Namba ya WhatsApp- 0683944333
________________________________________
Tulienda mpaka nyumbani na tulipofika akanambia kuwa nisitoke nay eye ataenda kumleta mtoto, nilikuwa nina wasiwasi sana, akawa ananiondoa hofu kisha akaondoka na kuniahidi kuwa atarudi na mtoto nisijali….
Niliingia kwenye maombi maana nilikuwa nina mashaka sana , nilikuwa nampigia simu paul kila wakati ila hakuwa anapatikana, nikazidi kuwa na mashaka maana nilijua kuwa huenda kuna kitu kibaya kimemkuta wakati anahangaika kumtafuta mwanangu, nilijikuta najuta kuingia kwenye maisha ya paul…
Muda ulizidi kwenda na hofu juu yangu ikawa inazidi kuliko kawaida, ilifika kama saa sita usiku bado hakukuwa na dalili ya paul wala mwanangu, nikajikuta nazidi kuomba, mara nikasikia mlango unagongwa, nikaenda kufungua kwa hofu, alikuwa ni paul amembeba mtoto ambae alikuwa amelala, na baada ya kunikabidhi mtoto nikashangaa kapoteza fahamu, maana ni kama alikuwa anajikaza kwa ajili ya mwanae maskinio…
Sikujua shida ilikuwa ni nini, kwa sababu kwanza hata sikujua ameenda kumpatia wapi, nilihisi kuchanganyikiwa na kuanza kupiga kelele kama mwehu, majiran wakatoka na kuja kunisaidia kumpeleka hospital….
Nilimpeleka hospital jardan pamoja na paul, nilikuwa nina mashaka sana maana sikujua kimewakuta kitu gani, paul alianza kuamka kabla ya jarden na alipoamka kitu cha kwanza aliulizia hali ya mwanae,,,
: bado hajaamka nab ado madaktar hawajanipa taarifa kuhusu yeye ile anaonekana kama yupo sawa…
“ hapana chichi hayupo sawa, Yule kapewa dawa za kumfanya alale kwa siku kadhaa ili wamtoe viungo vya ndani wakaviuze, ila paulina ni shetani sana, yaan nisingefika kwa wakati nadhani tungekuwa tunaongelea maiti sasa hiuvi, twende nataka nikamuone mwanangu, akasema paul kisha akasimama na akaanza kuelekewa kwenye wosi ambayo yupo Jordan maana alikuwa chini ya uangalizi maalum…
Tumefika paul akaanza kuuliza hali ya mtoto, “ hana shida sana na nadhan leo ataamka, na ndio maana tumemuweke drip ya glucose ili akiamka awe na nguvu maana si unajua atakaa siku kadhaa bila kula, akasema daktar ila sio mimi wala frank ambae alikuwa na amani…
Kweli kwenye majira ya saa nane mchana mwanangu alimka na neno la kwanza alilolisema ni “ msiniue nipelekeni kwa mama yangu…
Chozi lilinitoka maana niliona huenda mwanangu ameteseka sana, na alikuwa anawaomba sana wasimfanyie kitu kibaya ila hata hawakuwa wanajali kabisa, na alipoamka akaniona mimi, akawa kama haamini, na kwa sauti ya uchovu akasema “ mama umekuja kunichukua, hawa walikuwa wanataka kuniua…
Hapo nilishindwa kuyazuia machozi yangu na nikajikuta nalia, aisee nililia sana maana moyo ulikuwa unaniuma sana, basi Jordan alipatiwa matibabu na tukaambiwa kwa sababu ya hali yake anatakiwa kukaa hospital siku tatu kwa ajili ya uangalizi na hakuna ambae alipinga juu ya hilo…
Baada ya siku tatu aliruhusiwa na namshukuru mungu alikuwa salama na alichangamka, sio mimi wala baba yake tuliamin kama tiunaweza kuwa familia tena, sasa baada ya kuhakikisha usalama wa kila mmoja nikataka kujua ilikuwaje mpaka Jordan akachukuliwa, na kwa maelezo ya paul ni kwamba aliekuwa amemchukua ni ex mke wake paulina…
Paul akanambia tuachane nae maana muda ule yupo polisi yeye pamoja na wajinga wenzake na nitahakikisha wanafia jela maana siwez kuwaruhusu watu wenye roho mbaya kiasi kile waendelee kukaa uraiani…
ITAENDELEA…
Full sh 1000
Njoo WhatsApp katika namb 0683944333.