Saa tatu asubuhi, katika ofisi ya mwanasheria mdogo wa jeshi iliyopo ndani ya kambi ya Lugalo, Giann na Dativa walikuwa wameketi upande mmoja wa meza ya mbao. Mbele yao, palikuwa na karatasi ya mkataba wa ndoa, ulioandaliwa kwa mujibu wa sheria za kijeshi.
“Mmekubaliana kufunga ndoa ya kiserikali? Mwanasheria aliwaangalia wote kwa zamu.
“Ndio,” walisema wote wawili kwa pamoja, ingawa sauti ya Dativa ilikuwa dhaifu kiasi.
Giann alichukua kalamu, akasaini kwa msimamo na ujasiri. Alimwangalia Dativa.
“Your turn,” alisema kwa sauti ya upole, lakini yenye heshima.
Mikono ya Dativa ilikuwa inatetemeka kidogo aliposhika kalamu. Aliangalia jina lake na nafasi ya sahihi… na kwa sekunde kadhaa, alisita.
Kisha, kwa mkono ule ule wenye wasiwasi, alitia saini yake rasmi.
Saini ya mwanzo ya mkataba… lakini huenda pia ilikuwa saini ya mwanzo wa safari mpya ya moyo.
BAADA YA KUSAINI
Walipotoka nje ya ofisi, kulikuwa na ukimya mzito kati yao. Walisimama kwa muda, kando ya bustani ya maua ya kijani. Giann alivaa miwani ya jua na kugeuka kumtazama.
“Asante kwa kufanya hili,” alisema. “Naahidi nitakuheshimu.”
Dativa alijibu kwa tabasamu dogo. “Usijali. Naamini tutapita salama.”
Mara simu ya Giann ililia — ilitoka kambini.
“Samahani, kuna dharura ya kijeshi. Nimeitwa kwa mazoezi ya ndani ya saa mbili.”
“Mazoezi ya aina gani?” Dativa aliuliza kwa wasiwasi.
“Survival camp. Lazima twende porini kwa siku mbili. Na… kwa kuwa sasa wewe ni mke wangu wa kisheria, kuna ruhusa uje kwenye eneo la karibu kama kuna sababu ya kiafya au dharura.”
Siku hiyo hiyo, saa kumi alfajiri, Giann alikuwa porini, kwenye mazoezi ya survival. Ghafla, alijeruhiwa mguuni alipokuwa akikwepa nguzo ya mti kwenye mbio. Hali ilikuwa mbaya — alikuwa akivuja damu.
Kwa haraka, afisa wa afya wa kambi alimpigia Dativa kama mtu wa dharura.
“Bi Dativa, mumeo ameumia. Tumeleta gari hadi kijiji cha karibu, lakini anahitaji uangalizi wa karibu. Tunahitaji ruhusa ya familia ili tumpeleke hospitali ya nje ya kijeshi.”
Dativa hakuweza kukaa kimya. Aliinuka haraka kutoka kitandani, akavaa koti na kuelekea huko.
Katika chumba kidogo cha wagonjwa, Giann alikuwa amelala na jeraha limefungwa vibaya. Dativa alifika akiwa na hofu usoni, macho yake yakiwa na wasiwasi. Alikaa pembeni yake, akamshika mkono.
“Unaendeleaje, Giann?” aliuliza kwa sauti ya chini.
Giann alitabasamu kwa uchovu. “Ndoa haijadumu hata masaa ishirini, na tayari mumeo yuko ICU…”
Dativa alicheka kidogo kwa huzuni. Akamgusa usoni polepole, mikono yao ikishikana.
“Nilihisi vibaya. Nilikuona kwenye ndoto jana usiku. Nilijua kuna jambo…”
Giann akamshika mkono, akavuta taratibu hadi kwenye kifua chake. “Sitaki kukuumiza, Dativa… lakini sijui kwanini unapunguza maumivu yangu kwa kunigusa tu.”
Wakati huo, joto la mwili lilikuwa likipanda. Ndani ya chumba kile, kimya kilitanda. Hakukuwa na daktari, wala kelele za mashine — ni mapigo ya mioyo yao tu.
Dativa alisogea karibu zaidi, uso wake karibu na wake. Giann alijaribu kuinuka, lakini maumivu yalikuwa makali. Alimgusa shingoni, kwa vidole vyake baridi lakini vyenye shauku.
“Naweza… nikakubusu?” aliuliza kwa sauti ya kuvuta pumzi.
Dativa hakusema. Badala yake, alifumba macho, akasogeza midomo yake karibu na yake… na kilichofuata kilikuwa busu la pole, la kwanza, la kuunganisha mioyo ya watu wawili waliokutana kwa mkataba… lakini sasa miili yao ilianza kuandika mkataba mwingine, wa tamaa na mapenzi.
Je, hisia hizi zitadumu zaidi ya jeraha? Au ni huruma tu ya muda mfupi? Na je, Dativa ataanza kuona kuwa ndoa ya mkataba inaweza kuzaa penzi la kweli?
Full 1000
Whatsp 0784468229.