Endelea ๐ป
Mwili wa mwanamke asiyejulikana amekufa au mzima ulionekana ufukweni mwa bahari.
Liam alisogea haraka akiwa kakata tamaa....aliwaita waokoaji waje kubeba maiti.
Vipimo vilifanyika, ilifahamika huyu naye amekufa pia
"Meli yetu inauwezo wa kubeba watu 280 tu hivyo uzito wa abiria hucheza kwenye 19600 kg....ukiachana na mizigo ya kwenye mabehewa inayokomea tani 15000, hii maiti iliyopatikana imeleta idadi ya watu 281 nadhani hii ndio sababu ya Meli kuzama.... uzito wa abiria ulipaswa ukomee 19600 kg au ushukue zaidi ya hapo cha ajabu inaonesha uliongezeka sababu ya mtu mmoja" Mkaguzi wa Meli aliongea
"Hakikisha hii taarifa haivuji kwanza....acha idadi ya maiti ibakie 280 na si 281" Liam aliongea
Maiti iliyopatikana ilipelekwa moja kwa moja kwenye chumba maalumu.
Liam alihitaji kujihakikishia mwenyewe kwa kuzihesabu maiti zote upya kabla hajafuatwa na waandishi wa habari kutakapo pambazuka
Akiwa katika kuhesabu kwa umakini mkubwa....ilisikika chafya.
Alisitisha zoezi lake akaanza kuangaza huku na kule.
Maiti iliyopatikana dakika chache zilizopita ilionekana ikitapata tapa ndani ya mfuko
Liam alisogea haraka akaufungua mfuko.... moyo wake ulishtuka baada ya kumuona Sultana aliyekuwa hoi taabani.
Machozi ya furaha yalimtiririka baada ya kujua angalau kuna mtu mmoja yupo hai.
"Watu hawapaswi kufahamu kuhusu yeye.....nitampeleka nyumbani kwangu. Kuna muda bahari inakuwa rafiki kwetu na muda mwingine huchafuka. Hivi ndivyo nitakavyo zungumza siku ya kesho....naamini katika wewe hivyo naomba usizungumze kuhusu mtu aliyeongeza uzito kwenye Meli" Liam aliongea
"Kwa ajili yako nitafumba macho...." Mkaguzi wa Meli aliongea kisha akaendelea na majukumu yake
Liam aliingia kwenye gari lake, safari ya kuelekea ndani ya Jumba La Dhahabu ilianza
๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป
Bi. Fatma na Ali wakiwa wamekaa sebuleni kwa masikito makubwa, walishangazwa na ujio wa Liam akiwa kambeba mtu aliyeonekana kuwa hoi taabani
"Mama..... naomba tumsaidie Sultana..." Liam aliongea huku akipitiliza kwenye chumba cha wageni
Bi. Fatma na Ali walimfuata kwa nyuma
"Huyu si ni yule Binti aliyelifananisha Jumba hili na hekalu...." Bi. Fatma aliuliza kwa mshangao
"Ni mmoja wa watu waliokuwa kwenye Meli, nina sababu zangu za kumleta hapa tafadhali sana naomba umsaidie" Liam alibembeleza
Bi. Fatma alikuwa Daktari bingwa katika hospitali ya Jiji la Odes, kutokana na umri wake kusogea mbele alistaafu. Ilimlazimu kumuokoa binti aliyeletwa na Kijana wake
Ali na Liam walimpisha.... mara nyingi anapendelea kufanya kazi yake bila kusimamiwa.
Japo ilikuwa ni usiku lakini Liam alienda katika Pharmacy kubwa zilizokuwa wazi masaa 24 kuchukua vifaa alivyo agizwa na Mama yake
"Kazi yangu imeisha.....ni swala la yeye na nafsi yake kuamua kufa au kuishi" Bi. Fatma aliongea
Liam alimshukuru Mama yake kwa msaada alioutoa.
Badala ya kwenda kulala alikuwa Mlinzi wa muda kwa Sultana.
Upande wa Bi. Fatma akiwa chumbani kwake alianza kufanya dua kwa ajili ya mgonjwa aliyemsaidia.
"Niliahidi kujipendekeza kwake kwa ajili ya Liam... tafadhali sana naomba umponye haraka iwezekanavyo " Bi. Fatma aliongea na mungu tembo
Baada Ya Siku Mbili Kupita๐ป
Hali ya Sultana ilitengamaa....uzuri wake uliendelea kung'ara maradufu kama mwanzo
"Ahsanteni kwa msaada wenu....watu wa Kijiji changu watakuwa wamenisubiria sana ni wakati wa Mimi kuondoka" Sultana aliongea ilihali hakuwa na mtu hata mmoja anaye msubiria
"Hapana, nahitaji uendelee kukaa hapa mpaka nitakapo jiridhisha mwenyewe kuwa unaendelea vizuri...." Bi. Fatma alisisitiza
"Mama yupo sahihi...bado unaonekana mgonjwa machoni mwangu" Liam aliongea
Sultana aliachia tabasamu na kufanya wote wamkodolee kwa namna alivyokuwa mrembo.
Kabla hajawauliza kwanini wana mshangaa namna hiyo, mlango ulifunguliwa baada ya kugongwa....ni wazi mtu aliyekuwa anaingia mahali hapa alikuwa mwenyeji
Sultana alishtuka baada ya kukutana macho na mwenyeji aliyeingia
Itaendelea ๐ฅ.