Hatukumjibu chochote kisha akasema haya kila mtu darasani, Tukawa tumerudi darasani,
Tulipoachiwa kutoka shule mimi nilifika nyumbani na kuwadanganya wazazi wangu kwamba kuna mahitaji muhimu tumeambiwa tununue pamoja na vitabu kwa ajili ya mtihani, Wazazi wangu walikuwa wanajitolea sana kunisomesha, Wakawa wamenipatia pesa ili nikanunulie mahitaji,
Ukweli ni kwamba ile pesa niliyoomba kwa wazazi wangu nilikuwa naenda kumpatia tina. Kesho yake nilipofika shule nilimtafuta tina na kumpatia ile pesa, Tina alifurahi sana alirukaruka na kunikumbatia, Kwa mara ya kwanza tina akanipiga busu katika shavu langu la kushoto, Nilihisi mwili kusisimka.
Lakini mwalimu Jose toka amenifumania na tina hakuniambia chochote. Ilinipa mawazo kidogo maana sijui anachopanga.
Siku moja kabla ya mtihani mwalimu jose alinifuata na kuniambia niachane na tina, Sababu ataniharibia masomo, Vinginevyo yatanikuta makubwa zaidi. Kiukweli alinichanganya sana harafu ukizingatia ni wakati ambao tunaelekea kwenye mtihani,
Siku ya mtihani ikawa imefika lakini mimi wakati wote nilikuwa nawaza suala la mwalimu jose kuniambia niachane na tina, Kitendo cha kuambiwa niachane na tina kilifanya niamini kati ya mwalimu jose na tina kuna kitu kinaendelea na wananificha,
Tulimaliza kufanya mtihani lakini mimi sikuelewa mtihani wenyewe umeenda vipi na umeisha vipi sababu wakati wote nilikuwa nawaza kuhusu mwalimu jose na tina, Tulipomaliza mtihani tukakaa tukisubiri matokeo,
Wakati tunasubiri matokeo niliamua kumuuliza tina kama kweli ana mahusiano na mwalimu jose na siku ile alilala wapi, Tina alifunguka na kusema ukweli kwamba alikuwa na mahusiano ya siri na mwalimu jose, Na ile siku ya sherehe mwalimu jose alimlazimisha tina kumpeleka guest. Nikawa nimepata jibu kumbe siku ya sherehe tina alilala guest na mwalimu jose, Dah niliumia sana kusikia kwamba mwalimu jose alikuwa anatembea na tina wakati mimi sijawahi hata kulala nae,
Tina akaniambia hata ile kupendeza pale shuleni alikuwa anahudumiwa kila kitu na mwalimu jose, Lakini tina akanihakikishia kwamba ameshaachana na mwalimu jose, Na atabaki na mimi, Nilifurahi kusikia hivyo.
Mapenzi mimi na tina yakaanza upya, Nikazidi kumpenda tina na nikaanza kupambana kutafuta kazi ndogo ndogo ili nipate pesa. Dada yangu pale nyumbani akawa amepata mchumba kutoka mjini, Yule mchumba akaleta na posa kabisa, Posa ilikubaliwa na mahari wakatoa, Kisha yakaanza maandalizi ya harusi, Nilimwambia tina asikosekane kwenye harusi ya dada yangu pale nyumbani kwetu.
Wakati huo tukisubiri siku ya harusi ya dada, Matokeo ya form four yakawa yametoka, Lakini mimi sikufaulu inamana kwamba nilifeli kuendelea na masomo, Wazazi wangu waliumia sana na kunifokea nilionekana kama mjinga pale nyumbani, Baba alifikia hatua ya kunifukuza pale nyumbani lakini mama na dada wakanitetea. Lakini upande wa tina yeye alifaulu kwenda Chuo, Na alipongezwa na wazazi wake. Na mimi nilipopata taarifa za tina kufaulu nilimpongeza Japokuwa yeye alihuzunika alipoona mimi nimefeli.
Maisha yakaendelea tarehe ya harusi ya dada yangu ikawa imekaribia, Tuliandaa kila kitu, Tukaalika na watu, Lakini pia sikumsahau tina.
Ilipofika siku ya harusi watu tulisherehekea na dada akawa amefunga ndoa na kupelekwa kwa mume wake kule mjini, Tulibaki tukimalizia sherehe huku mziki mkubwa ukichezwa pale nyumbani, Kiufupi ilikuwa ni hakuna kulala, Tina akasema leo nitalala kwako sitaenda nyumbani maana niliaga naenda kwenye harusi hivyo hata nikilala kwako haitakuwa kesi.
Mwanaume kama mwanaume ilibidi nifanye mpango wa kuandaa mazingira, Nilitafuta geto kwa washkaji nikawa nimepata, Mwenye geto ilibidi akeshe akicheza disco pale nyumbani kwetu, Muda ulipofika nilimchukuwa tina na kuelekea naye kule magetoni, Tulifika pale magetoni tina akagoma kuingia ndani,eti akasema atakuja siku nyingine,,,Mmmh nikamwambia acha kuvunga,mtoto nikamshika mkono nikazama nae hadi ndani...
Usiku ule ndio ilikuwa mara ya kwanza kulala na mwanamke kama tina, Hakika nilijionea ulimwengu mwingine nikiwa juu ya kifua cha tina, Nilikuwa nikijisemea moyoni kumbe mapenzi ni matamu kiasi hiki.π Kweli tina alikuwa ni fundi mtoto alijua kuninogesha.
Saa kumi za usiku kabla hapajapambazuka tina aliniamsha na kuniambia nimsindikize nyumbani ili asije kuonekana kama hakurudi nyumbani, Niliamka na kumsindikiza tina hadi nyumbani kwao, Tukaagana kwamba tutaonana asubuh, Wakati tina anaondoka kuelekea pale kwao sikuondoka mapema nilisubiri hadi nimuone tina anaingia ndani. Tina alienda na kusukuma mlango wa nyumba anayolala na kuingia ndani. Mimi nilirudi nyumbani na kumkuta mshkaji wangu anamalizia kucheza Disco, Nikampatia funguo. Kwakuwa nilikuwa nimechoka niliingia ndani mwangu na kulala.
Asubuh niliamka na kufanya kazi za nyumbani lakini ilipofika jioni nikaendelea na mambo yangu sikutaka kumtafuta tina, ila nilikuwa nimemiss kumuona, Na wakati huo sikuwa hata na simu lakini nikaona hakuna shida nitaonana nae tu.
Zilipita siku tatu bila kuonana na tina, Nilijikuta naanza kuwa na wasiwasi mbona kimya kimezidi harafu hata kuonekana haonekani, Nilijaribu kumtafuta sehemu ambazo nilitegemea kumuona lakini sikumuona, Ikabidi nimtafute rafiki yake na kumuuliza kama anafahamu tina alipo, Rafiki yake aliniambia kwamba tina ameshaenda chuo kwa ajili ya kuendelea na masomo, Moyo uliniuma sana kusikia tina ameondoka mbaya zaidi aliondoka bila hata kuniaga.
Nilianza kuishi maisha ya bila uwepo wa tina lakini mawazo yangu yote nilikuwa namuwaza tina, Siku zikasonga ikabidi nguvu kazi yangu niielekeze kwenye kazi nilianza kupambana ili nipate simu, Na wakati huo nikaanza pia kuwa naenda kwenye mazoezi ya mpira,
Nakumbuka siku moja nikiwa natoka mazoezini nikiwa na marafiki zangu wawili, Tulimkuta mwanamke mmoja akiwa na gari lakini gari lake limepata pancha na amesimama pembezoni mwa barabara...
Itaendelea...βπ»
Sikuombi pesa yako lakini naomba unapomaliza kusoma Simulizi hii hakikisha una comment na ku Like...
~Daudi~.