Naitwa David. Sikuwahi kufundishwa namna ya kupenda, Lakini hisia na pesa...
Katika familia ambayo siyo ya kimasikini sana,wala siyo ya kitajiri sana, Mimi na mdogo wangu wa kike, Mimi nilikuwa mtoto wa pili kuzaliwa, Dada yangu alikuwa anaitwa Zai, yeye alikuwa wa kwanza kupelekwa shule, Wakati anaamka kwenda shule nilikuwa natamani na mimi kwenda shule,
Miaka ikasonga nikafikia umri wa miaka 6, baba akanipeleka shule na kuniandikisha nikaanza darasa la kwanza, Nilifurahi sana kuanza kwenda shule niliipenda shule kuliko maelezo,
Nakumbuka siku moja niliamka mapema na kunawa nikaelekea shule lakini cha kushangaza sikuona mwanafunzi hata mmoja,zaidi yangu, Nilipofika shuleni pako kimya sana nikajiuliza mbona leo pamepoa sana shuleni au nimewahi sana leo, Ndipo alipotoka mlinzi wa shule na kuniuliza. Na wewe unafanya nini hapa? Nikamwambia si nimekuja shule, Akaniambia leo ni j-mosi kwahiyo kuja shule hadi J-tatu π nilirudi nyumbani na kumsimulia dada yangu kwamba nilienda shule alinicheka sanaπππ na kuniona kama mwendawazimu.
Nilipofika darasa la pili mwalimu wa sanaa na michezo aliagiza kila mmoja akatengeneze kitu anachokiweza na aje nacho shuleni, Nilitengeneza ufagio mzuri na kuuwekea urembo kwa kutumia mipira ya tyubu, Mwalimu alinipongeza sana, Kiukweli kwenye somo la sanaa nilikuwa na max nyingi kuliko mwanafunzi yeyote pale shuleni, Lakini kwenye masomo mengine nilikuwa ni kama mjinga mjinga frani.
Niliendelea na masomo nikafika darasa la nne nilijikuta nimeanza urafiki na wanafunzi mbali mbali nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa akihudhuria shule mara moja moja, Yule rafiki yangu kuna siku akawa ameniambia wao kuna sehemu huwa wanaenda kula maandazi, Nilitamani na mimi kwenda hatimaye tukaenda,
Kumbe hakuna maandazi wala nini lakini walikuwa ni wakwepaji wa kufika shule, Tulianza utoro waalimu wakajuwa kuna wanafunzi hawafiki shule, Siku moja waalimu wakaamuwa kutuma kundi la wanafunzi kuja kutukamata tulikamatwa baadhi tukapelekwa shule na tulichapwa sana, Nikaona hiyo sio njia nzuri nikaachana na yule rafiki yangu pamoja na kundi lake, Nikaanza kuzingatia masomo,
Hatimaye nikafika darasa la saba lakini kimasomo sikuwa vizuri nilikuwa napita kwa kubahatisha sana, Lakini hata hivyo nikafaulu kwenda secondary,
Nikaanza from one, Wakati naanza from one nilikuwa mpole sana baadhi ya wanafunzi wa from two walikuwa wakinionea na kunifanyisha kazi za kupanga madawati katika darasa lao.
Nikaendelea na masomo nikafika from theree kidogo nikawa sio mtu wa kuonewa, Lakini nikaanza urafiki na binti mmoja ambaye alikuwa anaitwa Tina; Mazoea ya mimi na Tina yalizidi siku hadi siku, Tukajikuta tumeanza kutumiana barua za urafiki, Lakini pia nilikuwa na rafiki yangu Side, Mimi na Side tulikuwa ni marafiki ambao tunaelewana sana,rafiki yangu Side akawa ameniambia kwamba kama sijawahi kumwambia Tina kama nampenda bas nimwambie mapema ili nisije nikamkosa hapo badae, Yani nimtongoze Tina kabla hajaanza mahusiano na mtu mwingine.
Mimi wakati huo sikuwa na hisia zozote za kumpenda Tina, Lakini Tina alionekana kunijali sana, Ila wakati mwingine nilikuwa nakosa furaha pale ninapomuona Tina akiwa amekaa na vijana wa kiume pale shuleni,
Lakini niliwaza Tina ni rafiki yangu, Harafu nikimuoma na mwanaume mwingine Moyo unauma, Je nisipomwambia kama nampenda harafu apate mwanaume mwingine si nitaumia, Dah chembechembe za kumpenda Tina zikaanzia hapo, Nikajiuliza atakubali kweli kuachana na urafiki ili tuwe wapenzi.
Nikawaza nikaona lakini Tina akichukuliwa na mtu mwingine ndio nitamkosa kabisa,harafu nikiangalia tayari nimeshamzoea, Nikaamua kuandika barua ya kumtongoza Tina, Niliandika maneno mazuri ambayo niliamini kabisa Tina akisoma barua yangu hawezi kukataa,
Niliandika barua yangu na kuikunja vizuri nikaiweka kwenye bahasha,kisha nikampatia rafiki yangu Side aipeleke kwa Tina.Side alienda na kumpatia Tina Baada ya kuwa barua imeshamfikia kwa mlengwa mimi nikakaa nikimsubiri majibu kutoka kwa tina,
Lakini wakati nasubiri majibu nakumbuka siku moja iligongwa kengele na wanafunzi wote tulikusanyika sehemu ya kupanga mstari, Mwalimu wa nidhamu alisimama mbele ya mbele yetu akiwa ameongozana na Tina, Mwalimu alinyanyua mkono huku ameshika barua, Nilishtuka baada ya kuona mwalimu ana barua mkononi huku Tina amesimama pembeni.
Mwalimu alisema aliyeandika hii barua apite mbele...
Tutaendelea...βπ»
~Daudi~
Like ziwe nyingi ili nipate nguvu ya kuendelea....