Taarifa zinazidi kusambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu Kitu cha ajabu, ambacho sasa kinaitwa 3I/ATLAS, ambacho kinaenda kwa kasi ya ajabu ya maili 130,000 kwa saa kuelekea kwenye mfumo wetu wa jua, na hivyo kuzua mjadala mkali kati ya wanasayansi na wafuatiliaji wa anga.
kiligunduliwa kwa mara ya kwanza tarehe 1 Julai 2025, kifaa hiki kinadhaniwa kuwa asili ya nyota, kumaanisha kuwa kinatoka nje ya mfumo wetu wa jua. Ukubwa wake unakadiriwa kuwa mkubwa kuliko mji wa Manhattan Marekani, na inatarajiwa kukaribia jua na Dunia yetu mwishoni mwa Novemba 2025, Kinachofanya tukio hili liwe la kustaajabisha zaidi ni uchunguzi unaopendekeza kuwa kitu hicho kinaweza kuwa chombo cha kigeni cha nadharia ambayo imezua hofu na vichwa vya habari vikali kuhusu uwezekano wa "shambulio la viumbe aina ya Aliens mnamo Novemba."
Utafiti huo, ulioandikwa na mwanafizikia wa Harvard Avi Loeb na wenzake, unaonyesha chombo hicho kinaongozwa na Teknolojia na jinsi kinavyopita kwenye mfumo wa jua kwa kasi yake ya juu kama ishara kwamba inaweza kuwa sio kimondo bali ni Dege kubwa la Aliens..