Alikuwa ni yule mzee aliyekuja kazini kwangu na kuanza kunisimulia hadithi za mafumbo, Lakini pia vijana wake wale walioniteka walikuwa wameshika bunduki, Yule mzee alikaa kwenye kiti huku ameshika kitabu chake kilekile anachotembeaga nacho, Mzee akajitambulisha kwa jina la Nchima; Kisha akaniambia kijana naona leo umeamua kuja mwenyewe ili kuniletea majibu yangu,haya niambie kwenye ile hadithi yangu nani wa kulaumiwa?
Nilimwambia mzee wangu usiniue nipo tayari nikuachie pale kazini kwangu ili uniache huru, Mzee alitoa kauli mpigeni. Wale vijana wake walioniteka walianza kunipiga na kunikanyaga kanyaga, Badae akawaambia acha (wakaacha) Kisha akaniuliza tena kwa mara ya pili swali ni lilelile, (Kwenye ile hadithi yangu nani wa kulaumiwa?) Nikamwambia mfanyakazi ni wakulaumiwa sababu hakuwa mwaminifu kwa boss wake,
Yule mzee akawaamrisha tena vijana wake wanipige, Walinipiga hadi nikaanza kutokwa na damu puani, Kisha akawaambia muacheni.
Dah kile kipigo nilibaki kidogo niropoke ukweli kwamba mimi sijawahi kulala na mke wako.
Yule mzee baada ya kuona natokwa na damu puani alianza kucheka na kuniambia kijana nilikuona mjanja lakini umeshindwa kujibu maswali yangu, kingine nasikitika sana kuona unafanya biashara kama zile wakati umri wako bado ni mdogo harafu huna hata mwanasheria, lakini wakati mwingine huwa nakupongeza sana sababu wewe ni mdogo lakini unafanya mambo makubwa, mimi nilikuwa mwanasheria kwenye ikulu ya raisi, kwahiyo nikikufungulia mashtaka unaweza ukanyongwa bila huruma kutokana na kazi ya kutakatisha pesa,
Mzee akaniuliza unafanya kazi chini ya nani? Nikamwambia hapana nipo peke yangu, Mzee akasema wewe jifanye jeuri lakini nitampata hadi huyo unayefanyanae kazi.
Kisha mzee akaanza kunisimulia...wakati nafanya kazi kwenye ikulu ya Mhe. Raisi, nilifanikiwa kuiba kiasi cha bilioni moja na nusu, lakini mpaka sasa miaka nane imepita bado sijafanikiwa kupata mtu wa kuzitakatisha zile pesa na kuanza kuzitumia, sitaki kuzichanganya kwenye biashara zangu kwa sababu nikizichanganya zile pesa kwenye biashara zangu bila mpangilio maalum serikali wanaweza wakafanya uchunguzi na wakibaini kama mimi ndiye niliyeiba zile pesa, mali zangu zote na utajiri nilionao utachukuliwa na kutaifishwa kuwa mali ya serikali,
Sababu baada ya mimi kuiba zile pesa nilisababisha watu wengi wasio na hatia kupelekwe jela, kwakuwa nilikuwa ni mwanasheria na msimamizi katika mambo ya fedha, wengine niliwabambikizia kesi na kuwafunga bila huruma, sababu nilikuwa najilinda kupitia cheo changu na wadhifa nilionao, Lakini zile pesa bado nimezihifadhi ndani mwangu katika chumba maalum na hakuna mtu anayeweza kuingia zaidi ya mimi, Kingine nasikitika kukuona unatembea na mwanamke ambaye anatarajiwa kuolewa na kijana wangu,
(Mwisho alimalizia kwa kusema) Nafikiri sasa utakuwa umepata jibu kama mimi ni yule niliyetoroka na pesa kwenye ile hadithi yangu.
Mzee akaniambia mambo ni mawili tu uingie mkataba na mimi kwa ajili ya kutakatisha pesa zangu au nikupige risasi ya utosi kama nilivyowaua wale ambao tulishirikiana kuiba zile pesa ikulu.
Nilikaa kimya kwa muda kidogo nikitafakari ni mwanamke gani ninayetembea nae harafu anatarajiwa kuolewa na mtoto wa yule mzee sababu mwanamke niliyenae ni tina na sakina. Lakini wakati nazidi kutafakari nilipigwa kitako cha bunduki na kuambiwa nitoe maamuzi,
Ilibidi nikubali kufanya kazi ya yule mzee ya kutakatisha pesa zake, Lakini nilimuomba asije akaniua sababu bado wazazi wangu wanahitaji msaada wangu. Yule mzee akasema utaendelea kufanya mpangilio wa biashara ukiwa katika hiki chumba hadi pale utakapo kamilisha.
Nilianza mpango wa kutakatisha pesa za yule mzee Ilibidi aniletee majina matatu ya watu ambao wanahusika na biashara zake, Lakini ndani ya yale majina nilishangaa kulikuta jina la sadiki,ila nikaona hakuna shida labda majina yanafanana,akaniletea pamoja na taarifa kuhusu faida anayopata katika biashara zake. Baada ya kuwa nimepata taarifa ni kiasi gani anaingiza kwa wiki, Nikamwambia awe analeta pesa kidogokidogo ili niwe naziingiza kwenye pesa halali, Kwakuwa mzee alikuwa na biashara kubwa pale mjini na mikoa mingine, Hivyo utakatishaji wa pesa haukuwa mgumu sababu mzee alikuwa hadi na vituo vya kujazia mafuta (Petrol Station) Harafu na mimi kipindi hicho nilikuwa nimebobea kwenye hayo mambo ya utakatishaji wa pesa,
ilibidi niwe nachukuwa ile pesa ambayo sio halali naiweka kwenye mahemezi, Yaani mzee kila anapotaka kwenda kuhemea mzigo wowote kwenye biashara zake na kwenye makampuni nilikuwa nampatia mpangilio wa kuiingiza ile pesa ya wizi katika mfumo wa kununulia mahitaji, Mzee aliendelea kuleta ile pesa hadi ikaelekea kuisha,
Nilikaa mateka zaidi ya mwezi mmoja lakini pia nilikuwa sielewi kinachoendelea nje, Wakati mwingine nilikuwa nawaza kuhusu tina maana nilitekwa wakati naenda kumpokea tina, Lakini pia nilikuwa najiuliza inamaana sakina hataki hata kunitafuta au kwenda kituo cha polisi, Na vipi kuhusu wazazi wangu na dada yangu wapo katika hali gani huwenda wanajuwa nimeshakufa, Na vipi kama tina alichukuwa simu yangu na kukaa nayo je kama sakina alinipigia!? Lakini nilikuwa bado najiuliza ni mwanamke gani ambaye natembea nae na anatarajiwa kuolewa na mtoto wa yule mzee!?!? (nilikuwa nawaza nikiwa kwenye kile chumba cha giza sababu yule mzee hakutaka hata nitoke nje ilikuwa ni zaidi ya jela)
Lakini kabla hakijakamilika kiwango ambacho alinitajia, Wakati tunaelekea kumaliza mpango wa utakatishaji, Nakumbuka siku hiyo alikuja na pesa kidogo sana na alipofika sehemu ambayo nimefungwa kama mateka alifika na kunitupia zile pesa kisha akawa kama anachanganyikiwa mara akune kichwa, Kiufupi alikuwa kama amedata hivi, Alianza kuzunguka kwenye kile chumba,
Ukweli ni kwamba yule mzee alikuta nusu ya ile pesa imeibiwa mulemule ndani mwake na mtu aliyeiba hajulikani. Inamaana kuna mtu alikuwa akiiba zile pesa kwa muda mrefu bila mzee kujua, Kwahiyo mzee alikuwa anajua pesa ipo kumbe kuna mwingine anachuwa.
Mzee alizunguka hatimaye alianguka na kuzimia, Wale vijana wake walivua mashati yao na kuanza kumpepe huku wakimuita Boss,Boss lakini hakuamka ilibidi wambebe harakaharaka huku mmoja wao akikusamya zile pesa na kuziweka kwenye begi na kulibeba, Walimbeba na kutoka nae nje, lakini wakati wanatoka hakuna aliyekumbuka kufunga mlango na mimi nikaona hii ni nafasi nzuri ya kutoroka, Wakati wanatoka na mimi nilikuwa nikiwafuata kwa nyuma, Walitoka hadi nje na kumpakia kwenye gari na wakaondoka kumpeleka hospitali.
Baada ya mimi kutoka nje niliangalia mazingira yalikuwa ni mageni harafu niligundua ile sehemu niliyokuwa nimewekwa ilikuwa ni kama handaki, Sababu ilikuwa ni katikati ya shamba kubwa ambalo ukiangalia huoni mwisho, Nilianza kukimbia kuondoka kwenye lile eneo...
Itaendelea...βπ»
~Daudi~.