.
UTANGULIZI
Sikujua kama mwanzo wa mapenzi ni mwisho wa amani yangu. Kila kitu kilibadilika siku ambayo nilimwona kwa mara ya kwanza mwanamke fulani wa hadhi ya juu. Alikuwa akibadilisha mavazi ndani ya gari bila kujua nimekaa siti ya nyuma nimekodoa macho namtazama. Huyu hakuwa mwanamke wa kawaida bali mwanamke mwenye SIRI za hatari. Alivaa gauni jekundu lililombana mwili na kiuno chake, ni kama gauni hili lilitengenezwa maalum kwa ajili yake peke yake. Alianza kutoa nguo zake moja baada ya nyingine. Nami sikujua kuendelea kumtazama mwanamke huyu nisawa na kufungua mlango wa kuingia kwenye dunia ya MAUAJI, USALITI, MATESO na mapenzi yenye nguvu na radha ya KIFO. Mwanamke huyu alipojigeuza, niliuona upande wa pili wa maajabu, kiuno chake kidogo kilichoegemea makalio makubwa yaliyojaa yakiwa yamefungwa vizuri kwenye chup ya bei ghali. Akavua kila kitu kiasi cha kunifanya kijana mdogo nikose pumzi kwa muda. Kifuani matit yake yalikuwa mazuri mno. Si makubwa sana wala si madogo. Yalijaa na kusimama vizuri utazani ni kitoto cha mwaka elfu mbili, la hasha, ni mama mtu mzima anayejua vema nini maana ya kuutunza mwili wake. Sikupata ahueni hadi pale alipojifunga khanga yake, angalau alijisitili ingawa mapaja yake meupe yalikuwa wazi.
Anaitwa Madam Sandra, mwanamke mwenye siri nyingi za KUTISHA nyuma ya maisha yake. Ni mwanamke anayejua jinsi ya kumvuta mwanaume bila hata kumgusa.
Siku hii niliyokutana naye ndipo ukawa mwanzo wa kushuhudia mambo niliyoyazoea kuyaona kwenye muvi pekee. Mauaji, usaliti, mapenzi ya dhambi, na mateso ya kimwili na kiakili.
Sasa tembea na mimi kurasa kwa kurasa ili kujua mbivu na mbichi za mkasa huu wa kusisimua. Nashauri kama si mpenzi wa simulizi/hadithi za CHOMBEZO basi hapa sio mahali pako.
Karibu tuanze...
Jua lilikuwa limeanza kupotea nyuma ya milima ya Mbeya, anga likiwa na mchanganyiko wa rangi ya machungwa na samawati. Onesmo alishuka kutoka kwenye basi akiwa amechoka baada ya safari ndefu kutoka Dar es Salaam. Harufu ya mvua ya asubuhi bado ilikuwa ikizagaa hewani, ikichanganyika na harufu ya mafuta ya magari na moshi wa nyama choma maeneo haya ya stendi ya mabasi. Alivuta pumzi ndefu, akiutazama mji huu mgeni machoni pake.
Hakuwa na mizigo mingi zaidi ya begi lake dogo la mgongoni. Alitembea kuelekea sehemu zinapopaki taksi, akapunga mkono kumuita dereva mmoja aliyekuwa ameketi ndani ya gari lake.
"Nahitaji taksi naenda maeneo ya Mbalizi" Onesmo alisema huku akifungua mlango wa nyuma na kuingia ndani.
Dereva, mwanamume mwenye umri wa makamo, aligeuza uso wake na kumtazama Onesmo kupitia kioo cha ndani.
"Utanipa elfu kumi na tano kijana" alisema kwa sauti nzito yenye lafudhi ya Kinyakyusa.
"Nina elfu kumi" Onesmo alijibu, akijaribu kupunguza gharama.
Dereva alitabasamu, akajibu kwa upole.
"Hebu twende tu, njiani tutapanga." Akatia gari moto na safari ikaanza.
Dakika chache baada ya kuondoka, simu ya dereva iliita. Aliitazama haraka na kisha akapokea.
"Halo, Madam! Nipo safarini na abiria..."
Onesmo alimsikia dereva akibadilika ghafla. Aliinama kidogo akisikitika mwenyewe. Uso wa dereva ulikuwa umebadilika, tabasamu lake likapotea.
"Ndio, nimeelewa. Ngoja nikamilishe hii kazi kwanza?" Dereva alisema kwa sauti ya kuomba.
Kilichoendelea upande wa pili wa simu hakikusikika, ni wazi hakuelewana na mtu anayezungumza naye. Dereva alikata simu akatazama mbele kwa sekunde chache, kisha akashusha pumzi ndefu.
"Samahani kijana, kuna kazi ya dharura ambayo bosi wangu anataka niifanye haraka." dereva alisema huku akimuangalia Onesmo kwa jicho la samahani.
"Kazi gani? Afu mimi inanihusu vipi kaka?" Onesmo aliuliza akishangaa.
"Sihitaji muda mwingi, natakiwa kupeleka kitu sehemu fulani, halafu tunaendelea na safari yako" dereva alieleza.
Onesmo alibadilika uso.
"Lakini mimi nilishakukodi, mbona utanipotezea muda wangu sasa?"
Dereva akatikisa kichwa.
"Najua, lakini sikufahamu kwamba nitapokea kazi nyingine ya dharura. Basi nitakupunguzia nauli, utalipa nusu tu au vipi" alijaribu kumpooza.
"Nusu ambayo ni shingapi?"
"Buku nne tu" Dereva akashusha gharama zaidi hata ya nusu yenyewe.
Onesmo alifikiria kwa sekunde chache, akajua hana chaguo zaidi ya kukubaliana naye.
"Sawa basi, lakini usichukue muda mrefu."
Dereva akatabasamu akageuza gari na kuongeza mwendo.
_______________
Baada ya dakika kumi na tano, gari liliingia barabara ya vumbi iliyokuwa imezungukwa na miti mirefu. Mwanga wa jua ulikuwa unazidi kufifia. Onesmo alihisi kama wanaingia mahali pa siri.
"Wapi huku bosi?" Akauliza kwa wasiwasi.
"Shii! Usiogope huku ndo kwa bosi wangu, hatakiwi kujua kama nimekuja na wewe huku sawa jamaangu"
Onesmo akatikisa kichwa kukubali japo kwa mashaka.
Hatimaye, gari liliwasili kwenye geti dogo jeupe lililojengwa kwa kuunganishwa na ukuta mfupi lakini wa kisasa. Dereva alipiga honi mara mbili. Geti lilifunguliwa na mlinzi mwenye miwani myeusi.
"Kaka lala chini mlinzi asikuone, samahani"
Onesmo bila kusema neno alilala kwenye siti, gari lilipopita usawa wa geti akainuka.
Alishangaa kuona mazingira yaliyokuwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Nyumba ndogo lakini ya kisasa ilijitokeza katikati ya bustani ndogo yenye maua ya kupendeza. Kilichomshangaza zaidi ni watu waliokuwa nje ya nyumba hiyo.
Mabinti kadhaa warembo walikuwa wameketi kwenye viti vya bustani, wakicheka na kupiga soga huku wakinywa vinywaji taratibu. Ajabu walikuwa wamevaa nguo nyepesi sana, wengi walivaa vichup na sidiria pekee. Kana kwamba wako maeneo ya bichi na wala hawakujali.
Onesmo alishtuka.
"Hapa ni wapi?" alijiuliza kimoyomoyo. Dereva aligeuka na kumtazama.
"Upo salama, lakini usishuke. Tafadhali kaa ndani ya gari hadi nitakapomaliza."
"Utakapomaliza nini? Si ulisema unaacha mzigo tunaondoka?"
"Tulia kaka, tulia uone mambo mazuri" dereva akacheka kidogo.
Onesmo alikaa kimya, akishika begi lake vizuri kwa tahadhari. Alishaona mambo ni kama hayaeleweki. Akawa anaomba tu atoke akiwa salama.
Dereva alisogea hadi kwenye viti vya bustani. Alionekana kufurahi kuwaona mabinti wale. Wakasalimiana kwa furaha, walijuana vizuri.
Kisha, Onesmo aliona kitanda kizuri kikiwa kimewekwa nje ya nyumba hiyo huku kikipambwa na mashuka meupe pee. Si hivyo tu, pia kulikuwa na Kamera kadhaa zilikuwa zimewekwa pembezoni mwa kitanda hicho. Pamoja na mashuka ya kuakisi mwanga yale yanayotumiwa na waigizaji ili kupata picha nzuri.
Wanawake wawili walisimama na kumkaribisha dereva kwenye kitanda. Onesmo alishangaa kuona dereva akivua shati lake kisha suruali na kubaki na boksa pekee. Alilala kifudifudi kitandani. Wale wanawake walipanda juu ya mwili wake na kuanza kumpaka mafuta na kumfanyia masaji taratibu.
Mwanaume mmoja mwenye kamera akawa anarekodi kila kitu. Onesmo alianza kuelewa kuwa ilikuwa ni tangazo linalotengenezwa.
Wakati Onesmo akitafakari hali hiyo ya kushangaza, mwanamke mmoja mrembo mwenye umbo la kuvutia alitokea. Alikuwa amevaa gauni jekundu lenye mpasuo mrefu pembeni, macho yake yakiwa na ujasiri wa kiongozi. Huyu alikuwa ndio bosi wa shughuli hiyo. Ni mtu mzima haswa lakini ameutunza mwili wake akionekana mtoto mbichi kabisa.
Alisimama na kuangalia kile kinachoendelea. Alipiga makofi mara mbili, akitikisa kichwa.
"Hapana, hapana, hapanaaa hamfanyi kwa mvuto. Masaji ni sanaa, inahitaji mguso wenye mashauzi" alisema kwa sauti ya upole lakini yenye mamlaka.
Aliwasogelea wanawake wale wengine pembeni.
"Hivi si tulitumia siku nzima kujifunza? kwa nini sasa mnafanya haya madudu?"
Mabinti wakatazama chini kwa aibu.
"Sipendi hizi tabia zenu za hovyo, haya nitawaonesha hapa kwa mara ya mwisho"
"Sawa Madam Sandra" wanawake wakaitika kwa furaha. Mwanamke huyu aliitwa Madam Sandra kama walivyomtaja.
"Nipeni khanga nataka kubadili nguo kwanza." Alisema Madam Sandra kisha akageuza macho yake kwa dereva taksi.
"Naweza kubadilisha nguo ndani ya gari lako?"
Dereva akacheka.
"Ndani ya gari? Hakuna shida kabisa, mmm! nenda ubadilishe." Alijibu kwa wasiwasi. Alishindwa kukataa kwani hakutaka wajue kama kuna mtu amekuja naye. Lakini kukubali pia ilikuwa ni hatari nyingine, akajipa moyo akiamini kijana ndani ya gari hawezi kumuangusha. Atajificha kama alivyokwisha mpanga.
Madam Sandra halichukua kanga yake akatembea upesi huku makalio yake makubwa yakitikisika kwa zamu hadi alipofika kwenye gari. Alifungua mlango wa gari na kuingia ndani siti ya pembeni ya dereva. Bila kuchelewa akaanza kuvua gauni lake taratibu.
Hakujua kuwa ndani ya gari, siti ya nyuma, Onesmo alikuwa amekaa kimya, akiona kila kitu.
Onesmo alishusha pumzi ndefu. Hili lilikuwa jambo la kushangaza kwake. Akaendelea kujituliza kimya hadi pale Madam sandra alipovua gauni lake. Akaona kiuno kidogo kilichoegemea makalio makubwa yaliyojaa. yamefungwa vizuri kwenye chup ya bei ghali. Akavua kila kitu kiasi cha kumfanya kijana mdogo Onesmo kukosa pumzi. Alimtazama Madam Sandra kifuani, akaona matit yake mazuri yaliyokaa mahali pake kwa uzuri wa kiasili. Mviringo wake ulikuwa wa kuvutia, si makubwa mno wala si madogo. Mapaja yake yalikuwa laini mno na manene yanayotengeneza umbo namba nane la mwanamke huyu.
Madam Sandra alipochukua khanga ili ajifunge ghafla macho yake yalikutana na ya Onesmo.
Alishtuka...
"NANI WEWE?" Madam Sandra alifoka kwa sauti kali, macho yake yakimtazama Onesmo kwa hasira huku akijaribu kujistili kifuani kwa kutumia ile khanga.
"NANI WEWE NAKUULIZA?" alifoka, macho yake yakimchoma Onesmo kwa hasira kali.
"Mimi... ni mimi" Onesmo alimeza mate kwa wasiwasi, akijitahidi kujieleza kwa utulivu.
"Mimi ni abiria tu..." Onesmo alijibu kwa sauti ya chini, akiwa na hofu isiyoelezeka..
"Dereva aliniambia anapitia hapa kwa dharura kabla ya kunifikisha ninakokwenda." Akaendelea kujitetea.
Madam Sandra akajifunga khanga yake haraka akatoka huku akipiga hatua kali kuelekea kwa dereva wa taksi. Akawa anamtazama kwa macho yaliyojaa lawama.
"Kwa nini hukuniambia kuna mtu ndani ya gari yako? Unajua umefanya uzembe wa aina gani. Umeharibu kila kitu wewe mpuuzi."
Dereva alionekana kukosa maneno, akashika kichwa na kujikuna kisogo kwa wasiwasi na aibu.
"Samahani Madam Sandra, sikujua kama ni tatizo..." alijitetea kwa sauti ya chini.
"Samahani? Wewe ni mjinga au vipi? Kwanza umechelewa kufika kazini, halafu unaleta wageni waangalie kila kitu? Unajua unavyoharibu kazi yangu?" aliendelea kumfokea kwa sauti iliyojawa na mamlaka.
"Hili ni tangazo linatengenezwa kwa umakini. Huwezi kuruhusu mtu wa nje aone kila kitu, haya unajua ataenda kuongea nini akitoka hapa" Madam Sandra aliendelea kumkaripia kwa sauti kali.
"Nisamehe sana madam, naomba msamaha wako"
Madam sandra hakusema kitu tena, akaikunjua sura yake yenye hasira kali. Angefanya nini tena, tayari imeshatokea. Akasogea kitandani kuendelea na kazi yake akiwa ndani ya khanga moja.
Alisimama juu ya mwili wa dereva, akamkalisha kwenye kitanda cha masaji huku akimwaga mafuta ya harufu nzuri mikononi mwake. Alianza kazi yake kwa ufundi wa hali ya juu, mikono yake ikicheza juu ya mgongo wa dereva kwa umahiri mkubwa. Kila mguso wa mikono yake ulionyesha ujuzi wa hali ya juu wa masaji. Wale wanawake pembeni wakawa wanatazama kila kitu kwa umakini mkubwa.
Onesmo alishuhudia kila kitu akiwa bado ndani ya gari, moyo wake ukimdunda kwa hisia mchanganyiko. Alijaribu kutazama pembeni ili asishuhudie yote. Alihisi aibu na mshangao kwa wakati mmoja, lakini macho yake yaliendelea kuvutwa kwa namna Madam sandra alivyokuwa akifanya kazi yake. Huku akijiachia ndani ya ile khanga yake aliyovaa.
Baada ya dakika kadhaa, zoezi lilikamilika. Dereva alinyanyuka na kuvaa nguo zake. Madam Sandra alitoa fedha na kumpa kama malipo yake ya kwanza.
"Hakikisha hutafanya makosa tena. Na uje haraka sana tukikuhitaji kwa leo tunaishia hapa" aliongeza kwa sauti ya amri.
Dereva alikusanya vitu vyake na kurudi kwenye gari, huku akiwa na aibu ya kuomba msamaha kwa Onesmo.
"Ndugu yangu, naomba radhi kwa yote yaliyotokea. Sikutegemea kama mambo yataendae hivi" alisema huku akiwasha gari tayari kwa safari.
"Hakuna shida, twende tu" Onesmo alijibu kwa sauti tulivu, akitaka tu kutoka eneo hilo haraka.
Safari ya kuelekea kwa mjomba wake ilianza. Njiani, dereva alimtupia maswali ya mtego.
"Vipi kijana, hujazungumza hata kidogo hivi kweli haukupendezwa na kile ulichokiona kule?"
Onesmo alitabasamu kwa aibu.
"Sikuja hapa kwa ajili ya mambo hayo, nataka tu nifike ninakoenda kwa amani."
Dereva alicheka kidogo.
"Haya bwana, lakini najua uliona kitu cha kukuvutia."
_______________
Baada ya muda, walifika katika nyumba ya mjomba wake maneo ya Mbalizi. Mlinzi alimfungulia geti na kumruhusu aingie, tayari alikuwa na taarifa ya ugeni huu.
Onesmo alishuka baada ya kulipa nauli. Akaingia ndani kupitia geti dogo. Baada ya salamu kwa mlinzi akafika kwenye mlango wa sebule na kugonga kwa muda mrefu bila majibu. Hatimaye, mlango ulifunguliwa na mjomba wake, sura yake ikiwa na wasiwasi fulani.
"Karibu Onesmo! Karibu sana anko, heheh ila umefika mapema mbona..." alisema kwa sauti ya uchangamfu. Lakini kabla Onesmo hajajibu, binti mdogo alitokea ndani, akijifunga mtandio kichwani kuficha nywele zake zilizovurugika. Onesmo alihisi kuna kitu hakiko sawa. Alimtazama mjomba wake kwa macho ya kuuliza.
Mjomba wake alitambua hali hiyo, akajifanya kutojali.
"Ah, huyu ni rafiki wa mke wangu, alikuja kuniletea ujumbe fulani anaitwa Vicky. Vicky huyu ni anko wangu anaitwa Onesmo" alijitetea huku akitabasamu kwa kuigiza.
Onesmo na Vicky wakasalimiana. Mwisho Onesmo aliingia ndani, lakini wazo la mjomba na kasichana kadogo halikumtoka kichwani. Mjomba wake alikaa naye kwa muda mfupi. Baada ya kumuonesha chumba chake akasimama na kusema...
"Ninatoka kidogo namsindikiza mgeni, lakini huenda mke wangu atafika kabla sijarudi. Jisikie huru Onesmo." Aliaga na kutoka.
Onesmo alifungua pazia kidogo kuchungulia nje akamuona Mjomba P akiondoka na kale kasichana ndani ya gari yake.
"Anko hajawahi acha mambo yake ya totoz"
Aliwaza Onesmo wakati akitafuta kinywaji ndani ya friji. Akaendelea kunywa taratibu huku akitazama Tv.
Baada ya nusu saa kupita mara mlango wa mbele ulifunguliwa taratibu. Onesmo aligeuza macho yake akihisi anko wake amerejea. Lakini alichokiona kilimfanya kubaki ameduwaa.
Mke wa mjomba wake alikuwa amerudi. Lakini hakuwa mwingine bali Madam Sandra yule mwanamke wa kwenye tangazo la masaji. Macho yao yalikutana kwa mshangao mkubwa. Onesmo alihisi mshipa wa damu ukipiga kwa kasi mwilini mwake. Madam Sandra akiwa ndani ya kigauni kifupi kilichoacha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake alipigwa na butwaa kumuona kijana aliyemchungulia ndani ya gari yuko hapa tena mbele yake, ndani ya nyumba yake.
Je, nini kitafuata. Simulizi hii inapatikana kwa Tsh 1500 tu lipa kwa namba 0756862047 -SAUL kisha njoo WhatsApp kwa namba hizo hizo. Epuka matapeli
ITAENDELEA...
Kujiunga na CHANEL ya stor WhatsApp binya hapa
https://whatsapp.com/channel/0029VaylcIKAInPiI2v4Cc0R.