, nilimchukua Ili aje tuwe tuna saidiana dukani na saluni, Mimi Nina duka la vipodozi na salun pembeni hivyo nikataka yeye awe anakaa dukani huku Mimi nikikomaa na saluni.
Huyu mdogo wangu nilikaa naye kwangu miaka miwili na nilikuwa namlipa mshahara na kwangu alikuwa hachangii chochote na nguo nilikuwa namnunulia na nikampa na uhuru kabisa, nilimwambia Kila akitaka kutoka awe tu anakuwa huru kunipa taarifa.
Badae aliniita na kuniambia kuwa amepata mchumba hivyo anataka akampangishie na anataka amfungulie Biashara, nikamwambia sawa naomba unitambulishe Kwa huyo mwanaume mana haiwezekani nikuruhusu utoke hapa ukaishi na mtu simjui, Hilo jambo lilileta mzozo wiki nzima tukawa hatuongei ndani na kazini akawa haendi, kisa tu hataki nimuone huyo mwanaume, mwisho wa siku mume wangu akaniambia nimruhusu tu mdogo wangu aondoke, kesho yake akawa ameondoka.
Akawa anakuja sana nyumbani na kazini, Yani licha ya kuondoka kwangu ila mara nyingi akawa anashinda kwangu, nikawa naona sawa tu, mwisho wa siku akapata ujauzito, na ujauzito ulivyo fikisha miezi 7 akaniomba aje kukaa kwangu, nikasema sawa haina shida, alikaa kwangu mpaka alipo jifungua na nikasimamia mambo yote ya uzazi mwezi mzima ndo akawa ameomba kurudi kwake, lakini muda wote huo nikawa nikimuuliza kuhusu mzazi mwenzie anadai Yuko Arusha kikazi anafanya kazi za utalii, na pesa akawa anatumiwa na Mimi nikawa ndo naenda kuzitoa .
Alivyo rudi kwake Sasa ikapita kama miezi miwili, Kuna siku nikawa namsuka mdada mmoja hivi saluni kwangu, na bahati nzuri mume wangu akawa amekuja na gari lake akapaki mbele pale akaja mpaka saluni alitusalimia vizuri akawa amenikabidhi pizza akawa ameondoka, alivyoondoka ndo huyu mteja wangu akaniuliza kwani huyo ni nani yako? Nikamjibu mume wangu, kwani na wake wawili? Nikamjibu hapana, ni Mimi tu na tuna watoto wawili, yule dada ndo akaanza kuniambia, hapana dada huyu baba ana mke mwingine jirani na kwangu kabisa na analalaga hapo mara nyingi namuona sijamfanannisha na Kila jioni namuona pale na gari hili hili, nikabaki kushangaa kichwa kikawaka moto, yule dada akasema na ukitaka uhakika tutoke hapa twende tukae kwangu uone kama jioni hutomuona.
Kwakweli ilibidi tu nifunge saluni nikamuaga dada wa dukani tukaongozana na huyu dada mpaka kwake, tulivyo fika kwake akanisontea nyumba ambayo mume wangu inasemekaka ana mke hapo, huyu dada akaniambia tulia tu hapa hapa na huyo mwanamke utamuona tu ila mumeo huwa anakuja saa 12 jion, niliendelea kukaa hapo huku macho muda wote yapo kule kwenye Ile nyumba, mara nikamuona mdogo wangu ndo anatoka ndani huku kashikilia mtoto, huyu dada akasema mke mwenzio ndo huyo hapo Sasa, niliishiwa na nguvu, hatujakaa sawa mara gari la mume wangu nalo likafika pale na mdogo wangu akawa ameenda kumpokea, mume wangu akachukua mtoto huku mdogo wangu akienda nyuma ya gari kutoa vitu, nilijikuta nawakimbilia walipo ila nilijikuta napoteza fahamu nikiwa mbele ya mume wangu.
Leo ndo nimetoka hospital Toka jumatatu, sielewi nifanye Nini, nahisi Dunia yote imeniangukia, kushea mwanaume na ndugu wa damu hii kitu ni ngumu kuipokea Mimi Kwa upande wangu, moyo ni kama unavuja damu.
Muda wote naagwa kuwa mwanaume kasafiri, namuombea Kwa MUNGU Ili amlinde kumbe mtu yupo hapa hapa dar tena na mdogo wangu wa damu..