Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Tukaungana watu watatu na kuanza kutafuta vifaa vya kutengenezea kengele... Tunaendelea... Sehemu Ya 3

31st Jul, 2025 Views 8



Tulifanikiwa kupata vifaa na kuanza kazi ya kutengeneza kengele, Lakini wakati huo tulikuwa tunakaribia kuhitimu kwahiyo waalimu wakapendekeza kabla ya mtihani, Tufanye kwanza sherehe ya Mahafali, Waalimu walikaa na kupanga tarehe ya sherehe za form 4, Wakapanga na kiasi cha mchango kwa ajili ya sherehe,

Mwalimu ambaye aliteuliwa kusimamia mambo yote na ukamilishaji wa sherehe,vyakula na michango, alikuwa ni yule mwalimu ambaye alisimamia kesi ya Tina kupelekewa barua na Side. Yule mwalimu alikuwa anaitwa mwalimu Jose,

Mwalimu Jose alinifuata na kunipatia kazi ya kukusanya mchango wa pesa kutoka kwa wanafunzi wenzangu wa form 4, Nilianza kuchangisha mchango kwa ajili ya sherehe huku tukiendelea na mpango wetu wa kutengeneza kengele,

Wakati naendelea kukusanya mchango, Nilimuona Tina amekaa peke yake nilimfuata na kumuuliza mbona kama huna furaha tatizo nini? Tina akasema mwalimu Jose amekuwa akinitongoza mara kwa mara na nimekuwa nikimkataa lakini bado anang'ang'ana kutaka kuwa na mimi.

Dah nilikosa cha kumjibu tina, Ikabidi nimwambie maneno angalau ya kumfariji. lakini moyoni niliumia kusikia kwamba mwalimu aliyenipa kazi kumbe ndiye anamtongoza Tina wangu.

Niliendelea kukusanya mchango hadi nikakamilisha lakini nilimlipia na Tina pamoja na mimi. Siku ambayo napeleka mchango wa mwisho kwa mwalimu Jose,ili nimpatie na ripoti kuhusu hesabu na kiasi kilichopatikana, Niliingia ofisini na kumkuta Tina akiwa anaongea na mwalimu Jose, Moyo uliniuma mno sababu Tina ni mpenzi wangu harafu naelewa kwamba mwalimu Jose anamtongoza,

Nilimpatia ripoti na kuondoka.

Nilienda kukaa darasani huku nawaza au Tina ananidanganya! mbona alionekana kuwa msikivu sana na nilipofika walistopisha maongezi na Tina akaondoka! Nilianza kuhisi wivu kwa Tina. Aliingia mwalimu wa kipindi na kuanza kufundisha kiukweli sikumuelewa hata kidogo.

Badae nilikutana na Tina lakini sikumuuliza chochote, Mahusiano yakaendelea mimi na Tina, Lakini hadi wakati huo Tina alianza kuniambia kila mwanaume anayemtongoza, Yaani ukimtongoza Tina lazima anifikishie, Nilikuwa namwambia tu,achana na hao wapuuzi, Lakini hadi hapo nilikuwa bado sijawahi kulala na Tina, Hata hivyo wale marafiki ninaotengeneza nao kengele walikuwa tayari wameshajuwa kama mimi na tina ni wapenzi.

Badae mwalimu Jose aliniita tena kwa mara nyingine na kunipatia kazi ya kufanya mahesabu kuhusu kununua vitu na kupanga matumizi, Alinipatia karatasi ambazo amezitayalisha, Nilizichukuwa na kuondoka nazo ili nikipata muda nizifanyie kazi,

Badae nilipata muda nikamtafuta Tina na kumuomba anisaidie kupanga vitu vya kununua na matumizi mengine lakini pia kama kuna vitu nimesahau atakuwa akinikumbusha, Tulikaa tukapanga kila kitu mimi na tina, Kisha nilimpelekea mwalimu Jose na kumpatia.

Mwalimu Jose alipokagua kazi niliyoifanya alifurahi na kunipongeza sababu nilipanga vitu kama inavyotakiwa,kama kuna vitu vya kuongeza niliongeza kama ni kupunguza nilipunguza.

Ikabidi tuendelee na kutengeneza kengele yetu, Lakini wakati tunaelekea na utengenezaji wa kengele siku ya sherehe ilikuwa imekaribia. Tina alikuwa akiniahidi siku ya sherehe atatumia muda wake kufurahi na mimi, Kwakweli siku zilivyozidi kwenda nilijikuta nazidi kumpenda Tina.

Hatimaye siku ya sherehe ikawa imefika na kengele yetu tayari imeshakamilika, Tulifanya maandalizi ya sherehe za Mahafali ya form 4, Kila kitu kikawa sawa, Mwalimu Jose alikuwa ananituma mara kwa mara alinifanya kama msaidizi wake pale shuleni. Muda ulipofika sherehe ikaanza..

Ulifika muda wa viongozi kutambulishwa walikuwepo wageni na viongozi wa serikali, Nakumbuka pia alikuwepo na wazili wa sanaa na michezo, Ulifika muda wa sisi kutambulisha kazi yetu, Tuliiweka kengele yetu mbele ya viongozi na wageni waalikwa kisha tukaifanyia majaribio, Kengele ilikuwa na mlio mzuri na wenye kusikika vizuri, Watu wote walitupigia makofi na kitupongeza kwa kazi yetu nzuri, Wazazi wetu pia walikuwepo na walifurahi kuona tumetengeneza kitu cha maana na chenye kukumbukwa muda mrefu,

Tina yeye alipewa hongera ya kuwa mschana msafi kuliko wote pale shuleni. Ukweli Tina kwa usafi na kupendeza alikuwa yupo vizuri sana, Mimi nilikuwa sina pesa za kumpatia lakini alikuwa anapendeza sana.

Baada ya sherehe kuelekea mwisho yule wazili wa michezo na sanaa akasema ile kengele iwekwe sehemu husika na itakuwa inafanya kazi pale shuleni.

Mimi na marafiki zangu ambao tulishirikiana kutengeneza ile kengele tulifurahi sana,

Sherehe ilienda vizuri hadi mida ya jioni, Tulipiga picha mimi na Tina tukiwa tumeshikana kwa furaha na tabasamu tamu, Kisha tulicheza dance nikiwa nimeshika kiuno cha Tina, Hadi wanafunzi wenzangu wakawa wanashangaa nimepata wapi ujasiri wa kumshika kiuno mschana mzuri kama tina,,,

Muda ukaenda hadi mida ya saa moja hivi, Lakini ghafla nikawa nimepotezana na tina na sielewi ameelekea wapi...

Tutaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Tukaungana watu watatu na kuanza kutafuta vifaa vya kutengenezea kengele... Tunaendelea... Sehemu Ya 3  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-tukaungana-watu-watatu-na-kuanza-kutafuta-vifaa-vya-kutengenezea-keng
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest