Mwanza....
Wiki moja tu baada ya kuludi nyumbani kutoka masomoni nikiwa nimemaliza elimu ya chuo nje ya nchi. Jioni moja mama yangu alikuja chumbani kwangu. Alinikuta nimejilaza kitandani nipo mbali kimawazo.
Alikaa pembeni yangu na kunitazama usoni Kwa muda mrefu. Tayari mapenzi yalikuwa yashanuvuluga. Mpenzi wangu alikuwa kichomi balaaa yaani navyosema kichomi namaanisha ni muhuni. Hata sijui nilimpendea Nini nilijikuta tu nimempenda sana Jafari.
Ni mwanaume wa kawaida tu, anayemiliki chumba kimoja Cha kupanga na humo ndani ya chumba hakuna chochote Cha maana zaidi ya kitanda Cha kawaida tu na godoro la kudumbukia. Sikujali kama mimi ni mtoto wa kishua, nilimpenda hivyo hivyo na umasikini wake na mala nyingi nilikuwa nikimsaidia pesa anaponiomba.
Nilikuwa masomoni nje ya nchi ila mapenzi yetu yalikuwa pale pale. Nilishawakataa wanaume wa maana kibao kwaaajil yake ila mwenzangu hakuwai kuheshimu mahusiano yetu.
Jafari ni muhuni balaaa. Yaani nilishaongea mpaka nimechoka na kumuacha nilikuwa siwezi kabisa. Aliyasema mapenzi ni uchizi hakukosea.
Baada ya mama kunitazama Kwa muda mrefu alinishika shavuni Kwa mkono wake ndipo nilishtuka.
"Upo sawa kweli?"
"Yes mom".
"Hukuniona?".
"Kwani umekuja muda gani mrefu".
"Haaaaa! Nadra!. Una shida Gani mwanangu, niambie mimi ni mama Yako na ndo msiri wako".
"Mama nipo sawa tu Wala usijali. Kuna kitu nilikuwa nakifikilia hapa yaani napanga mwenyewe kwenye almashauri ya kichwa changu na kupangua". Niliongea hayo huku najichekesha chekesha.
"Wee mtoto wewe"
"Niambie mama yangu".
"Nimekuja na habari njema mwanangu kipenzi".
"Enheee! Habari Gani hiyo mama".
"Ila usiniamgushe mama Yako. Naamini nipo sahihi kwa hili na ni kwasababu nakupenda sana Binti yangu.
"Wala usijali mama yangu. Niambie tu".
"Mwanangu, umepata mchumba".
"Niniii!". Nilimuuliza mama Kwa mshangao.
"Umepata mchumba mwanangu Tena ni Kijana mzuri mno na anaweza kukutunza vizuri tu".
"Jamani mamaaa!".
"Yeah!
"Hapana bhana mama msinifanyie hivyo".
"Nadra tafadhali Binti yangu. Wazazi wako tupo sahihi kabisa. Ni mwanaume mzuri mno ukimuona unaweza ukapagawa ujue. Alafu ana maisha mazuri tu".
"Mama tatizo sio maisha mazuri. Maisha yanatafutwa mama. Tatizo moyo kupenda. Je ananipenda?, je nampenda?. Mie sitaki kuukatili moyo wangu na ishtoshe namtu wangu tunapendana sana".
"Mama Yako mimi sio mkatili. Mwanangu najua zama za kutafutiana mke au mume zimepitwa na wakati ila wazazi wako tupo sahihi kwa upande kwengine. Unataka kuniambia mwanaume unayemsemea kuwa mnapendana sana ni huyo Jafari?". Nilishtuka kidogo baada ya mama kumtaja Jafari. Sikuwai kuhisi kama mama anajua kuwa Nina mahusiano na Jafari.
"Unamjua?". Nilimuuliza mama.
"Namjua vizuri, ni ni yule mvuta Bangi na mlevi kupindukia au sio?".
"Huenda sio huyo mama. Jafari ni mwanaume mzuri tu na Wala si mlevi na sio mvutaji kabisa".
Mama aliwasha simu yake na kutachi Kwa sekunde kadhaa, aliigeuza simu yake na kumuonyesha. Nilikutana na picha ya Jafari akiwa ameshika chupa mbili za bia. Huku mkono mwengine ameshika Bangi. Niliishiwa pozi hata kumtazama mama mlnilishindwa.
"Au sio huyu Jafari wako?". Mama aliniuliza.
"Lakini mama mimi nampenda hivyo hivyo na mapungufu yake".
"Na unampenda hivyo hivyo na mademu zake pia?, usipokufa Kwa presha utakufa Kwa ukimwi. Unafikiri sisi wazazi wako wapumbavu eeeeeh!". Mama aliongea Kwa paniki ni dhahiri alikuwa amechukia.Sikuwa na lakujitetea zaidi ya kukaa kimya.
"Msubili baba Yako aje". Mama alitoka chumbani kwangu. Majira ya usiku baada ya chakula baba aliomba kuzungumza na Mimi.
"Sio hapa kwaajili ya kukuomba Bali nipo hapa kwaajili ya kukupa taarifa. Nadhani mama Yako ameshakwambia Kila kitu kwaiyo sina haja ya kuyaludia. Jiandae wiki hii unachumbiwa na kuanzia Sasa hutakiwi kutoka hata nje ya geti. Nadhani umenielewa Nadra?".
"Lakini baba mnaniozeshaje kwa mwanaume nisiyemtaka na pia hata simfahamu. Hamnitendei haki".
"Unaijua haki wewe mtoto. Kwaiyo unaona ni bola kutupa wazazi wako aibu kutembea na yule mvuta Bangi si ndiyo. Mbona hata wewe hututendei haki pia. Nadra na elimu Yako hiyo wewe wa kutembea na yule mvuta Bangi kweli?. Ipo hivi utake usitake utaolewa".
"Kwaiyo mlinisomesha ili niolewe au?, Sasa huna haja Gani ya kunisomesha. Nimemaliza chuo hata mwezi haujafika tayari mshanitafutia mwanaume. Niacheni basi nitumize ndoto zangu".
"Tatizo umeshindwa kujilinda acha ukalindwe na mumeo. Kuanzia Sasa hakuna kutoka nje ya geti". Baba aliyasema hayo na kuelekea chumbani kwake.
Nilichukia mno ila sikuwa na jinsi upande wengine ni kweli wazazi wangu walikuwa sahihi ila upande mwengine hawakunitemdea haki kabisa.
Upande mwengine alionekana mmama mtu mzima akiwa amekaa na mwanae wanaongea.
"Sio kwamba ninakulazimisha ila mwanangu ni miaka mingi imepita yafaa kuoa tena. Au unadhani Mwamini ataludi Tena?. Mtu akifa ndo amefuka mwanangu hawezi kuludi tena".
"Lakini kama mtoto ninae mke Hana maana Tena kwangu mama".
"Ana maana vizuri sana. Mtoto mmoja hatoshi mwanangu. Unajua nini maana ya mke?, huoni hata wazee wa miaka mingi Bado wanaoa tu. Mwanamke kwa mwanaume hayupo kwaajili ya kuujaza ulimwengu tu, mwanamke ana maana kubwa sana mwenye maisha ya mwanaume.
"Ni sawa kama umeamua hivyo".
"Samir mwanangu nakupenda na ndo maana napambana kuludisha furaha Yako. Tangu mkeo atangulie mbele ya haki ni miaka mingi Sasa ila Bado haupo sawa. Ona na mwanao pia amekushinda. Lazima uoe ili usaidiwe malezi na mke wako au unataka mpaka mtoto aingie kwenye udangaji kabisa na sidhani kama yupo salama mpaka sasa. Nimesikia tu amekuwa mnenguaji huko Ngoma kungwi".
"Sijakuelewa mama. Umesema Samira amekuwa mnenguaji Ngoma ya kungwi?". Samiri aliuliza Kwa mshangao....... ITAENDELEA.........
SIMULIZI : NYOTA YANGU
MTUNZI : NURU HALISI
WHATSAPP NAMBA 0683009150
PAGE : Hadithi Za Nuru Halisi
SEHEMU 02
ENDELEA......
"Nimesikia ananengua huko Ngoma ya kungwi sijui kama ni kweli, ila mwanangu si unaona mtoto ametushinda yaani ni vulugu Kila siku ndani ya nyumba".
"Ni kweli mama, Sasa tunafanyaje maana kumpiga tu haisaidii".
"Kama nilivyokwambia ukioa huenda itasaidia. Huenda Samira atakutamaza kama baba na ataanza kukuheshimu na kukutii".
"Ni sawa nitaoa". Samiri alikubali kuoa ila hakumfahamu mwanamke anayemuoa.
Upande wangu. Kesho yake asubuhi na mapema nilipanga nikakutane na Jafari siku hiyo. Sikujua ni namna Gani nitatoka nyumbani maana tayari mlinzi ameambiwa asiniluhusu kutoka nje ya geti pasipo ruhusu kutoka Kwa mama.
"Mtu mwenyewe ana njaa njaa yule. Nilimpa Hela kidogo anafungua geti. Kweli nilipamaliza kujiandaa nilimvizia mama alipokuwa chumbani kwake na mimi nilitoka haraka sana. Nilifika sebleni nilikutana na dada wa kazi pamoja na mdogo wangu wa kike hiliam.
"Dada unaenda wapi?". Aliniuliza kwa mshangao baada ya kuniona nimevalia vizuri. Haraka nilimnyamazisha Kwa kutumia kidole changu ili mama asiweze kusikia.
"Sikieni. Natoka mala Moja sichelewi kuludi. Na mama akiniulizia mwambieni nipo chumbani kwangu nimelala sawa?".
"Lakini mimi naogopa mama akijua nimemdanganya atachukia".
"Hawezi kujua nawai kuludi'. Walikubali shingo upande, sikuwajali nilitoka. Nilifika nje nilimkuta mlinzi getini. Nilimpanga vizuri na mbele ya pesa alikubali.
Nilitoka nje ya geti. Niliita boda boda, safari kuelekea Kwa mpenzi wangu ilianza. Nilifika mtaa anaoishi Jafari. Nilishuka na kumlipa boda boda Hela yake.
Nilifika nje ya chumba anachoishi Jafari. Ni mtaa wa uswahili sana. Nilikuta baadhi ya wapangaji wapo nje wamekaa wanapiga umbea. Baada ya kuniona walianza kunong'onezana. Sikuwajali niliwasalimia na kupita mpaka mlango wa chumba Cha Jafari.
Nilikuta mlango umeludishiwa tu. Niliusuka na kuingia ndani. Sikuamini baada ya kumkuta Jafari akiwa na mwanamke wamepakatana wanafanya yao. Niliishiwa nguvu nilikaa chini taratibu machozi yalianza kunitililika mashavuni.
"Nadra si nilikukataza kuja bila taarifa. Unafanya nini Sasa?". Jafari aliongea Kwa paniki hakuonyesha kujali chochote kuhusu Mimi.
"Baby ni nani huyu kwani?". Yule mwanamke alimuuliza Jafari kwa sauti ya madeko.
"Inuka bhana uondoke. Tabia ya kuja kwangu bila taarifa nishakukataza mala kibao ila husikii".
Nilimtazama Jafari kwa hasira. Mtu amenikosea ila Bado ananikandamiza.
"Hata hivyo sikuja hapa kukufumanika kama ulivyozoea. Tabia ya mtu ni kama ngozi. Jafari nipo hapa kukupa habari kuwa naolewa hivi karibuni. Nimepata mwanaume wa types yangu. Mwanaume mzuri mwenye elimu yake ya juu na maisha ya majuu ambaye anauwezo wa kukulisha mwaka mzima wewe na ukoo wako wote. Sikia Leo nikwambie. Mimi nilikupenda kweli kweli na mapungufu Yako ya kibinadamu ila sio ya kukubali kusalitiwa Kila siku. Umeshindwa kuheshimu mahusiano yetu Kila siku ni usaliti tu Bado nakulisha na hata pesa unazowahonga hawa wanawake ni zangu".
"Nakuacha Sasa na maisha yako. Tuone kama Kuna mwanamke atakayekutaka maana naamini baada ya kuachana na mimi utakuwa unanuka shida". Nilijikuta nimeongea hayo yote kwa ujasiri mkubwa mpaka Jafari mwenyewe alibaki kunishangaa tu.
Baada ya kumaliza kuongea hayo nilitoka mule chumbani na kuondoka zangu. Roho ilikuwa inaniuma sana jamani. Nilimpenda sana Jafari kwa moyo wangu wote. Na nilivumilia mapungufu yake niliamini ipo siku atabadilika.
Nilifika nje ya geti la nyumba yetu nilibonyeza kengere. Mlinzi alikuja kufungua alishtuka baada ya kuniona mimi. Aliangalia juu gorofani alimuona mama amesimama anatuangalia.
"Tafadhali tetea kibarua changu". Mlinzi aliniambia hayo kwa hofu. Sikumjibu niliingia ndani ya geti na Moja Kwa moja nilielekea ndani.
Nilifika ndani nilimkuta Hiliam na Husna dada wa kazi wamekaa sebleni.
"Dada mbona upo hivyo una shida Gani". Hiliam aliniuliza.
"Kwema dada?". Sikumjibu nilianza kupandisha ngazi kuelekea juu gorofani. Nilipanda ngazi tatu tu mama alinistopisha Kwa kuzungumza.
"Unatoka wapi Nadra?, uliambiwa nini na baba Yako Jana?". Sikumjibu mama nilikaa kimya.
"Si nakuuliza unatoka wapi, hujibu ni bubu wewe?".
"Mamaa!". Nilimuita mama kwa sauti tulivu.
"Niambie ni wapi ulienda, kwa Jafari eeeeh!".
"Nisamehe mama. Nipo tayari kuolewa na mwanaume mnayemtaka nyie. Nipo tayari hata mkisema kesho ni sawa tu". Niliongea hayo nilijikuta uvumilivu unanishinda. Machozi yalianza kunitililika mashavuni.
Nilimpandisha ngazi kwa kukimbia huku nikiwa nalia. Niliingia chumbani kwangu na kufunga mlango Kwa ndani.
"Mama dada ana shida gani?".
"Hata sijui kapatwa na Nini. Ebu nenda kamtulize chumbani kwake.
"Unafaa kwenda wewe mama. Unadhani mimi atanielewa. Nenda wewe kaongee nae kama mzazi".
"Najikuta na hatia Kwa hili tunalotaka kumfanyia Nadra ila si hata wewe unaona Jafari hafai kuwa shemeji yako, Sasa sielewi tunafanyaje na dada Yako ndo ameshapenda".
"Ni kweli mama, hata Mimi sijawai kumuelewa kabisa Jafari. Dada yangu ni mzuri mno sijui Jafari amempa Nini?". Hiliam aliongea hayo Kwa masikitiko. Mama alipandisha juu gorofani mpaka nje ya chumba changu. Aligonga mlango mala kadhaa huku akinisii nifungue anataka kuzungumza na mimi.
Nilifungua mlango na kumkumbatia mama yangu. Niliendelea kulia. Mama alinibembeleza kwa kunipapasa mgongoni Kwa mikono yake. Tulikaa kitandani ndipo mama alizungumza.
"Nisamehe mwanangu. Najua tunakukosea kuingilia furaha Yako kwa mwanaume unayempenda".
"Nooo! Mama usiseme hivyo unakosea. Sina furaha yoyote. Ona mwanao nalia kwaajili ya Jafari. Mama mimi nipo tayari kuolewa na huyo mwanaume mliyenitafutia haijalishi awe mfupi, mwembamba, mnene, mweupe, mweusi, kiwete mimi nitaolewa nae. Nimechoka mama bola wali nyama vitani". Niliongea hayo huku nikiwa nalia na kumuacha Mama kwenye mshangao....... ITAENDELEA...... Nadra kachagua wali nyama vitani πππ...
SIMULIZI : NYOTA YANGU
MTUNZI : NURU HALISI
WHATSAPP NAMBA 0683009150
PAGE : Hadithi Za Nuru Halisi
SEHEMU 03
ENDELEA......
Mama alibaki kunishangaa namna nilivyokuwa naongea huku nikiwa nalia.
"Umepatwa na nini Nadra".
"Mama nipo sawa, nimeona mpo sahihi kwasababu mnanipenda. Nataka kuolewa na huyo mwanaume haijalishi na Wala sitojali atakuaje".
"Sawa , Sasa Kwanini unalia nini shida?. Niambie mwanangu mzuri".
"Nimechoka usaliti mama. Nampenda sana Jafari lakini nyakati zote amekuwa wa kuniumiza tu. Kwani mama mimi ni mbaya?".
"Mwanangu wee mzuri sana tu. Tena sanaaa! Najivunia wewe sana na hilo unalijua. Hivi ushawai kujua wanaume wanataka Nini?, nikwambie tu ukweli. Kuna baadhi ya wanaume hawajui wanataka nini yaani unaweza kuwa na sifa ya Kila aina ila Bado akakusaliti. MUNGU anakupa kile unachostahili na sio unachokitaka na ukilazimisha madhara huja baadae.
"Nimekuelewa mama".
"Vizuri Binti yangu. Basi nikuache upumzike kidogo.
"Sawa mama". Mama alitoka chumbani muda mchache simu yangu ilianza kuita. Mpigaji alikuwa Jafari. Iliita mpaka ilikata pasipo kupokea.
Baada ya kuona hapokelewi simu alituma ujumbe. Niliusoma ule ujumbe alikuwa anaomba msamaha tu na kuniambia ananipenda sana sijui nisiolewe na maneno kibao.
Baada ya kuusoma ujumbe nilimpigia simu, sekunde chache alipokea.
"Kuanzia Sasa mimi na wewe tusijuane. Kwa usalama wa maisha yangu nimeamua nikuache na maisha yako. Mwanaume Gani wewe hubebeki. Jafari nilikupenda sana ila nyakati zote umekuwa ukiniumiza. Nimechoka.
"Usiseme hivyo mpenzi wangu. Bado nakuhitaji mno Nadra wangu. Nimeteleza tu mama". Jafari alianza kujiliza kinafiki kwenye simu. Nilikata simu na kublock namba yake kabisa.
Taratibu za mimi kuchumbiwa zilianza. Baada ya wiki moja nilitolewa barua. Mpaka muda huo sikuwai kumuona huyo mwanaume ambaye ndiye mume wangu mtarajiwa na Wala sikuwai kuwasiliana nae.
Jioni baada ya kupokea barua na walioleta kuondoka nilimlalamikia mama kutaka kumjua huyo mwanaume mwenyewe.
"Una hofu huenda ni mbaya au ana Tisha?".
"Sina maana hiyo ila hata kama ungekuwa wewe lazima ungetaka kumjua kabda mama".
"Ondoa shaka mwanangu. Ni mwanaume mzuri haswaa ukimuona unaweza ukapagawa kabisa".
"Khaaa! Mamaaa!".
"Sio utani. Nakwambia kweli. Samir ana sifa zote za kuitwa mwanaume. Ushindwe wewe tu".
"Nimuone basi hata Kwa picha jamani maana sio kwa sifa hizo".
"Picha yake ndo sina. Wewe tulia utamuona siku ya posa".
"Mh! Aya buana". Nilikuwa nashahuku ya kumfahamu huyo Samir anayemwagiwa sifa kedekede na mama.
Siku zikizidi kusonga mbele. Hatiyame siku ya posa ilifika. Nilivalia abaya langu zuri lililonistili vizuri. Nilikuwa nimekaa zangu chumbani sikuluhusiwa kutoka siku hiyo kwenda hata jikoni. Niliambiwa Kila kitu nitakachotaka nitaletewa chumbani.
Majira ya saa tano asubuhi. Nilisikia honi ya gari nje ya geti. Haraka nilisogelea dirisha na kutamaza Kwa nje. Niliweza kuona Magari mawili ya kifahari yanaingia ndani ya uzio. Niliendelea kuwa sambamba kutaka kumuona bwana Samir. Gari Moja walishuka wamama wawili mmoja alikuwa mtu mzima sana mwengine alikuwa kiasi pamoja na mbaba mtu mzima wa makamo.
Gari lengine walishuka Vijana wawili na wasichana wawili. Sikuweza kuwaona vizuri sura zao ila mavazi waliyovalia yalikuwa ni ghali sana.
Walipokelewa na mama na baba pamoja na baadhi ya ndugu waliokuja kwaajili ya jambo langu.
Walikaribishwa ndani na baada ya muda taratibu za posa zote zilifuatwa. Baada ya chakula Cha mchana mmama yule mtu mzima aliomba kuonana na mimi.
"Hiliam mpeleke mama chumbani kwa dada". Mama alimwambia hilliam.
"Nafaa na mimi kwenda". Kijana Samir aliongea hayo.
"Hakuna shida". Hilliam aliwaleta chumbani kwangu. Walinikuta nimekaa kitandani nachezea simu yangu. Baada ya kuwaona niliweka simu pembeni na kutengeneza ushungi wangu.
Niliinamisha kichwa chini, mwanamke stara si mnajua eeeh!. Basi nilikuwa mtulivu na viaibu aibu. Hiliam alitoka nje, yule mama aliongea.
"Naweza kukaa mwanangu?".
"Bila shaka mama. Karibu sana". Nilimjibu hayo huku nikiwa nimeinamisha kichwa chini. Samir alikuwa amesimama mbali kidogo ananiangalia kwa kuibia ibia ila hakuwa kuniona vizuri maana nilikuwa nimejifunika na mtandio.
"Ni Mimi mkwe wako. Mama wa samiri na huyo unayemuona hapo ni samir mwenyewe. Nadhani hujawai kutujua kabda".
"Nafurahi kuwafahamu mama". Nilimsalimia yule mama Kwa heshima.
"Nadra naamini wewe ni Binti mzuri na unaweza kuwa mama Bora kwa wajukuu zangu. Nimekupenda na natamani uwe sehemu ya maisha ya mwanangu hata kesho".
"Asante mama".
"Okay! Mie nipo nje. Samir njoo ukae hapa uongee na mwenzio hata mfahamiane kidogo. Samir alisogea mpaka kitandani na kukaa pembeni yangu. Mama Samir alitoka chumbani na kutuacha wawili tu. Ukimya ulitawala kwa dadika kadhaaa. Samir alivunja ukimya Kwa kuzungumza.
"Kwanini umekubali kuolewa na mimi ikiwa huujui undani wangu?". Aliniuliza swali gumu.
"Naamini wewe si mtu mbaya, au na wewe ni msaliti?". Niliongea hayo na kumtazama Samir usoni. Kwa mala ya kwanza ndipo nilimfahamu Samir nilipatwa na kiwewe baada ya kumuona Samir mwanaume aliyeniposa........ ITAENDELEA......
SIMULIZI : NYOTA YANGU
MTUNZI : NURU HALISI
WHATSAPP NAMBA 0683009150
PAGE : Hadithi Za Nuru Halisi
SEHEMU 04
ENDELEA........
Samir bwana ni bonge Moja la handsome la mjini. Yaani ni mzuri uwiii!. Baada ya kumuangalia naye aliniangalia. Nilijikuta nimekosa ujasiri wa kuendelea kumuangalia maana kaumbwa jamani sikujua tu huko ndani alikuja ila nje anamuonekano mzuri sana.
Niliinamisha kichwa chini Kwa haiba ya kike.
"Naitwa Samir ni mume wako mtarajiwa Mimi. Najua hatuwai kufahamiana kabda nitazame usoni vizuri na useme kama umeniridhia kuwa mume wako au laaah!". Samir aliongea hayo. Kwakweli sikuwa na ujasiri wa kumtazama kabisa.
"Unaniogopa?". Aliniuliza.
"Hapana".
"Sasa Kwanini hutaki kunitazama". Nilijikaza na kumtazama usoni ila sikumaliza hata sekunde tano niliinamisha kichwa chini.
"Nafaa kuwa mume wako. Kuwa huru ili badae tusipeane majuto".
"Upo sawa tu Samir".
"Ukiwa na maana kwamba umeniridhia?". Niliitikia kwa kichwa nikiwa na maana ndiyo nimemridhia.
"Nashukuru kama kweli. Basi nikuache kidogo nipo nje". Samir alisema hayo na kutoka chumbani kwangu. Nilishusha pumzi Kwa nguvu hapo uso ulikuwa umeolewa jasho la uoga acha tu.
"Mmmh! Mbona balaaa hili. Kwaiyo huyu ndo ananioa mimi. Woiiiih π". Samir mzuri nyie acheni tu. Na mwili wake wa mazoezi yaani sijui nimuelezeaje ila kiufupii Kila mwanamke anatamani kuwa na mwanaume kama Samir. Uzuri ukichanganya na utanashani wake basi ndo anazidi kuwa handsome la kwenda.
Kama lisaa limoja alikuja Tena mama Samir akiwa ameongozana na Binti mmoja wapo kati ya wale wawili niliowaona wanashuka kwenye gari.
"Ni wifi Yako huyu. Mdogo wake na Samir. Najma huyo ndo mke mtarajiwa wa kaka Yako.
"Ni mrembo. Karibu nyumbani". Najma aliongea hayo ila uongeaji wake sikuuelewa kivile.
"Asante. Karibu pia".
"Okay!.
"Nadra mwanangu sisi tunaenda nilikuja kukuaga tu".
"Sawa mama. Karibuni tena".
"Tutakaribia". Walitoka chumbani ila nilishangaa roho inauma eti kwasababu Samir hajaja kuniaga.
Kama kawaida nilisimama dilishani kuwachungulia Kwa chini wanavyoondoka.
Niliwaona wanaelekea parking ya magari, walianza kupanda mmoja mmoja kwenye gari, sijui Samir alijua kama napiga chabo dilishani. Kabda hajapanda alitazama juu na kuniona nimesimama dilishani. Aliachia tabasamu na kunipungua mkono. Na mimi nilifanya hivyo hapo kiroho kikasuuzika sasa. Aliingia kwenye gari na muda mchache waliondoka. Niliwasindikiza Kwa macho mpaka walipotokomea.
Ndani ya gari Samir alikuwa ameshika usukani. Yupo makini na Sheria za barabarani.
"Usiniambie baba kumbe wanamke mwenyewe ndo yule aliyekuwa anachungulia dirishani?, na wewe umempenda kabisa yule mwanamke loooh!.
"Samira!" Samir alimuita mwanae Kwa hasira.
"Usimfokee bhana ni kweli hata haendani na wewe. Samira yupo sahihi maana hata mimi pia nimemuona". Najma aliongea hayo. Samir alipotaka kumjibu Kijana mwengine ambaye alikuja kama mshenga alimtuliza.
Upande wangu nilikuwa chumbani, mama aliingia akiwa amepambwa na tabasamu usoni mwake.
"Mambo yamenoga mwanangu".
"Umefurahi mwenyewe?".
"Sana mwanangu. Ujue unaenda kutupa heshima kubwa sana naomba usituangushe tu huko kwenye ndoa. Uwe mtulivu na mtii Kwa mumeo, mapungufu madogo madogo mnamvumilia sawa?".
"Ni sawa mama ila mpaka naogopa mwenzio".
"Unaogopa Nini?".
"Mama Samir mbona kama amenizidi uzuri hata mimi jamani. Nawezaje kuongozana nae kama mume wangu, mwanaume mzuri mpaka anaogopesha". Mama alianguka kicheko Cha nguvu.
"Sio utani mama". Niliendelea kumlalamikia mama.
"Ujue Nadra wewe ni mzuri sana tatizo hujijui. Ila si nilikwambia ukimuona unaweza kupagawa, umeamini Sasa?".
"Kabisa mama nimeamini na nimeogopa pia".
"Usiogope, hata wewe ni mrembo mno na hapo tu ulikuwa hujapata mwanaume wa maana, mwanangu wewe mzuri bhana jiamini. Sura unayo, shepu unayo. Macho Yako Sasa yalivyo mazuri, Rangi Yako ya dhahabu. Bado una elimu Yako nzuri tu. Wewe sio wakuumizwa na mapenzi bhana. Sasa na NYOTA unayo. Umepata mwanaume wa maana ukatulie huko.
"Sawa mama nimekuelewa". Mama alitoka chumbani muda mchache aliingia Hiliam mdogo wangu. Na yeye alimmwagia sifa kibao Samir.
Upande wa Samir walifika kwake. Samira alikuwa amenuna balaa.
"Mbona upo hivyo Samira?". Bibi yake alimuuliza.
"Hivi bibi ni mwanamke Gani yule baba anataka kumuoa?, mimi sijampenda kabisa.
"Kwaiyo unataka utakayempenda wewe ndiye amuoe baba yako. Sio lazima umpende wewe, nakujua ulivyo mkorofi usije ukasubutu kumfanyia fujo Nadra utanitambua mimi ni nani". Mama Samir aliongea hayo Kwa ukali. Simira alimuangalia bibi yake Kwa hasira na kupandisha juu gorofani.
Muda mchache alishuka gorofani akiwa amebadilisha nguo. Namna alivyovaa Sasa unaweza kusema ni kahaba.
"Unatoka?". Shangazi Najma alimuuliza.
"Yeah!".
"Unaenda wapi, na si nilishakukataza uvaaji wako huko Samira?". Baba yake alimuuliza.
"Achana na maisha yangu, nilishakwambia achana na maisha yangu Samir hayakuhusu". Dharau za Samira Kwa baba yake zilipigiliza. Sijui alikuwa anamtazamaje baba yake.
"Umeniitaje?". Samir alimuuliza Samira na kupiga hatua ila kabda hajamfikia alishikwa mkono na mama yake.
"Usimpige muache aende". Mama Samir aliongea hayo. Simira alifungua mlango na kuondoka.
"Nenda chumbani kapumzike mwanangu". Samir alipandisha juu chumbani kwake.
"Lakini mama mbona yule mwanamke ni wakawaida tu. Hata haendani na kaka kabisa. Kwanza anaonekana mshamba" Najma aliongea hayo.
"Mshamba kwakuwa hajavaa kimini kama unavyovyaaga wewe?, alafu hawahendani kivipi?".
"Ujue kaka yangu ni handsome sana. Sasa yule mwanamke sura yake hata sijaielewa.
"Mpuuzi wewe wivu utakuuwa. Hivi unadhani wewe unasimama mbele ya Nadra?, Nadra amekuzidi Kila kitu mpaka heshima. Binti ana heshima yule. Hana majigambo na Wala Hana maringo. Ana elimu yake ya ngazi za juu sio kama wewe uliyekimbia shule saivi umeganda tu hapa Kwa kaka Yako. Usitake niongee mabaya Yako zaidi ukaona sikupendi. Chunga hizo tabia zako za kujiona wewe ni bola kuliko mwengine". Mama alimsema najma. Najma alikaa kimyaa maana anamjua mama yake vizuri.
Majira ya usiku nilikuwa chumbani, akili yangu ilikuwa inamtafakari Samir tu. Mala niliona simu yangu inaita. Namba ilikuwa ngeni. Sikutaka kupokea nilihisi huenda ni Jafari. Iliita mpaka ilikata.
Ile namba ilipiga tena. Simu ilianza kuita na muda huo mama aliingia chumbani kwangu.
"Huoni simu inaita?".
"Achana nayo, kwanza hata simjui ni nani anayepiga. Nahisi ni Jafari mama".
"Pokea huenda ni Samir".
"Hana namba yangu".
"Wee pokea umsikilize". Nilipokea simu na kuiweka sikioni.
"Hello!. Nilisikia sauti ya kiume.
"Hello!, naongea na nani?".
"Ni mimi Samir. Baada ya kujitambulisha kuwa ni yeye. Mapigo yangu ya moyo yalianza kwenda mbio. Nilijikuta napatwa na kiwewe hata kushindwa kuongea......... ITAENDELEA..........
SIMULIZI : NYOTA YANGU
MTUNZI : NURU HALISI
WHATSAPP NAMBA 0683009150
PAGE : Hadithi Za Nuru Halisi
SEHEMU 05
ENDELEA......
Nilijikuta napatwa na kiwewe mpaka kushindwa kuongea chochote.
"Niambie Nadra".
"Safi tu. Niliongea huku nikiwa natabasamu.
"Okay. Nikutakie usiku mwema".
"Na kwako pia Samir".
"Nashukuru". Alikata simu. Nilishusha pumzi na kumgeukia mama, mama alikuwa ananiangalia kwa tabasamu.
"Anakupenda si unaona uvumilivu umemshinda ameona akupigie simu hata kukutakia usiku mwema".
"Mama na wewe mpana loooh!".
"Sio mpana si umeona hata wewe. Mwanaume anayekupenda hawezi kulala pasipo kukutakia usiku mwema".
"Tatizo huwajui wanaume vizuri mama. Anaweza kukuigizia upendo ili akuchezee tu".
"Ni kweli ila sio wote. Wengine wanawaheshimu sana wanawake. Wanawatazama kama dada zao na mama zao. Hawawezi kuwavunjia heshima Wala kufanya jambo Kwa kuwakomoa ama kuwaumiza. Yupo radhi aumie yeye".
"Mwanangu unatakiwa ujiamini. Ukijiamini unaaminiwa pia, Ukijipenda unapendwa pia, ukijikubali unakubalika pia, sijui umenielewa vizuri?".
"Nimekuelewa mama".
"Sawa. Bado wiki mbili tu na wewe uwe mother house". Kesho Kuna kungwi anakuja hapa kukufunda.
"Habari za kungwi achana nazo mama. Hizo habari za kishamba na za kizamani mie hapana".
"Hakuna uzamani wale Wana umuhimu wake ujue?".
"Mie sitaki bhana mama. Achana nao".
"Mmmh! Sawa, basi nitakufundisha Mimi".
"Kama ni wewe sawa".
Baada ya Samir kumaliza kuongea na Mimi kwenye simu. Alitazama ukutani kilikuwa na picha kubwa ya mke wake.
"Nakukumbuka sana my love wife. Mpaka Sasa Bado unaishi moyoni mwangu. Wewe ndiye mwanamke pekee uliyewai kuuteka moyo wangu na kuufanya vile utakavyo. Mpaka Leo Bado unaishi moyoni mwangu. Nisamehe kwa haya maamuzi nayofanya ya kuoa mwanamke mwengine ikiwa Bado nakupenda. Umeondoka mapema na kumuacha mwanao Bado mdogo. Huenda ungekuwepo mpaka Leo hii. Samira asingekuwa hivi alivyo, huenda Samira Leo angenitazama kama baba yake na kuniheshima". Samir aliongea hayo Kwa hisia Kali na maumivu ndani ya moyo wake mpaka alidondosha chozi mtoto wa kiume.
Alimpenda sana mke wake na mama wa mtoto wake Samira japo ndoa hazikosi changamoto ila upande wake alifanya hata Yale yaliyo nje ya uwezo wake ila tu Aishi na mke wake milele, alijitahidi kumtunza vizuri mke wake na kumpa Kila kitu atakacho ila ndo hivyo. MUNGU alimuondoa mapema kwenye uso wa DUNIA na kumuachia mtoto Samira kipindi hicho akiwa na miaka miwili mpaka Sasa ana miaka 21.
Siku zilizidi kusonga mbele maandalizi ya harusi yalipamba moto Kwa upande wetu. Hatukutaka jambo liwe dogo. Haikuwa Siri tena. Kila mtu alijua Nadra anaolewa ila wengi hawakuju anayenioa ni nani.
Siku Moja kabda ya harusi nilipigiwa simu na Jafari. Jafari hakuamini kama kweli naolewa. Alinipigia simu na kuniomba sana nisiolewe lakini hakuwa na jipya la kunifanya nimuelewe. Nilijua tayari maisha yameshampiga na Hana kimbilio. Nilikata simu na kublock namba.
Hayawi hajawi yamekuwa siku ya ndoa iliwadia nikiwa ndani ya Shera langa nzuri. Nimepambwa nikapambika.
Taratibu zote za Nikkah zilifanyika hatimaye ndoa ulipita. Sikuamini kama ndo nishaolewa Tena na Samir Kijana Handsome na tajiri. Naitwa Mrs Samir Sasa.
Baada ya ndoa niliwaaga familia yangu. Safari kuelekea Kwa mume wangu ilianza. Sikuwai kufika kabda na Wala sijui alikuwa anaishi wapi.
Ndani ya gari tulipanda Mimi na Samir. Pamoja na dereva huku tuliongozana na msafara wa magari matatu nyuma yetu.
Tulifika nje ya nyuma kubwa ya gorofa honi ilipigwa sekunde chache geti lilifunguliwa. Tulipokelewa na baada ya ndugu waliokuja kwaajili ya harusi yetu. Nilishuka kwenye gari.
"Mshike mkono mke wako". Samir aliambiwa na mama yake mdogo. Alinishika mkono na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani huku tukiimbiwa nyimbo za kilugha chao(wasambaa).
Tulifika lango kuu la kuingilia ndani kabda hatujaingia mama mkwe aliongea.
"Yafaa tumkaribishe vyema mkwe wangu Nadra. Naombeni mkalete maziwa kwenye glass. Haraka Binti mmoja alienda kuleta maziwa muda huo Bado tulikuwa hatujaluka kizingiti Cha mlango. Maziwa yaliletwa mama mkwe wangu alininywesha na kumnywesha Mwanae Samir.
"Karibu sana mkwe wangu mzuri". Aliyasema hayo huku akituruhusu kuingia ndani. Baada ya kuvuka kizingiti Cha mlango, mwanaume mmoja wa kamako alimwambia Samir anibebe.
"Yafaa kumbeba mke wako na kumpeleka chumbani".
"Ni kweli kabisa" wapambe welikazia. Nilishangaa tu hii familia mbona Ina mambo kama ya kihindi vile. Hapo nilikuwa nimefunikwa kuzibwa uso baadhi ya ndugu walikuwa wanatamani kuniona. Mwanamke wa Samir sukari ya warembo.
Samir alinibeba Kwa mikono yake miwili na taratibu alianza kutembea kuelekea juu gorofani huku nyuma yetu tulifuatiwa na wapambe wetu. Tulifika kwenye Moja ya mlango wa chumba. Tulifunguliwa mlango na kuingia ndani ya chumba hicho. Chumba kilikuwa na harufu nzuri balaaa hapo Bado sijakiona maana Bado nilikuwa nimejifunika uso.
Samir alinishusha na kunikalisha kitandani. Ndugu walikuwa na shahuku ya kunifaham. Mdada mmoja alitusogelea na kutaka kunifunua ila kabda ya kunifunua mama mdogo wa Samir aliongea.
"Anayetaka kumuona bibi harusi anamuona Kwa Hela. Anamuwekea Hela juu ya nguo mapajani kwake ndipo unamchungulia Kwa Siri wengine wasimuone. Kama huna hela huluhusiwi kumuona, si ndiyo dada?". Aliongea hayo na kumuuliza dada yake mama mzazi wa Samir.
"Ndiyo, wanafaa wamuone Kwa Hela". Hawakuwa na namna zaidi ya kutoa Hela ili kuniona Nadra Mimi. Wakiwa wanaendelea kutoa pesa ili kutaka kunifahamu Mrs Samir mala tulisikia Ngoma na matarumbeta yanalia huko nje........ ........Timu Ngoma ya kungwi imefika mjengoni Kwa Mr Samir Kwa mala la kwanza wakiongozwaa na mtoto wa Mr Samir.... MUENDELEZO ELFU MOJA TU MDAU WANGU. NAMBA YA MALIPO NI 0743770612 JINA JOFREY BIDADILE.
Ukishalipia nichek whtsp Kwa namba hii 0683009150.......