoja na barua. Niliifungua barua haraka nione nini kimeandikwa

"Nakupenda, nipatie nafasi ya kukupenda ni kuoneshe furaha iliyojificha kwenye dunia ya mapenzi" ujumbe ulisomeka

Nilijikuta nikicheka kwa sababu mwandishi wa barua hii haelewi maana ya barua, alipaswa aache mawasiliano ili Kama nitakuwa nimevutiwa na barua yake niweze kumtafuta....kitu kingine hajiamini alipaswa atafute nafasi azungumze na Mimi uso kwa uso na si kuniandikia barua. Pia pete aliyoniletea ni kubwa inanilegea kama angenivika mbele za watu basi angeaibika na mwisho kabisa Mimi ni mweusi napendelea kuvaa mapambo ya Silver na si Gold kama alivyofanya yeye, kwa kifupi mtu huyu hajafanya utafiti kuhusu Mimi amekurupuka

Nilimuita Dada wa kazi anisaidie kutoa maboksi yote huku akikumbuka kupanga zawadi sehemu niliyomuelekeza. Niliingia jikoni kuandaa chakula cha mchana muda wa kunywa chai ulikuwa umepita.
Nikiwa jikoni nilishangaa kumuona Mama kwa sababu ulikuwa ni muda wa kazi alipaswa kuwa ofisini

"Tumealikwa nyumbani kwa Rais Golden kupata chakula cha mchana, jiandae sasa hivi Baba yako anakuja kutuchukua.... shika hii nguo nimekuletea" Mama alizungumza huku akinikabidhi mkoba wenye nguo

Rais Golden pamoja na Wazazi wangu ni marafiki wakubwa....hivyo mara nyingi wamekuwa na kawaida ya kula pamoja hasa muda ambao wanakuwa hawana majukumu mengi. Nilifanya kama Mama alivyosema.... niliingia bafuni ni kaoga kisha ni kavaa nguo aliyoniletea. Nilijiona kupitia kioo namna nilivyopendeza.

Dakika 30 hazikupita Baba alikuja kutuchukua.... sielewi kwanini lakini Mama alikuwa ananiangalia kwa kuibia.

"Simamisha gari mara moja kuna kitu nahitaji kuchukua" Mama alimuambia Baba
Gari ilisimamishwa kisha Mama aliingia Supermarket, hakumaliza hata dakika saba alirudi kwa kukimbia...nilitazama nione nini kanunua lakini sikuona kitu. Baba aliondoa gari, nilishangaa tu Mama ananiwekea lipstick mkononi...haah! ndipo nilielewa kwanini Mama alikuwa ananitazama sikuwa nimeuremba mdomo wangu. Niliachia tabasamu kwa namna Mama anavyonijali.

Tulifika nyumbani kwa Rais Golden, tulipokelewa vizuri sana....niliulizwa maswali mengi na Rais Golden kuhusu masomo yangu Jijini Dar

Nilimkumbusha ujio wetu ni kwa ajili ya chakula cha mchana na si maswali mengi. Baba na Mama walinitazama kwa jibu nililolitoa lakini Rais Golden alicheka sana huku akinibatiza jina la Mwanasiasa.

Tulikaribishwa kwenye meza ya chakula, Mke wa Rais Golden alikuwa kavalia mavazi ya jikoni kumaanisha yeye ndio kaandaa chakula, alitukumbusha tujisikie kama tupo nyumbani. Chakula kilikuwa kizuri sana na sikuona sababu ya kujivunga, Mama alinikanyaga mguu nilivyomuangalia machoni alinipa ishara ya ni punguze kula.
Sikutaka kumsikiliza kwa sababu nilikuwa na njaa.

Wakati na nyanyua kijiko nipeleke mdomoni, nilikutana macho na Kijana Mtanashati aliyekuwa kaweka earphones masikioni mwake, nilibaki kumtazama kwa sababu sikuelewa katokea wapi

"Nahisi chakula changu hakipo hapo....wakubwa shikamooni" Kijana huyu alizungumza vitu viwili kwa wakati mmoja huku akitoa earphones zake masikioni

"No...No... usinifanyie hivyo, njoo ujumuike na sisi, Baba Sasha... Kijana wangu amekuwa mbali na Mimi zaidi ya miaka 10 nahitaji aje kula hapa nisaidie kumshawishi" Rais Golden alizungumza huku akimuangalia Baba
Ndipo niligundua kijana huyu ni mtoto wa Rais Golden bila shaka jina lake ni Biden...

Biden alisogea kujumuika chakula pamoja nasi baada ya Baba kumsihi. Mama alinikanyaga kwa mara nyingine nilinyanyua kichwa kumtazama, macho yangu yalikutana na ya Biden na si Mama. Niligundua aliye ni kanyaga kwa wakati huu ni Biden na si Mama

Itaendelea

Whtsp 0773792227
Nash stories
Full 800

SASHA (nauchukia mlango wa siri 02๐Ÿ˜ญ)

Nash stories

Tsap 0773792227

"Sorry, nilisahau kukusalimia" Biden alizungumza baada ya kumtazama
"Usijali, siku zote mtu mweusi huchelewa kuonekana" nilizungumza

Baba na Mama waliniangalia kwa jibu nililotoa, Rais Golden na Kijana wake waliangua kicheko. Baba na Mama walicheka pia japo mwanzo walionesha kutofurahishwa

"Baba Sasha, nampenda binti yako sioni ajabu kwanini amekuwa Profesa kwa umri huo....kichwa chake kimejaa madini" Rais Golden alizungumza ya moyoni
Baba alishukuru kwa namna navyosifiwa

"Biden itapendeza kama ukimuonesha Sasha mazingira ya hapa, hata wewe unapaswa ujionee namna nyumba yetu ilivyo badilika....kwa kifupi kila kitu kimebadilika" Mke wa Rais Golden alizungumza akiwa anatoa vyombo mezani
Nilielewa watu wazima wanahitaji kuzungumza, hivyo Mimi na Biden hatukutakiwa kuwa hapa.

Kwa pamoja tulitoka nje tukaanza kuzunguka huku na kule
"Siku zote Mama huwa anatumia lugha chanya kuniondoa sebuleni pindi anapohitaji kuzungumza na Mzee" Biden alianza kuzungumza

"Kuna mazungumzo Mtoto hapaswi kusikia...ila kama unataka kusikia unaweza rudi kwa kunyatia usikilize, ila usikose furaha utakapo kuta una jadiliwa" Nilimuambia Biden

Biden alicheka kisha akasimama
"Hongera kwa kufikia kiwango cha kuitwa Profesa, kwa umri wako huo ulipaswa uwe bado unasoma lakini ulivyo na haraka umemaliza kila kitu"

"Ahsante, hongera pia kwa kufikia kiwango cha kuitwa Profesa" nilizungumza
"Umejuaje kama nimefikia kiwango hicho" Biden aliniuliza
"Siku zote wezi wakikutana kwenye sherehe hufahamiana haijalishi wamependeza kiasi gani, hivyo hivyo hata kwetu ni rahisi kufahamiana haijalishi tumekutana mazingira gani" Nilimjibu Biden

Biden aliachia tabasamu, aliendelea kunitembeza maeneo ya nyumbani kwao, kuna mahali hata yeye alikuwa ana shangaa kwa namna kulivyo badilika. Tukiwa bado tuna zunguka huku na kule nilisikia kishindo mfano wa miguu ya farasi ikikimbia....nilinyanyua macho ni katazama mbele. Moyo wangu ulishtuka baada ya kuona bonge la Mbwa mfano wa ndama aliyenona likija kwa kasi usawa wetu.

"Usikimbie, Tom kanusa harufu yangu hivyo anakuja kunisalimia....hakika hazeeki" Biden alizungumza kisha akanivuta mkono ni kae pembeni nilifanya hivyo. Tom(Mbwa) baada ya kufika sehemu tulipo alimrukia Biden...kwa lugha nyingine walikumbatiana.

"Nimefurahi kuona unaendelea vizuri, kama unavyoona nipo poa sina shida yoyote.... kuanzia sasa utakuwa unaniona mara kwa mara sidaiwi na shule tena" Biden alimuambia (Mbwa)

Tom(Mbwa) baada ya kuambiwa hivi aliondoka, sijui nini kilimpata alifunga breki kisha akanirudia Mimi nilipokuwa nimesimama....aliniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaondoka

"Kamaanisha nini kuniangalia namna hiyo au hajapenda kuniona na wewe, anaonekana anajisikia eeh hajanisalimia zaidi ya kunikadria kwa macho ya dharau" nilizungumza

"Pengine ndio maana Rais Golden anakupenda, una maneno ya kufurahisha....ni mara yangu ya kwanza kusikia Mbwa ana macho ya dharau, tukionana kwa wakati mwingine nitafurahi endapo nitasikia hadithi kuhusu Mbwa anayejisikia..." Biden alizungumza kisha akaondoka

Nilitaka kumuita lakini nilijizuia, niligeuka nyuma nilikutana na Kijana aliyevalia sare kama Polisi hivi
"Ni muda wa kuondoka Wazazi wako wana kusubiria kwenye gari"

"Nashukuru kwa taarifa..." Nilimjibu kisha ni kamfuata kwa nyuma, nilijisemea moyoni Biden atakuwa alimuona huyu Kijana ndio maana alifupisha mazungumzo...

Mama alivyoniona aliachia tabasamu macho yake yalionekana kuzungumza vitu vya furaha. Baada ya kuingia tu kwenye gari safari ilianza. Njia nzima Baba na Mama walizungumza mambo yanayohusu kazi. Niliweka earphones zangu masikioni ni kaanza kusikiliza Mziki.

Tulivyo fika nyumbani, nilipitiliza chumbani kupumzika....Mama alikuja kuniambia chakula cha usiku tutasaidiana kuandaa hivyo nisilale sana. Niliweka alarm kwani tofauti na hapo nisingeamka. Saa kumi na mbili ilivyo fika nilienda jikoni tayari Mama alikuwa kashaanza kupika mboga

"Nisaidie kutengeneza juisi.... vingine nitafanya mwenyewe" Mama aliniambia

Nilichukua matunda ni kaanza kukata kata
"Biden ni kijana mzuri, nimempenda hakika...." Mama alizungumza

"Ulipaswa umuambie pale pale sebuleni ukiniambia Mimi haisaidii kwa sababu sijui ni lini tutakutana nimpe hizi habari" nilizungumza

"Kwani hamjabadilishana namba?..." Mama aliniuliza
"Namba huwa hazitolewi ovyo hasa kama watu hawana vitu vya kuzungumza" Nilimuambia Mama

"Ulikuwa una kula kama una kimbizwa siyo ajabu kwanini hajachukua namba zako" Mama alizungumza
"Hiyo ndio asili yangu nikiwa na njaa... kitu kingine hata kama angenipa namba yake isingekaa kwenye simu yangu kwa sababu sina vitu vya kuzungumza naye" Nilimuambia Mama

Mama hakuzungumza chochote tena aliendelea kupika mboga yake, hata nilivyoongea habari zingine alijitia hasikii. Najua Mama yangu anatamani Mimi na Biden tuwe marafiki....ni kawaida ya familia zenye ukaribu kutamani watoto wao wawe na ukaribu pia.

Niliendelea kutengeneza juisi baada ya kumaliza niliingia bafuni kuoga... na mida ya usiku ilivyofika tulikaa mezani kupata chakula kama familia

"Mama, ile mizigo ulizoagiza ndio zimefika sasa hivi" Dada wa kazi alimletea Mama taarifa

"Kanisaidie kuikagua" Mama aliniagiza Mimi
Niliweka kijiko mezani kisha ni kaongozana na Dada wa kazi, yalikuwa ni mashuka kutoka Jijini Pali...mbali na Mama yangu kufanya kazi Serikalini ni mfanya biashara.
Nilikagua mizigo yote baada ya kuridhika niliwaruhusu waondoke.

"Dada samahani..." Dada wa kazi aliniambia wakati nataka kuingia ndani
"Niambie...." Nilizungumza
"Kuna mtu alileta maua kwa ajili yako....nilitaka kugoma kuchukua lakini aliniambia endapo atagundua nimegoma kupokea maua atakasirika" Dada wa kazi alizungumza
Niliachia tabasamu kwa maneno ya uongo aliyopatiwa na mtu aliyeleta maua,

"Chumbani kwangu pako wazi nenda ukaweke...." Nilimuambia Dada wa kazi kisha ni karudi sebuleni kula

Nilisahau kumpa Mama mrejesho kuhusu mashuka yake niliendelea kula.
"Nitajuaje kama mizigo iliyoletwa ni mizuri au mibaya kama unaendelea kuweka vijiko tu mdomoni" Mama alizungumza ndipo nilishtuka

"Mashuka yaliyo letwa ni mazuri, nitanunua pia" Nilimuambia Mama
Baba na Mama walicheka sielewi kitu gani kiliwa furahisha
Baada ya kushiba nilielekea chumbani kwangu, macho yangu yalitua kitandani kwa sababu kuliwekwa maua.
Yalikuwa ni maua ya bei ndogo sana...niliyakaugua kwa lengo la kuona ujumbe ulioambatanishwa

"Wewe ni mrembo kuliko Wanawake wote niliowahi kuwaona.... nakupenda Sasha naogopa kujitokeza kwako kwa sababu Mimi siyo hadhi yako. Nahofia kukataliwa" Ujumbe ulisomeka

Mwanaume anayejiamini huwa hatawaliwi na hofu kama za huyu Kaka aliyejieleza kwenye barua. Nilimfuata Dada wa kazi ni kampiga marufuku kupokea vitu kwa ajili yangu. Aliniomba msamaha kumaanisha tumeelewana....niliyatupa maua dustbin kisha ni kapanda kitandani kulala

Kulivyo pambazuka niliwahi kuamka kuna vitu nilitaka ni kachukue Supermarket kabla ya jua kuwa kali. Nyumbani kwetu kuna magari ya kutosha lakini
sikutaka kutumia gari....nilitembea taratibu huku ni kijiambia wakati wa kurudi nitapanda bajaji.

Sielewi kibaka alitokea wapi lakini nilipokonywa pochi....nilimshuhudia Kijana aliyeniibia akiongeza mwendo wa Pikipiki ndio mara ya kwanza kuona wizi wa namna hii. Ilikuwa ni asubuhi hivyo barabarani kulikuwa na watu wachache hata ningesema nipige kelele za mwizi nisingesaidika.

"Nakuletea pochi yako sasa hivi" Mwanaume nisiye mfahamu aliniambia kisha akasimamisha bajaji tayari kwa kumfukizia Mwizi

Niligeuza miguu nirudi nyumbani kwa sababu sikuwa na pesa ya kutumia Supermarket tena, sikumuamini Mwanaume aliyesema ataniletea pochi kwa sababu pindi atakapoishika itamvutia tu hivyo hataweza kutunza ahadi yake. Kilichoniuma ndani ya pochi yangu ni simu kwa sababu ilikuwa na namba za watu muhimu, akili ya kwenda Polisi iliniijia

"Dada, pochi yako hii hapa na mtu aliye kuibia ni huyu Kijana'' Nilishtuliwa na sauti nikiwa katika kufikiria
Ilinilazimu kegeuka nyuma ni yaone maajabu ya Musa.
Nilikutana macho na Mwanaume aliyemshika kwa nguvu Kijana mdogo...pochi yangu ilikuwa mikononi mwa Kijana aliyesemekana ni Mwizi

Itaendelea

Whtsp 0773792227
Nash stories
Full 800.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SASHA (nauchukia mlango wa siri 01___02๐Ÿ˜ญ)  >>> https://gonga94.com/semajambo/sasha-nauchukia-mlango-wa-siri-01___02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest